Alifariki mmoja,, ila nimegundua gari ikipinduka juu chini chini juu ina uwezekano isiue watu wengi kuliko ikipinduka kiupandeupande..
Kuna siku nilienda kutembea milimani kule barabara ya chunya wakati narudi nakuta ajali ya basi ilikuwa imebeba wanajeshi wadogo wadogo ndiyo wametoka kupiga course tabora wanaenda mbeya kupewa ajira na hilo basi walikodiwa na jeshi ila ndiyo lilikuwa bovu hasa kwenye usukani
Ikafika sehemu likapinduka kiupandeupande,, kwa mara ya kwanza nilishuhudia live utumbo wa mtu unazolewa zilienda ambulance mbili na gari za jeshi ila maiti na majeruhi bado hawakuisha walikuwa wengi halafu ni vijana wadogo tu kwenye miaka 20 hivi
Walioumia sana na kufariki ni wale waliokuwa upande ambao lile basi lililalia baadaye ndiyo wakaja kulinyanyua,, ila ile barabara ya kuelekea chunya ni mbaya sana aise zile kona kona daah kama nyoka wenyewe huwa wanaziita kona za mkoa maana mkoa mzima hamna kona mbaya kama zile..