Safari za nje za Mhe. Rais Kikwete 2010 - 2015

Jamaa ana lengo la kuzunguka Dunia nzima. Ikiwezekana tupate hata zile safari alizofanya 2005 - 2010, ili ifikapo Oct, 2015 tufanye evaluation.
 
MHE. RAIS SAFARINI GENEVA, DAVOS NA ADDIS…!!!
January 24th, 2011

What a President... never like to live in HOT Dar-es-salaam?

RaisJakayaKikwete4-7119281.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa leo, Jumatatu, Januari 24, 2011, kwenda Uswisi ambako atakuwa na shughuli muhimu za kikazi katika miji ya Geneva na Davos.

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa kwanza wa Tume ya Kimataifa Kuhusu Afya ya Akinamama na Watoto.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa (UN) inaongozwa kwa pamoja na Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada, Mheshimiwa Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Tume hiyo.

Kazi ya kwanza ya Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper katika Tume hiyo itakuwa ni uzinduzi wa Tume yenyewe utakaofanyika keshokutwa kwenye Jengo la Salle de Presse, ambao pia utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon.

Uzinduzi huo utafuatiwa na kikao cha kwanza cha Tume kitakachofanyika kwenye Chumba cha Mikutano cha Bodi ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Rais Kikwete na Mheshimiwa Harper wataongoza kikao hicho cha siku moja kujadili kwa undani kazi na wajibu wa Tume yenyewe, matokeo yanayotarajiwa kutokana na Tume hiyo ya kitaifa.

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imeundwa kwa minajili ya kuweka mfumo wa kuyasaidia mataifa kuangalia upya afya ya akinamama na watoto kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) pamoja na kuainisha hatua za jinsi ya kupima mafanikio katika eneo hilo, na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kuboresha upatikana wa habari kuhusu afya ya akinamama na watoto.

Baada ya mkutano huo wa Geneva, Rais Kikwete atakwenda katika mji mdogo wa Davos ambako kwa siku mbili atahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani (World Economic Forum) wa mwaka huu.

Mbali na kuhudhuria shughuli za WEF kwa mwaka huu, Rais Kikwete atashiriki katika tukio muhimu sana la uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Maeneo ya Kilimo Kusini mwa Tanzania (South Agricultural Growth Corridor of Tanzania – SAGCOT).

Mpango huo wa aina yake utatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania, washirika wa maendeleo wa Tanzania, sekta binafsi na mashirika makubwa ya kusaidia maendeleo duniani ikiwamo Benki ya Dunia, na utalenga kuwatoa mamilioni ya wakulima wa Tanzania katika umasikini.

Rais Kikwete ataondoka Davos, Jumamosi, Januari 29, 2011, kurejea nyumbani na akiwa njiani, atasimama mjini Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa mwaka huu wa Umoja wa Afrika (AU). Rais Kikwete atakuwa mjini Addis Ababa kwa siku tatu na atarejea nyumbani Februari 2, 2011.
 
Nilijua sana huyu miguu ilivyokua inamwasha kukwea pipa kwenda mahala akakyepe joto la Dar na harufu mbaya ya samaki pale ferry Magogoni!!!!
 
Afadhali asafiri tupunzike kuzikiliza matamko maana akiondoka inchi inakuwa na nidhamu kidogo. Lakini hii mikutano mitatu ni halali yake kuhudhuria angalau aka-refresh mind maana CDM mmempa wakati mgumu tangu kampeni za uchaguzi zianze mpaka sasa.
 
Kwa intelejensia ya Mwema na wenzake inasemekana Kikwete ameenza kutembeza kopo la ombaomba, Kazi imeanza ya kuomba. Sio mimi nilosema hivyo bali ni INTELEJENSIA YA MWEMA:).

Kikwete tembeza tembeza kopo maana kuna deni la Dowans linahitajika kulipwa na wadanganyika wanaligomea tembeza tembeza baba
 
Kwenye kutembeza huko hilo likopo kamwe asitumie jina letu kwani sisi hatukumchagua kwa wadhifa huo anaousafiria kila kona ya dunia.
 
Atakaporejea nyumbani mh rais Dr mara 5 atapokea taarifa na stakabadhi halali ya malipo ya Dowans.
 
Huyu mtu hana hata haya mimi ananiudhi hivi ukoje wewe usiyesikia jamani?????
 
Huyu mtu hana hata haya mimi ananiudhi hivi ukoje wewe usiyesikia jamani?????

Tukuulize wewe kwamba ukoje? Hivi nyie mnadhani Rais ni kukaa tu nyumbani? Kama ni hivyo basi hata Rais Ben Ali angekuwa Rais bora au Mugabe. issue hapa siyo kusafiri maana hata baba wa Taifa enzi zake alisafiri sana, na hivyo hivyo mzee Ruksa na hata mzee Mkapa. Hiyo ni sehemu ya kazi za Rais na ndiyo maana hata marais wa nchi zilizoendelea kama China wanafanya ziara za dunia nzima na huko kote ni kuitangaza agenda ya nchi yako! Malalamiko mengine tunayazidisha na inaonekana sasa mzee huyu hata afanye zuri namna gani haonekani! Hiyo sasa CHUKI BINAFSI!
 
Tukuulize wewe kwamba ukoje? Hivi nyie mnadhani Rais ni kukaa tu nyumbani? Kama ni hivyo basi hata Rais Ben Ali angekuwa Rais bora au Mugabe. issue hapa siyo kusafiri maana hata baba wa Taifa enzi zake alisafiri sana, na hivyo hivyo mzee Ruksa na hata mzee Mkapa. Hiyo ni sehemu ya kazi za Rais na ndiyo maana hata marais wa nchi zilizoendelea kama China wanafanya ziara za dunia nzima na huko kote ni kuitangaza agenda ya nchi yako! Malalamiko mengine tunayazidisha na inaonekana sasa mzee huyu hata afanye zuri namna gani haonekani! Hiyo sasa CHUKI BINAFSI!

Tatizo aliishaharibu mwenyewe sasa hata afanye mazuri kiasi gani hakuna hata moja linaloonekana zuri pamoja na kuwa machoni mwa watu wengine linaweza kuwa zuri
 
Safari ni muhimu kwa manufaa ya nchi yetu kimaendeleo...muwe na subira mtaona matunda yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom