Sakata la Bodi ya Mikopo dhidi ya Nicholaus Komba

Sakata la Bodi ya Mikopo dhidi ya Nicholaus Komba

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,197
Reaction score
10,710
Kuna mambo yakitokea duniani basi moja kwa moja fahamu kuwa upo ndani ya bara la Afrika na kuna upuuzi ukitokea Afrika basi fahamu tu upo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1789124134457.jpg

Nadhani mahakama za kwetu Tanzania ndio zinaongoza kwa kutoa maamuzi kichwa kichwa sana, vitivo vya sheria ndani ya chuo kikuu Cha Harvard ama pale Stanford sidhani kama akili zao ni bogus kiasi ambacho mahakimu wetu wanakifanya kwa hakika, tuna wanasheria wa ovyo kuwahi kutokea.
1789124140850.jpg

Ni wiki iliyopita yaani siku ya Ijumaa, Septemba 4, 2026, Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma ilifika tamati yake kwenye kesi iliyomkabili Bwana Nicholaus Komba Mahitana (maarufu kwa jina la Abdallah Mahimbo).
1789124137087.jpg

Bwana huyu, aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma nzito za kughushi, kujifanya mtumishi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), na kuwalaghai wanufaika kuwa ana uwezo wa kuwafutia madeni yao, alikiri makosa kupitia (Plea Bargaining) baada ya kuandika barua kwa DPP.
1789124143137.jpg

Sasa ajabu sio bwana mkubwa kupewa hukumu ila ni hukumu iliyotoka kwani imetuacha wengi midomo wazi: Bwana Nicholaus anapaswa kulipa faini ya shilingi 1,600,000/=, kurejesha kiasi cha shilingi 3,000,000/= taslimu, huku pia akitakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Mbeya mara moja kwa mwezi kwa miaka mitatu.
1789124163782.jpg

Maamuzi haya yanaibua maswali mazito yasiyopaswa kufumbiwa macho. Hivi inawezekana vipi mtuhumiwa wa mtandao hatari wa kughushi na utapeli wa mfumo wa umma aachiliwe kwa adhabu ya namna hii?
1789124166591.jpg

Je, Nicholaus Komba amejipatia kiasi gani cha fedha nyuma ya pazia? Ikiwa tapeli huyu alifanikiwa kukusanya, tuseme, shilingi milioni 40 kutoka kwa wanufaika waliokata tamaa kote nchini, inakuaje mahakama inamtoza faini ya "kiboya namna hii" ya milioni 1.6 na kumtaka arejeshe milioni 3 pekee?
1789124169077.jpg

Hii ni sawa na futuhi ambapo mwizi wa bilioni 500 anapewa adhabu ya kulipa milioni 300 kisha anaambiwa awe anatembea kwenda kituo cha polisi kujulisha uwepo wake!
1789124171197.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, alishuhudia hukumu hii na kuishia tu kutoa wito kwa wanufaika kuepuka vishoka. Twende mbele turudi nyuma tukubali kuwa HESLB inaongozwa na viongozi wapuuzi kupita maelezo. Yaani hapa mmejaribu kuzima moto kwa mafuta ya taa.
1789124134457.jpg

Lakini swali la msingi linabaki: Je, taasisi na mamlaka za kisheria zinafahamu na zinatambua hatari ya kiutendaji iliyowekwa hapa? Adhabu hii laini kiasi hiki inatoa ishara gani kwa wahalifu wengine wa mtandao?
1789124140850.jpg

Na ukweli ni kwamba kuna kina Komba wengi mtaani na wamepata nguvu kuona hiki kilichotokea. Ikiwa Komba amefundisha mtandao mwingine wa vishoka au kuacha mbinu zake zikiendelea kufanya kazi, adhabu hii inawavunja moyo au inawapa moyo wa kuendelea kupiga pesa za umma wakijua faini ni kidogo kuliko faida wanayopata?
1789124143137.jpg

Wasiwasi mkubwa uliobaki kwa watanzania ni kuwa mfumo wa plea bargaining unapaswa kutenda haki na kutoa fundisho, badala ya kugeuka kuwa fursa ya wahalifu wenye fedha kununua uhuru wao kirahisi na kuacha maumivu kwa wananchi waliotapeliwa.

NB: MHALIFU ANAPIGA PICHA NA WATU ALIOWAZIDI MAARIFA HUKU AKIFURAHIA KABSA!
 
Sijakuelewa maanq maelezo mengi ila content hakuna! Sheria inasemaje?? Ni kiasi gani katapeli?? Maana hukumu imesema arejeshe 3000,000/= maanake hizo ndo pesa alizotapeli au??
 
Back
Top Bottom