Tatizo ni kuwa watu wamesahau umuhimu wa Mh Zitto ktk mageuzi Tanzania,Kabla zitto hajaingia Bungeni Mwaka 2005 chadema kilikuwa na wabunge wachache sana pamoja na kuwa Slaa alikuwepepo tangu mwaka 2000.
Hoja madhubuti za kitaifa zilizoibuliwa na kijana huyu,zilimfanya kuonekana shujaa mbele ya macho ya watanzania,ilipofika mwaka 2010 Zitto tulimtumia kama mtaji kwa chama alitembea nchi nzima kukinadi chama na kwakuwa jamaa alikuwa na mvuto aliweza kuwashawishi vijana wengi kupenda siasa na kuona kuwa kumbe vijana wanaweza,amesababisha kamii yetu kituamini vijana tofauti na zamani ambapo vijana tulionekana wahuni na hivyo hatustahili kuingka Bungeni.
Amewanadi vijana wengi bila hata kinyongo,na inasemekana alitumia muda mwingi kuwanadi wanachadema wenzie na akafanikiwa kuwashawishi vijana kuwaunga mkono vijana wenzao,
Sasa kazi nzuri aliyofanya Zitto imeanza kunajisiwa na vijana wasiojitambua kwa kuanza kuturudisha huko tulikotoka. vitendo vya kihuni vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ni kuwaharibia vijana wasiaminiwe tena na jamii kama ilivyokuwa zamani.na haya yanafanyika huenda kwa kutokujua,
Matarajio ya vijana wengi ilikuwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha zitto anafunikwa ili na wao waonekane mashujaa mbele ya macho ya watanzania.sasa wanatumia njia haramu kumpoteza zitto. hawa vijana wamesahau kuwa Zitto nsio chachu ya wao kuaminiwa na mwisho kuchaguliwa na jamii.hawapendi wanapoona Zitto akiendelea kufanya mambo yanayo mpatia umaarufu na kumfanya aendelee kuwa kuwa mwanasiasa bora ambae ni kijana,kiukweli Zitto bado ni kijana lkn namsifu kwa ubunifu wake anapojenga hoja,zitto amekuwa na vyanzo vingi vya taarifa nyeti za kitaifa ikiwemo baadhi ya maafisa wa serikali,Wenzake wanapomuona yuko karibu na nao huzusha kuwa wanamtumia wakati watu hao hawamsaidii zitto peke yake,Slaa amekuwa akipata nyaraka nyingi za siri toka serikalini ,hii ni ktk utaratibu kama wa zitto,vihana wenzake ktk chama na hata viongozi wa juu ktk chama wanamchukia kwakuwa anaonekana mtu muhimu sana kiasi cha kutishia nyadhifa zao ktk chama.
Tumwache zitto awatumikie watanzani kama wengi tunavyoamini,Zitto atafika mbali sana kutokana na kujiwekea malengo makubwa kisiasa,tusimkatishe tamaa kwa kengo la kumvunja nguvu.
Mwisho nawaomba wanachadema mkumbuke na kufuatilia historia ya lema ktk siasa kahama vyama vingapi na nini kilimfanya ahame,kwa kumbukumbu zangu ni kuwa lema alianzia ccm,akakimbilia Nccr mageuzi,kisha akakimbilia TLP na sasa yupo chadema, huyu lema hana tofauti Mlema ambae anatumika kama kibaraka wa ccm.tumtazame Lema kwa jicho la tatu,ni mtu hatari kwa ukombozi wa kweli wa Taifa letu.
nawasilisha.