Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

Sakata la Bomu: Pengo afichua siri

Maneno ya Baba Kardinali yamekaa kifalsafa zaidi, ngumu akili ya kawaida kuelewa....Baba ongea katika Muktadha wa kawaida kabisa. Naamini Mzee Mwanakijiji anaweza kutembea na mistari ya Kardinali wengine tutachemka tu
 
pengo+pix.jpg

Bomu Arusha: Pengo afichua siri

Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao."Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo," alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

"Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu," alisema Pengo.

Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.

"Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani," alisema Pengo.

Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.

"Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo," alisema.

Huwa sio mgumu wa kuelewa kiasi hiki lakini kila nikirudia kusoma natoka kapa!!

Hilo tamko la leo amelisemea wapi mkuu coz tunapata shida sana juu ya kauli za kardinal hapa jamvini. Jana zililetwa thread mara mbili mkuu Yerico akazitolea ufafanuzi mara zote mbili kuwa si za kardinal Pengo na mods wakaziondoa zile thread.
Leo asubuh ilikuja tena thread ikilinukuu gazeti la nipashe kwa kauli hiyo.Baadhi ya wachangiaji wakalalamika ikafungwa still tena saivi inakuja hii ni ya kweli?source ni wapi?
Ni vema tukaweka maslahi ya taifa mbele juu ya hili ili tukichangia tuchangie yaliyo +ve.
 
Kwa taarifa ya Bango la Balozi wa Papa atakuwepo nchini nimeliona katika Kanisa la Burka likisema kuwa kutakuwa ujio wa balozi wa papa katika kanisa, hiyo nadhani hiyo pia ingeweza kuchangia wahalifu kupata taarifa hizo kwani nadhani limewekwa wiki moja kabla. Kwa hivyo sio tu kwamba taarifa hizo zimetoka katika vyombo vya usalama tu, bali hata kwa taarifa kwa waumini ili washiriki katika kumpokea.
 
Iko siku watu watachoka
Serikali inabidi ifanye operesheni kubwa sana kutuepusha na balaa kubwa
 
Taarifa kwamba Balozi wa Papa nchini atahudhuria ufunguzi wa kanisa la arusha hazikutangazwa, ila taasisi za vyombo vya usalama ndizo zilizokuwa na taarifa kwa ajili ya kulinda usalama, na maana nyingine zinabeba lawama kuvujisha siri ya uwepo wa balozi pale. Vigumu kuamini kwamba magaidi walioko Somalia, Uarabuni na kwngineko wafahamu uwepo wa balozi wa papa pale Arusha. Kuna mengi lakini ukweli ni kikulacho kii nguoni mwako.
Kwa taarifa ya Bango la Balozi wa Papa atakuwepo nchini nimeliona katika Kanisa la Burka likisema kuwa kutakuwa ujio wa balozi wa papa katika kanisa, hiyo nadhani hiyo pia ingeweza kuchangia wahalifu kupata taarifa hizo kwani nadhani limewekwa wiki moja kabla. Kwa hivyo sio tu kwamba taarifa hizo zimetoka katika vyombo vya usalama tu, bali hata kwa taarifa kwa waumini ili washiriki katika kumpokea.
 
Ile skendo yake ya uuzaji wa madawa ya kulevya imeishia wapi? Yawezekana ni miongoni mwa watu wanaotuharibia amani yetu huyu mzee.

Kumbe umesahau kwamba Mh Jakaya Kikwete alikuwa anakwepesha kibao baada ya kujulikana motto wake wa kwanza Ridhiwani ni gwiji la kuuza madawa ya kulevya nadhani wakati mwingine usipende kuleta maudhi kwenye mambo ya maisha ya watu
 
pengo+pix.jpg

Bomu Arusha: Pengo afichua siri

Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.

Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.

“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.

Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.

“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.

Ili ule mswaada wa kuzuia maandamano na mikutano liwe na mshiko tukio la bomu arusha linaumuhimu wa aina yake, ila calculation imekosewa, kumuinvolve Barozi wa Vatican. Maana yake wamefanya imekuwa sio issue ya kitaifa tena bali ya kimataifa.
 
This is philosophical statement,ukisoma kwa kukurupuka huku ukitoa mapovu,huwezi kumwelewa baba Cardinal.
 
Jana katika kujadiri azimio la bunge katika kulaani na kupinga kitendo cha kigaidi kilichofanywa na watu wasio julikana katika kanisa katoliki huko Arusha, wabunge wote bila kujari itikadi za vyama vyao wala imani zao za kidini walionyesha kuamini kuwa tukio hilo linatokana na imani za kidini kulaani na kuonya juu ya mtafaruku unaoendelea kujitokeza kati ya wakristu na waislam.

Hii ni tofauti kabisa na tamko la kardinali Pengo ambaye kwa intelijensia yake ametamka kuwa shambulizi hilo alihusiani na na maswala ya kiimani.

Lakini mimi naomba kujua, hivi msimamo wa bunge na tamko la Pengo haviingilii uchunguzi wa polisi?

Hii ni kutokana na kwamba bunge lishajiaminisha na kuamisha watanzania walio wengi kwamba shamulizi hilo linatokana na mpasuko wa kidini unaolikumba taifa letu na huku Pengo kajenga imani na kuaminisha wengine kwamba shambulizi hilo halina mahusiano yoyote na maswala ya kiimani.

Wakuu mie naona pande zote mbili yaani Pengo na bunge wamewahi mno kutoa kauli zao kwani polisi inaweza kuja na matokeo ya uchunguzi yakiwa kinyume kabisa na imani ya matamko yao, je watakubali?
 
Kuna haja ya kuwa na minimum qualification bungeni
Haya mambo ya maswali magumu kujibiwa na majibu mepesi inataka kuwa tabia zoelefu
 
Jana katika kujadiri azimio la bunge katika kulaani na kupinga kitendo cha kigaidi kilichofanywa na watu wasio julikana katika kanisa katoliki huko Arusha, wabunge wote bila kujari itikadi za vyama vyao wala imani zao za kidini walionyesha kuamini kuwa tukio hilo linatokana na imani za kidini kulaani na kuonya juu ya mtafaruku unaoendelea kujitokeza kati ya wakristu na waislam.

Hii ni tofauti kabisa na tamko la kardinali Pengo ambaye kwa intelijensia yake ametamka kuwa shambulizi hilo alihusiani na na maswala ya kiimani.

Lakini mimi naomba kujua, hivi msimamo wa bunge na tamko la Pengo haviingilii uchunguzi wa polisi?

Hii ni kutokana na kwamba bunge lishajiaminisha na kuamisha watanzania walio wengi kwamba shamulizi hilo linatokana na mpasuko wa kidini unaolikumba taifa letu na huku Pengo kajenga imani na kuaminisha wengine kwamba shambulizi hilo halina mahusiano yoyote na maswala ya kiimani.

Wakuu mie naona pande zote mbili yaani Pengo na bunge wamewahi mno kutoa kauli zao kwani polisi inaweza kuja na matokeo ya uchunguzi yakiwa kinyume kabisa na imani ya matamko yao, je watakubali?
kama polisi wanajua kazi yao barabara wanatakiwa wamkamate Pengo kama shahidi namba moja
 
haya ni matokeo ya akili ndogo mno kupewa majukumu makubwa..
Bunge+ polisi= kizunguzungu tu....
 
Back
Top Bottom