Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

Ukimwamini uşipomwamini sisi haituhusu. Serkali yako hauiamini, kiöngözi wako wa kiroho pia haumwamini sasa ni nani tena utakae mwamini?
 
Wewe kwa akili zako ulitaka asema kwa kutumia lugha yenu ya kinyiramba ndo uelewe? au ulitaka aseme moja kwa moja kuwa ni shambulio la kidini kabla ya uchunguzi kukamlika? na kwa akili zako ulitaka aseme ni WAISLAM ndo walishambulia? Jaribu kufukiria kwa makini kwanza, hili ni jukwaa la fikraa kwanza.
 
Watu wa aina hii ni hatar sana kw mustakabali wa Taifa letu ambao siku zote wao hupenda kuona inatokea migawanyiko miongoni mwetu, mi nahis akili zako hazipo sawa maana umefikia mpaka kulikataa tamko la kiongoz wako wa kiroho!
 
Masome vitabu vya kinabii.Kama haujasoma scripture interpretation hutaambulia kitu.katika vitabu hivi vimeandikwa kwa staili ya kinyume yaani mtu akitaka kulia anacheka na akitaka kulaani anapongeza.chezea theology wewe

waambie ndugu,i had my school rector,alisema hakuna haja adhabu ya viboko.
unachapwa na counselling tuu,its up to your guilt-conscious...
chezea maestros wa Catholic weye..
 
Mtu katoa mawazo yake badala ya kujadili hoja mnatokwa povu kumjadili mtu, nani aliwaambia tunatakiwa kumwamini Pengo? Nae ni mwanadamu ana mapungufu yake. Anaweza kuwa ameongea kwa nia ya kutuliza hasira za waumini wake,lakini hotuba yake ukiifikiria bila kukurupuka ina maswali mengi kuliko baadhi yenu mnavyodhani. Nilini Pengo aliwahi kutambia kuwa Arusha wakatoliki wanamgogoro kiasi cha kutaka kuuana? Hiyo intelejesia mnayosema anayo haikumuonyesha mgogoro uliopo bali inaonyesha baada ya bomu kulipuliwa? Na hao waliotaja hayo majina mojamoja walikuwa na uharaka gani wa kutaja hivyo wakati waliokamatwa kwa tuhuma hizo ni 10? Jamani acheni kucheza na akili za wananchi, tafadhali tuambiane ukweli.
 
Pengo kasema shambulio lililolenga IBADA ya kikristo haliusiani na udini!!sawa, kichwa cha habari ile kilisomeka Pengo afichua siri nzito mlipuko wa arusha!!!sikuiona siri hiyo ndani ya content ile,nilitegemea atuambie mbadala wake na hakufanya hivyo,zaidi sana alisisitiza tu imani kubwa aliyo nayo kwa chanzo chake hicho cha habari,nikasema hata mimi wakati fulani nilikuwa naamini kabisa tales za sungura na fisi,sikuamini kama watu wakubwa,wasomi wangeweza tu kuandika na kuchora picha ili wanidanganye,leo siziamini tena!!!je Pengo akija kutilia shaka reliability ya hiyo source yake atakuja tena kueleza. Shaka yake juu ya hao ma informer??
 
Nataka kujua kama akina nape nauye,lukosi na mwigulu nchemba wanakubaliana na azimio la bunge au wataendelea na maneno yao ya cuf ni chama cha visiwani na cha kiislamu?je wataendelea kusema chadema ni cha kikristo?je tutaendelea kupost jf kuwa kuna mfumo kristo...?napenda kujua itakavyofuata apo mbeleni.
 

Dares Salaam/Arusha.Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.

“Jana (juzi), niliongeleakwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini.Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuwezakuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababuya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu yamsimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

“Lengo la msingi kabisa,langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwaupande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu waamani katika nchi yetu,” alisema Pengo.

Alisema kuwa kilaanayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwaikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotoshaukweli kwa namna yoyote ile.

“Tusipojua kusema ukweliulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja nakuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi memakuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya ainayoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huuunamgusa nani,” alisema Pengo.

Alisema kujaribu kufichaukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya yawatu na ieleweke hivyo.

“Naomba kila mtuakubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo lamsingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusemaukweli kama ulivyo,” alisema.
Source: Mwananchi la Leo
 
Huyu mzee ana kihehrehere.nani kampa yeye usemaji wa wakatoliki wa tanzania?msemaji mkuu wa wakatoliki sio yeye bali ni rais wa baraza la maaskofu tanzania na yeye ni askofu mkuu wa jimbo kuu la dar.
 
pengo+pix.jpg

Bomu Arusha: Pengo afichua siri

Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:


“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.

Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.

“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.

Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.

“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.
 
Matuko haya ya mfululizo, mara ugaidi kubambikizwa akina Rwekatare, mara kuuawa Mapadre kule Zanzibar, mara mabomu Arusha, kuna kitu ambacho kinaendelea hapa nchini kupitia mtandao fulani iwe wa vyombo vya dola, siasa, serikali, kwa kisingizio cha mtafaruku wa kidini ili kuingiza ugaidi wanaokusudia kuendelea kujikinda kulinda himaya waliyoizoea, maana kuna dalili supo kuanza kuamishiwa shemu ambayo wataikosa.
 
Wanafiki walokanusha akina Yerricko Tunawataka waje kuomba Radhi
 
Ile skendo yake ya uuzaji wa madawa ya kulevya imeishia wapi? Yawezekana ni miongoni mwa watu wanaotuharibia amani yetu huyu mzee.
 
Taarifa kwamba Balozi wa Papa nchini atahudhuria ufunguzi wa kanisa la arusha hazikutangazwa, ila taasisi za vyombo vya usalama ndizo zilizokuwa na taarifa kwa ajili ya kulinda usalama, na maana nyingine zinabeba lawama kuvujisha siri ya uwepo wa balozi pale. Vigumu kuamini kwamba magaidi walioko Somalia, Uarabuni na kwngineko wafahamu uwepo wa balozi wa papa pale Arusha. Kuna mengi lakini ukweli ni kikulacho kii nguoni mwako.
 
Mimi sipendi unafiki, kama ana taarifa sahihi azipeleke kwenye vyombo vya usalama kusudi isije kutokea wakabambikizwa kesi wasio na hatia.Suala siyo intention ya uhalifu bali kosa ni kufanya tukio la uhalifu lililogharimu maisha ya watu wasio na hatia yoyote.
 
Back
Top Bottom