Selasini on BBC: Mabomu yalikuwa yame-expire! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selasini on BBC: Mabomu yalikuwa yame-expire!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by superfisadi, Feb 23, 2011.

 1. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbunge wa Rombo kaamua kuweka hadharani chanzo mlipuko G'Mboto; anadai yalikuwa yame-expire...

  Ameongea kwa kofia mbili: 1 kama mkazi wa Gongo la Mboto na 2 kama Waziri kivuli wa ulinzi.

  Amesema kuna taarifa makombora yalikuwa yame-expire na jeshi lilishaomba fedha serikalini kwa ajili ya kuyaharibu lkn serikali imekaa kimya.

  Amepinga taarifa za jeshi kuwa wananchi wamewafuata akitoa ushahidi kuwa kulikuwa na stesheni ya treni na kanisa lililojengwa 1930's.

  Pia jeshi liliingia hapo 1975 wakijenga kambi kwa ajili ya ulinzi wa kiwanja cha ndege hivyo baadaye ndiyo wakabadili na kuifanya ghala la silaha
   
 2. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  tujuze zaidi mkuu... Anasemaje selasini??? Tupe detail... Thanx alot
   
 3. Miss X

  Miss X Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  tupe habari zaidi mkuu!!!
   
 5. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa..
   
 6. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  alikuwa akiongea kwa kofia mbili 1 mkazi wa g mboto 2 waziri wa ulinzi kivuli .
  Alisema kuwa kuna taarifa makombora yalikuwa yamexpire na jeshi lilishaomba fedha serikalini kwa ajili ya kuyaharibu lkn serikali imekaa kimya.
  Pia amepinga taarifa za jeshi kuwa wananchi wamewafuata akitoa ushahidi kuwa kulikuwa na stesheni ya treni na kanisa lililojengwa 1930's wkt halijatulia inayoonyesha kulikuwa na watu wanaoishi hapo ndiyo sababu vikawekwa .
  Pia jeshi liliingia hapo 1975 wakijenga kambi kwa ajili ya ulinzi wa kiwanja cha ndege hivyo baadaye ndiyo wakabadili na kuifanya ghala la silaha
   
 7. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pia kuna Mkenya amesema Wanajeshi wanahusika na lawama kwani kuna njia ya kuyazuiya yasitoke nje kwenda kwenye makazi ya watu.
   
 8. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  msemaji wa jeshi jina sijalisikia vizuri yeye anasisitiza kuwa wananchi wamewafuata na mabomu hayajaexpire vinginevyo yasingelipuka
   
 9. I

  Inkognito Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waache waendelee kuchakachua ukweli,pale yatakapolipuka na kuiangamiza ikulu ndipo watakapojua
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  wakubwa na wanazi wa simba na yanga...bomu liki-expire maana yake limeisha muda wake wa kufanya kazi ile inayotakiwa kufanya..."KULIPUKA"......na hivyo maana yake haliwezi kulipuka tena........! KILICHO-EXPIRE HAKIWEZI LIPUKA BANDUGU...!
   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yaani jeshi limefikia hatua ya kujitetea kwa kigezo cha nani alikuwepo mwanzoni hapo g.mboto?
  Basi tumekwisha..hatuna jeshi ila ni usanii kwenda mbele
   
 12. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
 13. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  alisema wakati makombora yanaendelea kulipika mwamunyange alikuwa eneo la tukio
   
 14. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Expire=go beyond use by date.
  Mkuu mabomu siyo nyama za shoprite au dawa baridi. Zina uwezo wa kupitiliza muda hata miaka mingi tu kulingana na yalivyohifadhiwa.
  Kikubwa kinachoharibu mabomu/risasi ni baridi na unyevu ambayo kwa joto la DSM hakuna.
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  this is a very serious event..lakini naona viongozi wote--wa jeshi na serikali--wanachukulia kimzaha tu!!
   
 16. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mhhhhh
  Bora sie wa simba na yanga
  eti bomu liki expire haliwezi kulipuka . We ulipitia mgambo gani?

  hahaha dah mkuu basi japo google upate majibu


  • Nini kinafanya bomu kuexpire
  • Content ya mabomu ni nini
  Kifupi kitu ki kiepxeire ndo kinakuw ana mdhara makubwa tena mbaya zaidi binadamu anakuwa hana njia ya kukcontrol tabia za ulipukaji wake
   
 17. m

  mwanafyale JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nasikitika sana kama kuna baadhi ya wabunge kama Selasini wanathubutu kusema kwamba milipuko ya mabumu gongo la mboto imesababshwa na JWTZ kuhifadhi mabomu yaliyo expire ! Sifa kubwa ya Mbunge timamu ni kutosikiliza maneno ya mitaani na kuyatumia katika mijadala ya Kimataifa kama vile alivyofanya huyu mbunge leo hii alipokuwa anachangia mjadala wa BBC.

  Mbunge anapaswa kujiuliza na ikibidi kufungua vitabu ili apate cha kusema vinginevyo akae kimya tu ! Ajali ya Moto, tetemeko la ardhi, Elinino, etc ni vitu ambavyo vikitokea huna uwezo wa kuvidhibiti sana sana unaweza kupunguza madhara tu lakini huwezi kusema kwamba utakuwa salama kwa asilimia 100.

  Majanga ya mabomu yamekuwa yakitokea katika nchi mbali mbali duniani kama vile Russia, Nigeria, India, etc kwa zaidi ya mara moja.

  Imefika wakati watanzania kuwa na akili timamu kwa kutafuta chanzo cha tatizo badala ya kutoa lawama zisizokuwa za msingi ili mradi tu uonekane umechangia hoja kumbe unaonekana mpuuzi tu kwa kutoa pumba badala ya mchele.
   
 18. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Acha kupiga siasa ndugu yangu,

  Maneno ya yule msemaji wa Jeshi kule BBC yalikuwa yanatia aibu. Alikuwa anaongea kama mswahili wa mtaani kabisa ndo akatumia kibwgizo hicho ulichotumia kwenye bandiko hili: eti mabomu kama yame-expire yasingelipuka. Sipendi kuingilia sana mambo ya utalaam wa Mabomu lakini ku-expire kwa mabomu si lazima kilicho expire iwe ni explossive. Kama kilicho-expire ni fuse za kuyalipua huoni kuwa bado yanaweza kulipuka ikiwa yatalipuliwa na kitu kingine external?

  Turudi kwenye mjadala wa BBC, Mtaalam kutoka Kenya alielezea vizuri sana kushangaa kwake kuwa;
  1. Jeshi hawakuweka buffer zone
  2. Ma explossive makubwa kama yale maghala yake yanatakiwa yawe na uwezo wa kuhimili milipuko na kuzuia kusambaaa kwa milipuko hiyo.

  Mtaalam amekiri kulikuwa na matatio ndani ya jeshi letu kwani kwa utalaam wake Mabomu hayatakiwi kuhifadhiwa kwenye ghala lisilokuwa imara kuweza kuhimili milipuko. Haya masuala msemaji wa Jeshi saa zote alikuwa akiyakwepa na kuingilia hoja laini laini za wananchi kuhamia pale na za mabomu ku-expire. Tena majibu yake yalikkuwa yanaelea sana.

  Imekuwa ikisemwa humu kuwa lazima kuna uzembe ulifanyika na ni vizuri Jeshi wakakiri tu kuwa kuna uzembe ulifanyika. Hifadhi ya explossives haiwezi kufanywa katika ghala sawa na lile la kuhifadhia mahindi. Kwa maana hiyo hata kama milipuko ikitokea ikiwa ghala limejengwa kwa kuzingatia aina ya milipuko inayotakiwa kuhifadhiwa humo basi madhara yasingekuwa kama yale tunayoshuhudia.

  Hii inazidi kulifunua jeshi kuwa, inawezekana matatizo haya ni ya muda mrefu na ni mapana kuliko tunavyofikiria. Ikiwa ghala la Mbagala halikuwa imara, la gongo la mboto halikuwa imara (pamoja na kuwa rais alisema ndo ghala kubwa kabisa nchi hii), hali inaonesha kuwa maghala yetu hayakujengwa kufuata viwango na aina ya mali inayohifadhiwa humo. Kuna uwezekano mkubwa hili ni tatizo la maghala yote kwani kama alipewa contractor tapeli katika mazingira yetu ya ten percent kwa kila kitu, maghala yote yalijengwa substandard na hayafai kuhifadhia milipuko.

  Sasa ikiwa hali iko hivyo, ni vizuri jeshi letu likatoka kwenye gamba lake. Liwaambie wananchi wote kuwa maghala yetu ya kuhifadhia milipuko si salama. Hii maana yake ni kuwa mji kama wa Dar es Salaam wote unatakiwa uwe evacuated, yes, hali ni tete. Walisema range yake inaweza kwenda hadi kilomita kumi, sasa ukiangalia makambi yote yaliyoko mjini Dar es Salaam, ukachora duara la kilomita kumi kuzunguka kambi, ni wazi Dar yote haiko salama. Ukichukulia kuwa kambi zote za jeshi ndani ya Dar most likely zinahifadhi milipuko ya aina moja au nyingine.

  Hatari ni kubwa zaidi kwani milipuko hiyo inaweza ikasababisha chain reaction kwa kulipua maeneo kama kurasini yenye kuhifadhi mamilioni ya lita za mafuta.

  Ni ama jeshi liingie gharama za mradi wa dharura kubomoa maghala hayo mabovu na kujenga mengine au lihakikishe milipuko yote inahamishwa umbali wa zaidi ya kilomita kumi kutoka nyumba ya mwisho ndani ya jiji hili.

  Hali hii haiashirii jeshi linalofanya kazi zake kitaalam, bali inaonesha kuzagaa kwa ubabaishaji kila mahali!
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  kwanza hayo maghala yenyewe vyuma vyake,mabati,mbao zilizojengea vilishaoza!ndugu acha kutetea upuuzi kulipuka mara 3 unasema ajali?zilipuke kambi ngapi ndipo useme ni uzembe?
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huyu mkuu hana hoja...Amemsikia Selasini anaongea, akakurupuka kuja kuweka lawama zake hapa.
  Mbona unakuwa wa kuhukumu upande mmoja zaidi kuliko kubalance situation, wakati unajua wazi kuwa yule mjeshi amechemsha kwenye engo nyingi sana...Anasema kuwa wakati jeshi linahamishiwa pale hakukuwa na watu, wakati yule mzee mwenyeji wa eneo hilo amesema jeshi liliwakuta wanaishi eneo hilo, tokea mwaka 1960!...
  Chunguza pande zote za habari kabla ya ku'amplify hisia zako!
   
Loading...