Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,264
Anachojaribu kukifanya huyu msemaji ni kutaka wasiokuwa Wakatoliki waamini kuwa Kanisa Katoliki bado lina nguvu ile ile iliyokuwanayo kabla ya sakata la "Waarabu" na Bandari ya Dar-es-Salaam.
Kanisa Katoliki katika sakata hili halikupata kile ambacho wamezoea kupata kuanzia wakati wa ukoloni hadi kufikia hili la bandari kupewa "Waarabu," katika Tanganyika huru.
TEC imefedheheka na hili limewaumiza na kwa mara ya kwanza wameshindwa kupata walichotaka kama ilivyokuwa mazoea.
Hawa walikuwa wakikataa kitu basi hakipiti.
Hawakuitaka EAMWS.
Hawakuitaka OIC.
Hawakuitaka Mahakama ya Kadhi.
Hili la bandari hawakulitaka kama ilivyo kawaida.
Wameshindwa safari hii kwa mara ya kwanza.
"Waarabu" wamekabidhiwa bandari.
Imekuwaje kwa TEC kushindwa?
Imeshindwa kwa sababu kuu moja ingawa zipo nyingi.
Hapa nitaeleza hii sababu moja kuu.
Waislam katika sakata la bandari walijikusanya pamoja na kujiweka mbali sana na wale ambao kila wamuonapo "Mwarabu" wao wanauona Uislam ambao lazima upigwe vita kwa hali yoyote ile.
Lakini kulikuwa na kitu kilichoongeza ladha katika kachumbari iliyokuwa ikitengenezwa na TEC.
Waliokuwa wanapinga Waarabu kuendesha bandari walikuwa wa imani moja na pamoja na CHADEMA.
Mifano iko mingi lakini hapana haja kueleza yote hapa.
Waislam kimya kimya wakaiunganisha CHADEMA katika orodha yao.
Chama hiki kikawekwa kundi moja na TEC na hii haikuwa kazi kubwa ya kumtoa mtu jasho la kwapa.
Ndani ya serikali na CCM kuna watu waliona mapema kabisa asubuhi kuwa nchi imeshagawanyika mapande mawili katika misingi ya imani.
Walio ndani ya serikali na CCM iliwadhihirikia kuwa Waislam wamejitenga wako mbali na wanaowapiga vita "Waarabu" na kwa mara ya kwanza kwa namna ya ajabu kabisa Waislam wakawa wanasubiri muda uwadie wapambane na TEC na mwenza wake CHADEMA.
Zikavuja taarifa kuwa Waislam nje ya BAKWATA wanajiandaa kwenda mahakamani kuhoji mengi yanayowasibu ndani ya serikali.
Waliokuwa serikalini na CCM walitambua watuhumiwa watakuwa nani.
Wenye akili zilizotimia ndani ya serikali na CCM haraka wakajiuliza tumefikaje hapa?
Hawa Waswahili si ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana?
Wenye akili timamu wakatambua vipi wamefika hapo.
Waingereza wana msemo, "You do it once too often."
Wakatoliki wamejidekeza kupita kiasi kwa kuhodhi kila kitu kuanzia serikali yenyewe, bunge, vyama vya siasa na kila kitu bila ya kukutana na kizingiti chochote.
Waislam wako nje na katika hili la "Waarabu," na bandari wamejiweka pembeni makusudi ili Ukristo ndani ya Tanzania ujivue nguo wenyewe hadharani.
Wametishika na wakarudi nyuma.
Hatari iliyokuwa inawakabili waliitambua.
Serikali ikatimiza maamuzi yake.
Taifa likabakia limetulia.
Kanisa likabakia limefedheheka.
Ile nguvu waliyodhani bado TEC inayo kumbe haipo tena.
TEC bila shaka imejiuliza baada ya haya nini kitafuatia?
Sababu ya kushindwa kwao wanaijua fika.
Sasa msemaji anasema Vatican siyo iliyomwalika Rais wa Tanzania bali serikali imeombwa ialikwe Vatican.
Nani mwenye kawaida ya kuongopa?
Kinachotafutwa hapa ni kujaribu kujifuta tope baada ya kuanguka.
Inataka ieleweke kuwa Rais wa Tanzania ana hofu na amejisalimisha Vatican.
Msemaji ananadi kuwa Kanisa Katoliki lina nguvu si watu wa kupuuzwa.
Ukweli ni kuwa hakika Kanisa limehodhi serikali kwa uwiano wa 80% kwa 20%.
Hali hii leo si mtaji tena kwao kwa sababu zilizo wazi kwani mengi yasiyopendeza yanaelezwa dhidi ya Kanisa na hatari yake ishajitokeza.
TEC imedhoofika bila yenyewe kutambua.
Hii ndiyo sababu ya TEC na CHADEMA kujikuta wako peke yao katika sakata la bandari na vita yao dhidi ya "Waarabu."
Iwe iwavyo hali ya siasa imebadilika.
Hizi propaganda kuwa Rais wa Tanzania ana hofu hazitasaidia kitu.
Zinaweza zikaamsha makubwa ambayo hawayategemei.
Zinaweza hizi propaganda pengine zikazua makubwa kuliko ule ukimya walioonesha Waislam wakati wa sakata la bandari.
Wasisahau ukimya mwingi una kishindo.