Salamu za wiki kwa ZITTO NA LEMA

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,440
Moja ya mambo yaliyonisukuma nianike jambo hili ni mwanzo wa story hii ya miamba hawa wawili . Story ilianzia FB kwa mkuu Zitto kuweweka bandiko hili:
Zitto juu ya Posho;

"Enyi Watanzania, wabunge wenu wanataka posho ziongezwe na mishahara. Mbunge mmoja wa upinzani kanisemea mbovu huko Dodoma kwenye kikao cha wabunge eti mimi ni kikwazo kwa wao kuongezewa posho. Kasema nikiwa Arusha nakaa chumba cha dola 600 kwa siku. Hivi Hoteli gani Arusha ina chumba dola 600 kwa siku? Albert Msando naomba msaada nikija Arusha unionyeshe hiyo hotel japo nione chumba cha dola 600 kinafafanaje...."
Kama ulivyoona hapo juu alitajwa ndugu yetu Albert Msando, sasa leo kamanda Albert Msando amevunja ukimya na kuweka haya kwenywe wall yake ya FB kama Salamu kwa Godbless J Lema na Zitto.

by Msando Alberto
Salaam Zitto na Lema...

Tatizo lenu sio posho. Si vyema kuwadanganya watu au kuwaaminisha kwamba tofauti iliyopo kati yenu ni mawazo au misimamo tofauti kuhusu Posho.

Kama ingekuwa hivyo basi isingekuwa tatizo. Kuwa na mawazo au misimamo tofauti sio tatizo hata siku moja.

Mtu hauhitaji rocket science kuona kwamba kuna zaidi nyuma ya pazia.

Ila kabla sijasema sana niweke mambo machache wazi.

1. Zitto na Lema ni marafiki zangu. Nawafahamu wote kiasi cha kuweza kusema kwamba najua uwezo wa kila mmoja wenu.

2. Sioni tatizo kutumia socia media kugombana au kukosoana. Najua wapo ambao wanasema vikao vitumike. Lakini vikao hivyo wengi wetu hatuhudhurii kwa sababu sio wajumbe. Yatokanayo na vikao hivyo hubaki siri na tunayoletewa ni muhtasari wa vikao. Hatupati nafasi ya kujua nani kasema nini na kwa nini na amesemaje.

3. Chama lazima kikue. Na kukua lazima mambo fulani fulani yatokee. Najua yanaweza yakapitiliza na kuathiri chama ila ni bora yatokee na kuathiri chama kuliko yaje yatokee na kuathiri NCHI. Kama tutavurugana na kugombana chama kikasambaratika basi ni kheri kuliko tuje kufarakana, kuvurugana na kugombana wakati tumepewa madaraka kuongoza watanzania.

Baada ya kuweka hayo mambo matatu wazi niseme kwamba suala la kupokea au kutopokea posho ni suala binafsi sana. Ni suala la NAFSI.

Kama nafsi yako inakutuma upokee posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma upokee rushwa, useme uongo, ukose maadili nk.

Kama nafsi yako inakutuma ukatae posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma usipokee rushwa, usiseme uongo, uwe na maadili nk.

Lakini, nafsi pia inaweza kukutuma kuchanganya mazuri na mabaya. Ukapokea posho ukakataa rushwa. Au ukakataa posho ukapokea rushwa. Ni nafsi yako.

Zitto na Lema mjipime kwa kile kilicho ndani ya nafsi zenu. Uzuri ni kwamba mwanadamu huwezi kuidanganya nafsi yako.

Ila kumbukeni yafuatayo;

1. Nyinyi ni vijana ambao mmepewa nafasi za kuongoza wananchi ambao wanawaamini.

2. Nchi yetu inahitaji viongozi ambao ni WAKWELI na WASIO NA TAMAA.

3. Lazima mtofautishe KUJULIKANA na KUWA MAARUFU. Nyie wote mnajulikana. Hamna umaarufu wowote. Sidhani kama mmekuwa viongozi ili muwe maarufu.

4. Mna nafasi kubwa sana kwa vijana kwa sababu ya kujulikana kwenu. Nchi hii itasonga mbele tu kama vijana wataamua kushiriki kikamilifu kwenye siasa. Lakini vijana hawatashiriki ipasavyo kama tutawavuruga na kuwachanganya.

5. Wananchi watapima uongozi wenu sio kwa idadi ya mabandiko FB, tweets au articles. Wananchi hawakuchagua bloggers au waandishi wa articles. Walichagua viongozi wa kuwawakilisha.

Jiulizeni ni watanzania wangapi wako FB na Jamii Forum? Kwa nini idadi yao ni hiyo!? Ukweli wenu au uongo wenu unawafikia?!

Nimesoma andiko la Lema. Limejaa hasira, jazba na kiasi fulani chuki. Nimesoma majibu ya Zitto. Yamejaa kujiamini, kupuuzia na kiasi fulani dharau. Nawajua jinsi mlivyo kwa hiyo sishangai na wala hainikeri.

Lakini mwisho wa siku najua itakavyokuwa. Ukweli utajulikana. Kuna mmoja atabaki mwingine atatwaliwa. Kuna mmoja historia yake itakuwa ni kufundishia mwingine itakuwa kwa ajili ya kukemea. Kwa mlipofikia sasa lazima tujue nani Muongo nani Mkweli.

Kwa sababu mmeamua kufulia nguo kisimani basi zianikeni tuone madoa na usafi wake. Hatutarajii mrudishe kwenye tenga mkaanikie nyumbani.

NB:

Kila mmoja wenu kwa nafasi yake awajulishe watanzania amefanya nini kama Mbunge na Kiongozi wa chama. Kwenye mambo haya;

1. Elimu

2. Afya

3. Ajira

4. Uwajibikaji.

Hayo tu manne. Sitegemei mtatuangusha katika hili. Mkishatoa taarifa zenu basi tutaamua kama mpokee au msipokee posho. Tutatoa msimamo wetu pia.

Wakiweza kujibu hoja kutokana na mambo hayo manne kweli naamini utakuwa mwanzo mzuri wa kumaliza tofauti za manguli hawa wawili

Majibu ya Zitto kwa hili
By Zitto Kabwe

Siku zote najitajidi kutowaangusha. Kila nikifanya jambo najiuliza naweza kujitetea mbele ya ndugu na rafiki zangu? Naweza kujitetea mbele ya umma? Ni suala la misingi tu maana ukiwa muumini wa misingi hutetereshwi. Mimi mjamaa, maisha yangu yanaakisi hivyo tofauti kabisa na watu wanavyotaka kuaminishwa. Lakini silazimishi kila mtu awe kama Mimi ndio maana nina marafiki wakubwa mabepari na wengine Marxists haswa. Tunapishana kimawazo lakini tunaheshimiana mawazo ya kila mmoja wetu.
Wasiwasi wangu huu mjadala wa posho sio mjadala wenyewe, labda ni kianzio tu
 
Tatizo ni kuwa watu wamesahau umuhimu wa Mh Zitto ktk mageuzi Tanzania,Kabla zitto hajaingia Bungeni Mwaka 2005 chadema kilikuwa na wabunge wachache sana pamoja na kuwa Slaa alikuwepo tangu mwaka 2000.

Hoja madhubuti za kitaifa zilizoibuliwa na kijana huyu,zilimfanya kuonekana shujaa mbele ya macho ya watanzania,ilipofika mwaka 2010 Zitto tulimtumia kama mtaji kwa chama alitembea nchi nzima kukinadi chama na kwakuwa jamaa alikuwa na mvuto aliweza kuwashawishi vijana wengi kupenda siasa na kuona kuwa kumbe vijana wanaweza,amesababisha kamii yetu kituamini vijana tofauti na zamani ambapo vijana tulionekana wahuni na hivyo hatustahili kuingka Bungeni.

Amewanadi vijana wengi bila hata kinyongo,na inasemekana alitumia muda mwingi kuwanadi wanachadema wenzie na akafanikiwa kuwashawishi vijana kuwaunga mkono vijana wenzao.

Sasa kazi nzuri aliyofanya Zitto imeanza kunajisiwa na vijana wasiojitambua kwa kuanza kuturudisha huko tulikotoka. vitendo vya kihuni vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ni kuwaharibia vijana wasiaminiwe tena na jamii kama ilivyokuwa zamani.na haya yanafanyika huenda kwa kutokujua.

Matarajio ya vijana wengi ilikuwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha zitto anafunikwa ili na wao waonekane mashujaa mbele ya macho ya watanzania.sasa wanatumia njia haramu kumpoteza zitto. Hawa vijana wamesahau kuwa Zitto ndio chachu ya wao kuaminiwa na mwisho kuchaguliwa na jamii.hawapendi wanapoona Zitto akiendelea kufanya mambo yanayo mpatia umaarufu na kumfanya aendelee kuwa kuwa mwanasiasa bora ambae ni kijana

Kiukweli Zitto bado ni kijana lkn namsifu kwa ubunifu wake anapojenga hoja, zitto amekuwa na vyanzo vingi vya taarifa nyeti za kitaifa ikiwemo baadhi ya maafisa wa serikali,Wenzake wanapomuona yuko karibu na nao huzusha kuwa wanamtumia wakati watu hao hawamsaidii zitto peke yake,Slaa amekuwa akipata nyaraka nyingi za siri toka serikalini ,hii ni ktk utaratibu kama wa zitto, vijana wenzake ktk chama na hata viongozi wa juu ktk chama wanamchukia kwakuwa anaonekana mtu muhimu sana kiasi cha kutishia nyadhifa zao ktk chama.

Tumwache zitto awatumikie watanzani kama wengi tunavyoamini,Zitto atafika mbali sana kutokana na kujiwekea malengo makubwa kisiasa,tusimkatishe tamaa kwa kengo la kumvunja nguvu.

Mwisho nawaomba wanachadema mkumbuke na kufuatilia historia ya lema ktk siasa kahama vyama vingapi na nini kilimfanya ahame,kwa kumbukumbu zangu ni kuwa lema alianzia ccm,akakimbilia Nccr mageuzi,kisha akakimbilia TLP na sasa yupo chadema, huyu lema hana tofauti Mlema ambae anatumika kama kibaraka wa ccm.tumtazame Lema kwa jicho la tatu,ni mtu hatari kwa ukombozi wa kweli wa Taifa letu.

nawasilisha.
 
mwobho

Naungana mkono na wewe mia kwa mia, vijana tunatakiwa tupunguze mihemko(munkari) . Hii nchi tutaijenga kwa kushirikiana sote uwe cdm ,cuf ama ccm, tunapoteza muda mwingi kulumbana kwa mambo yasiyo na na msingi
 
Last edited by a moderator:
Zito aache ushmba aende akatembelee mbuga za wanyama kama serengeti na ngorongoro, hoteli za dola 600 zipo kama anahitaji
 
Nimependa sana hiki kipande,kina mengi ndani yake.
Lakini, nafsi pia inaweza
kukutuma kuchanganya
mazuri na mabaya.
Ukapokea posho ukakataa
rushwa. Au ukakataa
posho ukapokea rushwa.
Ni nafsi yako.
Cc:mad:Zito
 
Hii ni philosophy ya hali ya juu sana,inahitaji ukae na utafakari kwa utulivu na umakini sana
 
Zitto na Lemma mjue sisi tunawajua vyema sana .Mimi namjua Zitto vyema mno na zaidi kama ndugu yangu .Na Lemma namjua kama rafiki si wa karibu but abcd ninazo za kufa mtu .Chadema na uongozi wake sisi tunaujua vyema .Niseme neno moja sitaki kuegamia .Nadhani Zitto kasema mengi ikiwamo kujiuliza nk litokeapo jambo .Jiulize tena Zitto na ingia mitini hutapoteza lolote .Nakueleza hili kama kaka yako maana nasumbuliwa sana na simu na mails .Umekuwa siku zote unakaa kimya na maisha yana endelea .Hebu na hili liache tuangalie mbele .
 
Kama ni umaarufu tu,hata shetani alikuwa nao mbinguni kabla ya kuasi na kutupwa chini.Nawaomba viongozi wa Chadema,tupa chini waasi na wote wanaokiharibu chama hata kama wana umaarufu na walishiriki kuimarisha chama kwani hata shetani alikuwa karibu sana na Mungu lakini alipoanza uasi alitupwa chini yeye na wafuasi wake
 
Wahenga walisema mgema akisifiwa, tembo huitia maji. CHADEMA ilikuwa kitu kimoja hadi pale uchaguzi ngazi ya taifa ulipofika, mkoroganyo ukaanza hapo. Since then hali si shwari. By then nliona wazee wamefanya jema kumshauri Zitto asigombee uenyekiti, now naona kosa kubwa lilifanyika.

Walitakiwa waachwe Mbowe na Zitto kwenye contest, wanachama wangeamua mshindi nani, hadi leo hii CHADEMA ingekuwa moja na salama. Nnachokiona ni Mbowe kutumia madaraka yake ku-protect nyadhifa yake ndani ya chama, bad enough muda wake umeisha haoni mafanikio aliyoyapata, leo hii Zitto angekuwa mwenyekiti, chama kingekuwa kimefika mbali, tayari tungekuwa tunaandaa kijana kushika dola, ila just because haki haikutendeka back then, chama hakijatulia hadi leo. CHADEMA kama chama hakitotambua wapi kiliteleza basi yale makosa ya CCM kupangiana viongozi kirafiki yataicost CHADEMA very soon na chama kitasambaratika kabisa. Mwisho wa siku tutaanza sema Wasira alisema hivi, kumbe chama tumekiua wenyewe.

Narudia tena kusema, waacheni wanachama waamue nani akiongoze chama, sio Mtei.
 
Mkuu MWAKALINGA Y.R inaonekana huu uzi uneuanzisha kwa nia njema ila kuna hatari ya uzi huu huu ukatumika kama sehemu ya mnyukano. Nawashauri tu akina lema na zitto wa come down. Wao kwa kuwa ni viongozi, ni bora wakawa wanachagua zaidi mambo ya kuzungumza kuliko sisi ambao ni watanzania wa kawaida tu.
 
Salaam Zitto na Lema...

Tatizo lenu sio posho. Si vyema kuwadanganya watu au kuwaaminisha kwamba tofauti iliyopo kati yenu ni mawazo au misimamo tofauti kuhusu Posho.

Kama ingekuwa hivyo basi isingekuwa tatizo. Kuwa na mawazo au misimamo tofauti sio tatizo hata siku moja.

Mtu hauhitaji rocket science kuona kwamba kuna zaidi nyuma ya pazia.

Ila kabla sijasema sana niweke mambo machache wazi.

1. Zitto na Lema ni marafiki zangu. Nawafahamu wote kiasi cha kuweza kusema kwamba najua uwezo wa kila mmoja wenu.

2. Sioni tatizo kutumia socia media kugombana au kukosoana. Najua wapo ambao wanasema vikao vitumike. Lakini vikao hivyo wengi wetu hatuhudhurii kwa sababu sio wajumbe. Yatokanayo na vikao hivyo hubaki siri na tunayoletewa ni muhtasari wa vikao. Hatupati nafasi ya kujua nani kasema nini na kwa nini na amesemaje.

3. Chama lazima kikue. Na kukua lazima mambo fulani fulani yatokee. Najua yanaweza yakapitiliza na kuathiri chama ila ni bora yatokee na kuathiri chama kuliko yaje yatokee na kuathiri NCHI. Kama tutavurugana na kugombana chama kikasambaratika basi ni kheri kuliko tuje kufarakana, kuvurugana na kugombana wakati tumepewa madaraka kuongoza watanzania.

Baada ya kuweka hayo mambo matatu wazi niseme kwamba suala la kupokea au kutopokea posho ni suala binafsi sana. Ni suala la NAFSI.

Kama nafsi yako inakutuma upokee posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma upokee rushwa, useme uongo, ukose maadili nk.

Kama nafsi yako inakutuma ukatae posho basi ndio ulivyo. Nafsi hiyo hiyo itakutuma usipokee rushwa, usiseme uongo, uwe na maadili nk.

Lakini, nafsi pia inaweza kukutuma kuchanganya mazuri na mabaya. Ukapokea posho ukakataa rushwa. Au ukakataa posho ukapokea rushwa. Ni nafsi yako.

Zitto na Lema mjipime kwa kile kilicho ndani ya nafsi zenu. Uzuri ni kwamba mwanadamu huwezi kuidanganya nafsi yako.

Ila kumbukeni yafuatayo;

1. Nyinyi ni vijana ambao mmepewa nafasi za kuongoza wananchi ambao wanawaamini.

2. Nchi yetu inahitaji viongozi ambao ni WAKWELI na WASIO NA TAMAA.

3. Lazima mtofautishe KUJULIKANA na KUWA MAARUFU. Nyie wote mnajulikana. Hamna umaarufu wowote. Sidhani kama mmekuwa viongozi ili muwe maarufu.

4. Mna nafasi kubwa sana kwa vijana kwa sababu ya kujulikana kwenu. Nchi hii itasonga mbele tu kama vijana wataamua kushiriki kikamilifu kwenye siasa. Lakini vijana hawatashiriki ipasavyo kama tutawavuruga na kuwachanganya.

5. Wananchi watapima uongozi wenu sio kwa idadi ya mabandiko FB, tweets au articles. Wananchi hawakuchagua bloggers au waandishi wa articles. Walichagua viongozi wa kuwawakilisha.

Jiulizeni ni watanzania wangapi wako FB na Jamii Forum? Kwa nini idadi yao ni hiyo!? Ukweli wenu au uongo wenu unawafikia?!

Nimesoma andiko la Lema. Limejaa hasira, jazba na kiasi fulani chuki. Nimesoma majibu ya Zitto. Yamejaa kujiamini, kupuuzia na kiasi fulani dharau. Nawajua jinsi mlivyo kwa hiyo sishangai na wala hainikeri.

Lakini mwisho wa siku najua itakavyokuwa. Ukweli utajulikana. Kuna mmoja atabaki mwingine atatwaliwa. Kuna mmoja historia yake itakuwa ni kufundishia mwingine itakuwa kwa ajili ya kukemea. Kwa mlipofikia sasa lazima tujue nani Muongo nani Mkweli.

Kwa sababu mmeamua kufulia nguo kisimani basi zianikeni tuone madoa na usafi wake. Hatutarajii mrudishe kwenye tenga mkaanikie nyumbani.

NB:

Kila mmoja wenu kwa nafasi yake awajulishe watanzania amefanya nini kama Mbunge na Kiongozi wa chama. Kwenye mambo haya;

1. Elimu

2. Afya

3. Ajira

4. Uwajibikaji.

Hayo tu manne. Sitegemei mtatuangusha katika hili. Mkishatoa taarifa zenu basi tutaamua kama mpokee au msipokee posho. Tutatoa msimamo wetu pia.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom