CCM fanyeni haya yaliyo ya faida kwa taifa acheni kuwahadaa wananchi na kutafuta kukubalika kwa lazima "Ng'ombe wanaojinenepesha mnadani"

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
CCM YARUDISHA BIASHARA YA UTUMWA KIVINGINE YASHINDWA KUFANYA YA MSINGI YENYE TIJA KWA TAIFA.

CCM FANYENI HAYA YALIYO YA FAIDA KWA TAIFA ACHENI KUWAHADAA WANANCHI NA KUTAFUTA KUKUBALIKA KWA LAZI

Nianze kwenye 1. UTALII;

Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) kwa vivutio vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil lakini bado ipo nyuma kwa utoaji wa huduma za utalii ikiwa ni nchi ya mia moja na kumi (110) kati ya nchi mia moja thelathini na tatu (133) hali inayoweza changia kupunguza pato la taifa ilinalotoka na sekta ya utalii.

Hivi vivutio vimewekwa na Mungu, Tanzania kupitia wizara ya Utalii imeshindwa kabisa kuboresha na kutangaza ili kupata watalii wengi, mbaya zaidi badala ya kuwaza kuendeleza sekta nyeti ambazo zitaleta maendeleo ya watu badala ya maendeleo ya vitu ambayo wananchi wa hali ya chini (maskini) hawaoani uhalisia wake kwani uchumi unaoimbwa hakuna ufungamanisho wa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi.

Yafahamu Maeneo Saba (7) Muhimu Ambayo Sekta Ya Utalii Tanzania Inatakiwa Kuwekeza zaidi;-
1. Hifadhi za Taifa (Tanzania National parks),
2. Mapori ya Akiba (Game Reserves),
3. Maeneo ya hifadhi Jamii (Wildlife Management Areas, WMAs) na Mapori tengefu (Game controlled Areas ),
4. Fukwe za Bahari na Visiwa (Coastline and Off-shore Island),
5. Maeneo ya kihistoria (Historical sites),
6. Milima (Mountains),
7. Maziwa (Lakes).

Serikali ya CCM imefeli kabisa kuweka mikakati inayotekelezeka ili kuhakikisha sekta hii inainua uchumi wa Tanzania Kwa maslahi mapana ya wananchi wake badala yake imeanzisha biashara ya Utumwa kwa kununua wapinzani chini ya *TIPPU TIP* mpya mwenye sura ya kikwetu ili tu chama kisimfie yeye bila kujua ndio anakiua kimyakimya hivi kumbuka waliwahi kusema kua chama hakitanifia mimi yupo kitakaemfia sasa huyu wa sasa naona ndio anaenda kukipoteza kabisa maana sio kumfia tu. Kama mikakati yenyewe ndio hii ya kununua *PANGA BOY SKREPA* tena bila hata mipango endelevu ni wazi kua chama kimempata wa kumfia.

2. MADINI

Zifuatazo ni nchi 5 zinazoongoza kwa utajiiri wa madini barani Afrika;-

1. Botswana
2. Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC)
3. Afrika ya Kusini (South Africa)
4. Tanzania
5. Namibia

Ajabu inakuja badala ya kupanga mikakati inayotekelezeka ya kuhakikisha rasilimali hii inatupa tija ili kuonyesha ufungamanisho sahihi wa ukuaji wa kiuchumi na maendeleo ya watu serikali ya CCM inatumia pesa kununu wapinzani *(Nonsense)*. Wakati hui miondombinu ya Elimu ipo ICU imezidiwa na idadi ya wanafunzi ambao Elimu bure imekua bure kabisa maana hakuna uiano wa wanafunzi na walimu,miundombinu nk..
Afya ndio Jihannamu kwani katika zahanati usishangae ukamiuta muuguzi mmoja au wawili hususani zile za vijijini ambako JIWE anajitapa kua Serikalini yake ni ya maskini wakati maskini wenyewe hawajaliwi. Haya yanaendelea vijana wa CCM wapo wanaona na wanapiga makofi na mayoe waonekane ili wapate uteuzi.

3. UTAJIRI WA GESI

TANZANIA ni nchi ya 10 barani Afrika kati ya nchi 16 kwa uzalishaji wa gesi asilia, huku ikishika nafasi ya 66 duniani.
Hatua hiyo imetokana na ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia.

Kwa mujibu wa Wakala wa Nishati wa Kimataifa (International Energy Agancy โ€“ IEA), nafasi ya Tanzania katika uzalishaji wa gesi asilia inatokana na rekodi za mwaka 2011, ambapo Tanzania tulizalisha meta za ujazo milioni 860 kwa mwaka , Tanzania hivi sasa itakuwa juu endapo takwimu mpya zitatolewa, kwani imefanikiwa kugundua gesi asilia katika maeneo mengi baada ya 2011 ambapo wakala wa Nishati wa kimataifa kutoa rekodi.

Hata hivyo, rekodi za sasa zinaonyesha kwamba Tanzania ina akiba ya gesi iliyothibitishwa ya meta za ujazo trilioni 17.0688 ambazo ni sawa na futi za ujazo trilioni 56.
Ongezeko hilo linatokana na kugundulika kwa akiba kubwa ya gesi katika maeneo mbalimbali tangu mwaka 2010 hadi 2015.

Katika orodha hiyo ya mwaka 2011, Tanzania iko mbele ya Angola (meta za ujazo milioni 752 kwa mwaka), Cameroon (meta za ujazo milioni 150 kwa mwaka), Gabon (meta za ujazo milioni 70 kwa mwaka), Morocco (meta za ujazo milioni 60 kwa mwaka), Ghana (meta za ujazo milioni 50 kwa mwaka), na Senegal (meta za ujazo milioni 20 kwa mwaka).

Uzwazwa unakuja pale tunaposhindwa kutumia rasilimali hii vema kwa kutumia fedha kuwekeza katika maslahi mapana ya wananchi kupitia Gas bali CCM na Magufuli wanatumia mabilioni ya walalahoi kununua wapinzani huku umeme ukiwa si wa uhakika na bado wananadi Tanzania ya Viwanda; *(Kuwaza Viwanda bila umeme wa uhakika ni Ujuha wa Kiwango cha MTATIRO ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€).*


*4. ZAO LA UFUTA*

Tanzania ni kinara wa uzalishaji ufuta; Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya Kilimo ya Naliendele imetoa ripoti na kueleza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Afrika na ya tatu duniani kwa uzalishaji wa ufuta:
Tanzania yawa kinara uzalishaji ufuta Afrika | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Ujuha unakuja pale tunapoagiza mafuta ya Kula nje badala ya kuwekeza katika sekta za msingi ili kuzalisha mafuta ya kula hapahapa nchini lakini leo hii Vijana wanaojiita shupavu wa CCM wanashupaza mashingo kufurahia biashara ya utumwa iliyorudishwa na CCM kama kinara wanawaza vitu vya kijinga na kuacha vya msingi vyenye tija Kwa kila daraja la maisha halisi ya Mtanzania.

Hapa sijazungumzia Mawese (Michikichi) yanayopatikana zaidi Kigoma, Karanga zinazolimwa zaidi kanda ya kati Dodoma na Singida pamoja na kanda ya kusini mikoa ya Lindi na Mtwara hususani wilaya za Nachingwea na Liwale Kwa Lindi na Mtwara Masasi, Nanyumbu, Tandahimba, Newala na Mtwara vijijini. Pia kuna Alizeti inayolimwa zaidi mkoa wa Singida na Manyara. CCM inatakiwa kuwaza kuwekeza huko badala ya kuwekeza katika biashara ya Utumwa mambo leo inataka kutawala milele Ila haitaki kuwapata wananchi wake furaha ya maisha bora.

*5. UZISHAJI WA MAHARAGE*

Tanzania inatajwa kuwa ndio kinara wa uzalishaji na uuzaji wa maharage barani Afrika: Tanzania yaongoza kwa uzalishaji na uuzaji wa Maharage Afrika | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Cha kushangaza maisha ya wakulima wa kawaida wa zao hili ni magumu sana hayana uhalisia na taarifa hizi tembelea SONGEA na baadhi ya mikoa inayolima zao hili utaamini kua hizi takwimu haziendi sambamba na maendeleo ya wakulima wa zao tajwa; Sasa CCM kama chama kilichopewa dhamana ya kuongoza badala ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili wao wanaanzisha biashara ya Utumwa ilihali hakuna uuiano Kati ya wakulima wa maharage na takwimu za uuzaji wa zao hili barani Afrika na bado vijana wanaojiita shupavu wa CCM wanapiga makofi hapa ni wazi kua hata wao wakiwa viongozi huko mbeleni watafanya mambo ambayo anafanya mtu aliechoka kufikili yaani akili Imefika kikomo. Naona nao wanalalamika kama Sisi wakati wanayo hii nchi mikononi mwao zaidi ya miaka 50 sasa Ila wanavyolalamika utazani Uhuru tumepata Jana Kwa ufupi Serikalini ya CCM haina mbinu mbadala za kuendeleza Taifa hili Kwa maslahi mapana ya Nchi. Sijagusia Mbaazi na Tangawizi achana na zao la mpunga ambalo leo hii tunaagiza mchele toka nje ilihali tuna mabonde ya kutosha ya kuzalisha zao hili likawa ni zao la kutuingizia fedha za kigeni Kitaifa kama inavyonufaika Vietnam.

*6. UZALISHAJI WA NAZI*

Tanzania ni mzalishaji namba moja wa nazi barani Afrika na namba kumi na moja duniani, Licha ya uzalishaji huu bado haikidhi mahitaji ya soko lake: Tanzania ni kinara kwa uzalishaji wa nazi barani Afrika | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

Hapa unaweza kujiuliza nataka kuzungumzia zao hili Kwa muktadha upi ndugu msomaji ni hivi zaidi ya tafiti 1500 zimethibitisha kuwa mafuta ya nazi ndiyo mafuta bora zaidi chini ya jua. Pia bidhaa nyingi za vipodozi ukizichunguza utagundua huongezwa pia mafuta ya nazi ndani yake.

Katika hali ya kushangaza ni kwamba pamoja na umuhimu wa zao hili na nafasi ya kua kinara barani Afrika na dunia sijawahi kuona wala kusikia zao hili likipigiwa chapuo ama Kwa kuwatafuta wawekezaji wa Viwanda vya vipodozi nchini kutokana na uhakika wa Malighafi yake kama haitoshi sijawahi kuona wala kusikia kakiwanda kadogo kokote kanakokamua mafuta ya nazi (Original) tofauti na wadau kukamua na kujiuzia kutokana na kuona fursa ya uhitaji wa mafuta kama dawa na kulainisha ngozi hususani kwa watoto wadogo zaidi.

Kwa mikoa yote inayolima zao hili hususani iliyoko pembezoni mwa bahari kuanzia Tanga - Pangani, Pwani tukianza na Bagamoyo, Mkuranga na Mafia, Dar es salaam kwa uchache, Lindi kuanzia Kilwa yote Lindi mjini Kwa uchache , vijijini kuanzia mnazi mmoja, Ng'apa, Kiwalala, Mahumbika , Mtama (Kwa Nape) Nyangao Kwa uchache wake, Mtwara Kwa baadhi ya sehemu chache.

Katika pitapita yangu nikakutana na article hii iliandikwa *25 December, 2010 na mjumbe mmoja wa Jamii forums anaeitwa CHEMA* naomba uipitie ;-
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Nazi Zao Yatima Hana Mzazi Hana Mlezi

Nikianza kwa kunukuu maneno ya Rais Kikwete kuwa zao la minazi limepatwa na " Ugojwa usiotibika kwa sasa ",nakuwataka wakulima wa zao la mnazi kulima kokoa kama zao mbadala .Wazo kama hili si geni ,kwani hapo nyuma wakulima huko Mwanza walitakiwa kubadilisha zao la pamba kwa kahawa .

Inaniwia vigumu kukubaliana na Rais hasa pale alipowahakikishia wakulima wa zao la minazi kuwa atawapa wataalamu kushirikiana nao ili kuweza kufanikisha zoezi hili la kubadilisha Mnazi kwa Kokoa, na ndiyo hapo sera ya kilimo kwanza ninapohisi kushindwa.

Lengo kuu la kilimo kwanza ni kumkomboa mkulima mdogo toka kilimo cha kuchumia tumbo hadi kilimo chenye kunyanyua kipato cha mkulima na serikali . Na ndipo hapo ninakuwa na shaka na mkulima wa minazi kumuona kuwa ni yatima hana mzazi wala mlezi.

Minazi mingi iliyopo imetokana na mashamba ya kurithi ambayo huenda tumerithi toka kwa wazee wetu ama mara baada ya harakati za ukombozi wananchi kujimilikisha kama matunda ya uhuru.
Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea.

Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo?........

Uzwazwa uko wapi?? Uzwazwa upo pale CCM badala ya kufanya ya msingi kuhakikisha zao hili adhimu ninaendele kuwepo tena Kwa uwingi na kunufaisha wakulima wa hali ya chini kuanzia Zanzibar na Tanganyika (Tanzania bara) kama inavyonufaika Sri Lanka; balaaale *TIPPU TIP* anaporudisha biashara ya Utumwa Kwa staili ya kipekee kabisa na wapambe wanampigia makofi badala ya kujiuliza pesa zinazotawanywa kununua wapinzani na kurudia uchaguzi Kwa nini tusiwekeze kwenye vitu muhimu vinavyonufaisha na kuinua taifa kiuchumi ??

Leo ukiingia vichwani mwa hawa wanaojiita vijana shupavu wa CCM utakachokutananacho ni Mawazo ya kuongea porojo ili wateuliwe Ukuu wa wilaya nk.. ili akawe wakala wa *TIPPU TIP* kuhalalisha biashara ya Utumwa iliyorudishwa kivingine , Leo kijana wa CCM badala ya kuwaza kuandaa mradi wa kusaidia kuhuisha mambo ya msingi kama zao la Nazi badala yake anawaza ateuliwe apewe gari afunguliwe mlango, achongewe chungwa, aveshwe koti, abebewe briefcase lake , avalishwe viatu, na nk.. kama vile alivyowaza Yule jamaa wa SEGEREA juzijuzi *(MKURYA WA DAR๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€)*

Hapa nikubaliane na mwana falsafa *PLATO* kua;- Moja ya madhara ya kukataa kujihusisha na siasa ni kwamba utaongozwa na watu uliowazidi akili. Na kwa upungufu wao wa akili watafanya maamuzi ya kila kitu kinachohusu maisha yako.


*7. ZAO LA KOROSHO*

Tanzania ni moja ya wazalishaji wakuu zaidi wa korosho katika Afrika, mauzo ya karosho ya Tanzania huchangia asilimia kumi na tano 15% ya fedha za kigeni.

Tanzania ni mkulima wa 8 mkubwa zaidi duniani na wa 4 katika Afrika ikiongozwa na Nigeria, Cote D'Ivoire na Guinea Bissau.
Takwimu iliyotolewa mwaka 2012 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Tanznaia imekuwa imefanya vizuri katika uzalishaji wa zao la korosho tangu kabla ya uhuru: KOROSHO YA TANZANIA: Tanzania ni mkulima wa 8 mkubwa zaidi duniani na wa 4 katika Afrika. | Focus Media

TAKWIMU za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) za Februari, 2017, zao la Korosho limeingiza jumla ya dola za Marekani milioni 346.6, kulinganisha na mwaka 2016 ambazo zilikuwa milioni 184.9. Kiasi hicho cha maingizo kinafanya Korosho kuwa zao namba moja kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni nchini.Takwimu hizo zilitolewa katika mkutano wa kujadili mustakbali wa zao hilo, Dodoma hivi karibuni. korosho huendesha maisha ya kaya zaidi ya 500,000 kama zao kuu la kibiashara katika wilaya zaidi ya 30 katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga hadi kupelekea kuitwa *"DHAHABU YA KIJANI"*.

Mbali na wakulima wa asili wa Korosho, Mikoa ya Pwani, Lindi, Tanga, Mtwara na Ruvuma, sasa utafiti umeonyesha Korosho inastawi pia katika Mikoa ya Dodoma, Mbeya, Njombe, Iringa, Morogoro, Tabora na Singida. Lakini pia, Waziri, Dk. Tizeba aliwatangazia wadau wa Tasnia ya Korosho kwamba Serikali msimu wa 2017/18 itagawa bure dawa ya sulphur ambayo ni muhimu sana katika kilimo cha Korosho na kwamba magunia yanayotumika kama vifungashio muhimu, nayo yatatolewa bure.

Shida inakuja Serikalini ya CCM inaposhindwa kusimamia zao hili muhimu lenye tija kwa wananchi na Taifa Kwa ujumla tena tija isiotafutwa Kwa tochi wao wanagawa pesa kwa mtu mmoja mmoja (wapinzani) eti CCM iongoze milele, mabilion kama si matirioni ya fedha yanatumika kurudia uchaguzi kila leo lakini wanashindwa kuwalipa wakulima wa korosho pesa zao wanazodai kutoka kwenye ushuru wa usafirishaji wa korosho ghafi nje (Export levy) TSh 201.2 bilioni. Kati ya fedha hizo, TSh 91.1 bilioni ni za mwaka 2015/16 na TSh 110.1 bilioni ni fedha za mwaka 2016/17, kwamba mfuko huo unaidai Serikali TSh81.1 bilioni katika msimu wa 2016/17.

Hatua hiyo ya Serikali imeathiri zao hilo kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa pembejeo, viuatilifu, ujenzi wa maghala na kuendeleza utafiti wa zao hilo katika kituo cha utafiti wa zao la korosho cha Naliendele kilichopo Mtwara pamoja na kuathiri tasnia ya korosho katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19.
Kumbuka serikali ilijitapa kugawa bure dawa ya Sulphur na Magunia (Vifungashio) kitu ambacho serikali imefeli Kwa 100%. Hio haitoshi hivi leo ukipita mikoa inayolima korosho kuna ugonjwa mpya umeingia ambao hupelekea mikorosho kunyauka na kufa kabisa na hadi sasa kituo cha utafiti cha Naliendele wameshindwa kujua aina ya ugonjwa huo na tiba yake kutokana na kukosa fedha za kufanya utafika. Moja ya maeneo makubwa yaliyoathirika na ugonjwa huu ni maeneo ya NANGANGA mkoani Lindi na Mtwara (Hili eneo lina Pande mbili kuna NANGANGA ilioko upande wa Lindi na upande mwingine upo mkoa wa Mtwara (Pande zote Kwa ujumla wake mikorosho yao imeathiriwa na ugonjwa huu wa kukauka mikorosho)

Achana na hayo kuna kero za muda mrefu katika zao hili ambazo wakulima wa korosho wanazilalamikia Kwa kuona wanaibiwa mfano;- tozo tisa 9 zikiwemo tozo TANO (5) ni ya kusafirisha korosho Tsh. 50 kwa kilo; gharama ya Mtunza Ghala Tsh. 10 kwa kilo kulipwa na mkulima; ushuru wa Chama Kikuu cha Tsh. 20 kwa kilo; Kikosi Kazi cha ufuatiliaji zao Tsh. 1 kwa kilo; na Makato ya unyaufu. Hapa sijagusia Pamba na Kahawa mazao ambayo yapo mahututi- ICU.

๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘† Haya CCM hawayaoni kua ya msingi kwao badala yake wanayoyaona ya msingi ni kuharibu fedha za kodi za walalahoi kununua wapinzani ili watawale milele *TIPPU TIP* amerudi na biashara ya Utumwa kivingine halafu bado tunawaza maendeleo eti Kwa sababu ya kununua *PANGA BOY SKREPA* na hii iliyobuma juzi. CCM leo haioni umuhimu wa zao la Korosho bali kitu muhimu kwao ni kuanzisha biashara ya Utumwa ambayo haina ufungamanisho wa kiuchumi na mwananchi mmoja mmoja.

*Ujuha zaidi ni pale unakuta badala ya kutatua tatizo tunalolinyooshea vidole wanamtatua anaeonyesha tatizo (wanashindwa kutofautisha Kati ya Uzalendo na Ushabiki/ukada)*

*8. MADINI YA MAKAA YA MAWE (Coal Mines)*

Katika nchi yetu ya Tanzania madini haya yanapatikana maeneo ya fuatayo (kwa sasa):-
-KIWIRA
-LUDEWA
-RUVUMA
-MBINGA
-SONGEA

UTAFITI umebaini kuwa madini ya makaa ya mawe ambayo yanachimbwa kwenye Mgodi wa Ngaka, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma yanaongoza kwa ubora duniani.

Kabla ya kuanza rasmi mgodi huo, taarifa zinaonesha kwamba zaidi ya tani 1,000 za makaa ya mawe zilisafirishwa kupelekwa nchini Afrika ya Kusini ili kuchunguza ubora wa madini hayo.

Matokeo ya utafiti huo uliofanyika kuanzia mwaka 2008 umeonesha kuwa ubora wa madini hayo haufanani na madini ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika nchi yoyote duniani. Utafiti umebaini kuwa mgodi huo unakadiriwa kuwa na zaidi ya tani milioni 400 za makaa ya mawe. Kiasi hicho, kwa mujibu wa wataalamu waliofanya utafiti, kinaweza kuchimbwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100 mbele. Mkuu wa Masoko wa Mgodi wa Ngaka, Christopher Temba anasema mgodi huo unazalisha tani za makaa ya mawe laki tano kwa mwaka ; Madini hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia na Malawi.

Mgodi wa Ngaka, unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 30, na Kampuni ya Intra Energy ya Australia yenye hisa ya asilimia 70.Kaimu Meneja Mkuu Uzalishaji wa Kampuni ya TANCOAL, Boscow Mabena anasema, kampuni hiyo kuanzia Julai 2014 hadi Desemba 2015 imezalisha tani 272,852 za makaa ya mawe na kati ya hizo, tani 257,570 zimeuzwa na kuwezesha Serikali ya Tanzania kuingiza fedha kwa kodi zaidi ya Sh bilioni 2.
Mabena anawataja wateja wakuu wa madini hayo hapa nchini kuwa ni viwanda vya Lake Cement, Tanga Cement, Mbeya Cement, Dangote, Mufindi Paper Mills na Mohamed Interprises.

umeme unaotokana na madini hayo ndio unaotegemewa zaidi na mataifa mengi yaliyoendelea duniani.Takwimu zinaonesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 ya umeme unaozalishwa duniani, umeme wa maji asilimia 16, umeme wa gesi asilia asilimia 20, nyuklia asilimia 15 na umeme wa mafuta kwa kutumia jenereta ni asilimia sita 6 tu kutokana na kuwa umeme ghali.

Ukweli ni kwamba miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kiuchumi duniani ni yale ambayo yanatumia umeme wa makaa ya mawe.
Mataifa hayo ni pamoja na ;- Afrika Kusini inayotumia asilimia 93 ya umeme wa makaa ya mawe, Poland asilimia 92 na China asilimia 79. Nchi nyingine ni Australia asilimia 77, Kazakhstan asilimia 70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia 60, Morocco asilimia 55, Ugiriki asilimia 52, Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia: 46.TSN : 404 - Page Not Found

Ufinyu wa kufikili unakuja pale CCM na Magufuli wao wanaposhindwa kuwekeza kwenye mambo ya msingi Kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa Kwa ujumla na kuanza kumwaga fedha kununua wapinzani ili chama kiongoze milele *(So what??)* Kiongoze milele wakati wananchi wanaingia kwenye Umaskini uliotopea ilihali Mungu katujalia kila aina ya Neema muhimu.

Wanawakalilisha wanafunzi mashuleni kuimba wimbo wa *"LUCK OF FUND"*, *"COLONIAL LEGACY"* ili wapate marks wakati sababu ni kua *TUMERUHUSU AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA* maana FUNDS zenyewe ni hizi zinazomwagwa kwenye Utumwa na chaguzi zisizoisha hata walimu wenye ueledi mashuleni wanapata ukakasi kumpa tiki mwanafunzi anaeandika hoja hii ya "Luck of funds" wakati anayaona haya yanayoendelea CCM kununu watu

Nikiongezea hapa kwenye makaa ya mawe nchi nilizozitaja hapo juu kua ni wateja wetu bado hatujaweza kuwahakikishia 100% kua wanaweza kupata huduma hio na ndio maana wanaagiza na mataifa mengine nje kukidhi uhitaji wao, kama haitoshi hata umeme wa uhakika Tanzania ni kilio kila kona, madini hayatuingizii mapato tunayostahili hata wateja wa ndani nao wanaagiza nje kutokana na kukosa uhakika wa kupata Nishati hii (Rudia mgogoro wa Dangote na Serikali); CCM badala ya kuhakikisha tunalikamata Soko hili Kwa 100% wao wanamwaga pesa kununua wapinzani

Ng'ombe wanaojinenepesha mnadani ndio mbinu peke sasa kwa ccm
 
Sekta ya utalii inao uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya Anga. Awamu ya tano inapoleta ndege maana yake hayo yaliyotamkwa wenye hii uzi yanawekwa kwenye nafasi ya kipaumbele.

Cha ajabu ni kwamba mwanahabari alishawahi kupandisha uzi ukikejeli sekta ya anga kwa kuonyesha huko vijijini namna ambavyo watu wanakunywa maji machafu!!.
 
Sekta ya utalii inao uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya Anga. Awamu ya tano inapoleta ndege maana yake hayo yaliyotamkwa wenye hii uzi yanawekwa kwenye nafasi ya kipaumbele.

Cha ajabu ni kwamba mwanahabari alishawahi kupandisha uzi ukikejeli sekta ya anga kwa kuonyesha huko vijijini namna ambavyo watu wanakunywa maji machafu!!.
hivi yale ni maji masafi au ndio ccm mpya kwa wananchi ile?
 
Sekta ya utalii inao uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya Anga. Awamu ya tano inapoleta ndege maana yake hayo yaliyotamkwa wenye hii uzi yanawekwa kwenye nafasi ya kipaumbele.

Cha ajabu ni kwamba mwanahabari alishawahi kupandisha uzi ukikejeli sekta ya anga kwa kuonyesha huko vijijini namna ambavyo watu wanakunywa maji machafu!!.
So unataka kusema Utalii huko nyuma haukufanyika vizuri sababu kama Nchi hatukuwa na Shirika la Ndege..
That's big NO.
Sio Mataifa yote ulimwenguni y ana Mashirika ya Ndege na mambo yao yapo vizuri..
Zaidi ya hapo kama tumeleta Ndege lakini tunaambiwa mpaka 2022 ndio zinaanza safari za nje.
Kwanini kama lengo ni kukuza utalii hizo safari za nje zisianze hivi sasa?
 
hivi yale ni maji masafi au ndio ccm mpya kwa wananchi ile?
Uwezo wenu unaishia kwenye kejeli. Yote uliyoyaandika yanatekelezwa, tatizo ni uwezo wako wa kukosoa kuwa mkubwa halafu uwezo wa kuuona uhalisia kuwa mdogo.

Typical mbunge wa upinzani, uwezo mkubwa wa kusema hapana halafu uwezo mdogo wa kuona nini kinafanyika.
 
So unataka kusema Utalii huko nyuma haukufanyika vizuri sababu kama Nchi hatukuwa na Shirika la Ndege..
That's big NO.
Sio Mataifa yote ulimwenguni y ana Mashirika ya Ndege na mambo yao yapo vizuri..
Zaidi ya hapo kama tumeleta Ndege lakini tunaambiwa mpaka 2022 ndio zinaanza safari za nje.
Kwanini kama lengo ni kukuza utalii hizo safari za nje zisianze hivi sasa?
Hiyo ya kusema ni mpaka 2022 ndio safari za nje zitaanza ni kutoka kwenye radio mbao.

Mleta mada anapiga siasa, yote aliyoyaandika yanafanyiwa kazi tena kitaalam kuliko uwezo wake wa kuona nini kinafanyika.
 
Chadema ya Mbowe iache kuhadaa wananchi.
Hivi mtu atabaki Chadema ili afanye mini?
Hakuna mijutano kutokana na ubabe wa Mbowe kupinga shughuli za kuendeleza chama badala yake anatisha kiongozi wenzake tu.

Mbowe ameshindwa kuongoza chama ambacho kina wanachama wengi na mashabiki.
Mbowe akiwa Bungeni utafikiri ni kiongozi wa maana kumbe ni pandikizi anayekiua chama ili kufidia hasara aliyoipata kwa Mali zake kufilisiwa.
Wanajua kabisa kuwa Mbowe ana upinzani mkubwa ndani ya chama na watu wengi hawampendi. Wanajitahidi kumsifu ili aendelee kubaki mwenye uenyekiti ili Chama kiendelee kupukutika.Watakapomtimua kwa vurugu naye atarudi CCM na kukiacha chama kama alivyofanya mchaga mwenzake Mrema kwa NCCR.

Ni endelee kutoa wito kwa Madiwani waliobaki wote ndani ya Chadema wajiuzulu na kulaani unyama wa Mbowe kwa Watanzania wasio na hatia anaowalaghai kwa faida yake binafsi na genge lake.

Eti uchaguzi unapoteza pesa za serikali. Mbina hamzungumzii ruzuku kwenye vyama?
Pesa zikitoka serikalini wakati wa uchaguzi hazitupwi shimoni Bali zinaingia kwenye mzunguko wa fedh wa wananchi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sekta ya utalii inao uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya Anga. Awamu ya tano inapoleta ndege maana yake hayo yaliyotamkwa wenye hii uzi yanawekwa kwenye nafasi ya kipaumbele.

Cha ajabu ni kwamba mwanahabari alishawahi kupandisha uzi ukikejeli sekta ya anga kwa kuonyesha huko vijijini namna ambavyo watu wanakunywa maji machafu!!.
Acha kujitoa ufahamu wewe mbwiga wa jiwe
 
Hiyo ya kusema ni mpaka 2022 ndio safari za nje zitaanza ni kutoka kwenye radio mbao.

Mleta mada anapiga siasa, yote aliyoyaandika yanafanyiwa kazi tena kitaalam kuliko uwezo wake wa kuona nini kinafanyika.
Naona wewe ndio unapiga blabla..
Hayo ni maelezo ya MD wa ATCL alipohojiwa na gazeti la Citizen.
 
Sekta ya utalii inao uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya Anga. Awamu ya tano inapoleta ndege maana yake hayo yaliyotamkwa wenye hii uzi yanawekwa kwenye nafasi ya kipaumbele.

Cha ajabu ni kwamba mwanahabari alishawahi kupandisha uzi ukikejeli sekta ya anga kwa kuonyesha huko vijijini namna ambavyo watu wanakunywa maji machafu!!.
Suala la usafiri wa ndege wa moja kwa moja kuja Tanzania ni mojawapo tu ya changamoto nyingi sana katika Sekta ya Utalii. kubwa zaidi ni kuwa na "linkage" kati ya utalii na shughuli ya uchumi inayowaathiri watanzania walio wengi, ambayo bila shaka ni kilimo. sasa hapo panahitaji mikakati, fedha ya bajeti, kuhusisha sekta mbalimbali. fedha inayotakiwa hapa siyo nyingi sana kama hiyo ya kununua ndege sita: Bombadier 4 na Boeing 2, pamoja na gharama za uendeshaji wake, na hasara ambayo shirika litatuingizia katika hatua za mwanzo, na hatuna uhakika kama tutakwama katika hii biashara ya ndege huko mbele. Lakini mrejesho kwa kukuza "linakage" na Kilimo ni mkubwa zaidi na utakaochangia kuinua hali za watanzania kwa haraka zaidi. sisi tumerukia kwenye hilo la ndege, ambalo pia ni pata potea.

Jingine ambalo tafiti zinaonesha lingeweza kusaidia sana ni kuinua utalii wa ndani. Kihistoria, kwa kuwa utalii ulianza enzi za ukoloni, ambapo mbuga nyingi zilianzishwa na Wajerumani na kisha Waingereza, Waafrika walikatazwa kuingia huko. Hii ilijenga dhana kwamba mambo ya utalii ni ya kikoloni, na wengi hawakuona kwamba utalii ni fursa ya kiuchumi. tafiti zinaonesha kwamba Nyerere alitambua umuhimu wa sekta ya utalii mapema, na kuchukua hatua kuuimarisha. lakini tegemeo letu kubwa la utalii ni kutoka nje. tunaambiwa kwamba kukuza utalii wa ndani kunasaidia sana kuimarisha sekta na kuiendeleza kimiundombinu, utaalamu wa ndani, na ushiriki wa watanzania kwa ujumla. pia inasaidia kui-stabilize sekta pale ambapo watalii toka nje wanapungua kutokana na kuyumba kwa uchumi duniani. jingine ni kwamba watalii toka nje wanakuja kwa msimu, hivyo wakati usiokuwa wa msimu kunakuwa na matatizo. utalii wa ndani ulioimarishwa unasaidia kupunguza athari kama hizi

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yangeweza kufanyika bila kuanza kuagiza madege kwa gharama kubwa mno. hapo tungeshuhudia kuimarika kwa sekta ya utalii kuliko hii mbinu moja tu ambayo kwa kweli ni kisingizio tu cha kuficha ushamba wa viongozi wa awamu ya tano, ambao wanafurahi kupiga picha ndani ya ndege, na hata rais anatafuta nafasi ya kupata ujiko kwa kupigwa picha akisalimiana na wasafiri. ni kama bado haamini kwamba kweli kanunua ndege, na pengine Magufuli anaamini kwamba hizo fedha ni zake kutoka mfukoni. sasa haya ni matatizo ya mtu binafasi na siyo mbinu za kukuza utalii
 
Back
Top Bottom