Usafiri wa ndege ni salama sana kuliko aina nyingine za usafiri,wengi wameongelea turbulence na wengi nimeona hapa bongo wanaogopa sana hivi vi turbulent vidogo vidogo.Kiufupi turbulent hazi crash ndege kiurahisi tena siku hizo, kutokana na technolojia.Kuna turbulent kubwa jamani,watu wanarushwa hadi top roof na kudondoka sakafuni na baadae ndege inatulia kama haikutokea,pia pilots wanajua aina ya turbulent watakayokutana nayo kwa radar maalumu ma kama wanahisi iyaleta usumbufu basi wataenda route ya juu zaidi kama hakuna equipment nyingine muda huo.Turbulent nyingine husababishwa na ndege kubwa mfano airbus A360 ikapita anga la juu na uelekeo huohuo kukawa na ndege ndogo ni lazima nyie wa ndege ndogo cha moto mkione,na kama captain hayupo makini basi ndege yake itashushwa chini kwa speed kubwa sana.
Suala la vifo kwenye ajali ya ndege,wachunguzi wengi wanasa ndege inapo crash watu wengi wananusurika ila vifo huanza kutokea ndege ikiwa tayari chini either kwa kukosa hewa,au ndege kuwaka moto baada ya kuanguka hii huitwa after impact casualties.Kukaa mbele kati nyuma kote ni sawa,afterall business class huwa mbele na kwa nini isiwe nyuma.Marubani wanajitahidi sana kuzia mdege isianguke uelekeo wa pua chini,na hata ndege ikaishiwa mafuta na engine kuzimika bado ndege inaweza kufanya gliding kati ya km 100 hadi 200 bila engine kizinguka wakati huo huo ikishuka low altitude ikitafuta uwanja wa karibu kutua au barabara ilionyooka na ikatua bila kuua watu japo watu wataumia kutokana na kutua kwa kwa ovyo.
Mafuta ya ndege hukaa kwenye mabawa yote ya kati na ya nyuma,hivyo kama ni mlipuko basi utaanzia kati kurudi nyuma.
Naomba niishie hapa leo.