Umeeleza vema sana, ngoja nirudi nikakupe like, sasa naomba utudadavulie kidogo kuhusu fitna za ma don wa town! Am interested kujua walau kidogo! Ahsante!
Ndugu uko wapi? Mbona hii issue ishaelezwa sana hapa jamvini???
Davido alikua ashachukua advance ya mpunga kutoka Times Promotion kwa ajili ya show ya climax inayofanyika tarehe 1 Novemba hapa Bongo. Na kwenye matangazo ya Radio Times Fm walikua washaanza kumfanyia Promo.
Kwenye ratiba ya Fiesta Davido toka awali hakuwemo. Kama unavyojua ile watoto ya mjini issue ya davido wakaamua kuipiga juu kwa juu. Wakamlambisha mpunga kimyakimya wakasanda, wiki ya mwisho ya fiesta Davido akatangazwa ndani ya mjengo kuwa Fiesta inamhusu.
Times wakawa hawaamini kama itawezekana akaimbe fiesta wakati washamalizana naye mikataba na washamchukulia kibali Baraza la Sanaa(BASATA).
Jumanne Clouds wameenda kumchukulia kibali Basata wakanyimwa wakaambiwa washotoa kibali kwa kampuni nyingine iliyowatangulia wao kwenda Basata. Kwa maana msanii wa nje hawezi panda jukwaani bila kibali cha basata.
Clouds hawakuishia hapo kwenye promo za Fiesta wakaendelea kuutangazia umma kuwa Davido atakua uwanjani anakamua kama kawa.
Ijumaa msanii huyo anatua uwanja wa ndege na kupokelewa na watoto ya mujini. Times fm ndo wakaona kumbe jamaa wako serious, wakaamua kukimbilia maakamani kuweka zuio la mahakama. Siku ya ijumaa mchana(juzi) Mahakama ikatoa kibali Cha kusitisha Davido asipafom fiesta mpaka amalize kesi yake na times fm.
Jiulize jana jmos ofisi hazifanyi kazi sio mahakama wala basata sasa jamaa wameyamaliza vipi mpaka davido apate kibali cha kupanda jukwaani kuimba? Na hiyo clouds wamewafanyia makusudi times fm au tuseme wamewahujumu ili tamasha lao la climax la tarehe 1 novemba lifulie. Jiulize mtu aliyemuona leo davido aki-pafom fiesta anaweza kwenda tena kumuona huyohuyo davido tarehe 1 yan wiki 2 zijazo akipafom climax?
Lakini nasikia kibali kimetoka China kwa vasco da gama. Si unajua tena bongo daresalama ukitaka kuwin cheza dili na wale magwiji.