Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Alivyokuwa muongeaji sasa!!!! Ni Yule wa kuwananga wenzie yani aibu ilikua yake mbona sasahivi tangu ahame ameshatutambulisha wanaume kama watatu hivi mwezi huu unatambulishwa huyu mwezie ujao yule.... kiukweli ndoa sio mchezo sio suala la kukurupukia ndoa zina mengi mno!
Maskini atulie yatamshinda tena.
 
Maskini atulie yatamshinda tena.
Mungu amsaidie apate hitaji la moyo wake na mwanaume ataempenda na kutulia nae.
Yani anajituma jamani yule mwanamke anajituma anachakarika kweli kweli alikua anawapenda na kuwajali Ndugu wa mumewe wanaokuja kuwasalimia yani anawajali balaa sijui kwanini hapo tu ndio amekwama mambo ya wawili wanayajua wenyewe! Anyway tuseme God's time haijafika !
 
Kuna work Mate mmoja bana alilazimisha ndoa wakafunga ya serikali na aliyemuita mumewe...
Ilikua 2016 kaona madam A ameshaolewa B ameshaolewa C ameshaolewa... alafosi kamlazimisha mwanaume aliekuwa nae kipindi hiko nae alikua mwalimu mwenzie mpaka wakaenda kufunga ya serikali ilimradi tu asibaki madam pekeake ambae hajaolewa Wakafunga. Balaa likaanza ikawa ni visa na vituko tu humo ndani ikafikia pahala likizo kila mmoja anaenda anakojua yeye na hakuna kuulizana wala kumaindi mwenzio likizo ikiisha wanarudi wanaendelea na drama ndoani...
Ikafikia hatua kila mmoja akawa analala chumba chake hali ikawa mbaya zaidi mwanaume akawa analeta wanawake humohumo ndani kwenye chumba chake.
Mbona mwanamke aliomba uhamisho ghafla bila kutaka. mpaka leo wana hiko cheti cha serikali hawajaenda kuvunja ndoa ila kila mmoja anaendelea na mahusiano mengine huko aliko!!
Halafu alikua yule mtu wa show off masaa yote ofisini ni "Mimi me wangu Mimi mme wangu.. mimi na mme wangu Mimi na mme wangu utadhani wengine hawana waume au hawajaoa na kuolewa!!!! Mbaya zaidi sijui tuseme mwanaume hakumpenda au sijui hata tusemeje.
Mtu mmeamua kufunga ndoa nyie kama nyie wawili badae wewe mwanamke ukampeleka mumeo kumtambulisha kwenu wanamtambua ila yeye mwanaume hana hata dalili ya kukupeleka kwao ukiuliza utanipeleka lini unajibiwa acha kiherehere cha kutaka kujulikana hapo mwanaume huyo ana watoto wawili alishazaa na wanawake wawili tofauti huko Nyuma kabla hawajakutana na baadhi ya likizo eti anaendaga huko kusalimia watoto zake anakaa likizo nzima ikiisha anarudi kwako !! Mshahara wote hana habari za kupanga maendeleo nawewe ndiokwanza anaangalia watoto wake wewe unabaki tu kulia nanafsi yako! Alihama bila kupenda mbona!

Na hili ndio tatizo lililopo ma binti wanaona kama wamechelewa hivi...
 
Wanaume waoaji wapo, sema waolewaji vigezo mob. Tutapinga hadharani lakini ukweli ndio huo….

Kuna mtoto wa mtu hapa ananielewa mwenyewe, anasema fanya mpango tuhalalishe.. lakini mimi ndiyo naona kama he doesn’t fits kwenye vigezo vile si unajua
Siwezi kumwambia kwamba hatuendani, naishia tu kumwambia I CANNOT MARRY MY COLLEAGUE.
Kwamba

Ana kiba100 na wewe wataka tango

Ama ndio kina sie kimoja tu chali

Akati unataka ziki la kufunga ntaa

Wewe wataka wa vigezo gani
 
Alivyokuwa muongeaji sasa!!!! Ni Yule wa kuwananga wenzie yani aibu ilikua yake mbona sasahivi tangu ahame ameshatutambulisha wanaume kama watatu hivi mwezi huu unatambulishwa huyu mwezie ujao yule.... kiukweli ndoa sio mchezo sio suala la kukurupukia ndoa zina mengi mno!

Huyo mwanamke yuko so desperate.

Asipoangalia ataishia pabayaa..
 
Mungu amsaidie apate hitaji la moyo wake na mwanaume ataempenda na kutulia nae.
Yani anajituma jamani yule mwanamke anajituma anachakarika kweli kweli alikua anawapenda na kuwajali Ndugu wa mumewe wanaokuja kuwasalimia yani anawajali balaa sijui kwanini hapo tu ndio amekwama mambo ya wawili wanayajua wenyewe! Anyway tuseme God's time haijafika !

Kinachomuharibia ni kiherehere cha kutaka ndoa,mwanaume ukionyesha au kulazimisha ndoa lazima akimbie ..
 
Yaan wewe hukunielewa, mpenzi anapatikana popote tu lkn muda wa kuingia love connect huo ndio sina zingatia hili. Nilishadate mtu humu tena nilimpata hapa hapa Selfika lkn tulianza kwa namna nyingine kabisa kabla hatujafikia kudate. Sijasema hamna wanaume wa kudate humu wapo sana ila ni uchaguzi tu nje ama ndani.
Litakuwa

Li KENZY

Jamaa likorofi sana
 
Back
Top Bottom