Mtumishi Mimi kwa upande wangu; mabinti wengi ninaofahamiana nao na wapo above 30; wengi wamejikuta umri huo bilabila kwa sababu ya uvumilivu/loyalty yao. Walianza mahusiano high school na wengine vyuoni na hao maboyfriend wakiwa na matumaini ya kuja kuspend the rest of their lives pamoja. So hata walipotokea watu wengine wenye nia za kuwaoa; wao walikataa kwa sababu waliamini tayari wana mahusiano yao serious yatakayozaa ndoa. Wanaume walipoanza kusimama kiuchumi ndiyo wengi walianza kuonesha makucha yao and eventually waliishia kuwaacha Wanawake wao wa zamani; wakaoa mabinti wapya kwao.
Wanawake Mungu atusaidie tu kwa kweli; unakaa na mtu mkihustle miaka na miaka afu unakuja kuachwa solemba. Umri umeshaenda jamii inakusimanga, huku bado unaonekana ni malaya umetumika miaka mingi na ex wako, umebaki na majeraha ya moyo. Ila pia ungemuacha huyo mwanaume wakati bado hajiwezi kiuchumi, ukaenda kuolewa kwingine; ungelaaniwa hadi makaburi ya kwenu teh.
Sio tu Wanawake hatujui tunachotaka, hata wanaume hawajui pia wanachotaka. Na kiukweli wapo wanaume wengi tu ambao wameoa bado uchumi wao ukiwa unasuasua; ila bado comments za wanaume zitakufanya uhisi wote waliooa wana hela au kwenye ndoa zao hawapitii changamoto za kiuchumi kabisa; yaani hakuna wanaume waliooa ambao hawana hela.