Uchaguzi 2020 Samora, Iringa: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Rais Magufuli

IMG_20200928_214840.jpg
IMG_20200928_202904.jpg

Yaani ccm kijani kibichi mmejaza kweli watu au vipi?
 
Kwa CCM idadi kubwa ya wahudhuriaji ni wanachama kinda kinda, watanzania walioguswa na utendajikazi wa Rais Magufuli na ni wapiga kura. Kwa Chadema ni wanaokuja kuwashangaa na Oktoba 28 wanaungana na wapenda maendeleo na wanaipigia kura CCM.
 
Mkataba wetu na mgombea upo kwenye ILANI, kupitia huo mkataba tunajua atatufanyia nini na kipi hatafanya, na kwa vigezo hivyo ndiyo maana tunamchagua. Kama atafanya kinyume na huo mkataba maana yake ni kuvunja mkataba.

“Nakumbuka 2015 yapo ambayo wala hayakuwa kwenye ilani ya Uchaguzi. Ilani haikuagiza kununua Ndege 11 tumenunua, haikuagiza kujenga Bwawa la Nyerere kwa Trilioni 6.5, tumefanya, haikueleza tujenge SGR kwa Trilioni 7.026, tumejenga”. Dkt. Magufuli.

Kwahiyo Magufuli anamaanisha kwamba hata hii ilani ya zaidi ya page 300 anayoinadi kwa sasa haina maana, hatoitekeleza ni porojo tu wala siyo muhimu kwake.

Nataka mwana CCM mwenye uwezo wa kujenga hoja atufafanulie hili. Je, tuendelee kumwamini kwa ahadi anazotupa kupitia ilani hii ya 2020 au tujue ni porojo tu za kuombea kura na kudanganya wananchi.
 
Huyo Dikteta Uchwara hawezi kufuata Sheria,Katiba wala makubaliano yoyote Yale,anafanya kinachompendeza yeye na genge lake la ufisadi.
 
Ukiona hivyo maana yake, Uwezo wa Magufuli kusimamia Kodi za Watanzania katika kutekereza Ilani anayokuwa imeandaliwa aitekeleze ni kubwa kuliko Ilani inayoandaliwa

Na hakuna dhambi, kama mtu umeambiwa kukimbia mbio za kuzunguka uwanja mara 24 ukamaliza na hukuchoka ukaona uendelee na Kwa Kasi Kwa kuwa nguvu unayo, kunatatizo gani mkuu
 
Una uhakika ahadi zote amezitekeleza?
 
Back
Top Bottom