Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

ili kuondoa utata wa matamshi hayo ni vema akaitisha mkutano na waandishi wa habari akaweka bayana
ili watu waelewe na serikali ilifanyie kazi
sijajua ni kwa nini serikali inakuwa na kigugumizi
amesema hana shaka na matamshi yake. serikali inangoja nini? Au inahusika?
 
Hongera Pengo kwa kauli yako hiyo, ila mleta thread ungetuwekea chanzo cha nukuu ya kauli ya Pengo tafadhali kwa kujiridhisha.

Source pls!
 
ili kuondoa utata wa matamshi hayo ni vema akaitisha mkutano na waandishi wa habari akaweka bayana
ili watu waelewe na serikali ilifanyie kazi
sijajua ni kwa nini serikali inakuwa na kigugumizi
amesema hana shaka na matamshi yake. serikali inangoja nini? Au inahusika?

Mkuu Nsera Ndawani,
Hebu tuwekee CHANZO, maana napata ukungu kuamini mabandiko yako kwa habari hii.
 
Last edited by a moderator:
Mbona sijaona siri aliyofichua sasa?nilitegemea kuona akiainisha sababu za shambulio,hajafanya hivyo,just a hearsay kama tu mamburula wengine wanavyo pass hoaxes from one to another,haya sasa ewe mwandishi mwaminifu wa pengo na uje sasa na utumegee siri hiyo ya mlipuko,hata mimi nilikuwaga sina shaka yoyote na hadithi za sungura na fisi,sikuamini kama mtu mzima na akili zake angeweza kuandika kitabu kikuubwa ili anidanganye,lakini sasa naelewa wapi juu wapi chini.
 
Dar es Salaam/Arusha. Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana shaka nao.
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

Msimlishe maneno Pengo. Mbona waislam mnahangaika sana? tulieni mbivu na mbichi zitajulikana tu
 
Haya sasa naona mambo yanazidi kucottonfire hapa.
 
Pengo siku hizi kawa Mwislam mtamkataa hata Yesu akisema hayo maneno.Nyie mnachotaka mwislamu ahusishwe ndo mkubali Shame on you
Msimlishe maneno Pengo. Mbona waislam mnahangaika sana? tulieni mbivu na mbichi zitajulikana tu
 
siri gani we mwendawazimu hapa chadema hawachomoki.
 
My gawwddd...!!kumbe tena kuna joseph na davy...dah.!!
Yawezekana pengo alisema ukweli,mi nikadhani amechemsha.
 
Sasa unachobishania ni nini? Au wewe ni miongoni mwa mahekalu ua shetani.

Mkuu hao ndio wenzao walipuaji sasa wanaona azma yao haijatimia wanaanza kuropoka-lakini Mungu bado ana watu wake wema duniani mmoja wao akiwa Pengo, tunamuombea maisha marefu
 
hiyo ni kauli ya pengo mkuu wa kanisa katholiki tanzania.
hajalishwa maneno, ila serikali inatakiwa ichukue huo ushahidi alio nao ili tuondokane na hii sintofahamu. kigugumizi kiko kwa serikali.
 
Pengo siku hizi kawa Mwislam mtamkataa hata Yesu akisema hayo maneno.Nyie mnachotaka mwislamu ahusishwe ndo mkubali Shame on you

Huyo aliyerusha bomu ni mkristo na miongoni mwa waliokamatwa ni wasaudia 4

Something has to give..

Pengo ni kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania na kwa nafasi yake alichaguliwa na Papa nadhani ameongea hayo yote baada ya kupata proof na sio unsubstantiated rumours...hakuna anayependa tukio hili lihusishwe na dini yoyote, lakini hakuna anayependa kuchezewa akili kwa maslahi binafsi

I stand to emphasize the truth
 
Maneno haya ya busara na hekima.
"Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo," alisema Kadinali Pengo . Ila yangitoka kwenye kinywa cha mtu mwingine yeyote yasingekuwa ya busara na angejuta kwa kejeli, matusi na kashfa humu JF.
 
Back
Top Bottom