Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Nakemea na napinga vikali hoja hii Mimi ni mtumishi wa jehova sinaga mambo ya dunia!. Kama ameshindwa kukutongoza asituseme wengine akirogwa aje aanze kusema kimeenda kimerudi!.
Hahahaha
 
Kweli mlikuwa serious. Vijana wa kileo baada ya mimba wangekimbia
Yeye ndio alikomaa hakunikatia tamaa !! Yani chuo sijasoma kwashida kabisa jamaa alikua anaprovide huku hom nako napewa! Mwaka wa tatu akaona nikimaliza nitamkimbia akawekeza🤣🤣🤣😂😂😂😂!Na alipoteuliwa kuwa mmoja wa waenda nje akasema tufunge kwanza!
 
Yeye ndio alikomaa hakunikatia tamaa !! Yani chuo sijasoma kwashida kabisa jamaa alikua anaprovide huku hom nako napewa! Mwaka wa tatu akaona nikimaliza nitamkimbia akawekeza🤣🤣🤣😂😂😂😂!Na alipoteuliwa kuwa mmoja wa waenda nje akasema tufunge kwanza!
Kwa jinsi ulivyo lazima mjeda akomae na wewe. Inawezekana alikuwa anakipata alichokuwa anakihitaji.
 
Thenki yu !!!

Karibia wote waliovuka 30 bila kuolewa ishu zao zinafanana. Kuna mabraza mob waliotaka kuwaoa wakati wa kilele cha ujana wao (18-25; 26-29) lakini mabraza hao hawakukidhi vigezo vyao - ama vya kimwonekano (tall dark guy) au kiuchumi (gari, kazi, nyumba). Kipindi hiki ni kipindi ambacho mabinti wengi wanakuwa very arrogant. Kuna mmoja nilitaka kumuoa lakini aliishia kunicheka tu. Hata sisi wanaume huwa tunaumia sana. Unampenda sana mtu lakini ndo utasikia we siyo type yangu; au subiri kidogo kwa sasa siko tayari kumbe amekuona hufai kwa vile tu bado unapambana.

Na tatizo ni kwamba katika umri wa 18-30 hata mpaka 35 huko wengi wetu tunakuwa bado tunahangaika na maisha. Lakini mabinti wao wanataka mtu ambaye tayari keshajiimarisha. Na kweli wanachukuliwa na hao wenye kukidhi vigezo vyao vya wakati ule. Na wapo wanaoolewa na wapo wengi tu wanaoachwa. Ndo hawa sasa akija kushtuka oops yuko 30+. Na vigezo ndo kidogo vinaanza kupunguza makali sasa.

Wengi tu mlishakataa mabraza kibao waliotaka kuwaoa kwa sababu hawakuwa na vigezo vyenu mlivyovitaka. Lakini ukiuliza utasikia ooo nilikuwa naye akanicheat...na always makosa ni ya mwanaume.

Tuwafundishe mabinti zetu kuangalia utu wa mtu kama inawezekana. Some of you have lost real good men and soulmates kwa sababu tu wakati ule hawakuwa vile mlivyotaka wawe kiuchumi...

But again; life is a process of making choices and living with the consequences of those choices.

Na swali la muhimu zaidi ni hili: Ni lazima kuoa/kuolewa? Kwani mtu ukiishi tu kivyako bila kuoa/kuolewa kuna tatizo gani?
Mtumishi Mimi kwa upande wangu; mabinti wengi ninaofahamiana nao na wapo above 30; wengi wamejikuta umri huo bilabila kwa sababu ya uvumilivu/loyalty yao. Walianza mahusiano high school na wengine vyuoni na hao maboyfriend wakiwa na matumaini ya kuja kuspend the rest of their lives pamoja. So hata walipotokea watu wengine wenye nia za kuwaoa; wao walikataa kwa sababu waliamini tayari wana mahusiano yao serious yatakayozaa ndoa. Wanaume walipoanza kusimama kiuchumi ndiyo wengi walianza kuonesha makucha yao and eventually waliishia kuwaacha Wanawake wao wa zamani; wakaoa mabinti wapya kwao.

Wanawake Mungu atusaidie tu kwa kweli; unakaa na mtu mkihustle miaka na miaka afu unakuja kuachwa solemba. Umri umeshaenda jamii inakusimanga, huku bado unaonekana ni malaya umetumika miaka mingi na ex wako, umebaki na majeraha ya moyo. Ila pia ungemuacha huyo mwanaume wakati bado hajiwezi kiuchumi, ukaenda kuolewa kwingine; ungelaaniwa hadi makaburi ya kwenu teh.

Sio tu Wanawake hatujui tunachotaka, hata wanaume hawajui pia wanachotaka. Na kiukweli wapo wanaume wengi tu ambao wameoa bado uchumi wao ukiwa unasuasua; ila bado comments za wanaume zitakufanya uhisi wote waliooa wana hela au kwenye ndoa zao hawapitii changamoto za kiuchumi kabisa; yaani hakuna wanaume waliooa ambao hawana hela.
 
Back
Top Bottom