Salamu za wiki kwa ZITTO NA LEMA

Salamu za wiki kwa ZITTO NA LEMA

Albert ana wambia wenzie wajiulize kuwa ni watanzania wangapi wanatumia fb?

Anaendelea kuwauliza ni watanzania wangapi watajua ukweli na uongo wao?

Hapo albert kaonesha dharau kwa mitandao na pengine alitamani lema aitishe vyombo vya habari.

Albert anakubaliana na alicho fanya lema kakini alitamani atumie njia itakayo wezesha watanzania wote kujua tuhuma za lema dhidi ya naibu katibu mkuu.

Albert ni mnafiki kajificha kwenye maneno lakini anaumbuka kuwa ni mnafiki ana mlinda lema.

Albert bado anataka lema aendelee kubandika humu makala akiamini kuna mshindi ndio maana amesema lazima muongo na mkweli ajulukane, kifupi amependezwa na reaction ya lema.

Albert anatakiwa kufahamu katika haya malumbano hakutakuwa na mshindi bali ni kurudisha nyuma chama.

Albert acha unafiki ni heri unge kaa kimya.
 
Ukimya wa rafiki unaumiza kuliko kelele za adui...

Sishangai mtu kuniita mnafiki. Ni mawazo au fikra. Ila katika hili sina unafiki wowote. Simuogopi Lema na wala simtetei. Sina sababu ya kumuogopa.

Suala hapa ni Lema na Zitto kuangalia kile kilicho kwenye nafsi zao. Posho sio tatizo.

Kuhusu vikao sijadharau vikao. Ila kukimbilia kwenye kichaka cha vikao ni unafiki. Tabia ya kuficha mambo kisa eti itaathiri chama ni unafiki. Tutakuwa na tofauti gani na CCM? Chama kinaathirika vipi kama Zitto ni mla rushwa na mnafiki? Au kama Lema ni muongo na aliyejaa fitna?

Chama kitaimarika pale ambapo tutajua mla rushwa ni nani, muongo nani na mnafiki nani. Tuache woga wa kufikirika.

Kuhusu Mwigamba kuhukumiwa sijawahi kusema ni sawa au si sawa. Sikuwepo wakati yanatokea na sijaongea na mtu yeyote kuulizia. Sina double standards hata kidogo.

Mazungumzo yangu niliyamaliza kwa kusema wajipime kwa utendaji wao na baada ya hapo tutaona kama wapokee au wasipokee posho.

Sina allegiance kwa yeyote kati yao. Sijaongea na Lema wala Zitto kuhusu hili. Mawazo au maoni yangu yanabaki kwangu. Mapungufu au kutokukubalika kwake hakumaanishi sistahili kusema. Nastahili kupuuzwa na yule ambae anaona hayafai.

Mwisho, wahusika wanahaki ya kujibu au kutokujibu. Pia kupuuza.
 
Hafanyiwi fitina.. Anajifanyia fitina kwa kurubuni vijana wasaliti chama.

Huu ni unafiki... Mnajenga nchi na majangili? Mnajenga nchi na mafisadi... Mwakalinga acha unafiki... Kwenu nyie ni watu wenye misimamo inayo heshimika si unafiki huu.
Nashukuru kaka kwa kunikumbusha ,nafuta usemi na nasisitiza nchi haiwezi jengwa na ccm hii inayokumbatia uchafu wa kila aina.
 
Hivi ni kweli kwamba ili Kinyonga azae ni lazima yeye mwenyewe apasuke tumbo??
 
Ruttashobolwa, kaka kama umeangalia nilichosema na kama ungeniuliza ungegundua simtetei Lema hata kidogo.

Kuna hoja kwamba sio sahihi wao kutumia mitandao ya jamii na watumie vikao kwa sababu chama kinaumia. Nilichosema ni kwamba sioni tatizo. Acha watu wajue ukweli.

Sidharau mitandao, nilichomaanisha ni kwamba umasikini wa wananchi wengi unachangia uchache wao kwenye FB na kwingineko. Wajiulize kwa nini tuko wachache huku.

Kama tukijua ukweli na kuchukua hatua dhidi ya yeyote mwenye makosa Zitto au Lema basi tutaendelea na hatutarudi nyuma. Hakuna haja ya kuwa na watu kwenye chama kwa sababu ya woga wa kuathiri chama. Mbona tulifukuza madiwani na chama kikabaki imara??

Tatizo sio tofauti ya mawazo. Tatizo hakuna kuheshimiana na kujadiliana kistaarabu. Kuna chuki, jazba, mihemko, kiburi, dharau nk. Tukubali na tutatue.
 
Salaam Zitto na Lema...

Tatizo lenu sio posho. Si vyema kuwadanganya watu au kuwaaminisha kwamba tofauti iliyopo kati yenu ni mawazo au misimamo tofauti kuhusu Posho.

Kama ingekuwa hivyo basi isingekuwa tatizo. Kuwa na mawazo au misimamo tofauti sio tatizo hata siku moja.

Mtu hauhitaji rocket science kuona kwamba kuna zaidi nyuma ya pazia.

Ila kabla sijasema sana niweke mambo machache wazi.

1. Zitto na Lema ni marafiki zangu. Nawafahamu wote kiasi cha kuweza kusema kwamba najua uwezo wa kila mmoja wenu.

2. Sioni tatizo kutumia socia media kugombana au kukosoana. Najua wapo ambao wanasema vikao vitumike. Lakini vikao hivyo wengi wetu hatuhudhurii kwa sababu sio wajumbe. Yatokanayo na vikao hivyo hubaki siri na tunayoletewa ni muhtasari wa vikao. Hatupati nafasi ya kujua nani kasema nini na kwa nini na amesemaje.

3. Chama lazima kikue. Na kukua lazima mambo fulani fulani yatokee. Najua yanaweza yakapitiliza na kuathiri chama ila ni bora yatokee na kuathiri chama kuliko yaje yatokee na kuathiri NCHI. Kama tutavurugana na kugombana chama kikasambaratika basi ni kheri kuliko tuje kufarakana, kuvurugana na kugombana wakati tumepewa madaraka kuongoza watanzania.

Baada ya kuweka hayo mambo matatu wazi niseme kwamba suala la kupokea au kutopokea posho ni suala binafsi sana. Ni suala la NAFSI.

Kama nafsi yako inakutuma upokee posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma upokee rushwa, useme uongo, ukose maadili nk.

Kama nafsi yako inakutuma ukatae posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma usipokee rushwa, usiseme uongo, uwe na maadili nk.

Lakini, nafsi pia inaweza kukutuma kuchanganya mazuri na mabaya. Ukapokea posho ukakataa rushwa. Au ukakataa posho ukapokea rushwa. Ni nafsi yako.

Zitto na Lema mjipime kwa kile kilicho ndani ya nafsi zenu. Uzuri ni kwamba mwanadamu huwezi kuidanganya nafsi yako.

Ila kumbukeni yafuatayo;

1. Nyinyi ni vijana ambao mmepewa nafasi za kuongoza wananchi ambao wanawaamini.

2. Nchi yetu inahitaji viongozi ambao ni WAKWELI na WASIO NA TAMAA.

3. Lazima mtofautishe KUJULIKANA na KUWA MAARUFU. Nyie wote mnajulikana. Hamna umaarufu wowote. Sidhani kama mmekuwa viongozi ili muwe maarufu.

4. Mna nafasi kubwa sana kwa vijana kwa sababu ya kujulikana kwenu. Nchi hii itasonga mbele tu kama vijana wataamua kushiriki kikamilifu kwenye siasa. Lakini vijana hawatashiriki ipasavyo kama tutawavuruga na kuwachanganya.

5. Wananchi watapima uongozi wenu sio kwa idadi ya mabandiko FB, tweets au articles. Wananchi hawakuchagua bloggers au waandishi wa articles. Walichagua viongozi wa kuwawakilisha.

Jiulizeni ni watanzania wangapi wako FB na Jamii Forum? Kwa nini idadi yao ni hiyo!? Ukweli wenu au uongo wenu unawafikia?!

Nimesoma andiko la Lema. Limejaa hasira, jazba na kiasi fulani chuki. Nimesoma majibu ya Zitto. Yamejaa kujiamini, kupuuzia na kiasi fulani dharau. Nawajua jinsi mlivyo kwa hiyo sishangai na wala hainikeri.

Lakini mwisho wa siku najua itakavyokuwa. Ukweli utajulikana. Kuna mmoja atabaki mwingine atatwaliwa. Kuna mmoja historia yake itakuwa ni kufundishia mwingine itakuwa kwa ajili ya kukemea. Kwa mlipofikia sasa lazima tujue nani Muongo nani Mkweli.

Kwa sababu mmeamua kufulia nguo kisimani basi zianikeni tuone madoa na usafi wake. Hatutarajii mrudishe kwenye tenga mkaanikie nyumbani.

NB:

Kila mmoja wenu kwa nafasi yake awajulishe watanzania amefanya nini kama Mbunge na Kiongozi wa chama. Kwenye mambo haya;

1. Elimu

2. Afya

3. Ajira

4. Uwajibikaji.

Hayo tu manne. Sitegemei mtatuangusha katika hili. Mkishatoa taarifa zenu basi tutaamua kama mpokee au msipokee posho. Tutatoa msimamo wetu pia.

.
.
.
.
.
.
.
dah!sina la kuongeza mkuu,we noma.
nimekubali sana mkurugenzi
 
Lema aje na ukoo wake wote na vizazi vyote vyake ( kama rijali) hawezi kufikia rekodi ya zitto kwa mageuzi nchi hii, kuimarisha chama, kuikamata serikali na hoja nzito, kuheshimiwa na jamii nzima.......
 
Tatizo la CHADEMA rogue elements kibao, ukichanganya hilo na uongozi dhaifu ndo unapata huu upuuzi wa akina Lema na Zitto.
 
Ukimya wa rafiki unaumiza kuliko kelele za adui...

Sishangai mtu kuniita mnafiki. Ni mawazo au fikra. Ila katika hili sina unafiki wowote. Simuogopi Lema na wala simtetei. Sina sababu ya kumuogopa.

Suala hapa ni Lema na Zitto kuangalia kile kilicho kwenye nafsi zao. Posho sio tatizo.

Kuhusu vikao sijadharau vikao. Ila kukimbilia kwenye kichaka cha vikao ni unafiki. Tabia ya kuficha mambo kisa eti itaathiri chama ni unafiki. Tutakuwa na tofauti gani na CCM? Chama kinaathirika vipi kama Zitto ni mla rushwa na mnafiki? Au kama Lema ni muongo na aliyejaa fitna?

Chama kitaimarika pale ambapo tutajua mla rushwa ni nani, muongo nani na mnafiki nani. Tuache woga wa kufikirika.

Kuhusu Mwigamba kuhukumiwa sijawahi kusema ni sawa au si sawa. Sikuwepo wakati yanatokea na sijaongea na mtu yeyote kuulizia. Sina double standards hata kidogo.

Mazungumzo yangu niliyamaliza kwa kusema wajipime kwa utendaji wao na baada ya hapo tutaona kama wapokee au wasipokee posho.

Sina allegiance kwa yeyote kati yao. Sijaongea na Lema wala Zitto kuhusu hili. Mawazo au maoni yangu yanabaki kwangu. Mapungufu au kutokukubalika kwake hakumaanishi sistahili kusema. Nastahili kupuuzwa na yule ambae anaona hayafai.

Mwisho, wahusika wanahaki ya kujibu au kutokujibu. Pia kupuuza.

MsandoAlberto narudia tena wewe ni mnafiki na umejichanganya mwenye?

Msando kama una bariki njia aliyo itumia lema kwanini usibariki njia aliyo hitumia Mwigamba?

Kama mwigamba alikuwa right kwa nini ame adhibiwa?

Alberto wambie wanajamvi kuwa Mwigamba alifanya jambo sahihi kama wewe si mnafiki?

Alberto unajaribu kujitetea eti tukupuuze, never ever hapa jf kila mtu ana jadiliwa na hatuna hulka ya kupuuza mtu.

MsandoAlberto naomba ujibu bandiko langu pale juu pamoja na hili.
 
Last edited by a moderator:
Lema aje na ukoo wake wote na vizazi vyote vyake ( kama rijali) hawezi kufikia rekodi ya zitto kwa mageuzi nchi hii, kuimarisha chama, kuikamata serikali na hoja nzito, kuheshimiwa na jamii nzima.......
Kaolewe naye
 
Unamuuliza Ben mambo yanayomuhusu Zitto hiyo akili? Kesi ya mbuzi unaopeleka kwa fisi? Unategemea nini?

Wee hujuwi msimamo wa Ben juu ya Zitto? Hata mtoto aliyetumboni anajua Hilo tena lipo wazi kabisa!

Wee kweli hujuwi siasa pole sana!

Jifunze kujadili mada iliyopo mezani.Acha kuharibu mijadala na credibility ya JF.
 
Mnaosema Chadema ni chama cha wachaga msome Msando between the the lines!!
 
Kwenye hili Lema alipaswa kuambiwa kweli, kwamba yeye ni mtu mzima awe anatafakari kabla ya kulopoka hovyo, huwezi kumlipua Zitto, Mbowe au Dr Slaa bila kuiathiri Chadema. Lema amejisahau sana anaendesha siasa za kupumbaza vijana aonekane ana hoja za msingi wakati kiukweli anataka maslahi binafsi, Lema usidhani kila mtu ni kijana wako wengine tumeanza mbali nahiki chama ukikivuruga na tukajua source ni wewe utatafuta namna ya kutujibu
 
Ukimya wa rafiki unaumiza kuliko kelele za adui...

Sishangai mtu kuniita mnafiki. Ni mawazo au fikra. Ila katika hili sina unafiki wowote. Simuogopi Lema na wala simtetei. Sina sababu ya kumuogopa.

Suala hapa ni Lema na Zitto kuangalia kile kilicho kwenye nafsi zao. Posho sio tatizo.

Kuhusu vikao sijadharau vikao. Ila kukimbilia kwenye kichaka cha vikao ni unafiki. Tabia ya kuficha mambo kisa eti itaathiri chama ni unafiki. Tutakuwa na tofauti gani na CCM? Chama kinaathirika vipi kama Zitto ni mla rushwa na mnafiki? Au kama Lema ni muongo na aliyejaa fitna?

Chama kitaimarika pale ambapo tutajua mla rushwa ni nani, muongo nani na mnafiki nani. Tuache woga wa kufikirika.

Kuhusu Mwigamba kuhukumiwa sijawahi kusema ni sawa au si sawa. Sikuwepo wakati yanatokea na sijaongea na mtu yeyote kuulizia. Sina double standards hata kidogo.

Mazungumzo yangu niliyamaliza kwa kusema wajipime kwa utendaji wao na baada ya hapo tutaona kama wapokee au wasipokee posho.

Sina allegiance kwa yeyote kati yao. Sijaongea na Lema wala Zitto kuhusu hili. Mawazo au maoni yangu yanabaki kwangu. Mapungufu au kutokukubalika kwake hakumaanishi sistahili kusema. Nastahili kupuuzwa na yule ambae anaona hayafai.

Mwisho, wahusika wanahaki ya kujibu au kutokujibu. Pia kupuuza.

Mkuu Albert ujumbe wako umefika ila kwa vile watanzania wengi tunapenda unafiki na uzandiki watu wanataka kulitumia andiko lako kiuchonganishi ili wajue uko upande upi wa shilingi.

Kwa mwelevu atashangaa na kukaa kimya ila kwa mwendawazima atakulaani na kukulaumu kwa hiki ulichokuandika
 
Ruttashobolwa, kaka kama umeangalia nilichosema na kama ungeniuliza ungegundua simtetei Lema hata kidogo.

Kuna hoja kwamba sio sahihi wao kutumia mitandao ya jamii na watumie vikao kwa sababu chama kinaumia. Nilichosema ni kwamba sioni tatizo. Acha watu wajue ukweli.

Sidharau mitandao, nilichomaanisha ni kwamba umasikini wa wananchi wengi unachangia uchache wao kwenye FB na kwingineko. Wajiulize kwa nini tuko wachache huku.

Kama tukijua ukweli na kuchukua hatua dhidi ya yeyote mwenye makosa Zitto au Lema basi tutaendelea na hatutarudi nyuma. Hakuna haja ya kuwa na watu kwenye chama kwa sababu ya woga wa kuathiri chama. Mbona tulifukuza madiwani na chama kikabaki imara??

Tatizo sio tofauti ya mawazo. Tatizo hakuna kuheshimiana na kujadiliana kistaarabu. Kuna chuki, jazba, mihemko, kiburi, dharau nk. Tukubali na tutatue.

ASANTE KWA KUWEKA WAZI KUWA LEMA KAPOTOKA JAPO MWANZO ULIJICHANGANYA.

KAMA HUWEZI ZUNGUMZIA SWALA LA MWIGAMBA UNAZUNGUMZIAJE SWALA LA LEMA?

KWANINI USISEME WAZI MWIGAMBA ALIKOSEA AU ALIONEWA?UONI UNAJICHANGANYA TENA?

INA MAANA UNAJARIBU KUSEMA UJUI KANUNI ZA CHAMA?HEBU TWAMBIE KANUNI ZINA SEMAJE KWENYE HILI SWALA?

KAMA NJIA ILIYOTUMIWA NA LEMA SI SAHIHI KWA NINI UNAKOSA MSIMAMO KWENYE SWALA LA MWIGAMBA?

UNAJUA HAPA UWEZI KUWA HAKIMU MZURI MAANA UJUI LIPI NI KOSA NA LIPI SI KOSA.

MsandoAlberto unajichanganya jaribu kupitia bandiko lako na maswali yangu uone ulivyo kosa msimamo thabiti.
 
Last edited by a moderator:
ben haya mambo ya kujibishana kwenye social media kwa viongozi wetu ni sawa? naomba mtazamo wako mkuu@ben saanane
Hawezi kukujibu. jana nilimuuliza swali kama hilo hakujibu, akasepa kimya kimya. nikamuuliza tena Yericko swali kama hilo nalo hakujibu zaidi ya kutumia muda mwingi kumtetea Lema.
 
nchi haijengwi kwa mabisho kama hyo nliskitika nlipoona ujumbe wa mabisho kati ya ndugu Lema na Ndugu Zitto je watanzania wanajifunza nn kutoka na hyo mabisho yenu?
 
Ili kuwa fair, hapo kwenye mambo tunayotaka watueleze wananchi tuongeze
5. Kuongoza maandamano
 
Back
Top Bottom