




Usinichekeshe... kuna story moja ya kichekesho inakuhusu sana...
Kuna jamaa alikuwa anaumwa sana halafu ilikua ni village, sasa kufika night homa ikazidi ikabidi majirani wampeleke hospital huo usiku yapata saa 8, basi wakachukua kama kigunia flani wakatengeneza kama machela za kubebea wagonjwa, safari ikaanza pori kwa pori, njia kwa njia kuitafuta zahanati kuokoa roho ya mgonjwa mahututi.
Ebwanaeehh kufika mbele, si wakaona simba!!! Yupo pembezoni mwa njia halafu anawacheki tu, wale wabebaji wakaona ili kunusurika ni bora tumtoe huyu mgonjwa sadaka, simba ana njaa hatari anapiga mihayo tu



.
Wakaona wasipo mtoa sadaka, simba atawakamata mmoja wao, wakahesabu 1, 2, 3 fyuuuu!!! Wakamrushia mgonjwa kule simba aliko halafu wakatoka nduki hatari




...
Basi walikimbia vibaya sana, wakafika nyumbani wamechoka balaa, kuangalia mlangoni mgonjwa waliyemtupa ameketi mlangoni anakunywa na uji




amefika kitaaambo...



anawauliza mbona mmechelewa hivyo?

Kumbe jamaa kwa uoga wa kuliwa na simba aliporushiwa alimkwepa simba akapata nguvu, akakimbia akawapita wale wazima wote



Nahisi wewe ndio yule mgonjwa



..
Nb: not true story