Safari ya Israel kua statehood

Safari ya Israel kua statehood

Umeandika kiutu uzima kabisa , ata sisi wangoni ni Watanzania lakini ASILI yetu ni South Africa, inahitaji ujitoe akili kukataa ukweli uliopo wazi
Huyu jamaa kaeleza anbisha tu ili kukidhi cheti alichonacho cha ukadhi.
 
Mbona halalamiki juu ya Ishmael acha unafki wako
Thread inasema Israel ,kama unataka ya Ishmael fungua nitakuja huko, ukweli ni kwamba wa Israel ni wahamiaji pale kaanan , kiufupi Uzao wa Ibrahim ni wahamiaji pale kaanan awe Ishmael , isiaka au yakobo n.k wote wahamiaji tu
 
Thread inasema Israel ,kama unataka ya Ishmael fungua nitakuja huko, ukweli ni kwamba wa Israel ni wahamiaji pale kaanan , kiufupi Uzao wa Ibrahim ni wahamiaji pale kaanan awe Ishmael , isiaka au yakobo n.k wote wahamiaji tu
Ndugu yangu kuhama Ni sehemu ya Kawaida kabisa ya Mwanadamu nahisi Hata wewe moyoni unawaza ungekuwa na nafasi ungehama kwenda kutafuta maisha sehemu au nchi nyingine. Kwa hiyo Hauna cha kufanya Israeli ataendelea kuwepo pale na pale Ndipo pake kazaliwa pale na Ataishi pale.

Kama ambavyo wewe unaish hapa kwetu.
 
Hiki ni kikundi ni cha shetani tu. Kwasababu mafundisho yao yamejengwa kwenye Chuki (Hasa kwa Mtu yeyote anayejiita Mkatoliki) na Unabii wa Uongo. Tukifahamu kua Chuki sio Tunda la Roho bali mBegu ya shetani.

Kwenye unabii wa Uongo, yangu zamani hutumia bibilia ku decode maelezo yaliopo ndani ya Bibilia na kutoa unabii kwa masuala ya Apocalyptic na Mwisho wa Dunia kwa pointi za Ulaghai na kuwasingizia watu kwa uongo.

Wamelaaniwa kwasababu wanaifuata Sheria dhidi ya Kristo aliyeibadili Mauti na kutokuharibika kwa ile Injili.
Kueleza ukweli sio chuki, hata Yesu aliwaeleza Wayahudi ukweli na wakamchukia na kumuua. Ukweli unauma
 
Kueleza ukweli sio chuki, hata Yesu aliwaeleza Wayahudi ukweli na wakamchukia na kumuua. Ukweli unauma
Hawajawahi kuongea ukweli tangu dunia iumbwe. Kama wewe ni Free Thinker fuatilia masuala mbalimbali waliyowahi kuyatabiri na hayakutokea.
 
Hawajawahi kuongea ukweli tangu dunia iumbwe. Kama wewe ni Free Thinker fuatilia masuala mbalimbali waliyowahi kuyatabiri na hayakutokea.
Sijajua kama na wao ni watabiri. Mimi najua wanahubiri habari za Yesu huku wakitumia Biblia mkuu. Kutabiri labda utujuze walitabiri nini na hakikutokea
 
Ndugu yangu kuhama Ni sehemu ya Kawaida kabisa ya Mwanadamu nahisi Hata wewe moyoni unawaza ungekuwa na nafasi ungehama kwenda kutafuta maisha sehemu au nchi nyingine. Kwa hiyo Hauna cha kufanya Israeli ataendelea kuwepo pale na pale Ndipo pake kazaliwa pale na Ataishi pale.

Kama ambavyo wewe unaish hapa kwetu.
Mimi sijakataa hilo jambo la kuhama mzee, ila mimi nimekwambia kama alihama maana yake alitoka sehemu A kwenda sehemu B, hivyo tukitafuta ASILI ya Israel ni sehemu A huko walikotoka ambapo ni Mesopotamia, lakini kwenye URAIA anaweza kuwa raia wa sehemu B,kama vigezo na masharti vimefikiwa, mfano Mo Dewji ni Mtanzania kabisa wa kuzaliwa , lakini ASILI yake huko walipotoka babu zake ni INDIA , iko hivyo
 
Sijajua kama na wao ni watabiri. Mimi najua wanahubiri habari za Yesu huku wakitumia Biblia mkuu. Kutabiri labda utujuze walitabiri nini na hakikutokea

Wanatumia bibilia kujaribu ku decipher baadhi ya masuala ya kinabii yalioandikwa humo. Kwa tafsiri zao zinazowapendeza.

Kisha wanatabiri Masuala ambayo mara zote wamekua wakiangukia Pua. Na kuwafanya kua na wao ni manabii wa Uongo.

Bibilia peke yake haitoshi kukueleza Habari za Yesu Kristo. Ndio maana nikasema hawana Historia.
Ukristo ulihubiriqa pasipo Bibilia. Ukrosto ulikuwepo kabla ya Uwepo wa Bibilia. Imani ilianza Bibilia ikaja baadaye.

Hawana Historia, hawawezi kueleza chochote zaidi ya Kuhubiri masuala ya Upinga kRisto ambayo sikuzote wamekua wadanganyifu.

Na zaidi sana, uelewa wao kuhusu Yesu Kristo ni Potofu sana. Na kutokana na kuendesha imani kwa njia za Conspiracies theories. Wengi hua wanachuki ya wazi na muumini yeyote wanayesikia ni Mkatoliki.

Na Mungu ni Upendo. sasa utaona jinsi wanavyokwenda astray.
 
Wanatumia bibilia kujaribu ku decipher baadhi ya masuala ya kinabii yalioandikwa humo. Kwa tafsiri zao zinazowapendeza.

Kisha wanatabiri Masuala ambayo mara zote wamekua wakiangukia Pua. Na kuwafanya kua na wao ni manabii wa Uongo.

Bibilia peke yake haitoshi kukueleza Habari za Yesu Kristo. Ndio maana nikasema hawana Historia.
Ukristo ulihubiriqa pasipo Bibilia. Ukrosto ulikuwepo kabla ya Uwepo wa Bibilia. Imani ilianza Bibilia ikaja baadaye.

Hawana Historia, hawawezi kueleza chochote zaidi ya Kuhubiri masuala ya Upinga kRisto ambayo sikuzote wamekua wadanganyifu.

Na zaidi sana, uelewa wao kuhusu Yesu Kristo ni Potofu sana. Na kutokana na kuendesha imani kwa njia za Conspiracies theories. Wengi hua wanachuki ya wazi na muumini yeyote wanayesikia ni Mkatoliki.

Na Mungu ni Upendo. sasa utaona jinsi wanavyokwenda astray.
Naona na wewe una chuki nao!! I mean hao Wa SDA 😛 😛 😛 😛
 
Mkuu sasa nafikiri una ugonjwa wa kusahau kabisa, Ibrahim alitoka Mesopotamia baada ya kuonyeshwa na kuamriwa na huyo Mungu wake kuwa atawapa nchi yeye Ibrahim na UZAO WAKE, alipokuja kwenye hiyo nchi akawakuta wenyeji wakaanani pale , huyo Israel( yakobo) ni uzao wa yule yule Ibrahim aliedai kupewa nchi ya Wakaanani na Mungu , hivyo ni muendelezo wa Israel kudai kile alichopewa babu yao Ibrahim, wala hakuna Dai jipya na hoja yao ni ile ile ya Ibrahim kuwa Mungu ametupa nchi hii ya ahadi hivyo ni mali yetu, kuna maandiko mengi juu ya ubabe wa kuwaua na kuwaangamiza wenyeji wa maeneo yale ili wao ndio wachukue nchi
Mkuu naona unashusha nondo tupu,sijui jamaa hasichoelewa hapo n'nini!!
 
Nimesoma Uzi wako wa awali, nimesoma jinsi unavojibu kwa Hoja, niishie kusema una uweledi wa halia ya juu katika sanaa ya mabishano na kujenga Hoja, hata kama kuna baadhi ya point inaweza kuwa ngumu kuamini kwa sababu kadha wa kadha lakini nabaki kukiri wewe ni Mjenga Hoja mzuri sana Ndg yangu.... You got my attention , Big up.
Kuna vitu vingine unatakiwa ujiongeze wewe Mwenyewe.

Watu huama sehemu moja kwenda nyingine kwa nia ya kutafuta Maji, Chakula, na Usalama wake, mali na chakula cha mifugo yake,

Huku Afrika kuna makabila ya Nomads kama Maasai, kule Arabuni wanaitwa wabedui (Beduins). Wote hawa hamahama na wanyama wao

So Hii hata bila kuambia ni Mungu kamwelekeza Abrahamu kuhamia pale Kanaani, unaweza kujiongeza mwenyewe kua eneo hili lilikua lina sifa za mtu wengine kutamani kuhamia hapo na kuishi.

Ikumbukwe, Hata Israel alipohamia Misri, alipelekwa na sababu kama hizo. Hata angesema Mungu kamuagiza aende huko misri, isingeleta athari sana kwasababu factors nyingine zinatosha ku influence hatua gani ya kufuata. Nchi ina njaa ya kufa mtu. Unaishije sasa?. Lazima uhame.

Na Waliporudi wakitokea Egypt walikua wanarudi kwenye nchi walioambiwa ni ya Maziwa na Asali. Na walikuta watu wa huko wana maumbile makubwa, wako vizuri kuonyesha ni nchi yenyw Chakula cha kutosha.
Kwahiyo the whole point hapa ni Surviving.

There are Three Human basic needs.
1. Food
2. Shelter
3. Clothes
.
.
4. Sex


Additionally.
Ukisoma Legends utaona kua hata jamii ya Abraham walikua na Utamaduni wa kuua Mtoto wa Kwanza ili kumtoa Sadaka kwa Miungu.

Kitendo cha kutomuua Isaka ndio kilihitimisha rasmi vitendo vya mauaji ya uzao wa kwanza kwenye makabila yao. Lakini kimaandiko tunasoma ni Mungu aliingilia kati.

Kwasababu hizo, Tulihitaji Legends za wakanaani watakaosema Upande wa pili wa Shilingi na Baba yao Kanaan. Kuhusu Kuvamiwa na Abraham katika Ardhi yao.

Lakini mpaka tunakwenda Mitamboni wana wa Israel ndio warithi wa ardhi ya Kanaani hata leo.
 
Katika Yerusalem unaweza ongea chochote iwe Siasa, Dini ama Historia.

Kutoka kwa Abraham mpaka zama ya Trump na Netanyahu.

Katika Masada zipo story mbili.
Moja inamuhusu Mfalme Herode na nyingine inahusu Uasi waisraeli walioitwa sikarii.

1. Ardhi ya israel ilitekwa nyara na warumi kwenye mwaka 63BCE na kisha warumi waka iteka Judea.

2. Israel Haikutekwa kwa mara moja na warumi, bali ilikua inachukuliwa polepole kadri muda ulivyokwenda. Ilichukua miaka Mia moja , waisrael wakiwa wamepoteza kabisa uhuru wao.

3. Ukristo ukazaliwa na Hekalu la Jerusalem likaja kuharibiwa na Warumi miaka 70 CE. baadaye.
****


Mwaka 37BCE Warumi walimteua Herode Mkuu kua Mfalme wa Judea. Ambapo alitawala Jerusalem na maeneo kuzunguka mji.


Na miaka 10 baadaye Herode Mkuu akajenga jumba la kifalme (palace) hapo Masada

Kulikua na mtazamo hasi kuhusu Mfalme Herode kwa upande wa Wakristo. Kwasababu Moja.

Wakati Yesu kristo anazaliwa, ni Herode ndiye aliye agiza kuua vitoto vichanga kule Bethlehemu.

Lakini Kwa upande wa Wayahudi, walikua hawajui wafanyaje kwasababu;-

Mosi ni Herode ndiye aliwajenga hekalu kubwa likawa kama lile la awali Lililobomolewa.

Lakini pili alikua anawatoza kodi kubwa mno kiasi kwamba hawakumuona kama ndiye kiongozi wao.

Ingawa alitawala kwa miaka 34, watu pekee waliompenda ni Waongoza watalii wa kiisraeli(Israel tour Guides) kwakua aliwapatia kazi nyingi sana katika utawala wake kuliko kiongozi yoyote

Kwa mfano, Ukiwa umetembelea Israel kwa wiki moja, unakua na uhakika wa kutembelea angalau sehemu tatu muhimu ambazo ni:-
1. Masada,
2. The Temple Mount(Mlima Hekalu) ulio katika Mji mkongwe wa Jerusalem na
3. Kaisaria(Caesarea).

Mfalme Herode walimbatiza jina mfalme mjenzi 'the Builder King'. Herode alikua anakaa mara chache sana hapo Masada. Kwa mwaka anakaa wiki moja tu. Pamoja na kua alikua na sehemu nyingi, Alipapenda Masada kwa sababu alipaona ni sehemu nzuri kuifanya Ngome.

*****
Herode alikufa mwaka 4BCE. Baada yake akatawala Mwanae ambaye hakua na akili ya kisiasa ya namna ya kuchukuliana na watu.

Kwa haraka warumi wakaamua kumbadilisha na kumweka Mtawala ama Kiranja(Prefects) sehemu yake.

Hapa ndipo uhusiano kati ya Wayahudi na utawala wa Rumi ukaanza kupungua hata ikafika mwaka 67CE sehemu ya wayahudi wakaamua kufanya uhasi dhidi ya utawala wa Rumi.

Kulikua na Wayahudi wanaoitwa Sikarii wakaichukua mji wa Masada. Baada ya kukipindua kikosi kidogo cha jeshi la Warumi waliokua wakilinda ile ngome ya Masada.

Jeshi la Warumi kutokea Lebanoni likaenda hapo kuangamiza uhasi.

Mwaka 70CE wa Rumi wakauteka Yerusalemu na kubomoa Hekalu la Pili. (I.e. unabii wa Yesu kristo Ukatimia.)[B/]

Familia za wayahudi wengine waliokua na ugomvi na hawa Sikarii WAKALAZIMIKA kuikimbia Yerusalem na kwenda hapo Masada kuungana na waSicarii.

Wakawa wanatumia sehemu hiyo KAMA NGOME ili kuweza kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya kuzunguka mji yaliokua chini ya utawala wa Rumi.

Kipindi cha baridi waRumi kwenye mwaka 73-74CE wakaufikia Masada.


*Kuzingirwa kwa mji wa Masada.*

Ilikua ni vita ya kwanza kati ya warumi na Jewishi Iliyodumu Kuanzia Mwaka 73-74 CE (Baada ya Kristo)katika kilima kirefu eneo ambalo leo ni Israeli.

Masada ilikua ni kilima kirefu kilicho pande zote zaidi ya mita 450, hivyo kufanya kua sio rahisi kuingilika. na kwa juu kipo flati kama meza.

Masada ilikua na njia moja tu nyembamba inayokwenda kwa kupindapinda yaani zigzag kama nyoka mpaka juu ya huo mlima. Njia hii ilijulikana kwa jina la "Nyoka". Njia hiyo haitoshi hata kwa watu wawili kupanda kwa pamoja.

Wayahudi. Walioongoza Vita hiyo waliitwa
Sikarii. Walikua ni watu walioshika dini ya kiyahudi sana(Zealots). Wakiwa hapo Masada, Walijenga Hekalu lililotazama kuelekeaYerusalemu japo halikua limeshawekwa mabenchi. Kutokana na imani yao Sikarii hawakutaka kujisalimisha kwenye mikono ya Warumi waliokua na jeshi kubwa sana. Pia Sikarii walikua na misimamo isiyoelewana na wayahudi wengine achilia mbali waRumi.

Vikosi vya jeshi kwa Kila upande
Juu ya mlima walikua watu 960 wakiwemo wanajeshi na wasio wanajeshi. Wakiongozwa na kamanda Mkuu Eliazar Ben Ya'ir.

Wakati jeshi la waRumi chini ya Lucius Flavius Silva lilikua na watu wanaokadiriwa 15,000 wake kwa waume.

Ambapo ndani ya jeshi lake kulikua na mateka wa vita wa kiyahudi. wanaume wanakadiriwa kua kati ya 8000 mpaka 10,000. Na jeshi la watu wa Ruma rasmi 4,800. Jumla wanakadiriwa kufikia watu15000.


Warumi walipoona ngome ya Sikarii haingiiliki. Wakaamua kuuzingira mji ili asiwepo mtu Anayetoka na kuingia Katika Mji wa Masada. Kisha wakajenga Ukuta mkubwa kuuzunguka mji wote wa Masada.

Mbinu hii ililenga kuwafanya wasikarii wakose kutoka NjE ya mji ili kutafuta huduma yoyote kama chakula, nk. Ambapo mwishowe watakua dhaifu, na hata kujisalimisha wenyewe.

Hata hivyo Juu ya mlima wa Masada Waisraeli wa Sikarii walikua na vyakula na maji Ya kuwatosha. Na Walikua wamechimba Maji ndani visima vya maji ya kunywa. Hivyo maisha yaliendelea bila Wasiwasi.

Kuona hivyo, Warumi waliokua wameuzingira mji wa Masada, wakaamua kujenga muinuko (yaani Ramp)wa kuweza kupeleka jeshi ili kuvamia. Miinuko unaojulikana kwa jina la Ramp.

Kabla hawajaanza kujenga migongo hiyo. wakaanza kujaza tani za mawe eneo hilo na kuvunja miamba mikubwa na kuikusanya eneo hilo. Ikawa kama wanajenga mlima mkubwa. Wakamaliza kujaza kifusi kikubwa kama mlima. Ambapo ndio ikawa njia yao ya kuhusuru mji.

Kisha wakaunda Mnara mrefu na kibanda ambacho huwekwa silaha ya kuvunjia ukuta wa ngome(Battering Ram) ambacho huwekwa juu ya Mnara. hii ni silaha za antikwiti.

Ndipo Askari wa kirumi wakakokota Mnara na Mgongo wake kufuata muinuko waliokwisha utengeneza kwa kifusi kikubwa cha mawe na udongo. kikapelekwa kupanda juu eneo la ngome ya masada.

Wakaanza kuachia mabomu ya moto kwenye ukuta hadi ukuta ukavunjika. Waruma wakaingia ndani ya ngome kwajili ya vita na jeshi la waIsraeli(Sikarii). Wakakuta wayahudi wameshawapokonya ushindi kwa kwa kujiua wenyewe

Waliobaki hai ni watu 7 waliokua wamejificha. Wanawake 2 na watoto 5.


Inasemekana kupitia taarifa za hawa wanawake:

Kamanda wa Israeli Eliazar Eben Ya'ir na kundi lake walipoona Wamezingirwa waliamini Mwenyezi Mungu ameamua wafe.

Hivyo wakapanga kutokukubali kua watumwa wa utawala wa Rumi wala kuabudu miungu wengine isipokua Mungu mmoja tu alieumba Mbingu na Nchi.

Hivyo bora wafe wakiwa huru kuliko wakiwa watumwa.

Na ili Kuhakikisha kua Adui zao wajue kua wamechagua njia hiyo.

Kiongozi wao aliwaagiza waharibu kilakitu, isipokua wasiharibu vyakula ,ili kama warumi wakifika wajue kua walikua na uwezo wa ku ishi zaidi ila walichagua kufa kishujaa na huru kuliko kua Utumwa. Pamoja na yote, Imani ya Kiyahudi(Judaism) inakataza kujiua.

Pia Wako wanazuoni mbalimbali wanaokosoa ushujaa wa wasikarii wa kujiua

Muasisi wa Taifa La kiyahudi na Mwanasayansi na Baba wa Industrial Fermentation Raisi Chaim Weizmann. Akihutubia katika Bunge la Wazayuni Decemba 9Mwaka 1946, mjini Basle. Kwa kauli yake kali iliyojaa msimamo, Alikosoa uamuzi huo wa Wayahudi wa Sikarii uliopelekea kizazi chao kuangamia chote bila kuacha matumaini. Alikiiita kitendo chao ni Janga kwa historia ya Wayahudi. Alitaka Uzayuni iwe ndio mwisho wa Kujitoa Mhanga na Uwe mwanzo wa kutafuta njia mpya ya maisha.



Upinzani wa pili ulioletwa na Bar Kochba mwaka 131E - 135E ulikua mbaya kuliko uliopita. Ambapo Wayahudi walichinjwa na Warumi na kuogelea Damu.

Mpaka mji wa Judea ukabadilishwa jina ukaitwa PALESTINA, hii ni kulingana na wafilisti walioishi Gaza na Ashdodi milenia iliopita.

Mji mkuu wa Jerusalemu ukaitwa ILIA CAPITOLINA na jengo la ibada la Mungu Jupiter likajengwa hapo ambapo ndio kuna mlima Hekalu(Temple Mount).

Hali hii ilipelekea Wayahudi Kwa ujumla wao kupinga sana harakati zozote za Kijeshi.

Ikafanya hadi kiongozi wao mkuu anayeita HASMONEANS pamoja na kwamba alishinda vita dhidi ya Jeshi la Selucid na dhidi ya Warumi kutoku kuenziwa kwenye 'Mishnah na Talmud.'

Pia wakati wote wayahudi wakiwa uhamishoni wamekua wakionyesha hisia zao kupitia maombi na Mafunzo (Eretz Israel) lakini sio kwa njia ya Vita. Walikua Wakitumainia muujiza wa Messiah.


Vilevile Wanaharakati wa karne ya 19 waliotaka kuunda Taifa la Israel kama Theodore Herlz hakuweka mbele mkakati wowote wa kivita.

Waliamini bila uzoefu wowote kua Mataifa makubwa yangewapa nchi yao ya ahadi na waarabu ambao ni wenyeji wangewakaribisha bila matatizo yoyote kwenye nchi ya ahadi.

Hata hivyo Bwana Theodore Herlz mpaka anafariki, alishindwa kupata kibali (ie.Charter).

Baada ya Herlz kufariki.

Mwaka 1904, Weizmann mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Manchester na kiongozi miongoni mwa Wazayuni wa kiingereza. Kipindi ambacho Arthur Balfour alikua Waziri Mkuu na pia ni mbunge akiwakilisha wilaya ya Manchester. Balfour aliunga mkono makazi ya wayahudi.


Chaim Weizmann alipata kibali kwa waingereza kupitia mkataba wa Balfour declaration mwaka novemba 2 mwaka 1917 akiwahakikishia kupata Taifa lao bila Vita. Ambapo eneo lilikua sehemu ya Utawala wa Ottoman.(Sio waarabu).


Hata hivyo kwenye Vita ya kwanza ya Dunia Wayahudi walikua wameunda kikosi cha jeshi(Battalions) kilipigana sambamba na Uingereza, ambapo kilifanikiwa kuchukua eneo hili. hata hivyo kikosi hiki kilikuja kuvunjwa mara tu, baada ya Vita kuisha.

Mnamo Mwaka 1922 Uingereza kupitia Jumuiya ya Madola, walipewa haki ya kuisimamia Palestina (Palestine Mandate)

Waarabu hawakutumia kikamilifu jumuiya ya kimataifa kwa faida yao, ndio iliofanya wakafeli kwenye ku bargain kuhusu Eneo la Palestina. Israel akaibuka mshindi.

Hatimaye tangu Abraham mpaka Yesu Kristo mpaka Trump. Jerusalem imekua rasmi mji mkuu wa Israel.
Haaaa uko vzr sana na hao wauaji wakayi sisi tuna cema Yessu wa Izrael tuokoe wao wanatengeneza nyuklia vipi za kwetu haswa Historia ya kabila lako. Naukiza tu
 
kwa msiojua... Kitabu cha ezekiel kinasema, Kabla ya Yesu kuja, Mji wa Jerusalem wa Israel utatakaswa.

Kwa ufupi kinachoendelea sasa ni kuutakasa mji huu na Yesu karibu anakuja.

Tuko juma la mwisho la mwaka wa 7000 na halitopita ili Yesu alisema halitopita.
ezekiel ngapi nikasome haya uliyosema kuhusu utakaso wa mji???
 
Back
Top Bottom