Safari za Kikwete zazaa matunda...

Safari za Kikwete zazaa matunda...

Nasikia jamaa huwa anakuja na ndege imejaa mosquito net na anapisha angani na ndege zilizojaza madini na miongoni mwa mafanikio yake ni pamoja na kuwaletea watoto net zinazowasaidia kama hivi

ile ndege mh anayopishana nayo ikibeba madini  huku kirudi na ..............jpg
 
Kwani tatizo la Tanzania sasa hivi ni uchache wa walimu? Gharama zote zile za kusafiri tumsifu kwa kupewa walimu? We are not serious.
 
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.

Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,

Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.

Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.

Madini yote wanayovuna ni sawa waalimu 47???? Sasa unajisifu nini.... Hivi kweli tumeshindwa kuwapata waalimu 47? kwa miaka yote hawa jamaaa wanachukua gesi na madini????
 
WANAKUJA PIA NA MAABARA ZAO???? Maana kwa ninavyofahamu mimi Sayansi bila maabara ni bure...........lkn kumpongeza kwa KUOMBA NI MUAROBAINI??? au tunatakiwa kuzalisha wakwetu????
 
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.

Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,

Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.

Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.

Bwana Zomba hii ni program ya Peace Corps ambayo huleta volunteers(waalimu) kila mwaka.Haitokani na ziara za Rais Kikwete
 
Madini yote wanayovuna ni sawa waalimu 47???? Sasa unajisifu nini.... Hivi kweli tumeshindwa kuwapata waalimu 47? kwa miaka yote hawa jamaaa wanachukua gesi na madini????

Hayo madini wanavuna nyie mmelala? hivi kweli aje afyeke, aanze kuchimba, wewe unamtazama tu? huo ni ujinga wa hali ya juu.
 
Hayo madini wanavuna nyie mmelala? hivi kweli aje afyeke, aanze kuchimba, wewe unamtazama tu? huo ni ujinga wa hali ya juu.

Umewasahau wale watu waliopigwa Risasi Mara na sehemu zingine, umewasahau wale watu waliofukiwa Bulyanghulu???/, Umewasahau watu waliopigwa Risasi kigamboni juzi kisa kuwapa hadi machimbo ya Kokoto wawekezaji wa Kihindi????

Unaongea nini??? Mbona kama si mTZ????,,

Hivi ni watu wangapi wanapata ulemavu au kuuawa kwa ajili ya kupinga unyanyasaji wa serikali ya kifisadi ya CCM unayoitetea na kuisifia.

Ipo siku itafika na nyiye mtakuwa meshikilia makali huku wanyonge wakiwa na mipini.
 
Mwekezaji ni mwekezaji awe mhindi au mmerekani au mbantu. Jana niliona tv hapa Dar vijana wamevamia na kuvunja nyumba za watu kisa eti wao hawajengewi, khaa, huo sasa kama si ujinga ni nini?

Hizo kokoto unazosema mlikuwa hamjaziona kabla ya kuja mwekezaji? mbona hamjazichimba, mwekezaji kaja anachimba ndio mumletee fujo? wacheni zenu hizo, uchumi mnao mnaukalalia, wakija wanaojuwa kuuzalisha mnawaonea wivu.

Ngojeni Wamerekani waje kuwafundisha science ni nini. Si unaiona ile USA ilivyotajiri? wote ni watu wa nje wale, ndio walioijenga ile nchi na kuwa giant, wenyewe wenyeji wamewekwa kwenye hifadhi za taifa, wale, wanywe wakachukuwe posho, wanaoweza fursa zipo.

Na hapa ndio hivyo hivyo, tuibe, tule, tunywe (msiba tunywe, harusi tunywe), tucheze, tusifanye kazi, wakija wawekezaji tulalamike. Haya kachimbe na vidole ulizuiliwa? Hata sururu hujui kutengeneza unategemea hao hao wa nje, halafu unataka kuleta mdomo.

Hivi hii ardhi hapa ilivyo nzuri hata kulima kunatushinda halafu tukiletewa wataalaam wakapewa sehemu za kulima tujifunze, sisi tunakwenda kuwaibia halafu kulalamika. Maendeleo bila hawa wageni sahau.

Wacha Kikwete awaletee hawa mjifunze, mmeshindwa kila kitu, mmeuwa kila kitu. Huko mnasomeshwa au mnajazwa ujinga? Miaka yote tunaambiwa elimu inatoka huko St. Kayumba na kubenea, vipi, mbona haitusaidii?
 
Bwana Zomba hii ni program ya Peace Corps ambayo huleta volunteers(waalimu) kila mwaka.Haitokani na ziara za Rais Kikwete
Sio walimu tu bali Peace Corps hujumuisha watu wa kilimo, mazingira na ustawi wa jamii. Kwa kawaida hawa jamaa huwa sio walimu kwa taaluma bali hupenda kufundisha kwa sababu huwa na majukumu mengine mengi sana. Na ukibahatika kuona taarifa wanazozipeleka kwao kila mwezi unaweza ukamchukia hata huyo anayewasifia hapa kama zuzu! Nilibahatika kufanya kazi na hawa jamaa kwa miaka sita hakika sikuwapenda hata kidogo. Kwanza huwa hawana uwezo wa kufundisha, huwa kuna matatizo ya lugha na mawasiliano pia huwa kuna matatizo ya syllabus ambayo huwa hawawezi kufundishia kwa madai kwamba huwa ni "too much demanding". Huwa wana kaa nchini kwa kipindi cha miaka miwili tu. Sasa mwenzetu anaamini Kikwete amepiga bingo......Lo ujinga na umaskini ni kitu kibaya sana. Peace Corps wamekuwepo nchini tangu miaka ya 60 mara baada ya kupata uhuru kwa malengo mengi tu ikiwemo na kupambana na kuenea kwa ukomunisti na kueneza ubeberu wa kimarekani kupitia elimu.
 
Walikuwepo kabla ya Nyerere na Keneddy au hulijui hilo?

Sasa kama unakubali walikuwepo iweje unaona ni matunda ya asafari za JK?

Mhh... ama kweli swaumu! Vumilia zomba juma1 au juma2 yaweza kuwa kama kawa...
 
Hayo madini wanavuna nyie mmelala? hivi kweli aje afyeke, aanze kuchimba, wewe unamtazama tu? huo ni ujinga wa hali ya juu.
Upo sahihi kabisa maana serikali ya wajinga inayoongozwa na raisi dhaifu ndio inayowaalika,kuwamilikisha migodi na kuwalinda ili wavune mali za wajinga ambao wakiamua kudai haki zao serikali ya wajinga huwajibu kwa bunduki na maji ya kuwasha. Bravo mr.Zoba kwa uchambuzi wako!
 
Mnaotawaliwa na wenye sifa hizo mkoje? mmekufa?
 
Tanzania-has-been-receiving-US-Peace-Corps%E2%80%99-volunteers-every-year.jpg

[h=3]The government of United Republic of Tanzania has received 47 US teachers who will join with other Tanzanian Secondary school teachers to teach in schools allocated[/h]
 
Hiyo Heading ya topic yako umeandika kama Magazeti ya UDaKu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom