Selasini on BBC: Mabomu yalikuwa yame-expire!

huwezi kulinganisha dawa ku expire na mabomu ku expire ... hii ni aibu kubwa kwa msemaji wa jeshi ... mbona vyakula viki expire vinakuwa sumu ... hivyo kuna uwezekano mkubwa sana mabomu yaki expire yanakuwa hatari zaidi .... umekurupuka na post yako ..ukisikiliza BBC au taarifa yeyote tafakari kabla hujacharuka kupost
 
Nasikitika sana kama kuna baadhi ya wabunge kama Selasini wanathubutu kusema kwamba milipuko ya mabumu gongo la mboto imesababshwa na JWTZ kuhifadhi mabomu yaliyo expire ! Sifa kubwa ya Mbunge timamu ni kutosikiliza maneno ya mitaani na kuyatumia katika mijadala ya Kimataifa kama vile alivyofanya huyu mbunge leo hii alipokuwa anachangia mjadala wa BBC.

Mbunge anapaswa kujiuliza na ikibidi kufungua vitabu ili apate cha kusema vinginevyo akae kimya tu ! Ajali ya Moto, tetemeko la ardhi, Elinino, etc ni vitu ambavyo vikitokea huna uwezo wa kuvidhibiti sana sana unaweza kupunguza madhara tu lakini huwezi kusema kwamba utakuwa salama kwa asilimia 100.

Majanga ya mabomu yamekuwa yakitokea katika nchi mbali mbali duniani kama vile Russia, Nigeria, India, etc kwa zaidi ya mara moja.

Imefika wakati watanzania kuwa na akili timamu kwa kutafuta chanzo cha tatizo badala ya kutoa lawama zisizokuwa za msingi ili mradi tu uonekane umechangia hoja kumbe unaonekana mpuuzi tu kwa kutoa pumba badala ya mchele.
Mafyale!
Kabla hujaelezea kitu cha kitaalamu ambacho huna utaalamu nacho tafadhali sana fanya kwanza research. Bomu linaweza kulipuka kwa sababu ya ku-expire bila shaka yoyote... kutegemeana na limetengenezwa na chemical gani.
Kwa mfano, bomu lililotengenezwa na TNT. Hiyo TNT huwa ina-degrades kuendana na muda. Hii ni kwa sababu ya chemical inayoitwa nitro-glycerin inavyokuwa inaji-separates kutoka kwenye ule mchanganyiko. Matokeo yake panaweza kutokea mlipuko. Hapa tunaweza kusema huu mlipuko utakuwa umetokea kwa sababu ya 'bomu ku-expire'
 
Jeshi letu lazima likiri kwamba kulikuwa na uhifadhi mbaya wa silaha za hatari kwani wataalamu wanakiri kwamba mabomu hayo yangeweza kuhifadhiwa kwenye maghala ambayo yapo underground ambayo huzuia makombora kuruka nje ya kambi na hiyo technolojia ipo na ndiyo inayotumiwa na nchi zote duniani.
lakini cha kusikitisha msemaji wa jeshi kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari alidai eti serikali haina pesa za kutosha kujenga maghala ya aina hiyo, hili kweli ni janga kwenye janga la kitaifa.
 
MWANAFYALE...!
Nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuwaeleza watu kile wasichokitaka kiingie akilini mwao...! ukweli utabaki palepale...Sekasini kachemka katika maelezo yake.....watafute mbunge mwenye mlengo wa kupinga ambaye ana taaluma ya jeshi atoe maelezo...si kukurupuka
 
ukweli unabaki palepale bomu liwe lime expire au la kulihifadi kienyeji kama alivyosema yule jamaa wa Kenya milipuko inahifadhiwa sehemu ambayo hata ajali ikitokea haliwezi kutoka nje, hapa kwetu mabomu yameruka hadi 14.5km. Bado tunatetea uzembe huu? Jeshi lazima liwajibike kwa yaliyo tokea kwa UZEMBE
 
Nasikitika sana kama kuna baadhi ya wabunge kama Selasini wanathubutu kusema kwamba milipuko ya mabumu gongo la mboto imesababshwa na JWTZ kuhifadhi mabomu yaliyo expire ! Sifa kubwa ya Mbunge timamu ni kutosikiliza maneno ya mitaani na kuyatumia katika mijadala ya Kimataifa kama vile alivyofanya huyu mbunge leo hii alipokuwa anachangia mjadala wa BBC.

Mbunge anapaswa kujiuliza na ikibidi kufungua vitabu ili apate cha kusema vinginevyo akae kimya tu ! Ajali ya Moto, tetemeko la ardhi, Elinino, etc ni vitu ambavyo vikitokea huna uwezo wa kuvidhibiti sana sana unaweza kupunguza madhara tu lakini huwezi kusema kwamba utakuwa salama kwa asilimia 100.

Majanga ya mabomu yamekuwa yakitokea katika nchi mbali mbali duniani kama vile Russia, Nigeria, India, etc kwa zaidi ya mara moja.

Imefika wakati watanzania kuwa na akili timamu kwa kutafuta chanzo cha tatizo badala ya kutoa lawama zisizokuwa za msingi ili mradi tu uonekane umechangia hoja kumbe unaonekana mpuuzi tu kwa kutoa pumba badala ya mchele.

Mlinganisho ulio toa ni sawa ya kuongeza idadi ya wazembe.
Hivi mlevi kalewa wamembandua biggii, ikifikiwa nawe umelewa Na kubanduliwa.
Unaulizwa kulikoni!
Utasema mbona na fulani naye walimbandua wee vipi?
Mmbwa apigwe kwenye tukio
unaleta umakamba kwenye wajibu!
 
silaha za mahangamizi zina hifadhiwa kwenye ma-bunker. Hali ni mbaya katika makambi mengine, ni suala la lini yatalipuka. Mtoa mada hujui unaongea nini, tuulize tuliofanya miltary science enzi zile
 
Nasikitika sana kama kuna baadhi ya wabunge kama Selasini wanathubutu kusema kwamba milipuko ya mabumu gongo la mboto imesababshwa na JWTZ kuhifadhi mabomu yaliyo expire ! Sifa kubwa ya Mbunge timamu ni kutosikiliza maneno ya mitaani na kuyatumia katika mijadala ya Kimataifa kama vile alivyofanya huyu mbunge leo hii alipokuwa anachangia mjadala wa BBC.

Mbunge anapaswa kujiuliza na ikibidi kufungua vitabu ili apate cha kusema vinginevyo akae kimya tu ! Ajali ya Moto, tetemeko la ardhi, Elinino, etc ni vitu ambavyo vikitokea huna uwezo wa kuvidhibiti sana sana unaweza kupunguza madhara tu lakini huwezi kusema kwamba utakuwa salama kwa asilimia 100.

Majanga ya mabomu yamekuwa yakitokea katika nchi mbali mbali duniani kama vile Russia, Nigeria, India, etc kwa zaidi ya mara moja.

Imefika wakati watanzania kuwa na akili timamu kwa kutafuta chanzo cha tatizo badala ya kutoa lawama zisizokuwa za msingi ili mradi tu uonekane umechangia hoja kumbe unaonekana mpuuzi tu kwa kutoa pumba badala ya mchele.

Sitaki kuzungumzia uliyoandika hapo na wala sijui selasini amesemaje, bali ninataka kusahihisha title ya thread yako. Bomu lina sehemu tatu kubwa: casing, explosives , na detonation system ambayo imeungana na fuse. Katika sehemu hizo tatu, explosives ambayo ndiyo hulipuka na kusababisha madhara kutokana na pressure growth; hiyo haina expiration, na hivyo inaweza kulipuka wakati wowote hata kama ikikaa miaka mia na zaidi. Ndiyo maana mpaka leo unaweza kukutana na bomu la WW1 na likalipuka. Kinacho-expire ni ama detonation system au casing, kwa mfano bomu likikaa mahali likapata kutu kiasi cha kupunguza effective thickness ya casing, basi linaweza kulipuka lenyewe.

Detonation system nyingine za mabomu zimeshikiliwa kwa spring (spring loaded). Hivyo kama ilivyo kwa mechanical spring yoyote, baada ya kuwa loaded kwa muda mrefu, spring hizo huishiwa nguvu (creep failure) na huweza kushindwa kuishikilia detonator na hivyo kusababisha bomu kulipuka lenyewe. Watengezaji wanajua creep failure ya spring hizo na ndiyo wanayotumie kuonyesha expiration date ya bomu.

Kama wewe unayedai kuwa bomu likiexpire halilipuki ni mwanajeshi, basi kweli tuna hasara huko jeshini kwa sababu ulitakiwa uwe unajua vizuri sana kuhusu mechanism ya detonators za mabomu na kwa nini inashauriwa kuwa zinakaguliwa mara kwa mara. Mabomu mengi ya kisasa yanatunzwa bila kuwa na detonators, bali zinaweka wakati tu yanatakiwa kutumiwa. Hata hivyo sijui hayo mabomu yetu yalinunuliwa lini na wapi, kama ni yale aliyoacha Nyerere aliyokuwa amenunua wakati wa vita ya ukombozi basi ni wazi detonator springs zake zitakuwa zimeshachoka na inabidi yaharaibiwe ama sivyo yataendelea kutulipukia na kutuua kila kukicha.
 
Akina Hitler wa karne iliyopita walikuwa na bunkers za kuhifadhi silaha za maangamizi - sisi leo tunajiwekea mabomu hovyohovyo. Tunaendelea kwa kurudi nyuma!

Visingizio havifai. Jeshi limechemsha na hatua sahihi kwa ajili ya usalama wa baadaye zichukuliwe.
 
Msemaji wa jeshi letu kwenye ule mjadala alikuwa anaongea kama raia tu na si mtu mwenye utaalam. Kusema kuwa bomu liki-expire haliwezi kulipuka ni sawa na kusema bia iki-expire haiwezi kulewesha. Kwa mtu anayejua mambo haya unashangaa maneno hayo yanatoka kinywani mwa msemaji mkuu wa jeshi. Alikuwa anaongea political talk ambapo huwezi kumtofautisha na wanasiasa.

Msemaji wa jeshi, Pamoja na mama Tibaijuka (Mwanasiasa) walikuwa wanaongea kama vile wananchi walikuwa wanajua kuwa mle ndani kumehifadhiwa mabomu/makombora. Yaani kuhamishia lawama kwa wananchi ni uzushi mtupu, ni sawa na kukuta mtu kabakwa unaanza kumlaumu eti amebakwa sababu alivaa nguo fupi!! Haiingii akilini.

Mtaalam wa Kenya alihamishia lawama zote kwa jeshi kwani Jeshi ndo lilikuwa linajua kilichomo mle kambini na hatari yake. Wananchi wengi kukaa karibia na makambi ya jeshi ni faida kwani vibaka na majambazi wengi huogopa maeneo hayo. Kwa hiyo jeshi ndo lilitakiwa lijue ni nini cha kufanya baada ya wananchi wengi kuzunguka eneo hilo. Hata hivyo tunajua kuwa maeneo mengi ya jeshi hayaguswi, ukishaambiwa hapa ni eneo la jeshi hakuna raia anayesogelea. Ukiona raia wamejenga ujue eneo hilo halikuwa la jeshi na raia waliachiwa kujenga!

Kwa hiyo ni suala la jeshi kukubali jukumu badala ya kuanza kurusha mzigo. Halafu tayari kwenye mada hizi kwa sababu tayari Chadema ameshaongea basi kila aliyemo serikalini anaongea kutetea jeshi kama vile kuelekeza lawama kwa jeshi ni kukubaliana na Chadema. Nadhani hapa ndo kuna tatizo. Ni kweli Joseph Selasini alikuwa akiongea kwa passion sana na hili linaeleweka kwa sababu na yeye ni muathirika wa milipuko ile. Lakini jeshi ilitakiwa wajibu suala hili kitaalam kwani lilikuwa suala la kitaalam kuliko kisiasa.

Hata mama Tibaijuka jana kwenye ule mjadala wa BBC alipiga siasa zaidi kuliko kuongea kama professa mwenye heshima ya kiwango kile. Wananchi kujenga kuzunguka kambi ya jeshi haiwezi kuwa kosa lao! Wananchi hawana maarifa na kilichomo humo kambini. Hawajui kama hilo ni ghala la milipuko. Hawajui kuwa hiyo milipuko inatakiwa itunzwe vipi! Hawajui kuwa milipuko yetu haijatunzwa vizuri! Hawajui chochote kuhusu hatari iliyopo. Jeshi waseme walichukua hatua gani kuzuia watu kujenga kuzunguka makambi?

Na vipi makambi yaliyoko Kigamboni, Mabibo, Changanyikeni, Lugalo, n.k.? Jeshi linawajibika kwa hili, tusipoteze muda kutetea uozo!
 
wakubwa na wanazi wa simba na yanga...bomu liki-expire maana yake limeisha muda wake wa kufanya kazi ile inayotakiwa kufanya..."KULIPUKA"......na hivyo maana yake haliwezi kulipuka tena........! KILICHO-EXPIRE HAKIWEZI LIPUKA BANDUGU...!

Si kweli....liki expire linaweza kushindwa kufikia target lakini kulipuka litalipuka tu....mabomu yaliyo tarajiwa kutumika WW1 yamekuwa yakilipuliwa huko ulaya kila yanapopatikana...yakiwa yame expire vilevile...soma hapa Answers.com - Do bombs ever expire
 
wakubwa na wanazi wa simba na yanga...bomu liki-expire maana yake limeisha muda wake wa kufanya kazi ile inayotakiwa kufanya..."KULIPUKA"......na hivyo maana yake haliwezi kulipuka tena........! KILICHO-EXPIRE HAKIWEZI LIPUKA BANDUGU...!

Mimi nilidhani bomu kwa kawaida halitakiwi kulipuka lenyewe isipokuwa mpaka pale linapolipuliwa. Ukisikia mabomu yanalipuka yenyewe tu hata ndani ya maghala yalimohifadhiwa unapata picha gani?
 
Hii sababu ya kusema wananchi wamefuata jeshi ni sababu ya kijinga kuliko zote nlizowahi kusikia.....sasa ukihesabu kambi za jeshi zilizo Dar es salaam na jinsi zilivotapakaa , halafu tukasema wananchi wote wakae umbali wa km 11 kutoka hapo si ina maana watu wahame Dar?

Hii nchi inakera sana jamani, yaani tuna viongozi mabogus katika kila sekta...suluhisho tubadili tu mfumo mzima tuone badala ya kuendelea na huu upuuzi
 
Niliipenda analysis na uongeaji wa yule Mkenya....alisema ukweli....mabomu yakihifadhiwa vizuri yakilipuka kwa accident hayawezi kutoka nje ya makambi yalimo hifadhiwa...na akasisistiza kuwepo uzembe...Kanali wetu yeye ana ng'ang'ania suala la nidhamu...ati kuwa jeshi letu lina nidhamu...hivi hajui mtu naweza kuwa na nidhamu nzuri tu (au akajionyesha kuwa anayo) na bado akafanya uzembe hata hujuma...inabidi wambadili kama ndio msemaji....BTW Dr Mwinyi aliingia mitini
 
msemaji wa jeshi letu ni mbishi,anatetea hoja ambayo haina mantiki badala ya kukiri uzembe wa jeshi,ila nilifurahishwa na yule mtaalamu kutoka kenya kwani aliongea kitaaluma zaidi na kusema kwamba lazima kuna uzembe kutoka upande wa jeshi.
Kwani mtu akikiri kwamba wao ndio wazembe ndio angeonekana ni muungwana?wanasema jeshini hakuna siasa,je msemaji anapozungukazunguka na ubishi mwingi hiyo sio siasa? Kama kwenye milipuko iliyopita waliahidi kuwajibika ikiwa itajirudia,je inakuwaje wajiwajibike sasa?na hiyo sio siasa?
Lakini msemaji wa jeshi angekiri kuwa hawana utaalamu kuhifadhi hayo mabomu au wana utaalamu wa kuhifadhi ila wakati ule walipokuwa wanahifadhi hawakuzingatia utaalamu.
 
Nasikitika sana kama kuna baadhi ya wabunge kama Selasini wanathubutu kusema kwamba milipuko ya mabumu gongo la mboto imesababshwa na JWTZ kuhifadhi mabomu yaliyo expire ! Sifa kubwa ya Mbunge timamu ni kutosikiliza maneno ya mitaani na kuyatumia katika mijadala ya Kimataifa kama vile alivyofanya huyu mbunge leo hii alipokuwa anachangia mjadala wa BBC.

Mbunge anapaswa kujiuliza na ikibidi kufungua vitabu ili apate cha kusema vinginevyo akae kimya tu ! Ajali ya Moto, tetemeko la ardhi, Elinino, etc ni vitu ambavyo vikitokea huna uwezo wa kuvidhibiti sana sana unaweza kupunguza madhara tu lakini huwezi kusema kwamba utakuwa salama kwa asilimia 100.

Majanga ya mabomu yamekuwa yakitokea katika nchi mbali mbali duniani kama vile Russia, Nigeria, India, etc kwa zaidi ya mara moja.

Imefika wakati watanzania kuwa na akili timamu kwa kutafuta chanzo cha tatizo badala ya kutoa lawama zisizokuwa za msingi ili mradi tu uonekane umechangia hoja kumbe unaonekana mpuuzi tu kwa kutoa pumba badala ya mchele.

Haya ni mawazo mgando katika karne ya sayansi na technologia. Majanga na ajali vinazuilika au labda basi inawezekana kuweka tahadhali na mifumo ya kupunguza madhara. Ndiyo maana kuna vyombo vya ku detect mitikisiko ndani ya maji na vimbunga na tsunami ndani ya bahari ili ikitokea basi watu watahadhalishwe mapema waende sehemu salama. Ndiyo maana watu wanaoishi katika fault line za matetemeko wanashauriwa mapema namna ya kujenga nyumba zao kuepuka madhara ya tetemeko likitokea ghafla. Ndiyo maana watu wanafundishwa katika sehemu zenye uwezekano wa kutokea ajali na milipuko kutambua hazzards na kuweka mipango ya ku punguza au kuondoa kabisa madhara. Kuna hazzard audits zinafanywa, inspections. Kunapaswa katika sehemu kama hizi wawepo wataalamu wanaoshughulika na kutunza usalama na committees na ukaguzi wa mara kwa mara na ripoti zake. Kama mabomu yalikwisha expire sasa kwenye maghala yalikuwa yanfanya nini?
Mchangiaji mmoja amesema expiery sio tu kwamba hayatalipuka lakini ni kuwa yanaanza ku mis behave kama ilivyotokea. Use your analytical part of brain brother usije ukatuletea ya REDET!!!!
 
Hii sababu ya kusema wananchi wamefuata jeshi ni sababu ya kijinga kuliko zote nlizowahi kusikia.....sasa ukihesabu kambi za jeshi zilizo Dar es salaam na jinsi zilivotapakaa , halafu tukasema wananchi wote wakae umbali wa km 11 kutoka hapo si ina maana watu wahame Dar?

Hii nchi inakera sana jamani, yaani tuna viongozi mabogus katika kila sekta...suluhisho tubadili tu mfumo mzima tuone badala ya kuendelea na huu upuuzi

Wewe ndio bogus wa kutupwa. Unaelewa nini kuhusu jeshi wewe? Nyie mnapoliticize kila kitu. Yaani sasa mnaudhi mno. Nuyo Thelathini ana elimu gani ya kijeshi vile? Hivi unajua mpaka leo dunia inaumizwa na mabomu yaliyotumika world war II? Nani kakudanganya mabomu yana expire kwa kulipuka. Basi Angola kusingekuwa na haja ya kuunda timu maalum kulipua mabomu. Vipi Msumbiji nako ilikuwaje? Wacheni siasa katika mambo ya kijeshi. Mnajijengea picha mbaya tu. Mwenye busara atajua kwamba hata wanajeshi ni watanzania tena wazalendo kuliko wengi wenu hapa JF. Acheni kabisa siasa za vyama jeshini. Mnajijengea chuki tu ambazo hazikuwapo hapo kabla. Wanajeshi walijua kuwa yameexprire, then wakaendelea kufanya kazi humo? Si wange-vacate hiyo kambi? Au labda yalikuwa na tarehe ya ku-expire ya kulipuka? Mbona mnashabikia sana NEGATIVE news about the army? Ninauhakika hata kama mkiuluzwa ni mazuri gani jeshi limewahi kufanya hamuwezi kutaja hata moja. Wacheni matusi yenu kwani yanawaonyesha ujinga wenu tu.
 
Back
Top Bottom