Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,354
- 55,589
Sehemu ya kwanza
Aisee... nilibaki pale Njombe Stand kama kifaranga. Sina mbele wala nyuma. 🙆🏿♂️ Simu sina, na sielewi nifanye nini.
Nikaenda kwenye vibanda vya simu nikampigia jamaa mmoja wa Songea ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Baba. 😅 Kwa bahati nzuri, yule jamaa alikuwa ananikubali sana.
Nikamwambia:
Huyo jamaa alikuwa ameacha kazi serikalini, akaingia kwenye biashara ya madini na alikuwa amefungua biashara zake pale Songea mjini.
Hapo kwenye madini sasa... 😂
Nilikuwa na rafiki yangu wa damu ambaye mpaka leo bado ni mwanangu. Tumetoka U-Boys mpaka tumeshaanza kuingia kwenye U-Men pamoja. 😀
Baba yake alikuwa Afisa wa Serikali aliyekuwa ananunua madini.
Na sisi...
Tulikuwa tunamuibia madini tunaenda kumuuzia huyu Uncle niliyempigia simu. 😅
Jamaa akaniambia:
Lakini shida kubwa ilikuwa moja.
Kipindi kile hakukuwa na Mobile Banking.
Nisingeweza hata kumwambia nina shida anitumie hela.
Ikawa taarifa tu.
Nikampigia na mshikaji wangu huyo huyo tuliyekuwa tunaiba madini kwa baba yake. 😂
Akaniambia:
Lakini nayo ikabaki taarifa tu.
Nikaanza kusubiri magari ya kwenda Songea.
Cha ajabu...
Magari yote yalikuwa yananikataa🙆🏿♂️😔
Nikawa nahisi...
"Hivi huyu Mjomba kanitia gundu nini?" 🤣
Cha kushangaza zaidi...
Hela ya nauli nilikuwa nayo.
Nakumbuka kipindi kile nauli ya Njombe–Songea ilikuwa shilingi 4,000.
Lakini bado...
Magari yote yalikuwa yanakataa
Pale Njombe kulikuwa na jamaa ambaye alikuwa Shemeji yake rafiki yangu.
Tulisoma wote Sekondari.
Tuliishi jirani Songea.
Darasa moja shule ya Sekondari
Nikamuendea.
Nikamsimulia kila kitu.
Nikamsagia kunguni Uncle wangu. 😂
Kwa bahati nzuri tabia za Uncle zilikuwa zinajulikana.
Akanisupport yule niliyokuwa maelezea 😀
Akaniambia:
Ghafla akili za ujana zikaja.
Nikawaza...
"Labda niombe msaada kanisani. Nikipewa hela nilale Lodge, kesho nirudi Dar."🤣
Nikaenda Kanisa la Catholic.
Nikamkuta Paroko.
Nikamsimulia kila kitu.
Aisee...
Alinifukuza kama mwizi.😂
Akanambia:
Nikaanza kulia tena.
Nikiwa natembea kwenye barabara kuu ya Njombe–Songea, nikakutana na vijana wawili.
Walionekana wakubwa kunizidi.
Nikawaelezea matatizo yangu.
Wakanionea huruma sana.
😔
Wakanipa shilingi 4,000.
Hapo nikawa nina shilingi 29,000.
Lakini cha kushangaza...
Sikuwa hata na hamu ya kula.
### Mchungaji wa Kipaimara
Ghafla nikakumbuka jambo.
Mwaka 2000, mchungaji aliyetuongoza kwenye Kipaimara pale Songea alikuwa amehamishiwa Njombe.
Nikapata matumaini mapya.
Tatizo moja tu...
Kanisa la Lutheran lilikuwa mbali.
Karibu kilomita mbili au zaidi.
😑
Nikarudi tena kwenye kibanda cha simu.
Nikampigia mshikaji wangu Songea.
Nikamuambia:
Kwa bahati nzuri, mimi, yeye na mtoto wa mchungaji tulisoma pamoja Sekondari na tulipata pamoja mafunzo ya Kipaimara.
Akaniambia:
Nikakata simu.
Baada ya dakika zisizozidi tatu...
Yeye akanipigia.
Akanitajia namba.
Nikaanza tena kulipia simu ya kibanda. 😂
Nikampigia Mchungaji.
Nikajitambulisha vizuri.
Akawa amenikumbuka.
Kipindi cha 1998 mpaka 2000 kulikuwa na identity fulani kanisani iliyokuwa inamtambulisha Mshua wangu.
Nikachombeza pia.
Akanambia yuko mkoa mwingine kwa maandalizi ya Kidato cha Tano.
Nikajisikia vizuri.
Kisha nikamuuliza:
Akanikata stimu.
Nusu nianguke.
Miguu ikaishiwa nguvu.
Nilikuwa nimelipia karibu dakika nne za simu.
Na muda huo ilikuwa saa 12 kasoro jioni.
Nikarudi kwa yule jamaa aliyeniambia nisubiri malori.
Nikamsimulia kila kitu.
Nilivyofukuzwa na Paroko.
Nilivyompigia Mchungaji.
Nilivyokosa msaada.
Na jinsi ambavyo sikuwa na hela kabisa.😂
Akanambia:
Lakini akaongeza.
Nikaanza kutembea.
Mita kama 400 au 500.
Nikafika sehemu malori yalipokuwa yanapaki.
Ghafla...
Nikaona lori aina ya FUSO.
Lilikuwa limeandikwa jina la ukoo wa familia moja tajiri sana.😅
Baadhi ya watoto wa ile familia tulisoma pamoja.
Tulicheza pamoja utotoni.
Na hata familia yetu iliwahi kuishi kwenye nyumba zao.
Nililipuka kwa furaha.😁
Nikalisogelea.
Nikamuona Tingo.
Kumbe alikuwa mshikaji wangu.
Tulisoma pamoja.
Tulihitimu shule ya msingi pamoja😂
Akanikumbuka vizuri.
Mimi nilikuwa Class Monitor.
Na nilikuwa nampelekesha sana darasani.
Yeye alikuwa na uwezo duni mno. 😅
Safari ikawa imepata mwanga.
Uhakika wa kufika Songea ukawa asilimia mia moja.
Saa moja jioni safari ikaanza.
Njombe kulikuwa na baridi kali.🥶
Meno yanagongana tu.
Baada ya muda tukafika sehemu kwenye Bar.
Gari ikapaki.
Tukashuka.😄
Wakaagiza paja la mbuzi.
Lilikuwa limenona kweli.😋😋😋
Likachomwa vizuri.
Mimi nikanywa Grand Malt.
Wao wakawa wanakunywa bia.🍺
Tukavunja sana mifupa pale.
Kama mnavyojua...
Madereva wa malori (Kazi na mbususu). 😅
Wakapotea kama saa moja na zaidi.
Mimi nikawa nimelala.
Pale kulikuwa na sehemu ya kulala yenye godoro.
Walikuwa watatu.
Safari ikaendelea usiku.
Tukafika sehemu inaitwa Madaba.
Wakapaki.
Kulikuwa na ukumbi unapigwa disco.
Kesho yake ilikuwa Sikukuu ya Pasaka.
Wale watatu wakaenda kulewa.
Na kuzichakata mbususu.(Ukimwi na madereva wa malori aisee.)
Wakarudi usiku sana.
Wakajaribu kuwasha gari.
Likagoma.
Nikaamshwa usingizini.
Nikaanza kusaidia.
Sijui nini kilikuwa kimeharibika.
Baridi ilikuwa kali kama ya Njombe.
Mikono ilikufa ganzi.
Nilikuwa nashikilia vifaa tu.
Mwisho nikajichafua mafuta ya engine.😆
Mpaka alfajiri ndipo wakamaliza kutengeneza.
Safari ikaendelea.
Tukaingia Songea saa nne asubuhi.
Nikashukia njiani sehemu inaitwa Bombambili.
Hatua kama 30 tu...
Nilikuwa getini kwa mshikaji wangu wa damu.
Akanifungulia geti.
Nikakaribishwa ndani.😊
Nikaenda bafuni.
Nikaoga.
Nikabadilisha nguo.
Na kumbukeni...
Ilikuwa Sikukuu ya Pasaka.
Mama mwenye nyumba alikuwa ananipenda sana.
Alinichukulia kama mtoto wake wa kumzaa.
Wakati mwingine alikuwa anaonyesha upendo zaidi kwangu kuliko hata kwa mwanaye wa damu.
Nilikuwa kama mtoto wa ile familia tangu mwaka 1999 mpaka leo.
Mipango yote ya kufuatilia uhamisho wa mdogo wangu ikaishia hapo.
Sikuweza kwenda.
Kwa sababu tayari nilikuwa nimeshamtukana Mjomba.
Na hapo ndipo safari yangu ya misukosuko ikaisha.
Yote...
Yalianza kwa tamaa ya kutaka kumiliki Nokia 2600 ili niiuze kwa bei ya juu.🤣
Nikapoteza simu.😔
Nikapoteza shilingi 50,000.😭
Nikafukuzwa na polisi.😅
Nikafukuzwa na Paroko.
Nikateseka Njombe.
Lakini njiani nikakutana na watu ambao wema wao sitausahau mpaka leo.
Miaka ishirini imepita.
Nikikumbuka safari hii...
Nacheka. 😂
Lakini ndani yake kuna somo kubwa sana.
Tamaa ya faida ya haraka ilinigharimu, lakini wema wa watu niliokutana nao njiani uliniwezesha kufika salama nyumbani.
Mwisho.
Wakuu, leo nimekumbuka tukio la miaka 20 iliyopita. 😂 Nimeona si mbaya nikawasimulia ili tucheke kidogo, tufurahie simulizi, lakini pia tukumbuke kwamba maisha yanaweza kukugeukia kwa sekunde moja tu.
Mwaka 2006 nilikuwa nasafiri kwenda mkoani Iringa, kisha niende Njombe kwa ajili ya kufuatilia uhamisho wa mdogo wangu wa shule. Kipindi hicho nilikuwa below 20.
Nilifika Stendi ya Mabasi Ubungo mida ya saa 4 asubuhi. Nikakata tiketi, lakini bahati mbaya sikupata basi la moja kwa moja kwenda Iringa. Nikapata gari lililokuwa linaenda Kilombero, hivyo nikakata tiketi mpaka Mikumi. Gari...

- Manyanza
- kwanza safari
- Replies: 79
- Forum: JF Chit-Chats
Aisee... nilibaki pale Njombe Stand kama kifaranga. Sina mbele wala nyuma. 🙆🏿♂️ Simu sina, na sielewi nifanye nini.
Nikaenda kwenye vibanda vya simu nikampigia jamaa mmoja wa Songea ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Baba. 😅 Kwa bahati nzuri, yule jamaa alikuwa ananikubali sana.
Nikamwambia:
"Uncle, nipo Njombe. Ninapanga kuja Songea."
Huyo jamaa alikuwa ameacha kazi serikalini, akaingia kwenye biashara ya madini na alikuwa amefungua biashara zake pale Songea mjini.
Hapo kwenye madini sasa... 😂
Nilikuwa na rafiki yangu wa damu ambaye mpaka leo bado ni mwanangu. Tumetoka U-Boys mpaka tumeshaanza kuingia kwenye U-Men pamoja. 😀
Baba yake alikuwa Afisa wa Serikali aliyekuwa ananunua madini.
Na sisi...
Tulikuwa tunamuibia madini tunaenda kumuuzia huyu Uncle niliyempigia simu. 😅
Jamaa akaniambia:
"Sawa mdogo wangu, karibu."
Lakini shida kubwa ilikuwa moja.
Kipindi kile hakukuwa na Mobile Banking.
Nisingeweza hata kumwambia nina shida anitumie hela.
Ikawa taarifa tu.
Nikampigia na mshikaji wangu huyo huyo tuliyekuwa tunaiba madini kwa baba yake. 😂
Akaniambia:
"Poa poa, karibu sana."
Lakini nayo ikabaki taarifa tu.
Nikaanza kusubiri magari ya kwenda Songea.
Cha ajabu...
Magari yote yalikuwa yananikataa🙆🏿♂️😔
Nikawa nahisi...
"Hivi huyu Mjomba kanitia gundu nini?" 🤣
Cha kushangaza zaidi...
Hela ya nauli nilikuwa nayo.
Nakumbuka kipindi kile nauli ya Njombe–Songea ilikuwa shilingi 4,000.
Lakini bado...
Magari yote yalikuwa yanakataa
Pale Njombe kulikuwa na jamaa ambaye alikuwa Shemeji yake rafiki yangu.
Tulisoma wote Sekondari.
Tuliishi jirani Songea.
Darasa moja shule ya Sekondari
Nikamuendea.
Nikamsimulia kila kitu.
Nikamsagia kunguni Uncle wangu. 😂
Kwa bahati nzuri tabia za Uncle zilikuwa zinajulikana.
Akanisupport yule niliyokuwa maelezea 😀
Akaniambia:
"Dogo, tulia."
"Mida ya saa 12 jioni nenda pale bondeni karibu na Mto Luhuji."
"Malori hawana noma."
"Utapata usafiri."
Ghafla akili za ujana zikaja.
Nikawaza...
"Labda niombe msaada kanisani. Nikipewa hela nilale Lodge, kesho nirudi Dar."🤣
Nikaenda Kanisa la Catholic.
Nikamkuta Paroko.
Nikamsimulia kila kitu.
Aisee...
Alinifukuza kama mwizi.😂
Akanambia:
"Nyinyi ndiyo matapeli."
"Mnajifanya mmeibiwa kumbe ni wezi."
"Toka hapa mara moja."
Nikaanza kulia tena.
Nikiwa natembea kwenye barabara kuu ya Njombe–Songea, nikakutana na vijana wawili.
Walionekana wakubwa kunizidi.
Nikawaelezea matatizo yangu.
Wakanionea huruma sana.
😔
Wakanipa shilingi 4,000.
Hapo nikawa nina shilingi 29,000.
Lakini cha kushangaza...
Sikuwa hata na hamu ya kula.
### Mchungaji wa Kipaimara
Ghafla nikakumbuka jambo.
Mwaka 2000, mchungaji aliyetuongoza kwenye Kipaimara pale Songea alikuwa amehamishiwa Njombe.
Nikapata matumaini mapya.
Tatizo moja tu...
Kanisa la Lutheran lilikuwa mbali.
Karibu kilomita mbili au zaidi.
😑
Nikarudi tena kwenye kibanda cha simu.
Nikampigia mshikaji wangu Songea.
Nikamuambia:
"Mwanangu, nataka namba ya Mchungaji."
Kwa bahati nzuri, mimi, yeye na mtoto wa mchungaji tulisoma pamoja Sekondari na tulipata pamoja mafunzo ya Kipaimara.
Akaniambia:
"Labda Bi Mkubwa wangu atakuwa nayo."
Nikakata simu.
Baada ya dakika zisizozidi tatu...
Yeye akanipigia.
Akanitajia namba.
Nikaanza tena kulipia simu ya kibanda. 😂
Nikampigia Mchungaji.
Nikajitambulisha vizuri.
Akawa amenikumbuka.
Kipindi cha 1998 mpaka 2000 kulikuwa na identity fulani kanisani iliyokuwa inamtambulisha Mshua wangu.
Nikachombeza pia.
"Vipi kijana mwenzangu?"
"Tulimwacha Songea, sasa yuko wapi?"
Akanambia yuko mkoa mwingine kwa maandalizi ya Kidato cha Tano.
Nikajisikia vizuri.
Kisha nikamuuliza:
"Baba Mchungaji, upo Njombe hapo kanisani nije?"
Akanikata stimu.
"Nimekuja Dar es Salaam."😫
Nusu nianguke.
Miguu ikaishiwa nguvu.
Nilikuwa nimelipia karibu dakika nne za simu.
Na muda huo ilikuwa saa 12 kasoro jioni.
Nikarudi kwa yule jamaa aliyeniambia nisubiri malori.
Nikamsimulia kila kitu.
Nilivyofukuzwa na Paroko.
Nilivyompigia Mchungaji.
Nilivyokosa msaada.
Na jinsi ambavyo sikuwa na hela kabisa.😂
Akanambia:
"Mdogo wangu..."
"Jana nimelipia kibali."
"Leo mchana nimelipia mchezo."
"Hapa sina kitu kabisa."
Lakini akaongeza.
"Wahi pale chini."
"Omba ufike Songea kwanza."
"Akili ikatulie."
Nikaanza kutembea.
Mita kama 400 au 500.
Nikafika sehemu malori yalipokuwa yanapaki.
Ghafla...
Nikaona lori aina ya FUSO.
Lilikuwa limeandikwa jina la ukoo wa familia moja tajiri sana.😅
Baadhi ya watoto wa ile familia tulisoma pamoja.
Tulicheza pamoja utotoni.
Na hata familia yetu iliwahi kuishi kwenye nyumba zao.
Nililipuka kwa furaha.😁
Nikalisogelea.
Nikamuona Tingo.
Kumbe alikuwa mshikaji wangu.
Tulisoma pamoja.
Tulihitimu shule ya msingi pamoja😂
Akanikumbuka vizuri.
Mimi nilikuwa Class Monitor.
Na nilikuwa nampelekesha sana darasani.
Yeye alikuwa na uwezo duni mno. 😅
Safari ikawa imepata mwanga.
Uhakika wa kufika Songea ukawa asilimia mia moja.
Saa moja jioni safari ikaanza.
Njombe kulikuwa na baridi kali.🥶
Meno yanagongana tu.
Baada ya muda tukafika sehemu kwenye Bar.
Gari ikapaki.
Tukashuka.😄
Wakaagiza paja la mbuzi.
Lilikuwa limenona kweli.😋😋😋
Likachomwa vizuri.
Mimi nikanywa Grand Malt.
Wao wakawa wanakunywa bia.🍺
Tukavunja sana mifupa pale.
Kama mnavyojua...
Madereva wa malori (Kazi na mbususu). 😅
Wakapotea kama saa moja na zaidi.
Mimi nikawa nimelala.
Pale kulikuwa na sehemu ya kulala yenye godoro.
Walikuwa watatu.
- Dereva.
- Tingo.
- Na yule Classmate wangu ambaye lile lori lilikuwa la baba yake.