Safari za Kikwete zazaa matunda...

Safari za Kikwete zazaa matunda...

kwa taarifa yako hesabu huwezi kukariri na hapa nazungumzia pure advance mathematics yule mwalimu alikuwa anasolve hesabu kwenye computer lakini akija darasani alikuwa anashindwa kuzisolve na pia kuelewesha wanafunzi amewezaje kupata hayo majibu ndio maana nakwambia wacha kukurupuka
 
kwa taarifa yako hesabu huwezi kukariri na hapa nazungumzia pure advance mathematics yule mwalimu alikuwa anasolve hesabu kwenye computer lakini akija darasani alikuwa anashindwa kuzisolve na pia kuelewesha wanafunzi amewezaje kupata hayo majibu ndio maana nakwambia wacha kukurupuka

Kwa hiyo na wewe hujui hesabu, maana mwalimu wako alikuwa hajui hesabu.
 
Wewe nawe pumba zote za nini. Caliber ya juu unataka kwenda mwezini? hata sindano hujui kutengeneza?

Wehu si fani ya kujivunia.Huo mfano wa sindano ni wa kijinga na wa longtime sana.Sindano ipi siwezi?Unaamisha kuwa aina ya materials zilivyoutimika kutengeneza baadhi ya sindano au siwezi tengeneza?Kama ni Materials utakuwa kichaa zaidi ya hapo.Material zinazohitaji machine za hela nyingi ni wengi hatuna.Hata Apple pamoja na kuwa vitu kibao huwa wana subcontract.Mojawapo ni processor za Intel.Otherwise fuga mdomo ukalale, dukani kuna sindano kibao za cust iron, za still, na nyingine vyuma vya kawaida tuu(vinakuwa coated).Nadhani kama huna nazi kichwani unaweza ona jinsi gani kijana yoyote akiyewahi cheza kwa kutumia vitu alivyotengenza mwenyewe anavyoweza fanya ina matter of minutes.Wewe nadhani umecheza enzi za kununuliwa madoli na kuangalia "ze comed" hata ukiangalia movie kwa bahati mbaya huwa matukio mengi, vitu vingi huwa hureason possibilities za hivyo kuwepo au kufayika.

Sasa ya nini hutaki calibre ya juu kwanini?unataka blah blah?Hujui kuwa usipokuwa na mpangilio huwezi pata the best katik msaada wowote.sasa intern wa sayansi anayekuja hapa halafu anakuwa kilaza kuliko mwanafunzi wetu wa university wa nini sasa?Si bora vijana waingie field kipindi cha likizo.Pawe na program ya kuwa brush kabla ya kuingia field.Kwa taarifa yako nimekupa MIT nikasema na wengine kwa vile hao jamaa wanato aproducts kam viwanda vile.Wao kila wakifundishacho wanafunzi wao kwa ushirika na walimu wo huwa wanakitengeza.Na hawa jamaa wamecopyright na kuweka patent kibao na Kila siku wana ongeza.Hawa jamaa WANA LICENCE MAAALUMU KWA AJILI YA TAALUMA na hivyo ni rahisi kutumie technologia zao za ubora wa kibiashara bure.KUFUNDISHWA NA HAO WATAAFU NA WAGUNDUZI WA HIZO TECHNOLOGIA KUNATUSAIDIA KUPATA KITU BORA TOKA KWA WABUNIFU WAKE.watu wa literature wanakuambia kuwa 'from the horse`s mouth'.

Kwa vile huwa zaidi ya kusoma mambo ya siasa za maji taka huwezi jua MTI,Stanford Uni etc katika website zao wanaweka projects kibao,katika video, code, descriptions,tutorials etc.na kuna vyuo vikuu vinatoa elimu ya bure online na materials za fani yoyote zipo free na ya kiwango cha juu.Na hawa jamaa kwao elimu ni kama dini .Ni kama kiongozi wa dini anavyopenda dini yake iongeze waumini,tena waumini imara ndivyo baadhi ya hawa watu walivyo.Sasa kama hayo hujui umshauri JK aweke wataalamu wapitie hayo ili waweze frame request zao, na kuweka plan za kuyafaidi hayo basi si mwenzetu.

Sikatai kuwa na hao wana mchango kwa wanafunzi wetu katika kujiamini, kujifunza tamamduni na mara chache kupata sayansi ya kweli, ingawa nao wana mwendo mrefu wa kufikia katik akuinua mafaniako kwa taifa kwani wengi huwa wanakumbana navitu vingi vy kuwabadili njia,kuhama nchi etc.Kwanini hawa wavumbuzi tusijitahidi watumia na kuja kuwabrush wana vyuoo wetu, wafanyakazi wa viwanda kushuka chini?kwani hata wakitumia miezi 3 bado kwa mwana chuo ambaye anayo theory ila hajui kutengeneza robot,computer au kutengeneza program za utambuzi wa watu, au hata kujua ni vipi anaweza tengeneza chemical fulani.basi hawa jamaa wakija basi watawaambia nini kinahitajika na kinapatikana wapi, halafu wakatangeneza sample kadhaa za kuwafungua watu macho.baadaye hawa jamaa wanatoka walipokwama.
 
Kuna walimu wengi wazuri watanzania ambao walikuwa wanafundisha tution mmoja wao anaitwa Mwalimu Mrisho ndipo nilipokuwa naenda kupata nondo Pili sijasema hajui hesabu ila namna ya ufundishaji wake maana alikuwa anafanya kila kitu kwenye computer lakini akija darasani alikuwa anashindwa kutuelewesha ndio maana nikasema sysytem yao haiendani na ya kwetu lakini kwa wale waliofundishwa na walimu toka uk na urusi ya zamani walikuwa hawapati tatizo kama hilo kumbuka elimu yetu imefata mfumo wa uk
 
Mbona husemi ya Bill Gates:

President Jakaya Kikwete officially opened (UDOM University of Dodoma) yesterday, student capacity of 45,000 compared with UDSM (University of Dar es Salaam) student capacity of 20,000. UDOM is MASSIVE, you need to travel by car between faculties. Kikwete striked a deal with Bill Gates in building an IT Center of Excellent at UDOM.

UDOM will change Dodoma for sure.

Source: Dodoma | Tanzania | City Gallery - Page 2 - SkyscraperCity
.
Shida yako watu waki descuss kitu unakimbilia kutazama kwa macho yanayooona kuna JK anashambuliwa na wewe kazi yako kumlinda.

Hiyo Hiyo ya Bill Gate sijui hiyo deal ina content gani na hivyo siwezi predict success au failure yake.Ingawa niliisikia ila sijaweza pata full details."IT Center of Excellence" ni neno pana sana kutegemea na hiyo center inataka excell katika maeneo gani.Pia ujue kuwa Microsoft ni mojawapo ya notorius company linapokuja suala ku limit teknologia kuwa wazi kwa jamiii haswa kwa ule uelewa wa utengenezaji kuliko wa watumiaji na support ya kawaida.Mfano. wanaweza wafungue kituo kikubwa cha kuwafundisha watumiaji wa products zao wa level Normal users, na administrative users.Kuna faida zake kwa sehemu fulani katika taifa ila ukiangalia kwa makini ina faida kubwa sana katika kupanua soko la microsoft.Misaada ya japani ililenga kufanya product za kijapani kuwa maarufu sana.Leo hii karibu kila mtu akitaka nunua gari atakimbilia mojawapo ya toyota au mengine ya kijapani.Yes ,tuna wauzaji wakubwa, tuna mafundi wengi, tuna makampuni ya mtengenezo.Ila sijui kama kuna chochote kinachosaida kuunda magari yetu achilia mbali hata kutengeneza spare parts za toyota.South Africa wanafanya .

Amka ndugu yangu, tunahitaji tumia akili na ujanja wa hali ya juu kuwafanya hawa jamaa wakifungu avituo basi vijijenge kuweza fikia pa kuona tunapata wataalamu wetu wanofanya na microsoft deep kabisa, hadi katika ku deign windows, na vitu vingine ambavyo ni roho ya microsoft.Otherwise ni kama ukatoliki kuwa Tanzania bila kutoa Pope Mtz, au kuwa na ma-Sheikh bila uwezekano wa kutoa Sheikh mkuu wa Mecca.Ila wote wanaeneza dini zao kwa bidii na kama kuna micgango wanaiwakilisha.Kama ndivyo vitakavyotokea pale UDOM ,sidhani kama nahitaji kusema kuwa tupuuze,ila tusitemegee kunatufanya huru,ila kunatufanya tutumie bidhaa zao vizuri na kuwa waenezaji wazuri wa biashara yao.

Kwa kifupi ni kwamba kunaweza kuwa na matokeo kama vile Bill Gate ka stirke deal nakutendeka kama vile rais Microsoft itakuwa ndio supplier pekee wa software, na software zake zitapewa kipaumbele kuliko, na wasomi wetu watakuwa wainjilist wazuri wa bidhaa zao,watakuwa mashahidi wazuri wa bidhaa zao na microsoft kwa ukanda mzima wa africa mashariki na kati, na resources zetu zitatumika kufanya kazi zake.ndugu yangu India,china,Japan,Hong Kong etc walifanya kazi sana na ujanja wafanya hawa jamaa kuwaona kuwa wanaweza kuingia katika utengenezaji na kwa vile gharama zilishuka wakaona ni bora wafungue utengenezaji na si seminary za kuhubiri dini yao.HAPA RAIS ANAWEZA AMINI KAWASHIKA MICROSOFT NA MICROSOFT NAO WANASHANGAA DEAL LIMEPATIKANA KIRAHISI SANA.Kumbuka huyo Bill Gate wako namheshimu sana,kwani aliwahi toa jibu la kushangaza sana watu.Walipomuuliza kuhusu kuwepo kwa windows XP pirates kibao, ingawa wamefany ajuhudi kubwa sana kukamata maharamia.Alichojibu kilishangaza alipowaambia waliokuwa wakiiba ndio walikuwa wakipmataia faida kuliko wanaonunua.Wanaolewa wakajua kuwa hao ndio wanaoenza dini ya microsoft kwa kasi zaidi(kwani walionunua huwa wanaficha) na hivyo kufungua soko kubwa na lenye faida nono kwa bidhaa nyingine za microsoft.Soon mtajikuta ile kasi ya Linux ikipungua n akukimbilia certificate za microsoft ambazo nazo tuu ni hela la kumkamua m-TZ.Ndio nawasilisha mkuu wangu.
 
Ikiwa tutaziweka Rwanda shule zote zilizopo Tanzania, basi Rwanda watakosa nchi ya kufanyia shughuli zingine zozote. Usifananishe tikiti na zambarau. Unakijuwa kisa cha tikiti na zambarau?

Mbona kama hujaeleweka hivi,,,au wewe zombie ndo hujanielewa??nalinganisha mafanikio ya hawa viongozi wa hizi nchi mbili na mafanikio waliyoleta,strategy walizotumia n.k...hakuna aliyelinganisha ukubwa wa hizi nchi mbili maana hakuna la maana tutakalopata kwa kufanya hivyo..zaidi sana tutagundua kuwa tulitakiwa kuwa na spidi kubwa zaidi ya maendeleo kuliko tuliyonayo kama tungekuwa na uongozi imara na unaoweza kutupa modalities za ku-exploit resources nyingi tulizo nazo..
 
Mbona husemi ya Bill Gates:

President Jakaya Kikwete officially opened (UDOM University of Dodoma) yesterday, student capacity of 45,000 compared with UDSM (University of Dar es Salaam) student capacity of 20,000. UDOM is MASSIVE, you need to travel by car between faculties. Kikwete striked a deal with Bill Gates in building an IT Center of Excellent at UDOM.

UDOM will change Dodoma for sure.

Source: Dodoma | Tanzania | City Gallery - Page 2 - SkyscraperCity

UDOM>>Chuo kilichojengwa kwa fedha zilizoibiwa na serikali kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiongozwa na NSSF...yani huu wizi nao ni mafanikio ya kikwete jamani?si bora angekuwa amesign mkataba wa kurudisha hizi fedha za wastaafu tungesema ni muungwana??tangu kikamilike 2008 serikali haijalipa senti ya pango kwa mifuko hii inayosemekana itakuwa na uwezo wa kutulipa hapo tutakapofika miaka 55....wizi kabisa.

Unahitaji kuwa zombie tu kuunga mkono serikali hii ikiwa inafanya hivi.
 
Napita manzese yani mpaka raha naona shell ya mafuta ya lake oil eti ni ya ridhiwan jamani nzuri kweli hili nimeambiwa imejengwa eneo maalum kwa soko la machinga manzese........

CHAMA
SENGEREMA

Acha kutia shombo majina

Chama
Gongo la mboto DSM - in vacation Puerto Vallarta
 
Mbona kama hujaeleweka hivi,,,au wewe zombie ndo hujanielewa??nalinganisha mafanikio ya hawa viongozi wa hizi nchi mbili na mafanikio waliyoleta,strategy walizotumia n.k...hakuna aliyelinganisha ukubwa wa hizi nchi mbili maana hakuna la maana tutakalopata kwa kufanya hivyo..zaidi sana tutagundua kuwa tulitakiwa kuwa na spidi kubwa zaidi ya maendeleo kuliko tuliyonayo kama tungekuwa na uongozi imara na unaoweza kutupa modalities za ku-exploit resources nyingi tulizo nazo..

Uuuongelee na udikteta pia usiusahau.

Ku maintain nyumba ya vyumba 3 na nyumba ya vyumba kumi ni sawa? hata uwe tajiri kupindukia. Lazima nyumba ya vyumba kumi itakuwa na gharama zaidi. Na spidi ya Kikwete kwa hii miaka 7 hakuna Rais yeyote wa Afrika Mashariki, wa sasa na kabla yake aliyeifikia hata nusu, nakuuliza;

1) Ni yupi aliyeweza kuongeza life expectancy ya wananchi wake kwa zaidi ya mwaka mmoja kila mwaka kwa miaka saba mfululizo? (awe wa sasa au wa kabla yake yeyote yule).

2) Ni yupi aliyeweza kujenga vyuo vikuu zaidi ya kimoja kwa mwaka kwa miaka 7 mfululizo?

3) Ni yupi aliyeweza kuongeza barabara za lami kwa zaidi ya kilomita 1,000 kwa mwaka kwa miaka 7 mfululizo?

Hayo yote ni rekodi ya kutukuka mbali ya mashule ya sekondari kila kata, mbali ya zahanati kila kata, mbali vyuo vya ufundi vinavyochipuwa kila siku. Mbali ya mahoteli ya kitalii, bora duniani. Yes, bora duniani! mbali kwa mara ya kwanza tunaona wachimba madini wakilipa kodi za serikali, kwa mara ya kwanza tunatangaziwa kupatikana gas kwa wingi, unafikiri ilikuwa haijulikani kama ipo? inajulikana toka mwaka 1952, walikuwa wapi wa kabla yake? walikuwa wanakula tu fedha na kuvimbisha matumbo yao mpaka wanashindwa kutembea.

Kwa mara ya kwanza tunaona kwa makusudi kabisa somo la sayansi likitiliwa mkazo kwa vitendo. Ni juzi zimetangazwa kukamilika maabara 157 za shule za sekondari za kiwango cha kimataifa, na zingine zinaendelea mpaka zote shule 5,000 za sekondari alizojenga wakati wake zijitosheleze, dogo hilo? au hujui hilo?

Huyo Kagame wako kayafanya yote hayo? au yeyote wa kabla ya Kikwete Tanzania hii, alifanya hata nusu tu ya hayo? au zile cosmetics za juu juu mnazooneshwa? na juzi kaja kuchukuwa Watanzania wakamsaidie Mkonga wa Mawasiliano wa fiber optic ambao Kikwete kisha usambaza Tanzania nzima kwa muda mfupi aliokuwepo madarakani.

Usisikie humu watu wanapinga pinga hovyo, hao kawabania mianya ya kuiba kupitia sehemu zao wanaozijuwa ndio maana wanaleta chuki. Lakini kwa maendeleo ya Tanzania? hakuna zaidi yake wala wa kumlinganisha nae hii Afrika Mashariki, katutumikia kwa nguvu zaidi na anastahiki kila sifa.
 
UDOM>>Chuo kilichojengwa kwa fedha zilizoibiwa na serikali kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiongozwa na NSSF...yani huu wizi nao ni mafanikio ya kikwete jamani?si bora angekuwa amesign mkataba wa kurudisha hizi fedha za wastaafu tungesema ni muungwana??tangu kikamilike 2008 serikali haijalipa senti ya pango kwa mifuko hii inayosemekana itakuwa na uwezo wa kutulipa hapo tutakapofika miaka 55....wizi kabisa.

Unahitaji kuwa zombie tu kuunga mkono serikali hii ikiwa inafanya hivi.

Na hiyo mifuko ni ya Mbowe au Slaa? Nani aliyekwenda akashindwa kulipwa? Kikwete kawawekea dau pale, mambo yamebadilika pamekuwa pazuri, kabla ya Dau ilikuwa hata hujui mafao ni yepi na lini utayapata, wizi mtupu. Leo ukifika tu, kama una namba, majibu ni hapo hapo, instant. Bado mnataka kusema?
 
Nakumbuka tuliwahi kuwa na mwalimu wa kimarekani pale msalato, yule baba alikuwa akitufundisha out of syllubus kabisa. Basi kila tukijaribu kusolve past papers, tunashindwa kumbe alikuwa akitufundisha hesabu za chuo kikuu, lol. Tulipogundua tukaenda kuomba tusifundishwe naye, ikabidi arudi kwao. I tell you hawa wazungu wakiletwa hapa basi na mitaala ya elimu ibadilishwe ili waendane nao, La sivyo itakuwa ni 1+1-2=4
 
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.

Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,

Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.

Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.

Wale ni watalii sio walimu,wamekuja kuangalia namna bora ya kuvuna URANIUM toka kwenye nchi waliouziwa, fuatilia wanafunzi wanaokwenda kusoma marekani wa kidato cha tatu kwa mwaka mmoja wakirudi wanapelekeshwa sana na wenzao waliowaacha tanzania, timizeni na wapeni walimu wazawakipaumbele kwa kuwalipa stahiki zao na maslahi bora muone performance itakavyokuwa sio kupiga siasa tu
 
Wamekuja kwa makusudi kabisa kuboresha masomo ya science, au huelewi hilo?

Kufundisha, kutazama yanavyofundishwa na kisha kutoa ushauri.

We Zomba kweli unaona ni sahihi kuleta mamluki wa kuiangamiza elimu yetu kabisa!! Curriculum ya Tanzania ni tofauti na ya US, hawa walimu watafundisha kitu gani walichosoma US? Ukitazama hawa walimu kutoka US, mara nyingi wanakuwa shallow sana. Bora wangekuwa wametoka UK! Kuna ugumu gani kuandaa hawa walimu wa science na kuwalipa vizuri ili waweze kuitumikia Nchi yao?? Huku naona ni kuwapoteza kabisa watoto wa maskini. Hawa walimu wengi wanakuwa wanafundisha mamichezo tu!! Je hawa walimu watalipwa au kujitolea?? Zomba jiulize swali moja, "watafundisha mjini au ni hadi vijijini"? Kama watafika hadi vijijini, mtawaweka wapi, ni kule walimu wetu waliozea shida wanakoishi au?? Hapa mnazidi kutupoteza ndg yangu!!
Tujadili kwa kina Mkuu!
 
Kwani safari za rais ni miti mpaka zizae matunda?

Mbona kuna watanzania wengi wanaotafuta kazi za kufundisha hawapewi? Fedha zinazotumika katika safari zinatosha kuwaajiri zaidi ya walimu 47 wa Tanzania. Je hawa walimu wanaweza kuruhusiwa kuwafundisha watoto wa Kimarekani (huko kwao), au tumeletewa makapi kwa kuwa na serikali yetu ni makapi?
 
Hivi kati ya hao 47 uwiano wa dini ukoje!? maana yake wanawezaleta wa dini moja tu!

Mkuu haya mawazo ndio yamesababisha watu wakawa maskini..yaani bado mpaka leo unawaza kuajiri au kuajiriwa kwa misingi ya dini..kwani dini inauhusiana gani na skills za walimu wa sayansi..tuache ujinga
 
​
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliyemsindikiza katika uwanja wa ndege wa ,kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 16, 2012 muda mfupi kabla ya kuondoka kuekelea Msumbiji kuhudhuria mkutano wa SADC jijini Maputo
 
Hata aibu huna!!!!!!hivi waalimu 47 wanaweza kutoa elimu kwenye shule ngapi nchi hii?kwann asiboreshe maslah ya waalimu wazalendo walioko kwenye mgomo baridi ili wafanye kazi yao vizuri?kwann asijenge maabara zinazokidhi ili wanafunzi wa masomo ya sayansi wafanye practical?sasa hao wamarekani 47 wamekuja na maabara zao?hebu tubadilike tuwe na uchungu na mustakabali wa elimu katika nchi yetu,sio kusifia UJINGA.
 
Back
Top Bottom