Uchaguzi 2020 Samora, Iringa: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Rais Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Uwanja wa Samora umefurika na kutapika na hii haijawahi kutokea tangu uwanja huu umejengwa 1976.

Ni kampeni za kihistoria, karibu.

==========



Updates;

MIGORI, IRINGA

LUKUVI:
Tunaomba kawilaya, utawala ni mgumu sana. Wasiwe wanawafata wakurugenzi, wakuu wa wilaya kilomita 125. Namuombea kura mheshimiwa Magufuli, mtampa? Namuombea kura diwani, mtampa? Mzee Mungu akubariki sana, sisi tunajua unatupenda sana jimbo la Ismani, tunakukaribisha sana.

MAGUFULI: Nileteeni mheshimiwa Lukuvi ili tufanye nae kazi, angalau kama mnanipenda na mimi imebaki miaka yangu mitano, nimalize na Lukuvi. Amefanya kazi zake vizuri sana katika kipindi kilichopita na nimeshangaa kwanini hakupita bila kupingwa kwa sababu siku za nyuma alikuwa anapita bila kupingwa na mimi kule jimboni kwangu nimewahi kupita bila kupingwa. Mtamleta Lukuvi?

Amenisaidia sana katika kazi, amefanya kazi katika wizara ya Ardhi ambayo mimi mwenyewe nimewahi kuwa waziri wa Ardhi. Tukawezesha vijiji 920 katika nchi hii kuvirudisha katika matumizi ya wananchi badala ya kuwa hifadhi za taifa.

Ingawaje nafahamu, shujaa huwa hapendwi kwao. Hata mti wenye matunda ndio unapigwa mawe lakini umuhimu wa Lukuvi mimi nausema kwa wazi, nileteeni Lukuvi, nileteeni na diwani wa CCM. Matunda yake mtayaona, na mimi naomba kura.

SAMORA, IRINGA
POLEPOLE:
Leo hapa Iringa tumekuja na injini mbili za ziada kwa ajili tu ya kuweka mambo sawa. Tuna wana CCM waandamizi, makada waandamizi nitawatambulisha baadae. Sasa wameanza kuweweseka, mahala fulani wanasema, Kassim Majaliwa ni waziri mkuu, kwanini anazunguka?

Nikasema humu tayari, dozi imeingia maana kila anapoenda kuharibu, Rais anamtuma Majaliwa anasafisha. Ndugu Kassim majaliwa ni sehemu ya viongozi wa kitaifa wa chama cha mapinduzi na leo tunayo heshma, tunao wajumbe wengine wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa ambao wamepewa majukumu mahsusi ya kuzunguka kitaifa kupiga kazi njema ya kutafuta kura.

MAGUFULI: Iringa mwaka huu msiniangushe huwa mnaniumiza sana, Iringa mmechelewa, tunapata shida kupata connection, hakuna connection, ukikosa connection katika maendeleo ya Nchi mmepotea, Ubunge nileteeni Jesca muone yatakayotokea, mnanikatisha tamaa

Magufuli Iringa_2020.jpg


MAGUFULI: Nakumbuka 2015 yapo ambayo wala hayakuwa kwenye ilani ya Uchaguzi. Ilani haikuagiza kununua Ndege 11 tumenunua, haikuagiza kujenga Bwawa la Nyerere kwa Trilioni 6.5, tumefanya. Ilani haikueleza tujenge Reli ya Standard Gauge kwa Trilioni 7.026, tumejenga.

MAGUFULI: Ilani haikutueleza lazima tukarabati Treni kutoka Dar - Arusha iliyokuwa imesimama kwa miaka zaidi ya 26 ila tumefanya. Ilani ya haikusema tukarabati Meli zaidi ya 5 na kununua nyingine Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa ila tumefanya .

DKT. MAGUFULI: Tunataka kuibadilisha Iringa, naomba mtuamini. Naomba msituangushe kama ambavyo mmezoea kutuangusha. Mambo yaliyofanyika Iringa ni mengi. > Wakati Mimi nasoma tulikuwa tunaenda kusikiliza Mziki kwa Mbata, unatoka Makanyagio hadi pale
Magufuli Iringa.jpg
 
Bwashee huo uwanja aliujaza Nyerere mwaka 1995 na ndipo Mkapa aliposhindia. Hao wengine porojo tu. Konde boy ameshuka kwa kamba leo?
Nilikuwepo 1995 wakati Nyerere anamuombea kura Mkapa na kusema mbunge tuamue wenyewe kati ya Dr Kitina na mwalimu Kibasa.

Leo uwanja umejaa zaidi bwashee!
 
Back
Top Bottom