Salamu za wiki kwa ZITTO NA LEMA

Hakuna kipya alichokiongea ambacho hakijasemwa na watu wengine hapa JF na kwenye social media zingine. He just reward a tape and play again.

Anadai tatizo siyo posho bali kuna kitu kiko nyuma yake. Sasa kama kuna kitu kiko nyuma yake kwa nini asikiseme hapa jukwaa kwa sababu yeye mwenyewe amedai haoni taabu kugombana nao na pia haoni taabu kurumbana kwenye mitandao na huu ndiyo uwanja wake wa kujidai kwa sababu haingii kwenye vikao vya juu vya chama.

Maelezo yake yamejikita kwenye posho wakati anadai posho ni non-issue.

Viongozi wa CHADEMA wanataka kutoana macho kwa ajiri ya "sitting allowance", pesa inayotoka kwa wananchi walalahoi ambao wabunge hao hao wanaodai kuwapigania ili zifutwe kodi zisizokuwa na tija wakati hizo ndizo zinaongeza posho zao wanazotaka kutoana macho!. Gosh.

It's too good to be true but is true.

Yetu macho na masikio.
 
Unamuuliza Ben mambo yanayomuhusu Zitto hiyo akili? Kesi ya mbuzi unaopeleka kwa fisi? Unategemea nini?

Wee hujuwi msimamo wa Ben juu ya Zitto? Hata mtoto aliyetumboni anajua Hilo tena lipo wazi kabisa!

Wee kweli hujuwi siasa pole sana!

Nilisikia Ben kapata mwandani ambaye anamjua kuliko mtu mwingine yeyote. Hongera mama kwa kujitokeza hadharani.
 
Kama ni umaarufu tu,hata shetani alikuwa nao mbinguni kabla ya kuasi na kutupwa chini.Nawaomba viongozi wa Chadema,tupa chini waasi na wote wanaokiharibu chama hata kama wana umaarufu na walishiriki kuimarisha chama kwani hata shetani alikuwa karibu sana na Mungu lakini alipoanza uasi alitupwa chini yeye na wafuasi wake

you haven't overstepped the mark......

Highly remarked!!!!
 
ther is strong point toka kwa mwanasheria, well explained keep it up mzee!!!!

Nimesoma majibu ya Zitto kwa Lema, lakini niseme tu kwamba Zitto Kabwe anafanya kosa kubwa kwa kuendesha siasa zake ndani ya CHADEMA akidhani kuwa yuko Ulaya na Marekani ambako ukomavu wa siasa katika vyama na uelewa wa wanachama na wananchi kwa ujumla ni wa kiwango cha juu sana. Amekosa utambuzi wa kuelewa level ya utambuzi wa watu wake, hivyo kutaka kuwajaza demokrasia za Kimarekani na Ulaya ni sawa na yeye kukimbia km 50 kwa saa wakati anaowaongoza wanakimbia km 5 kwa saa,(Hata CCM hawakuwa wanafanya hivyo siku za nyuma, walijitahidi sana kwenda mwendo wa wajumbe wa mashina enzi ya Mwalimu). Mwisho wake Zitto anajikuta anakimbia peke yake na wenzake wachache na kuliacha kundi kubwa nyuma, ndio maana anaitwa msaliti. Ushauri wangu kwake kama anaweze ashike breki aamgalia nyuma wenzake kawaacha wapi, vinginevyo anaweza kupitiliza hata katika mstari wa kumaliza mbio na kujikuta hana hata mtu wa kumsghangilia
 
Hakuna kipya alichokiongea ambacho hakijasemwa na watu wengine hapa JF na kwenye social media zingine. He just reward a tape and play again.

Anadai tatizo siyo posho bali kuna kitu kiko nyuma yake. Sasa kama kuna kitu kiko nyuma yake kwa nini asikiseme hapa jukwaa kwa sababu yeye mwenyewe amedai haoni taabu kugombana nao na pia haoni taabu kurumbana kwenye mitandao.

Maelezo yake yamejikita kwenye posho wakati anadai posho ni non-issue.

Viongozi wa CHADEMA wanataka kutoana macho kwa ajiri ya "sitting allowance", pesa inayotoka kwa wananchi walalahoi ambao wabunge hao hao wanaodai kuwapigania ili zifutwe kodi zisizokuwa na tija wakati hizo ndizo zinaongeza posho zao wanazotaka kutoana macho!. Gosh.

It's too good to be true but is true.

Yetu macho na masikio.

ya tege mkuu,utasikia mengi ila hutaona unachokikusudia
 
Albert anatakiwa kujua kuwa waswahili wana misemo mingi. Maana hata wakati akina Nelson Mandela, Solomon Mahalangw, Steve Biko, Ernesto Che Guevara, Ken Saro Wiwa, Martin Luther na wengineo wakati wanapigania haki na ukombozi wa jamii yao, Watawala walisema wanatafuta UMAARUFU.

Sasa kama Lema anapigania haki, usawa na ukweli kwa kuwaanika wazi wanafiki na wasaliti ndani ya chama basi wacha waseme Lema anatafuta UMAARUFU.

Huwezi kufikiria kuchukua mamlaka ya nchi wakati ndani kwako kuna wanafiki na wasaliti ndani ya nyumba yako hujawasafisha. Labda tukubaliane njia inayofaa kuwashughulikia wanafiki, wasaliti na wabinafsi.

Kama kukaa kimya huku unawaza kuchukua nchi eti wengine wakuite Mzalendo kinafiki wacha Lema aitwe mkorofi, na ni heri akose ubunge kwa kutetea haki, usawa na ukweli ndani ya chama na nje ya chama kuliko kuwa mnafiki
 
Hii maneno imetufumbua macho, sasa tumeanza kujua kinacho endelea ndani ya chama!
 
nachojua mpk sasa uongozi wa juu ushafanya kazi yake ndiyo maana kwa sasa wameanza kujitokeza washauri wa karibu kama akina albert

Hicho ndiyo tunachotaka kukijua haswa,otherwise we will still hold them as a suspects.
 
Tuishazoea mambo hayo ni katika tabia na mambo kama hayo katika bijisiasa vyetu,
Ni katika yale ambayo sisi tunayaita yakupita tu, hakuna kipya, ngoja tutafute maji ya kuzima hizo kelele.
 
Acha watu wajadili wewe, mmekalili kila jambo la siasa lazima likajadiriwe kwenye vikao vya chama? kuna siasa gani katika hilio? Wakajidiri kwenye vikao vya chama, hizo posho wanalipwa na CHADEMA?

Mkuu nilitaka kujua maoni ya ben na wala hakuna katazo ndani ya andiko langu thus why tunajadili hapa mimi na ww mambo ya cdm
 
Dawa ya jeuri ni kiburi,aliwawahi kusema sugu.

Na jeuri ataendelea kumtandika mwenye kiburi hadi mwenye kiburi atakapoamua ama kuwa neutral,ama kutii,and if he's luck,aamue kuwa jeuri,when its far too late.
 
Nimesoma majibu ya Zitto kwa Lema, lakini niseme tu kwamba Zitto Kabwe anafanya kosa kubwa kwa kuendesha siasa zake ndani ya CHADEMA akidhani kuwa yuko Ulaya na Marekani ambako ukomavu wa siasa katika vyama na uelewa wa wanachama na wananchi kwa ujumla ni wa kiwango cha juu sana. Amekosa utambuzi wa kuelewa level ya utambuzi wa watu wake, hivyo kutaka kuwajaza demokrasia za Kimarekani na Ulaya ni sawa na yeye kukimbia km 50 kwa saa wakati anaowaongoza wanakimbia km 5 kwa saa,(Hata CCM hawakuwa wanafanya hivyo siku za nyuma, walijitahidi sana kwenda mwendo wa wajumbe wa mashina enzi ya Mwalimu). Mwisho wake Zitto anajikuta anakimbia peke yake na wenzake wachache na kuliacha kundi kubwa nyuma, ndio maana anaitwa msaliti. Ushauri wangu kwake kama anaweze ashike breki aamgalia nyuma wenzake kawaacha wapi, vinginevyo anaweza kupitiliza hata katika mstari wa kumaliza mbio na kujikuta hana hata mtu wa kumsghangilia

Wabeja sana nkoi.Unajua zitto anapungukiwa kitu kidogo sana kama akikifanyia kazi bado credibility inaweza rejea.Yeye anamuona mbowe na slaa kama wanapoteza muda kukaa majukwaaani wakati yeye anahangaika na kamati zake.Lakini ajue kwamba kule vijijini kabisa ndani, ukiongelea cdm kwa sasa wanakutajia mbowe na slaa.Kwa nini ni kwa sababu wale wanakuwa karibu na wanavijiji kwa kuwatembelea na kufanya mikutano.
Hii mbinu ndiyo iliyokijenga chama cha TANU na baadae CCM na diyo maana ccm bado inanguvu vjijini kwa sababu watu walitembelewa enzi hizo na bado wanakumbuka.

Uwekezaji alioufanya mbowe na slaa vijijini kwa muda mfupi utachukua karne kufutika na ndiyo maana ccm wamegundua kuwa siri yao imefichuka na sasa mzee kinana ameanza siasa kama za kina mbowe na slaa ni baada ya kugundua kuwa ccm walikuwa wameacha wameendelea kula faida ya GOODWILL huku wakisahau kuongeza uwekezaji.

Kwako zitto; siasa unazofanya za kujijenga mijini hazitakusaidia, uwekezaji wa maana uko vijijini, vinginevyo hata dogo mnyika atakuzidi soon kwani ameanza kuzunguka.chukua hatua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom