Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

Pale Addis Ababa asikose kupitia Gotera Junction (Flyover) na apige picha aende akawaoneshe Watanzania,Halafu awaelezee ni kwa nini Ethiopia waweze lakini Tanzania washindwe?
Angalieni hii link:

Jimma Times

Tunasubiri jibu.
Ahsanteni.
 
JamiiForums ni mahali pazuri kwa Watanzania kujadili Tanzania itapata nini kutokana na ziara za viongozi wake nchi za nje.

Uchambuzi wa JamiiForums unataka kuwawezesha kimawazo viongozi wetu kuanzia ngazi ya Urais kwenda chini Umakamo wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri kuwa wawazi juu ya nini wanaenda kufanya ktk ziara zao nje ya nchi na kuwa Tanzania itafaidika vipi.

Mfano ziara ya majuzi ya Raisi wa China nchini Marekani ilichambuliwa vilivyo na magazeti ya USA na China kuona nchi hizo zitafaidika vipi na ziara hiyo ya Rais Hu wa China huko USA nanukuu gazeti moja la Seattle Times likiiangalia kwa makini faida ya ziara hiyo:

''Most of the meeting's agenda will be the same as at previous Sino-U.S. summits. President Barack Obama will likely raise issues such as the bilateral trade imbalance, the Chinese government's manipulation of the renminbi's exchange rate, prevention of nuclear proliferation, recent tension on the Korean peninsula, international cooperation on climate change, and China's poor human-rights record.

Hu's reactions to Obama will also be familiar. China will blame the trade imbalance on America's ban on high-tech exports to China, deny engaging in currency manipulation, call on the U.S. and its allies in East Asia to negotiate with North Korea without preconditions, insist on China's entitlement as a developing country to an exemption from emissions caps on CO2, and refute criticism of its human-rights record.''
Unaweza kusoma makala nzima hapa Opinion | How to make China president's U.S. visit more meaningful | Seattle Times Newspaper

JamiiForums tumeanza utamaduni wa ku 'scrutinize' ziara za viongozi wetu nje na ni matumaini magazeti, vyombo vya habari, asasi za kijamii, vijiwe n.k tutakuza utamaduni huu mzuri ili viongozi wetu wajue tunafuatilia na kutaka kujua faida za ziara zao nje ya nchi kwa uchumi wa Tanzania kwa kuanzia. Maana pia kuna faida za kijamii, kimichezo n.k lakini hizo kwa kuwa Tanzania ni 'masikini' , macho na akili yetu ikite katika uchambuzi wa faida za kiuchumi na biashara.

Na isiwe ni hisani bali ni lazima kwa viongozi kabla hawajaenda ziarani kutupatia taarifa na wakirejea wanatuelezea mafanikio na ajenda walizozijadili kwa niaba ya Watanzania.

Mfano, Hapa kurugenzi ya habari Ikulu iwe ina utamaduni kwa kutujuza safari za Marais wetu nje kwa kutufahamisha ni ajenda gani zitaongelewa n.k n.k
 
MHE. RAIS SAFARINI GENEVA, DAVOS NA ADDIS!!!
January 24th, 2011

What a President... never like to live in HOT Dar-es-salaam?

RaisJakayaKikwete4-7119281.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa leo, Jumatatu, Januari 24, 2011, kwenda Uswisi ambako atakuwa na shughuli muhimu za kikazi katika miji ya Geneva na Davos.

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa Tume ya Kimataifa Kuhusu Afya ya Akinamama na Watoto.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa (UN) inaongozwa kwa pamoja na Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada, Mheshimiwa Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Tume hiyo.

Kazi ya kwanza ya Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper katika Tume hiyo itakuwa ni uzinduzi wa Tume yenyewe utakaofanyika keshokutwa kwenye Jengo la Salle de Presse, ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Uzinduzi huo utafuatiwa na kikao cha kwanza cha Tume kitakachofanyika kwenye Chumba cha Mikutano cha Bodi ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper wataongoza kikao hicho cha siku moja kujadili kwa undani kazi na wajibu wa Tume yenyewe, matokeo yanayotarajiwa kutokana na Tume hiyo ya kitaifa.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imeundwa kwa minajili ya kuweka mfumo wa kuyasaidia mataifa kuangalia upya afya ya akinamama na watoto kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) pamoja na kuainisha hatua za jinsi ya kupima mafanikio katika eneo hilo, na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kuboresha upatikana wa habari kuhusu afya ya akinamama na watoto.

Baada ya mkutano huo wa Geneva, Rais Kikwete atakwenda katika mji mdogo wa Davos ambako kwa siku mbili atahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) wa mwaka huu.

Mbali na kuhudhuria shughuli za WEF kwa mwaka huu, Rais Kikwete atashiriki katika tukio muhimu sana la uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Maeneo ya Kilimo Kusini mwa Tanzania (South Agricultural Growth Corridor of Tanzania  SAGCOT).

Mpango huo wa aina yake utatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania, washirika wa maendeleo wa Tanzania, sekta binafsi na mashirika makubwa ya kusaidia maendeleo duniani ikiwamo Benki ya Dunia, na utalenga kuwatoa mamilioni ya wakulima wa Tanzania katika umasikini.

Rais Kikwete ataondoka Davos, Jumamosi, Januari 29, 2011, kurejea nyumbani na akiwa njiani, atasimama mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika (AU). Rais Kikwete atakuwa mjini Addis Ababa kwa siku tatu na atarejea nyumbani Februari 2, 2011.

Kumekucha!!!!
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa tano usiku ITV Kikwete anaonekana kwenye kikao na Mkapa .Swali kwani Mkapa bado yupo kazini?au Kikwete kakosa wasaidizi wakumsaidia ili amwache mkapa apumzike.Nimeshangaa!!!ni hilo tu
 
Hivi na zile data za Wiki Leaks za watu waliojilimbikizia pesa Uswiss zinatoka lini? Wiki mbili bado?? Upopo ume-point out "the two influential people" automatically nikakumbuka wiki leaks na pesa za Geneva (Do not ask me why).
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa tano usiku ITV Kikwete anaonekana kwenye kikao na Mkapa .Swali kwani Mkapa bado yupo kazini?au Kikwete kakosa wasaidizi wakumsaidia ili amwache mkapa apumzike.Nimeshangaa!!!ni hilo tu

Uliza maswali ya akili kidogo basi mkuu! rais wa nchi akimaliza muda wake still anatumika katika issues nyingi tu za kimataifa! Nyerere alikuwa msuluhishi baada ya kumaliza muda wake na kazi nyinginezo nyingi, akina Mbeki, Mandela, mawaziri wakuu!

You mean mtu akiwa rais na miaka 40 akamaliza muda wake wa miaka mitano then aruhusiwi kui-attach na kazi yeyote ile??

swali lako halina kichwa wala miguu!
 
Ameamua kukumbuka shuka wakati kuna kucha. Anajua mzee mkapa ni genius hivyo anatka amsaidie hata english tu ili apunguze swa-english yake.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumapili, Februari 20, 2011, kwenda Nouakchott, Mauritania, kushiriki katika Mkutano wa wakuu wa nchi sita za Afrika waliopewa jukumu la kutafuta suluhisho la kisiasa katika nchi ya Afrika Magharibi ya Ivory Coast.

Mkutano huo wa kundi la nchi zinazojulikana kama High Level Panel for the Resolution of the Crisis in Ivory Coast utamshirikisha Rais Kikwete na marais wenzake wa Mauritania, Burkina Faso, Chad, Afrika Kusini, Equatorial Guinea ambayo inashikilia uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa sasa na, Nigeria ambayo ni uenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

Baada ya kumalizika kwa mkutano wa leo, kesho viongozi wa nchi zote sita wa kundi hilo watasafiri kwenda Abidjan, Ivory Coast ambako watakutana na viongozi hao wawili wa Ivory Coast wanaovutana kuhusu uongozi wa nchi hiyo.

Kundi la nchi hizo sita lilichaguliwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, mwezi uliopita kutafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa katika Ivory Coast ambao ulizuka baada ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Novemba 29, mwaka jana.

Katika kura zilizopigwa katika raundi ya pili ya uchaguzi mkuu huo kati ya aliyepata kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Alassane Quattara, na Rais Laurent Gbagbo, Bw. Quattara alitangazwa kuwa mshindi na Tume Huru ya Uchaguzi ya nchi hiyo kwa kupata asilimia 54.1 kulinganisha na asilimia 45.9 za Rais Gbagbo aliyekuwa anatetea kiti chake.

Matokeo hayo yalithibitishwa na Ujumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa katika Ivory Coast, ambao ulipewa jukumu la kusimamia na kuhakikisha unafanyika uchaguzi huru na wa haki nchini humo kulingana na Makubaliano ya Linas-Marcoussis ya mwaka 2004 na, kwa mujibu wa Makubaliano ya Kisiasa ya Ouagadougou ya mwaka 2007. Matokeo hayo pia yanakubaliwa na jumuia ya kimataifa, Umoja wa Ulaya (EU), Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), na Umoja wa Afrika (AU).

Hata hivyo, Baraza la Katiba la nchi hiyo lilibatilisha matokeo hayo, likafuta matokeo ya kura kutoka majimbo saba ya kaskazini mwa Ivory Coast ambako ndiyo ngome ya Quattara na hatyimaye kumtangaza Bw. Gbagbo mshindi.

Kutokana na hali hiyo, kila upande ulitangaza Serikali yake hata kama vyombo vya habari vya serikali, jeshi, utumishi wa umma na taasisi nyingine nyeti za Serikali zinabakia kwenye udhibiti wa Bw. Gbagbo.

Mkutano wa kutwa leo mjini Noaukchott utafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania Mheshimiwa Mohamed Ould Abdel Aziz na viongozi wote sita wanaoshiriki katika mkutano huo wanatarajiwa kutoa maneo ya ufunguzi.

Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
.
Dar es Salaam
.
20 Februari, 2011
 
That is JK at his best, mambo ya banana republic katika Africa sasa imekuwa ni fashion,hivi sasa huko Ugandans hali ni tete kuna mvutano katika uchaguzi mkuu kwa mbalimbali unaendaendana na ule wa Tz 2010, sijui itakuwaje mpinzani wa Mu7 kasema kama vp anitisha maandamano nchi nzima kama Tunisia na Misri, labda JK anaweza akaitajika huko.
 
kama nchi tunatakiwa kujifunza kuwa kumpa mtu wa Pwani urais wa nchi ni kosa kubwa la kujutia
 
Jamani nchi yetu si bado hata wahanga hawajazikwa?

Mie naogopa tena, sisemi zaidi.

Ahsante Max kwa taarifa ila inauma.
 
Ngoja tumuangalie mzee mzima JK tuone ka yeye alishinda kwa haki, basi ataweza kuwa wa kwanza kumponda mawe mwenzie. Si mnakumbuka enzi za Kenya alivyo jipeleka kifua mbele mbele. Saa hii laana itamtafuna!
 
Kaongeza Mauritania kwenye nchi alizotalii. Nadhani next uvumbuzi itakuwa Equatorial Guinea
 
kama nchi tunatakiwa kujifunza kuwa kumpa mtu wa Pwani urais wa nchi ni kosa kubwa la kujutia

Mkubwa sio watu wote wa Pwani tuko kama Fisadi Kikwete kwani hata huko bara mnao wengi watu wa dizaini ya Fisadi Kikwete tena wapo wengi kuliko Huku kwetu Pwani. List ya Mafisadi wa bara tena wakuogopwa kama ukoma ni Lowassa, RA nadhani huyu unamuwaza kila siku pale Tanesco wanakuadhibu takribani 22hrs bila ya mwanga, Chenge na list imalizie wewe wenyewe mkuu, huku Kwetu tunao lakini sio wengi tuna Kigoda, Mkapa huyu sio mgeni kwako nanzani unamjua kuwa ndio Architecture wa Ufisadi wa kuuza mali za umma na wengineo pia ukipenda unaweza kuwamalizia.

Kikubwa zaidi Mtalii wetu au waziri wetu wa Utalii na Urasi wa kuchakachua ndio ameshaondoka kwenda kula raha Huko Kwenye Jangwa. Ameshachoka kukaa magogoni kupart sasa amealikwa kwenye party nyingine za kwenda kuonyesha jinsi watu wanvyochakachua uchaguzi bila ya nchi nyingine kupiga kelele kama yeye alivyofanya.

Kwa Ufupi ameenda kutoa Elimu ya uchakachuaji

:mvutaji:
 
Sawa, lakini it is a pity that mkutano wao utaishia kuja na brief- cases zao zimejaa "ifs" na kukubaliana kutokukubaliana. Hakuna cha maana kitakachotoka hapo sana sana ni kumsimika power monger dictator mwenzao au waziri mkuu kama Tsvangirai, Odinga etc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom