Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Jf ur not being fair. Nilipost hapa maswali kadhaa kuhusu kadhia hii, nashangaa siioni tena. Na hii sijui kama itaona mwanga wa jua. Nilimuomba Mhe sana Tundu Lissu

1 Atunyambulie sheria inasemaje kuhusu kuiba email ama sms ya mtu bila ridhaa yake na kuianika mitandaoni?

2. Je, baada ya kuiba email na sms ya mtu na kuianika, ana uthibitisho gani kuwa yaliyomo kwenye hizo email na sms si za kughushi kama anavyodai video ya Lwakatare ni ya kughushi???

3 niliomba video tajwa ya Lwakatare iwekwe humu JF tuione na kuisikia ili tupete na kujua ukweli. Maana inatajwa tu lakini haionekani.

kwa kweli i am dissapointed with you JF. How dare you take sides when it comes to CDM being caught pants down?
Mie ningekuwa Michuzi ningeisak hio video na kuirusha kunako blog yangu dunia ijudge. Mkiiondoa hii nitamsaka Michuzi na kumsponsa aiweke hio video kwake watu waone.
 
Nilikuwa naamini kuwa kuna watu ndani ya CCM wana akili timamu ni pamoja na huyu mwana JF mwenzangu Ng'wamapalala lakini nimekuja kugundua huyu jamaa ni kati ya walio jaza mavi kichani...

Hata mimi arifu, nilikuwa nimemuweka kwenye group ya watu ambao ni lazima post zake niipitie......ila sasa nimemdharau sana
 
tunachoangalia hapa ni uhalicia wa lwakatare kutengeza hiyo njama je ni kweli ukiangalia clip inaonesha kweli na hakuna ulazima wa kumtetea muovu regadles kuna mazur amefanya wote tunapenda mapinduz ila kwenye uovu hatukubali na wa binafsi ni kinukuu uzi hapo wanakili live so nan mchaw? Hakuna haja ya kutafuta hata kama tunawapenda ndo walinusuru taifa anapofanya crimina lazma ashughulikiwe kama wengne
Uwe unasoma na thread zingine unaambiwa ni Denis Msacky,Ludovicky,Mwigulu Nchemba,Nape,Zitto na Ridhiwani ,nadhani mpaka kesho wengine watafahamika mida ya mazungumzo yao imewekwa, advertisement session ya hiyo video ,iliyofanywa na Zitto na Mwigulu Nchemba star TV nayo imeongelwa
 
Jf ur not being fair. Nilipost hapa maswali kadhaa kuhusu kadhia hii, nashangaa siioni tena. Na hii sijui kama itaona mwanga wa jua. Nilimuomba Mhe sana Tundu Lissu

1 Atunyambulie sheria inasemaje kuhusu kuiba email ama sms ya mtu bila ridhaa yake na kuianika mitandaoni?

2. Je, baada ya kuiba email na sms ya mtu na kuianika, ana uthibitisho gani kuwa yaliyomo kwenye hizo email na sms si za kughushi kama anavyodai video ya Lwakatare ni ya kughushi???

3 niliomba video tajwa ya Lwakatare iwekwe humu JF tuione na kuisikia ili tupete na kujua ukweli. Maana inatajwa tu lakini haionekani.

kwa kweli i am dissapointed with you JF. How dare you take sides when it comes to CDM being caught pants down?
Mie ningekuwa Michuzi ningeisak hio video na kuirusha kunako blog yangu dunia ijudge. Mkiiondoa hii nitamsaka Michuzi na kumsponsa aiweke hio video kwake watu waone.

DPP amefungua kesi kwa video iliyowekwa You tube na Jamii Forums,Email za akina Michuzi zililetwa JF ni ruksa tu kuzitumia baada ya DPP kuhalalisha matumizi yake mind you mimi sio mwanasheria lakini wakija wenyewe watakujibu
 
Hivi kweli ule mkanda unapaswa kutetewa kweli kama una waza vema....kama ni wa kweli basi wanaomtetea wote nao ni magaidi
 
Siku zote wakili/lawyer ni mtetezi wa wahalifu

mawakili haohao unaosema ni wahalifu ndio walimwita mkapa akatoe ushaidi mahakamani kwa kesi fulani ivi sasa sijui nae alienda kutetea uhalifu ama???siku nyingine usikurupuke kuongea ka unaenda chooni.....
 
Haya ni maswali anayoendelea kujiuliza Tundu lissu juu ya video ya lwakatare...ameyasema leo akiongea na waandishi wa habari, muelekeo wa maswali hayo ni kuwa lissu anaamini ile video ni genuine, ila anahoji kuhusu aliyemrekodi katumwa na nani, na kwa nn avunje katiba ya mtu kwa kuingilia privacy ya lwakatare.....sasa nataka wale wote waliokuwa wakiongea humu jamvini kuwa ile video imechezewa, na yule si lwakatare huku wakishindwa kutoa mifano ya watu walioweza chezea video yenye urefu kama ule waje humu, watuambie wana jipya gani sasa hvi!!!, na matusi mnaruhusiwa pia, mana najua wataonitukana, ila nawaombeni mnitukane matusi ambayo sijawahi kuyasikia....maswali ya lissu ni haya hapa......
  1. Nani aliyemrekodi Lwakatare?
  2. Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali?
  3. Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu?
  4. Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani?
  5. Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?
karibuni

Spartacus

Ukitafakari maswali yote hayo na mengine ambayo hujayanukuu, unaona kuwa hakuna mahali Lissu amesema video ni genuine, isipokuwa maswali hayo yanahoji zaidi hiyo genuine, ukishahoji iwapo video ni genuine tayari unaitilia shaka, hivyo unarudi pale pale kwenye kauli za hao unaowahoji.

Au unafikiri editing ni nini!?
 
Kama haijalishi video ilipatikanaje wakati ndio evidence wanayoitumia sasa watamshitaki kwa base ipi, wamlazimishe kwa nguvu kuwa alitamka hayo? Kwanza Mahakama lazima ijiridhishe with no doughts kuwa ile video ni genuine na matamshi yote yalitamkwa na mhusika na kazi hiyo inatakiwa ifanywe na waliomshitaki (polisi) vinginevyo ile kesi itakwisha kwa nusu saa kama anavyosema Lissu.

Afadhali kwa kulitambua hilo. sasa tuiachie mahakama ifanue kazi yake. kulumbana humu JF hakutamsaidia huyo mtu wenu ambaye anapanga kuwapa watu sumu na kuwateka. shame on you!
 
Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA ‘wafunguka’! By Fikra Pevu - On Mar 21st 2013 - in Featured Jamii Siasa Uchunguzi 0 Comment / 1451



Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.
Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha…

Kupitia hati hiyo ya dharura, mawakili hao wanaiomba Mahakama Kuu:
- Ifute hati ya DPP iliyotolewa jana ikifuta mashtaka ya awali
- Ifute amri ya mahakama ya iliyotolewa kumaliza kesi iliyofunguliwa awali kabla ya kufutwa jana
- Ielekeze Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itoe maamuzi kama ilivyokuwa imepanga kutoa kabla 'haijaingiliwa' kwa DPP kuifuta kesi mahakamani.
- Na pia wameiomba Mahakama Kuu, itamke kuwa hicho walichofanya waliomfungulia kesi Lwakatare ni matumizi mabaya ya;
1. Mamlaka ya DPP
2. Mfumo wa Mahakama na
3. Kuingilia uhuru wa Mahakama
Mbali ya maelezo hayo, Wakili Lissu pia amejibu maswali ya wanahabari, ambapo walitaka kujua masuala mbalimbali kuhusu kesi na mashtaka yanayomkabili Lwakatare, akisema:
Mosi, Ili kosa liwe la kigaidi, ni lazima kuwepo maelezo yanayofafanua kuwa kuwa mtuhumiwa alikuwa na malengo au nia ya kigaidi; lakini hakuna maelezo ya namna hiyo kwenye hatia ya mashtaka kueleza ‘terrorism intention’. Alifafanua kuwa kwa maoni yake, Lwakatare amefunguliwa mashtaka ya kigaidi kwa nia tu ya kutaka asote gerezani, kwa sababu waliofungua mashtaka wametaka hivyo… ateseke!

Pili, Nolle prosequi iliyowasilishwa jana na DPP kufuta kesi iliyofunguliwa Jumatatu Machi 18, 2013 kwa ridhaa yake inazua maswali sana (questionable) sana kwasababu hakuna mahali mazingira yanaonesha iliwasilishwa kukidhi masuala mawili muhimu, maslahi ya umma na kuboresha utendekaji wa haki.

Amedai inazua maswali zaidi kwa sababu kadhaa; mbali ya kwamba ilitolewa wakati ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa inakuja kutoa uamuzi kutokana na mabishano ya kisheria yaliyoibuka siku ya Jumatatu, hati mpya ya mashtaka haina kitu kipya isipokuwa hakimu na namba ya kesi. Vitu vingine vyote, ikiwemo aina, idadi ya mashtaka hadi nukta vimebaki vile vile kama vilivyokuwa kwenye hati ya mashtaka ya awali.

Lissu alisema ndiyo maana jopo hilo linaiomba Mahakama Kuu ihoji dalili za uingiliwaji uhuru wa mahakama kwa DPP kuamua kutoa nolle prosequi, siku ambayo mahakama ilikuwa inakuja kutoa maamuzi juu ya mabishano ya kisheria.
"Ingawa mimi sijui mahakama ilitaka kusema nini… wenzetu wana taarifa za kiintelejensia, inawezekana wamejua hakimu angekuja kuamua nini kutokana na mabishano ya kisheria yaliyotokana na hoja za upande wa utetezi, hivyo wakaamua kuleta hiyo hati ya kufuta mashtaka. Kwa sababu haiingii akilini mawakili kama hawa wa serikali ambao wawili ni mawakili wakuu na mmoja wakili mwandamizi, walikosea waliyokosea," alisema Lissu na kuongeza;

"Ingawa watu wengi wanasema na kweli inaonekana hivyo kuwa mamlaka ya DPP kuingilia kesi yoyote na wakati wowote kabla haijatolewa hukumu ni makubwa sana, lakini ikumbukwe kuwa kuna kumbukumbu za maamuzi ya mahakama ambazo zinasema wazi kuwa mamlaka hayo ya DPP yana mipaka, hayawezi kufanyika isipokuwa iwe kwa ajili ya maslahi ya umma au kwa ajili ya kuboresha utendekaji wa haki, lakini kilichofanyika jana ni matumizi mabaya ya mamlaka ya DPP."


Kuhusu video

Wanahabari walitaka kujua maoni yake kuhusu video na namna kesi hiyo ilivyo, hasa kutokana na alivyoielezea ‘charge’ ilivyo ‘defective’, ambapo Wakili Lissu kwa maoni yake, alisema kuwa kuna masuala mengi yanatakiwa kuwekwa wazi kuhusu video yake, akihoji maswali kadhaa:

- Nani aliyemrekodi Lwakatare? Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali? Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu? Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani? Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?

Ushahidi mwingine

Ameongeza kuwa, video inaonekana imechukuliwa tarehe 28 Desemba, siku iliyofuata, Desemba 29, kwenye kipindi cha TV, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akaanza kusema kuwa anayo video ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakipanga mipango ya mauaji ya dhidi ya Watanzania.

Amezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM.

Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.
"Ni mambo yale yale, walianza chama hiki cha familia ya Mtei na Mbowe, ikashindikana, chama hiki cha kikabila, cha Wachaga… ikashindikana, wakasema chama hiki cha kaskazini, imeshindikana, wamesema chama hiki cha wakatoliki, ikashindikana, wamesema chama hiki cha wakristo bado Watanzania wamekataa, iemshindikana pia… Sasa unafanyaje? Tengeneza hii kitu, sasa kiwe chama cha magaidi…ITASHINDIKANA pia," alisema Wakili Lissu
 
Je wajua eliza Feleshi ni mzawa wa nchi ganiii fuatilieni mtajua zaidi then mkonect ishu pamoja na wasaidizi wake
 
Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?

Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.

Mkuu unafatilia hii kesi ya Video ya Lwakatare au unafata upepo tu,Yaliyoandikwa ni kwamba Kutokana sheria za Tanzania kuchunguza vyama vya siasa ni kinyume cha sheria,kwahiyo kama hiyo video ni fake au genuine makosa yako kwa mwenye kuirikodi au yule alietuma hiyo video irikodiwe. halafafu labda ...................ndio...............lwakatare ................

umenisoma
 
Afadhali kwa kulitambua hilo. sasa tuiachie mahakama ifanue kazi yake. kulumbana humu JF hakutamsaidia huyo mtu wenu ambaye anapanga kuwapa watu sumu na kuwateka. shame on you!
JInsi Mwigulu alivyoiabisha IKULU ya KIkwete pamoja na kujifanya anamshipa wa kutokujali hili litmfanya akubaliane n wazee wa CCM kumfuta cheo Mwigulu na ubunge utaota mbao baada ya mahakama kumfunga kwa kuandaa mauaji ya mwanaccmkule ndago lenye mwanzo huwa na mwisho RIP mwigulu
 
Ni dhahiri kuwa CCM walikuwa wakimtumia Ludovick kijasusi. Mawasiliano kati ya Mwigulu Mchemba na Ludovick siku ambayo video ilichukuliwa yanaondoa shaka kuwa aliyeichukua video ni Ludovick, na aliyeifanyia editing ni Mwigulu na Ludovick.

Hii ni aibu nyingine ya Kikwete, viongozi wa chama chake kwa kushirikiana na polisi wanahusika na mbinu chafu na za kipu.mbavu. Big shame to Mwigulu, big shame to Ludovick, big shame to the police and big shame to CCM.


Kwenye red hapo mkuu ina maana kuna tafsiri pana.

Kama Mwampamba alisema anamfahamu vizuri Ludovick na walikuwa wote katika uongozi wa CDM-DUCE basi upo uwezekano kuwa Shonza na Mwampamba ndio walikuwa wanatumika kuisambaratisha CDM. Sasa basi, maneno ya Ben Saanane yatakuwa na kiini fulani cha ukweli! Tunabakia na swali moja kwanini Ben Saanane alioona Zitto anastahili kuhojiwa?
 
Hiyo press conference inatafuta public sympathy tu. Lakini ukiisoma hiyo taarifa ya Lissu na wenzake inaonesha:

1) Lwakatare hajawapa ukweli wote wanasheria wake. Kama angekuwa amewaeleza ukweli wasingesema kuna baadhi ya maneno yamekuwa edited. Lwakatare angewaambia ni kipi alikizungumza na Ludo?!

2) Kama issue ilikuwa ni ya kupanga basi ni kweli Lwakatare alikuwa na huo mpango wa kumpa maelekezo ya utekaji Ludo. Kilichofanyika inaonekana ni Ludo kuwatonya wahusika kwamba kuna a, b,c. Ndio pengine sasa njama za kumrecord atakayoyazungumza zikaanza.

Kwa mantiki hii, video sio feki ila walimrecord bila yeye kujua lakini Lwaka alikuwa pioneer wa mpango mzima wa kutemteka mlengwa.

3) Ludo anaonekana kuwa kama Masalia kama alivyokuwa Saanane lakini akawageuka wenzake na kuamua kusema ukweli.

4) CHADEMA ni wakurupukaji kwa kufanya press conference a day baada ya kukamatwa Lwakatare na kulaani bila kufanya uchunguzi.

5) Machadema mnajifurahisha lakini ukweli ni kwamaba kuna masalia ya kutosha CDM ambapo msipoangalia kifo chenu kitakuwa kibaya sana.
If wishes were horses.....!

Ni nani aliyeweka youtube?

Iko wapi video ya Mwigulu Nchemba?

Ni kwa nini polisi waweke video tofauti na ile iliyopo youtube?
 
Ni kama tamthilia fulani tunasikiliza na kuangalia ktk nchi hii, loo! Yaani mambo ya kuigiza ysiyoisha kama isindigo the need. utadhani yanatokea nchi ya kufikirika!!!!
 
Yule mama mwingereza aliyeidhalilisha serikali mtandaoni alisema rais anashirikiana na vyombo vya dola kudidimiza haki
Umenikumbusha ndugu samahani nilikuwa pori na shida ya umeme na digital unaijua,hivi yale maandamano ya majuha yaliyokuwa yafanyike kumpinga huyu mama yalifana???
 
SAKATA la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, kufunguliwa kesi ya ugadi akidaiwa kupanga mikakati ya kudhuru watu, limechukua sura mpya baada ya chama hicho kudai kunasa mawasiliano ya watu kinaowatuhumu kuandaa video hiyo.
Pia CHADEMA imesema kuwa mawakili wake wamepeleka hati ya dharura katika Mahakama Kuu wakiiomba iingilie kati kwa kuitisha mafaili yote mawili ya kesi hiyo inayomkabili Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph.
Lwakatare alikamatwa Machi 13 mwaka huu na kuhojiwa kwa siku nne kisha kufikishwa mahakamani Machi 18 na kufunguliwa kesi namba 37/2013 yenye mashtaka manne huku Ludovick akisomewa mashtaka matatu.
Akizungunza na waandishi wa habari jana makao makuu ya CHADEMA, mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, alidai kuwa wamenasa mawasiliano ya watu mbalimbali wanaowahisi kuhusika kurekodi video hiyo.

Lissu aliwataja watu hao kuwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky, Ludovick na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mwigullu Nchemba.
Alifafanua kuwa Desemba 27 siku moja kabla ya video hiyo haijarekodiwa kulikuwa na mawasilano ya simu kutoka kwa Msacky kwenda kwa Lwakatare akimuulizia sehemu alipo.
Alisema katika mawasiliano hayo, Msacky anayetajwa kudhuriwa na mkakati huo alimpigia simu Lwakatare na kumuulizia mahali alipo ambapo alijibiwa kuwa alikuwa yuko njiani kurejea Dar es Salaam.

Lissu ambaye pia ni mmoja wa jopo la mawakili wanaomtete Lwakatare, aliongeza kuwa Desemba 28, Ludovick alifika nyumbani kwa Lwakatare siku ambayo video hiyo ilirekodiwa saa 11:59.
Aliongeza kuwa kulikuwa na mawasiliano baina ya Ludovick na Nchemba kwa kutumia namba za simu ya Nchemba inayoonekana katika kitabu cha Bunge.
Lissu alidai kuwa baada ya mawasiliano hayo kati ya Desemba 29 mwaka jana na Januari 2 mwaka huu, Nchemba alinukuriwa katika kituo cha televisheni akisema anayo video inayowaonyesha viongozi wa CHADEMA wakipanga njama za mauaji.
“Tumegundua mengi katika haya na kama tutafika mahakamani jaji au hakimu atakayekuwa anasikiliza tukiwa na hoja zetu atamaliza kesi hii ndani ya saa zisizozidi tatu,” aliongeza Lissu.
Alipotafutwa Msacky kwa simu yake ya kiganjani ili afafanue madai hayo, alikataa akidai kuwa kesi iko mahakamani.
Kuhusu kupeleka hati ya dharura kuiomba mahakama iitishe mafaili yote mawili na kutengua uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka wa kumfutia Lwakatare mashtaka uliotolewa juzi, Lissu alisema wanatambua mamlaka ya kiongozi huyo katika kufungua na kuiondoa kesi mahakamani.
Alisema lengo ni kulinda maslahi ya taifa au kuboresha utendaji wa haki, suala alilodai halikufanyika katika dhamira nzima ya kufuta kesi ya kwanza ya Lwakatare.
“Tumekaa jopo la mawakili watano; tumeiomba mahakama kuu iingilie kati na kuitisha mafaili yote mawili ya kesi hii na kisha ijiridhishe kama sababu ya kufutwa kwa kesi ya kwanza ni kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema.
Alisema maombi mengine katika hati hiyo ni pamoja na kuiomba mahakama ichunguze ili kuona kama haki imetendeka kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, pia wameiomba ifute hati ya kufutiwa mashtaka kwa Lwakatare na ifute amri ya kumaliza kesi hiyo.
Pia alieleza kuwa wameiomba mahakama kuu iiamuru mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuendelea na kesi ya awali iliyofunguliwa Machi 18 mwaka huu na pia itamke kuwa kilichofanywa na mawakili wa serikali ni kuingilia uhuru wa mahakama wa kufanya uamuzi.
Aliongeza katika kesi ya awali walihoji uwepo wa hati ya ridhaa ya DPP juu ya mteja wao kushtakiwa kwa sheria ya kupambana na ugaidi na wakaonyeshwa makaratasi yasiyokuwa na nembo yoyote ya taifa, hali iliyowafanya wahoji na kumuomba hakimu aifute kesi hiyo ombi lililokuwa linatarajiwa kutolewa uamuzi juzi.

Lissu alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ugaidi ili kosa liwe la kigaidi lazima maelezo ya kosa hilo yaonyeshe kuwepo kwa malengo ya ugaidi hali aliyosema katika mashtaka yote mawili suala hilo halionekani.

Chanzo: Tanzania Daima



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Yapeleka hati ya dharura Mahakama Kuu iingilie kati


Na Abdallah Khamis



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Back
Top Bottom