Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

Safari ni muhimu kwa manufaa ya nchi yetu kimaendeleo...muwe na subira mtaona matunda yake

Suala ni gharama anazotumia kwa hizo safari na nini tunapata..
 
ukickia raic wa chna kasafir,ujue kenda kutafuta masoko,vyeo vya kipumbav hawatak,
 
Ahh well acha aende tu!Labda kuna umuhimu..labda hamna ila ndo hivyo tena!Binafsi angehamia huko angenifurahisha zaidi!
 
MHE. RAIS SAFARINI GENEVA, DAVOS NA ADDIS…!!!
January 24th, 2011

What a President... never like to live in HOT Dar-es-salaam?

RaisJakayaKikwete4-7119281.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa leo, Jumatatu, Januari 24, 2011, kwenda Uswisi ambako atakuwa na shughuli muhimu za kikazi katika miji ya Geneva na Davos.

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa Tume ya Kimataifa Kuhusu Afya ya Akinamama na Watoto.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa (UN) inaongozwa kwa pamoja na Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada, Mheshimiwa Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Tume hiyo.

Kazi ya kwanza ya Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper katika Tume hiyo itakuwa ni uzinduzi wa Tume yenyewe utakaofanyika keshokutwa kwenye Jengo la Salle de Presse, ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Uzinduzi huo utafuatiwa na kikao cha kwanza cha Tume kitakachofanyika kwenye Chumba cha Mikutano cha Bodi ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper wataongoza kikao hicho cha siku moja kujadili kwa undani kazi na wajibu wa Tume yenyewe, matokeo yanayotarajiwa kutokana na Tume hiyo ya kitaifa.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imeundwa kwa minajili ya kuweka mfumo wa kuyasaidia mataifa kuangalia upya afya ya akinamama na watoto kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG's) pamoja na kuainisha hatua za jinsi ya kupima mafanikio katika eneo hilo, na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kuboresha upatikana wa habari kuhusu afya ya akinamama na watoto.

Baada ya mkutano huo wa Geneva, Rais Kikwete atakwenda katika mji mdogo wa Davos ambako kwa siku mbili atahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) wa mwaka huu.

Mbali na kuhudhuria shughuli za WEF kwa mwaka huu, Rais Kikwete atashiriki katika tukio muhimu sana la uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Maeneo ya Kilimo Kusini mwa Tanzania (South Agricultural Growth Corridor of Tanzania – SAGCOT).

Mpango huo wa aina yake utatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania, washirika wa maendeleo wa Tanzania, sekta binafsi na mashirika makubwa ya kusaidia maendeleo duniani ikiwamo Benki ya Dunia, na utalenga kuwatoa mamilioni ya wakulima wa Tanzania katika umasikini.

Rais Kikwete ataondoka Davos, Jumamosi, Januari 29, 2011, kurejea nyumbani na akiwa njiani, atasimama mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika (AU). Rais Kikwete atakuwa mjini Addis Ababa kwa siku tatu na atarejea nyumbani Februari 2, 2011.

Hivi vyeo wanajotolea au wanachaguliwa? Kwa nini maraisi makini kwa maendele ya nchi zao kama Mwai Kibaki, Yoweri Museveni, na Kagame wa Rwanda hawahangaiki na hivi vyeo vya kimataifa? Tuna matatizo chungu nzima yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi chini ya usimamizi wa Raisi wetu lakini yeye anakazana na mambo ya kimataifa wakati tunataabika huku nyumbani. Ni aibu sasa kuwa siku hizi hatuna tena ari ya kuwauliza watoto wetu wamefundishwa nini shuleni au kuangalia homework zao kwa kuwa hakuna imeme, hili tatizo Raisi amekuwa nalo toka January 2006 na pengine 2015 ataliacha hivyo hivyo bila ya ufumbuzi.

Mimi nadhani uzalendo uanze nyumbani maana kuzungumzia vifo vya mama na mtoto katika ngazi ya kimataifa wakati nyumbani hakuna umeme mahospitalini na kama umeme hakuna hata kupamp maji kwenda mahospitalini ni tatizo litakaloongeza vifo vya mama na mtoto
 
MHE. RAIS SAFARINI GENEVA, DAVOS NA ADDIS…!!!
January 24th, 2011

What a President... never like to live in HOT Dar-es-salaam?

RaisJakayaKikwete4-7119281.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa leo, Jumatatu, Januari 24, 2011, kwenda Uswisi ambako atakuwa na shughuli muhimu za kikazi katika miji ya Geneva na Davos.

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa Tume ya Kimataifa Kuhusu Afya ya Akinamama na Watoto.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa (UN) inaongozwa kwa pamoja na Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada, Mheshimiwa Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Tume hiyo.

Kazi ya kwanza ya Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper katika Tume hiyo itakuwa ni uzinduzi wa Tume yenyewe utakaofanyika keshokutwa kwenye Jengo la Salle de Presse, ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Uzinduzi huo utafuatiwa na kikao cha kwanza cha Tume kitakachofanyika kwenye Chumba cha Mikutano cha Bodi ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper wataongoza kikao hicho cha siku moja kujadili kwa undani kazi na wajibu wa Tume yenyewe, matokeo yanayotarajiwa kutokana na Tume hiyo ya kitaifa.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imeundwa kwa minajili ya kuweka mfumo wa kuyasaidia mataifa kuangalia upya afya ya akinamama na watoto kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG's) pamoja na kuainisha hatua za jinsi ya kupima mafanikio katika eneo hilo, na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kuboresha upatikana wa habari kuhusu afya ya akinamama na watoto.

Baada ya mkutano huo wa Geneva, Rais Kikwete atakwenda katika mji mdogo wa Davos ambako kwa siku mbili atahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) wa mwaka huu.

Mbali na kuhudhuria shughuli za WEF kwa mwaka huu, Rais Kikwete atashiriki katika tukio muhimu sana la uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Maeneo ya Kilimo Kusini mwa Tanzania (South Agricultural Growth Corridor of Tanzania – SAGCOT).

Mpango huo wa aina yake utatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania, washirika wa maendeleo wa Tanzania, sekta binafsi na mashirika makubwa ya kusaidia maendeleo duniani ikiwamo Benki ya Dunia, na utalenga kuwatoa mamilioni ya wakulima wa Tanzania katika umasikini.

Rais Kikwete ataondoka Davos, Jumamosi, Januari 29, 2011, kurejea nyumbani na akiwa njiani, atasimama mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika (AU). Rais Kikwete atakuwa mjini Addis Ababa kwa siku tatu na atarejea nyumbani Februari 2, 2011.

Hivi vyeo wanajitolea au wanachaguliwa? Kwa nini maraisi makini kwa maendeleo ya nchi zao kama Mwai Kibaki, Yoweri Museveni, na Kagame wa Rwanda hawahangaiki na hivi vyeo vya kimataifa? Tuna matatizo chungu nzima yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi chini ya usimamizi wa Raisi wetu lakini yeye anakazana na mambo ya kimataifa wakati tunataabika huku nyumbani. Ni aibu sasa kuwa siku hizi hatuna tena ari ya kuwauliza watoto wetu wamefundishwa nini shuleni au kuangalia homework zao kwa kuwa hakuna umeme, hili tatizo Raisi amekuwa nalo toka January 2006 na pengine 2015 ataliacha hivyo hivyo bila ya ufumbuzi.

Mimi nadhani uzalendo uanze nyumbani maana kuzungumzia vifo vya mama na mtoto katika ngazi ya kimataifa wakati nyumbani hakuna umeme mahospitalini na kama umeme hakuna hata kupampu maji kwenda mahospitalini ni tatizo litakaloongeza vifo vya mama na mtoto
 
Jamani mwacheni akapunguze stress, angalau saivi kapunguza punguza!
 
Tatua kwanza tatizo moja kikwete acha kuwa bogasi wewe.ina maana huna washauri?we mbona likishazukaga suala serious huwa hukai we ni kukimbiakimbia tu?hivi ulifundwa japo kuwa baba kweli?sasa hao kina mama na watoto unaoenda kuwawakilisha kwenye giza ni wachawi au?unatutia aibu bure wananchi maliza kwanza suala la umeme ndo ukazurure duwange wewe.
 
They say "The Most s**pd president in Africa is the most respected in Europe.!" U know why?
 
Jamani mwacheni akapunguze stress, angalau saivi kapunguza punguza!


ngoja aende,akirudi atakuta Operation Sangara imetanda nchi nzima.Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo i wish you never come back.
 
Safari ni muhimu kwa manufaa ya nchi yetu kimaendeleo...muwe na subira mtaona matunda yake

Safari anazo enda kuomba net za mbu ndio za muhimu? Kwani malipo ya dowans hayatoshi ku-subsidize tupate net za bure?
 
Sindbad a.k.a. Vasco da Gama. Tumsamehe bure anaenda kuchakachua damu,wadudu wamechanganya sana ndiyo maana anashindwa hata kutoa tamko juu ya Dowans, si unajua ugonjwa ule ukishafika kichwani?
 
Ni vigumu kuelezea rais wa Tanzania anahudhuria warsha ya akinamama na watoto katika ngazi ya kimataifa wakati nyumbani kwake hawezi hata kuongelea kwenye TV ya taifa maana ni matatizo mpaka huwezi kuelezea maana hata alidhiriki kwenye kampeni kusema akishinda atatoa bajaji kwa ajili ya akinamama wakati wa kujifungua na mpaka sasa hata hizo bajaji hazijaonekana japo hospitali ni chache na wahudumu ni wachache pia

Nchi haina umeme,kila pande ya nchi ni maandamano halafu raisi anahudhuria vikao vya kimataifa Jamani watanzania bado tunasema yote shwari?

Tunaomba hata washauri wake wamshauri hata ajaribu kuwatembelea akina Kibaki,Mseveni,na Kagame labda atajirekebisha maana hajui kama anawakera watanzania kwa safari ambazo hazina faida kwa taifa
 
Tukuulize wewe kwamba ukoje? Hivi nyie mnadhani Rais ni kukaa tu nyumbani? Kama ni hivyo basi hata Rais Ben Ali angekuwa Rais bora au Mugabe. issue hapa siyo kusafiri maana hata baba wa Taifa enzi zake alisafiri sana, na hivyo hivyo mzee Ruksa na hata mzee Mkapa. Hiyo ni sehemu ya kazi za Rais na ndiyo maana hata marais wa nchi zilizoendelea kama China wanafanya ziara za dunia nzima na huko kote ni kuitangaza agenda ya nchi yako! Malalamiko mengine tunayazidisha na inaonekana sasa mzee huyu hata afanye zuri namna gani haonekani! Hiyo sasa CHUKI BINAFSI!

Nadhani akirudi huwa anakuletea chokoleti na pipi wewe....watu wanahoja TIJA ya hizi safari zake na wala sio suala la Rais kusafiri ambalo halina hoja....Mwalimu alisafiri akaleta Mtera...huyu akaleta Dowans sasa ulinganifu uko wapi?
 
Gud! Excellent!! tunahitaji hewa sasa ya kufanya VITUZZZZ Vyetu!! we actually needed some space....phew! all ze best if best is the best to say and wish!!!
 
Back
Top Bottom