Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Sehemu gani Dar haujawahi kufika?

Mwalimu wangu wa udsm aliwahi kuniambia hawezi kufika Mbagala kwa sababu hakuna kitu cha kumpeleka huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
anapadharau Mbagala hali hiyo ni Mwalimu tu haijalishi wa level gani

angekuwa Mh. Katibu Mkuu wa Wizara si angesema hajawahi kufika Magufuli Stand kwa kuwa hana cha kumpeleka huko

huwezi kusikia kauli hizo kwa wanaojua kusaka pesa kama kina Vunja bei maana huko ndio kuna machimbo ya Utajiri
 
Bado dar ndio jiji dogo kuliko majiji yote tanzania kijiografia ila ni jiji lenye watu wengi na miundombinu mingi kulingana na eneo lake na hii ni kwa sababu tu Dar es salaam ni business centre kutokana na uwepo wa bandari.
Bandari ikitoka hamna dar si ndivyo
 
Hata uwe umezaliwa na kulelewa Dar kuna maeneo mpaka unakufa hautakuwa umeenda

Kwa mfano wakazi wa Dar tuliozaliwa na kukulia upande wa Kaskazini wa Dar kuna maeneo mengine ya upande wa Kusini mwa Dar hatujawahi kufika japo tunayasikia

Sehemu ukiwa hauna mishe nayo ni ngumu kufika.
 
Yataje yapi mzee
 
Ukizungumzia mkoani Kwa sie Wadar es salaam, tunamaanisha mwisho wa mipaka ya mkoa wa Pwani na mikoa mengine. Mpiji unapanda daladala nauli haifiki hata 1500/=
Ni kwa sababu unapanda gari la Mpiji ukifika pale Mbezi. Kungekuwa na route za kutoka mjini hadi Mpiji nauli ingekuwa zaidi ya buku
 
Back
Top Bottom