Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Juzi nimefika sehemu inaitwa Mpiji magohe aisee kule sio dar ni mkoani.Hata watu wake wamekaa mkaoni mkoani eti kule ni dar nilichoka.
Ukizungumzia mkoani Kwa sie Wadar es salaam, tunamaanisha mwisho wa mipaka ya mkoa wa Pwani na mikoa mengine. Mpiji unapanda daladala nauli haifiki hata 1500/=
 
Wote tumeandika tuliyoandika...

Wanaotusoma wataelewa yupi yupo sahihi na yupi anaweka takwimu za vijiwe vya kahawa...

Jumapili/jumamosi njema popote ulipo...
Mzee acha ubishi yawezekana wewe unaongelea mipaka ya jiji kimamlaka mimi naongelea mkoa wa Dar es salaam dhidi ya mikoa mingine

kumbuka ndani ya mkoa kuna halimashauri za wilaya , manispaa na jiji nazo zina mipaka yake ya kijografia lakini vyote vipo ndani ya jiji au mkoa husika, ambapo hadhi ya jiji la Dar es salaam inabebwa na ilala tu , kama ambavyo mwanza hadhi ya jiji inabebwa na ilemela na nyamagana ,,usichanganye mambo hapo mzee.

Huwezi linganisha ukubwa wa mkoa wa dar es salaam ukasema eti Dar kubwa kuliko mwanza utaonekana wa ajabu mzee ndani ya serikali ya awamu ya sita mama samia.
 
Sijawahi kufika temeke,tandika,gongo lamboto
 
Wanaotusoma wataelewa yupi yupo sahihi na yupi anaweka takwimu za vijiwe vya kahawa...
Mimi ni mmoja wa wasomaji.

Nimeelewa kuwa wewe ni muongo.

Mshikaji ndio yuko sahihi.
 
eneo la jiji la dar es salaam ni ilala pekee

Mwendazake alituharibia hapa, mimi bado nalitambua Jiji la Dar likijumuisha wilaya zote, hata kama kiutawala mshatengenezewa hivyo (Ila pekee) na Mwendazake
 
Za jioni

Miaka 20 Dar sijawahi kufika maonesho ya Sabasaba.

Wapi haujawahi kufika au unapasikia kukaa kote Dar?

Mbopo napasikia.

Kina sehemu inaitwa king'ong'o kwa kweli hapa hapana sijawahi kufika.

Kijichi.

Kivule.

Hata huyo mgombea urais kuna sehemu hajafika sembuse wewe? Kawaida hauwezi kutembea zehemu zote nchini ,acha king'ong'o ushawahi fika King'oko?
 
Back
Top Bottom