Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Mchaki na Mwungulu inaonekana ndo directors wa hii movie

halafu Ludo ndio sterling,huku lwakatare akilazimishwa kuwa "kubwa la maadui".hii itakuwa movie ya kwanza duniani sterling kuuawa na adui!madairekta mmeikosea movie hii..kwi kwii!
 
Kuna kitu ambacho Wanasheria wa CHADEMA wanashindwa kukisema badala yake wanaweka privacy law mbele na kusema imevunjwa kwa Lwakatare kurekodiwa bila idhini yake.

Swala la mtu kurekodiwa anafanya kosa haliwezi kufunikwa na privacy law. Lwakatare amerekodiwa anatenda kosa na kosa hilo haliwezi kuwa siyo kosa kwa sababu privacy law imevunjwa.

Kitu cha muhimu kabisa katika kesi hii, ufunguo wa kesi hii uko na Ludovick kama kweli alikuwa ndiye anarekodi. Ushahidi wake ndiyo utatoa picha mbadala ya nini kilikuwa kinafanyika CHADEMA.

Tusibiri tusikie upande wa pili katika kesi hii kwa sababu kwa sasa tunafanya judgement kwa maelezo ya upande mmoja.
 
There are currently 220 users browsing this thread. (49 members and 171 guests), naona wameamua kuifuatilia thread kama guests. Jinsi wanavyoogopa.

Penye ndiyo hapana haipo,wapo lumumba kuchukua salio.
 
unaweza jiuliza ukimya wa nape na vile anavyokuwaga fasta kuropoka.mpango wa mwigulu utabackfire vibaya wahanga watakuwa mwampamba na shonza na mishe zao za kichina wenye ccm yao watawachukiaje!

Nepi mtoto wa mjini!alishalistukia hili toka mbaali,kabonyea bonyee!kawaachia jamaa liwalipukie wasambaratike ili baadae kwenye vikao vya chama wakimtibua apate pa kuanzia kumaliza wengine..."nyie si mlilipukiwa?!mie peke yangu nimebakia sina masizi wala harufu ya moshi,niachieni mie hii nafasi nipambane nao.nyie hamuwawezi".na ukishakuwa hivyo mkulu anakupa ulaji.
 
Kwani tunalaumu chama au individual people?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Kwan hujui kuwa polisi,usalama wa taifa na watajwa hapo juu wanafanya kazi kwa maelekezo ya ikulu ya ccm?
Kwan kwenu wapi ndugu? Hapa hapa mjini kweli? Haya mambo si lazima upitie shule kaka ila inahitaji uwe na akili kidogo tu.
Poa mkuu si dharau tunawekana sawa. Nawakilisha.
 
Kuna watu nawatafuta hapa siwaoni, mtaumbuka vibaya CCM, na mpotelee huko huko TISS
 
Nikijikita hapo hapo kwa SWOT, sidhani kama Weakness na Threat za CHADEMA zinakuwa identified kwa wakati muafaka na kufanyiwa kazi. Nafikiri kama chama kingekuwa kinafahamu Weakness zake vizuri, hata Threat isingekuwa inafikia kiwango hiki ambacho kwa sasa kinatumia muda mwingi kukabiliana nayo huku mambo mengine yakiwa yamesimama au yame slow down.

Ni vigumu sana kupata picha kamili ya damage kwenye chama inayosababishwa na matukio kama haya. May be, matukio kama haya yanaweza kuwa advantage kwa CHADEMA. Who knows, ukichukulia siasa za kwa Tanzania hazitabiliki.

Usije shangaa hili likaipatia umaarufu Chadema. Naanza kuiona kama ni movie iliyopangwa kila upande ukitaka kumwingiza mwingine matatani. Wasipocheza vizuri CCM watajikuta wamenasa kwenye mtego wa Chadema. Nani alijua Lema angerudishiwa ubunge baada ya kuvuliwa na mahakama? Katika mazingira haya kuna uwezekano wa kila upande kuwa na 'mapandikizi' Serikali inaangushwa na wataalamu wake ambao wamelewa madaraka kiasi cha kutoonyesha umakini katika utendaji wake loophole ambayo wataalamu wa Chadema wanaweza kuitumia kukuza majina yao na kukiongezea chama umaarufu. Ni mapema kujua nani atatoka na kicheko hapa. Tuvute subira ni mchezo usiotabirika!
 
Jamani mbona tunatoa hukumu hata kabla ya kesi kusikilizwa? Haya ni maelezo ya upande mmoja wa utetezi, mbona tunafanya haraka kabla ya kusikia upande wa pili? Kwa maelezo haya natoa majibu ya baadhi ya maswali ambayo kwa hayo hayajatoa mwelekeo wa nani mkweli kati ya pande zote mbili.

Tumeelezwa kwenye uzi ule mwingine kuwa polisi wana clip ambayo ina utofauti na ya youtube, hivyo hatujui ni clip ipi ina mashitaka mahakamani, hivyo naona ni mapema kusheherekea. Wanasheria wanachokifanya naona ni kutafuta uhalisia wa hizo clip, kitu ambacho nadhani, huenda DPP alijilidhisha kabla ya kwenda mahakamani. Tukumbuke kuwa, kwa hapa mshitaki hajatoa vielelezo vyake. Kwangu mimi, baada ya hapo ndio nitaanza kujua mwelekeo wa kesi lakini sasa ni mapema sana, bado nipo gizani.

Ume-make sense kidogo ila kuhusu Dpp hapana kaka ni mchezo. Walijua kuna makosa ya msingi yamefanyika kama wangeendelea na kesi basi ingefutwa( kumbuka siku iliyofutwa ndiyo siku iliyopangwa kutolewa hukumu). Sasa Dpp akatumika kufuta kesi ili wafungue nyingine ambayo makosa yao watakuwa wamerekebisha na ndicho kilicho fanyika.
Kumbuka waliofungua kesi pia wanajua sheria,baada ya mawakili upande wa utetezi kuhoji mahakamani kwa nn hati ya mashtaka haina nembo,wakajua ni kosa kubwa na kuokoka nalo ni kumseti Dpp afute kesi kabla ya kutupwa na mahakama.( kumbuka bado watu wengi ktk vyonbo vya usalama wanafanya kazi za kuibeba ccm)
 
U''fake" wa video ile hauwezi kuelezwa kwa kutumia taaluma ya sheria, wanataaluma wa IT wanaweza kueleza, au wapumbavu ''wanaojua kila kitu''
 
Mawakili wa Lwakatare, Tundu Lissu, Mabere Marando, Prof.Safari, Peter Kibatala na Nyaronyo Kicheere.

Kwa jopo letu la mawakili tumejiridhisha kuwa hakuna kesi ya kujibu , hii ni kutokana na hati ya mashitaka ambayo iliwasilishwa mahakamani.

Sasa maswali.

Sawasawa kabisa, nina swali mwalimu, hivi na wao wakiwa na kesi Riz1 naye atakuwa kwenye list ya mawakili?

Make kuna misururu ya kesi kutoka CHADEMA tumewalea sana naona wanatuzoea sasa!
 
Jf ur not being fair. Nilipost hapa maswali kadhaa kuhusu kadhia hii, nashangaa siioni tena. Na hii sijui kama itaona mwanga wa jua. Nilimuomba Mhe sana Tundu Lissu

1 Atunyambulie sheria inasemaje kuhusu kuiba email ama sms ya mtu bila ridhaa yake na kuianika mitandaoni?

2. Je, baada ya kuiba email na sms ya mtu na kuianika, ana uthibitisho gani kuwa yaliyomo kwenye hizo email na sms si za kughushi kama anavyodai video ya Lwakatare ni ya kughushi???

3 niliomba video tajwa ya Lwakatare iwekwe humu JF tuione na kuisikia ili tupete na kujua ukweli. Maana inatajwa tu lakini haionekani.

kwa kweli i am dissapointed with you JF. How dare you take sides when it comes to CDM being caught pants down?
Mie ningekuwa Michuzi ningeisak hio video na kuirusha kunako blog yangu dunia ijudge. Mkiiondoa hii nitamsaka Michuzi na kumsponsa aiweke hio video kwake watu waone.

....una hakika gani ameiba? Ndo maana hukuona maswali yako JF,

Awe amepewa sms, emails, amehamisha, kusogeza .....Mwanasheria anapaswa kujua, kupeleleza, kuhakikisha anapata ushahidi wa uhakika kuhusu mteja wake.

Ndugu mlalamikaji......Video imewekwa humu nakurudiwa mara nyingi kama hukuiona ungeitafuta ama, fuatilia posts na comments za watu utaiona. Ikishindikana kabisa, Njia rahisi ni nenda kuitafute youtube au msake huyo Michuzi akwambie ilipo anajua.

Kila mtu anajua ni video feki hata CCM ambao ndio wameitengeneza na kudhamini watengenezaji wanajua ni feki sasa nashangaa wakati wanaipangilia hiyo video.....walidhani hatutajua yaliyokuwa nyuma ya pazia? Ndo pamoja na hizo simu na emails ambazo unazipigia kelele ndugu Tarishi
.

Eti ungekuwa Michuzi, sa si ndio maana hujawa michuzi? kama una machungu sana fungua blog yako uweke hiyo video watu waangalie.

Watu mna macho na akili mnashindwa kuona na kutumia akili zenu. I am so dissapointed with you.
 
Wewe ni great thinker!

Ongezea na hii Festo Richard Sanga (Original owner wa Id ya TUNTEMEKE) alikua CHASO kama kiongozi baada ya Uongozi wa Ludovick na wenzake

Mawasiliano ya Festo Sanga Jioni hii akiwa Mbeya na mtu mmoja akiwa Dar(Simtaji kwa sababu maalumu) anasema ana uhakika kabisa kwamba Lwakatare hachomoki kwenye hili suala.Richard Sanga ndiye anayesimamia shughuli zote za Blog ya William Malecela(Kiongozi ndani ya jumuiya ya Wazazi CCM aliyeko karibu sana na Nape na Mwigulu)

Tarifa za Akina Shonza,Mchange,Mwampamba na Sanga kupitia ID ya TUNTEMEKE za Tarehe 12 January (wiki mbili baada ya Mwigulu kudai anayo video)humu kwamba kuna video watakayoiweka itakayokimaliza CHADEMA kabisa na kuwakatisha Tamaa ni kielelezo kwamba walijua kilichokua kinaendelea.Wahojiwe incase hawajampata aliyeweka hiyo video Youtube

Mazingira aliyosemea Mwigulu yabaweza kuwa mazingira yaliyopangwa kwa umakini ili apingwe hapo hapo katika mazingira hayo hayo ili kuondoa suspicion ya mojawapo wa collaborator katika mchezo huo

Devis Msaki+ Mwigulu+MASALIA= - --- -- --- -
safi sana kamanda
 
Im just asking.do u Hv supportive evidence to reclaim ur arguments?
 
Samahani mkuu saronga naomba tu kukuuliza! Sijui sitakusumbua?! Nauliza hivi, hujanione chama Ritz, @zemarcopollo humu ndani?! Sahamani ukiwaona waambie nawakumbusha kuwa "Ukweli huwa unakawaida ya kuchelewa lakini hauachi kufika kule uliko kusudiwa" mimi bado nazidi kuusubiri ukweli udhihiri.
Umemsahau Ng'wamapalala, utaifakwanza, Sumu na zubeda. Kama hii ikithibitishwa, nafikiri utakuwa ndiyo mwisho wa CCM.
 
Last edited by a moderator:
Ninachouliza ile video Mbona hawasemi.kama fake ili km jahaz lizame.kabisaaaa? Hapo tuu Ndo.nashindwa kuelewa
 
We nawe ni mwanasheria toka wapi? Unaitia aibu profession yetu mkuu. Kama katika utoaji wa hiyo nolle prosequi haukuwa wa kihalali mtu yeyote mwenye interst anaweza kuiomba mahakama ipitie uamuzi huo kama ulikuwa wa halali, YOU ARE SUPPOSED TO READ THE LAW INTANDEM MY FRIEND

Kwani ni wapi kwenye post uliyoniquote nimesema kuwa mimi ni mwanasheria?

Yaani un-assume tuu kuwa anayetakiwa kuijua sheria ni lazima awe mwanasheria?

Badala ya kupayuka kama baadhi ya wanasiasa, kama wewe ni loya wa ukweli unayesoma "LAW INTANDEM" basi tupe authority ya unachosema.
 
Umemsahau Ng'wamapalala, taifakwanza, Sumu na zubeda. Kama hii ikithibitishwa, nafikiri utakuwa ndiyo mwisho wa CCM.
Mkuu Lukolo , Tatizo la watanzania ni wepesi kuamini maneno kutoka kwa wanasiasa bila kuyachuja.

Hebu chukua kiti na ufikirie, unataka kuamini kama Mh. Lissu angeitisha press conference na kusema Lwakatare ni GUILT?.

Wanasheria wa CHADEMA wamekuja kwenye public court kutafuta sympathy na kutaka kubadilisha mtazamo wa watu kuhusiana na hili swala.

Hatuwezi kuanza kujenga mitazamo kuhusiana na kesi kwa sababu hata hatujasikia upande wa pili wa marumbano kisheria.

Nia ya Mh. Lissu ni kutaka kuwavuta viongozi wa CCM ili kuifanya kesi iwe ya kisiasa ndiyo maana ameanza kuwachokonoa ili waanze kutoa matamko ya kisiasa.

Kama kesi atashinda, kulikuwa na umuhimu gani basi wa kuanza kuwahubiria waandishi wa habari?. He's just pre-empting the coming court ruling for political reason. Hata hivyo kwenye maelezo yake aliyotoa kuna mapungufu kibao.

Let's wait and see. Imesemwa, hakuna haja ya kuandikia mate na wino upo.
 
Last edited by a moderator:
mgonjwa wa dr kigwangalla

Mgonjwa wake ingawa aliweza kumtetea kesi ya mgomo wa madaktari 2005 kigwangalla akiwa kiongozi wa mgomo.... Kama wagonjwa wanaweza kusimamia kesi zetu na tukashinda this is impressive....
 
Back
Top Bottom