Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Sam Mahela tena... Hivi ITV management hamyaoni haya?

Buhohela sio mwanzilishi wa kipindi hicho ,halafu pia Zembwela sio wa kumfaninisha na Musa ,Zembelwa uswazi kaiweza kweli kweli
Mwanzilishi alikuwa Seleman Simenyu, ila kwa uswazi naona Musa alikuwa bora kuliko Zembwela
 
hiyo ni auto style yake ya kuhoji. unajua wanaokuwa wanajibiwa ni viewers, yeye kazi yake ni kusikiliza na kuingilia kati inapobidi.....na kuendelea na swali lingine. Bado nasisitiza muda ni mchache, mambo ni mengi lazima kupata summary ili viewers wakiguswa na eneo iwe kazi yao kufuatilia.
Huwezi kutafuniwa halafu umezeshwe!!. Bado naona makosa ni kidogo........Mahela kaona maoni bila shaka atayafanyia kazi.
tusimpinge kama hakuna chochote anachofanikisha ikiwa baadhi yetu hatuwezi hata kuthubutu.
Yaani uulize swali halafu usijue kitu gani kimejibiwa eti uko busy kuuliza maswali mengine? 1 Nachojua kuna baadhi ya Maswali utokana na ulichokijibu...... Mkuu hapa nakupinga kwa dhati kutoka ndani ya moyo wangu.....
 
Mgema ukimsifia. Kesho anatia maji. Ni kweli sam ana upuuzi huu tena mwingi sana na kama anaona uzi huu basi ajirekebishe na kama hauoni. Basi bila shaka wahusika au team ITV watamfikishia kiukweli anatuboa watazamaji asitake kuharibu sifa alizoanza kujijengea anapouliza maswali anatakiwa atoe muda wa muhusika kujibu sio kumuingilia mtukila saa kiukweli huwa sioni anachokifanyaga wakati mwingne aige nyayo za buhohera mwenzie alikuwa vizuri sana. Kazi kwenu ITV mumrekebishe huyo sam la sivyo mtapoteza watazsmaji wa kipindi chenu ikiwemo mimi
 
Huyu jamaa vipi jamani?! Nimefuatilia kipindi cha DK45 ITV na leo mgeni ni N/Waziri wa Muungano na Mazingira na mada ilikua ni Mazingira.

Huyu Sam Mahela, kama kawaida yake kuingilia mzungumzaji wakati anatiririka vizuri kwenye mada husika. Anageuka kuwa mzungumzaji Mkuu, anatoa maoni yake Mfano...."Mimi/sisi waandishi wa habari tumefanya tafiti na ni kweli/sio kweli kwamba Kuna uharibifu wa Mazingira"..... Sasa kama ulikua unajua ukweli/uongo wa jambo ya nini kumwalika mgeni studioni wakati ulikua na misimamo yako kwenye topic husika?

Mfano alipokua akiagana na N/W huyo, akawa anamsisitiza "Fanya kazi, umesikia, fanya kazii, umepewa kazi ufanye, sawa... maana hata mm hapa ITV napiga kazi"..... Hapa ni kiherehere tu cha huyu maana sio wajibu wake kumweleza hayo.

Nimekuwa nikifuatilia kipindi hiki lakini watu wengi wanakereka sana na huyu jamaa..... Atulie, atoe nafasi ya mgeni husika kusema na baada ya hapo maswali.

Mwanzilishi wa kipindi hiki na Buholela walikua wazuri sana sio kama huyu kijana.

Hebu mwacheni jamani watu hawafanani..................halafu watu ambao si waandishi sisitunamuona yupo sawa 2..............Mwachen apiganie ugali wa familia yake na kama unadhan wewe ni bora zaid kuliko yeye si ukaombe kazi kwenye kipindi? maana ki ukweli hata mimi nammisi sana Seleman Semunyu.....nje ya yeye waliofuata hawafanani nae lakini ndo life
 
Kwa kweli jana kile kipindi na naibu waziri kimeboa, naomba kirudiwe tena lakini mwendesha kipindi asiwe huyu jamaa
 
Kwanza elimu yake, maana mi simuelewi huyu kijana namuona Kama sifa zinamlevya. Hata kwenye kutangaza habari anakuwa amepinda
 
Kuna ile jamaa nyingine ya BBC inaitwa Salim Kikeke, na nyingine yake Zuhura Yunusi, hovyo kabisa. Wanamuuliza swali mgeni halafu hawataki ajibu...sasa sijui unamualika mtu studio wa nini ikiwa huna cha kuongea naye
 
ELIMU ya hapa na pale ni nzuri sana kwa kipindi tulicho nacho.
 
Ana mapozi kama anataka kupaa, kiti hakikaliki vizuri!!!!!!!!! huyu jamaa bana..
 
Yaani uulize swali halafu usijue kitu gani kimejibiwa eti uko busy kuuliza maswali mengine? 1 Nachojua kuna baadhi ya Maswali utokana na ulichokijibu...... Mkuu hapa nakupinga kwa dhati kutoka ndani ya moyo wangu.....
Umeona eeh...interview si ku shoot maswali tu eti kisa muda...
Mbona wenzetu wa ulimwengu wa mbele wanaweza...wao muda wanautoa wapi? unajua fika una 45 minutes...jipange...
Yani 45 minutes ni nyiiingi saana kwa mtu anayejua anachouliza...tatizo wanaoulizwa wanajua kuliko wanaouliza au wanaouliza wanaogopa kuuliza au wanajikomba kwa wanaowauliza...
Otherwise inabidi wafanye homework kabla ya kuomba kukutana na hawa watu aisee...unaweza ukauliza swali ukadharaulika kwa unayemuuliza au wasikilizaji...yale maswali ambayo majibu ni obvious.

Kuwa good interviewer inabidi pia uwe good listener.
Maana kuna maswali yanakuwa hayana kazi kwani yameshajibiwa wakati muulizwaji anafafanua maswali mengine...na kuna maswali mapya yanaibuka on the spot...sasa kama mtu unategemea desa ulilonalo kama msaafu lazima ubore
 
Buhohera baada ya kuambatana na JPM kwenye kampeni sasa yuko mawasiliano Ikulu ya JPM. Mimi niliishawahi kuandika hapa kwamba, Mahela hana uwezo wa kuendesha vipindi kama kile cha Dakika 45. Nina wasi wasi sana na kiwango chake cha elimu katika taaluma ya uandishi wa habari, itawasaidia ITV na yeye mwenyewe kama ataendelea kuripoti matukio yanayotokea huko mitaani. Na hata huko afunzwe zaidi namna bora ya kuripoti habari kwenye matukio yanayogusa hisia za watu wengi. Tuliona alivyokuwa akiripoti wakati wa uchaguzi mkuu, ambapo alikuwa aki-side na polisi wazi wazi kiasi cha kupotosha mtiririko mzima wa habari! Ni mtu ambaye huwa anaiathiri habari husika kwa kuingia katikati ya habari na kugeuka yeye mwenyewe kuwa chanzo cha habari badala ya kukiacha chanzo chenyewe kiiachie hiyo habari husika!
There you are! Umesema sahihi kabisa kuwa Mahela linapokuwa tukio nyeti lenye kuvuta hisia za watu yeye hujigeuza chanzo, Na hata kwenye uchaguzi alikuwa hawaoji waandamanaji, yeye muda wote yupo Na polisi, nakumbuka vizuri Tu, kulitokea vurumai pale njia panda ya UDSM Sam Mahela alikuwa akirupoti, ilikuwa Ni muda ya usiku wa saa 2, wakati polisi wakikimbizana Na wale waandamanaji, Sam Mahela alikuwa akiwaita polisi Na kuonesha waandamanaji walipojificha, huku akisema "hawa huku wengine" kiukweli nilishindwa kushangaa, haya aliyafanya hata kule temeke, nikasema kwa namna hiyo anahatarisha usalama wake kwa kuonesha kuwa anasapoti upande mmoja.
 
Hata huyu Mzee wa mada Moto channel 10, anajali muda zaidi kuliko mada yenyewe, hasa kwenye siku zinazopigwa, Ni bora ukazungumza Na watu watatu Tu wenye hoja kuliko lundo la watu unawakatishakatisha bila Wao kutoa point zao.

Hovyo Sana huyu Mzee, ukiangalia kipindi chake Ni lazima upate stress
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom