Safari ya Israel kua statehood

2013

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
11,358
6,059
Katika Yerusalem unaweza ongea chochote iwe Siasa, Dini ama Historia.

Kutoka kwa Abraham mpaka zama ya Trump na Netanyahu.

Katika Masada zipo story mbili.
Moja inamuhusu Mfalme Herode na nyingine inahusu Uasi waisraeli walioitwa sikarii.

1. Ardhi ya israel ilitekwa nyara na warumi kwenye mwaka 63BCE na kisha warumi waka iteka Judea.

2. Israel Haikutekwa kwa mara moja na warumi, bali ilikua inachukuliwa polepole kadri muda ulivyokwenda. Ilichukua miaka Mia moja , waisrael wakiwa wamepoteza kabisa uhuru wao.

3. Ukristo ukazaliwa na Hekalu la Jerusalem likaja kuharibiwa na Warumi miaka 70 CE. baadaye.
****

Mwaka 37BCE Warumi walimteua Herode Mkuu kua Mfalme wa Judea. Ambapo alitawala Jerusalem na maeneo kuzunguka mji.

Na miaka 10 baadaye Herode Mkuu akajenga jumba la kifalme (palace) hapo Masada

Kulikua na mtazamo hasi kuhusu Mfalme Herode kwa upande wa Wakristo. Kwasababu Moja.

Wakati Yesu kristo anazaliwa, ni Herode ndiye aliye agiza kuua vitoto vichanga kule Bethlehemu.

Lakini Kwa upande wa Wayahudi, walikua hawajui wafanyaje kwasababu;-

Mosi ni Herode ndiye aliwajenga hekalu kubwa likawa kama lile la awali Lililobomolewa.

Lakini pili alikua anawatoza kodi kubwa mno kiasi kwamba hawakumuona kama ndiye kiongozi wao.

Ingawa alitawala kwa miaka 34, watu pekee waliompenda ni Waongoza watalii wa kiisraeli(Israel tour Guides) kwakua aliwapatia kazi nyingi sana katika utawala wake kuliko kiongozi yoyote

Kwa mfano, Ukiwa umetembelea Israel kwa wiki moja, unakua na uhakika wa kutembelea angalau sehemu tatu muhimu ambazo ni:-
1. Masada,
2. The Temple Mount(Mlima Hekalu) ulio katika Mji mkongwe wa Jerusalem na
3. Kaisaria(Caesarea).

Mfalme Herode walimbatiza jina mfalme mjenzi 'the Builder King'. Herode alikua anakaa mara chache sana hapo Masada. Kwa mwaka anakaa wiki moja tu. Pamoja na kua alikua na sehemu nyingi, Alipapenda Masada kwa sababu alipaona ni sehemu nzuri kuifanya Ngome.

*****
Herode alikufa mwaka 4BCE. Baada yake akatawala Mwanae ambaye hakua na akili ya kisiasa ya namna ya kuchukuliana na watu.

Kwa haraka warumi wakaamua kumbadilisha na kumweka Mtawala ama Kiranja(Prefects) sehemu yake.

Hapa ndipo uhusiano kati ya Wayahudi na utawala wa Rumi ukaanza kupungua hata ikafika mwaka 67CE sehemu ya wayahudi wakaamua kufanya uhasi dhidi ya utawala wa Rumi.

Kulikua na Wayahudi wanaoitwa Sikarii wakaichukua mji wa Masada. Baada ya kukipindua kikosi kidogo cha jeshi la Warumi waliokua wakilinda ile ngome ya Masada.

Jeshi la Warumi kutokea Lebanoni likaenda hapo kuangamiza uhasi.

Mwaka 70CE wa Rumi wakauteka Yerusalemu na kubomoa Hekalu la Pili. (I.e. unabii wa Yesu kristo Ukatimia.)[B/]

Familia za wayahudi wengine waliokua na ugomvi na hawa Sikarii WAKALAZIMIKA kuikimbia Yerusalem na kwenda hapo Masada kuungana na waSicarii.

Wakawa wanatumia sehemu hiyo KAMA NGOME ili kuweza kufanya mashambulizi kwenye maeneo ya kuzunguka mji yaliokua chini ya utawala wa Rumi.

Kipindi cha baridi waRumi kwenye mwaka 73-74CE wakaufikia Masada.

*Kuzingirwa kwa mji wa Masada.*

Ilikua ni vita ya kwanza kati ya warumi na Jewishi Iliyodumu Kuanzia Mwaka 73-74 CE (Baada ya Kristo)katika kilima kirefu eneo ambalo leo ni Israeli.

Masada ilikua ni kilima kirefu kilicho pande zote zaidi ya mita 450, hivyo kufanya kua sio rahisi kuingilika. na kwa juu kipo flati kama meza.

Masada ilikua na njia moja tu nyembamba inayokwenda kwa kupindapinda yaani zigzag kama nyoka mpaka juu ya huo mlima. Njia hii ilijulikana kwa jina la "Nyoka". Njia hiyo haitoshi hata kwa watu wawili kupanda kwa pamoja.

Wayahudi. Walioongoza Vita hiyo waliitwa
Sikarii. Walikua ni watu walioshika dini ya kiyahudi sana(Zealots). Wakiwa hapo Masada, Walijenga Hekalu lililotazama kuelekeaYerusalemu japo halikua limeshawekwa mabenchi. Kutokana na imani yao Sikarii hawakutaka kujisalimisha kwenye mikono ya Warumi waliokua na jeshi kubwa sana. Pia Sikarii walikua na misimamo isiyoelewana na wayahudi wengine achilia mbali waRumi.

Vikosi vya jeshi kwa Kila upande
Juu ya mlima walikua watu 960 wakiwemo wanajeshi na wasio wanajeshi. Wakiongozwa na kamanda Mkuu Eliazar Ben Ya'ir.

Wakati jeshi la waRumi chini ya Lucius Flavius Silva lilikua na watu wanaokadiriwa 15,000 wake kwa waume.

Ambapo ndani ya jeshi lake kulikua na mateka wa vita wa kiyahudi. wanaume wanakadiriwa kua kati ya 8000 mpaka 10,000. Na jeshi la watu wa Ruma rasmi 4,800. Jumla wanakadiriwa kufikia watu15000.

Warumi walipoona ngome ya Sikarii haingiiliki. Wakaamua kuuzingira mji ili asiwepo mtu Anayetoka na kuingia Katika Mji wa Masada. Kisha wakajenga Ukuta mkubwa kuuzunguka mji wote wa Masada.

Mbinu hii ililenga kuwafanya wasikarii wakose kutoka NjE ya mji ili kutafuta huduma yoyote kama chakula, nk. Ambapo mwishowe watakua dhaifu, na hata kujisalimisha wenyewe.

Hata hivyo Juu ya mlima wa Masada Waisraeli wa Sikarii walikua na vyakula na maji Ya kuwatosha. Na Walikua wamechimba Maji ndani visima vya maji ya kunywa. Hivyo maisha yaliendelea bila Wasiwasi.

Kuona hivyo, Warumi waliokua wameuzingira mji wa Masada, wakaamua kujenga muinuko (yaani Ramp)wa kuweza kupeleka jeshi ili kuvamia. Miinuko unaojulikana kwa jina la Ramp.

Kabla hawajaanza kujenga migongo hiyo. wakaanza kujaza tani za mawe eneo hilo na kuvunja miamba mikubwa na kuikusanya eneo hilo. Ikawa kama wanajenga mlima mkubwa. Wakamaliza kujaza kifusi kikubwa kama mlima. Ambapo ndio ikawa njia yao ya kuhusuru mji.

Kisha wakaunda Mnara mrefu na kibanda ambacho huwekwa silaha ya kuvunjia ukuta wa ngome(Battering Ram) ambacho huwekwa juu ya Mnara. hii ni silaha za antikwiti.

Ndipo Askari wa kirumi wakakokota Mnara na Mgongo wake kufuata muinuko waliokwisha utengeneza kwa kifusi kikubwa cha mawe na udongo. kikapelekwa kupanda juu eneo la ngome ya masada.

Wakaanza kuachia mabomu ya moto kwenye ukuta hadi ukuta ukavunjika. Waruma wakaingia ndani ya ngome kwajili ya vita na jeshi la waIsraeli(Sikarii). Wakakuta wayahudi wameshawapokonya ushindi kwa kwa kujiua wenyewe

Waliobaki hai ni watu 7 waliokua wamejificha. Wanawake 2 na watoto 5.

Inasemekana kupitia taarifa za hawa wanawake:

Kamanda wa Israeli Eliazar Eben Ya'ir na kundi lake walipoona Wamezingirwa waliamini Mwenyezi Mungu ameamua wafe.

Hivyo wakapanga kutokukubali kua watumwa wa utawala wa Rumi wala kuabudu miungu wengine isipokua Mungu mmoja tu alieumba Mbingu na Nchi.

Hivyo bora wafe wakiwa huru kuliko wakiwa watumwa.

Na ili Kuhakikisha kua Adui zao wajue kua wamechagua njia hiyo.

Kiongozi wao aliwaagiza waharibu kilakitu, isipokua wasiharibu vyakula ,ili kama warumi wakifika wajue kua walikua na uwezo wa ku ishi zaidi ila walichagua kufa kishujaa na huru kuliko kua Utumwa. Pamoja na yote, Imani ya Kiyahudi(Judaism) inakataza kujiua.

Pia Wako wanazuoni mbalimbali wanaokosoa ushujaa wa wasikarii wa kujiua

Muasisi wa Taifa La kiyahudi na Mwanasayansi na Baba wa Industrial Fermentation Raisi Chaim Weizmann. Akihutubia katika Bunge la Wazayuni Decemba 9Mwaka 1946, mjini Basle. Kwa kauli yake kali iliyojaa msimamo, Alikosoa uamuzi huo wa Wayahudi wa Sikarii uliopelekea kizazi chao kuangamia chote bila kuacha matumaini. Alikiiita kitendo chao ni Janga kwa historia ya Wayahudi. Alitaka Uzayuni iwe ndio mwisho wa Kujitoa Mhanga na Uwe mwanzo wa kutafuta njia mpya ya maisha.

Upinzani wa pili ulioletwa na Bar Kochba mwaka 131E - 135E ulikua mbaya kuliko uliopita. Ambapo Wayahudi walichinjwa na Warumi na kuogelea Damu.

Mpaka mji wa Judea ukabadilishwa jina ukaitwa PALESTINA, hii ni kulingana na wafilisti walioishi Gaza na Ashdodi milenia iliopita.

Mji mkuu wa Jerusalemu ukaitwa ILIA CAPITOLINA na jengo la ibada la Mungu Jupiter likajengwa hapo ambapo ndio kuna mlima Hekalu(Temple Mount).

Hali hii ilipelekea Wayahudi Kwa ujumla wao kupinga sana harakati zozote za Kijeshi.

Ikafanya hadi kiongozi wao mkuu anayeita HASMONEANS pamoja na kwamba alishinda vita dhidi ya Jeshi la Selucid na dhidi ya Warumi kutoku kuenziwa kwenye 'Mishnah na Talmud.'

Pia wakati wote wayahudi wakiwa uhamishoni wamekua wakionyesha hisia zao kupitia maombi na Mafunzo (Eretz Israel) lakini sio kwa njia ya Vita. Walikua Wakitumainia muujiza wa Messiah.

Vilevile Wanaharakati wa karne ya 19 waliotaka kuunda Taifa la Israel kama Theodore Herlz hakuweka mbele mkakati wowote wa kivita.

Waliamini bila uzoefu wowote kua Mataifa makubwa yangewapa nchi yao ya ahadi na waarabu ambao ni wenyeji wangewakaribisha bila matatizo yoyote kwenye nchi ya ahadi.

Hata hivyo Bwana Theodore Herlz mpaka anafariki, alishindwa kupata kibali (ie.Charter).

Baada ya Herlz kufariki.

Mwaka 1904, Weizmann mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Manchester na kiongozi miongoni mwa Wazayuni wa kiingereza. Kipindi ambacho Arthur Balfour alikua Waziri Mkuu na pia ni mbunge akiwakilisha wilaya ya Manchester. Balfour aliunga mkono makazi ya wayahudi.

Chaim Weizmann alipata kibali kwa waingereza kupitia mkataba wa Balfour declaration mwaka novemba 2 mwaka 1917 akiwahakikishia kupata Taifa lao bila Vita. Ambapo eneo lilikua sehemu ya Utawala wa Ottoman.(Sio waarabu).

Hata hivyo kwenye Vita ya kwanza ya Dunia Wayahudi walikua wameunda kikosi cha jeshi(Battalions) kilipigana sambamba na Uingereza, ambapo kilifanikiwa kuchukua eneo hili. hata hivyo kikosi hiki kilikuja kuvunjwa mara tu, baada ya Vita kuisha.

Mnamo Mwaka 1922 Uingereza kupitia Jumuiya ya Madola, walipewa haki ya kuisimamia Palestina (Palestine Mandate)

Waarabu hawakutumia kikamilifu jumuiya ya kimataifa kwa faida yao, ndio iliofanya wakafeli kwenye ku bargain kuhusu Eneo la Palestina. Israel akaibuka mshindi.

Hatimaye tangu Abraham mpaka Yesu Kristo mpaka Trump. Jerusalem imekua rasmi mji mkuu wa Israel.
 
Masada inavyoonekana katika Picha mbalimbali
300pxIsrael2013Aerial21Masada.jpg
3e81dd01f1ab14805d21a0658270c160israeltripvirtualtravel.jpg
 
Hii nimeipenda sana mkuu. Nilikuwa nasoma tu Massada Complex nikawa sijui kwa undani kumbe issue yenyewe ndo hii. Big up. Naona great Thinker inaanza kurejea JF
 
Hii ni nchi ya mauaji sio nchi ya ahadi, imegharimu maisha ya wengi kabisa
 
Kumbe Yuda ilibadilishwa Jina kutokana na uasi wao wa mpinga kutawaliwa na kuitwa Palestine ingawa Pia Palestine imetokana na Jina Philistine kwa maana ya wafilisti.
 
Nitajie nchi ambayo Haina Mauaji?
Ubaya ni mauaji kuasisiwa na kile kinachoitwa mafunuo ya Mungu, hii inakua ni kisasi siku zote , mtu anapanua mdomo wake akijitamba eti kapewa nchi na Mungu , huu ni upunguani
 
Si kweli.
WaIsrael walianza Harakati za Kurudi kwao pale kwenye Asili yao, kama njia ya kukimbia Jewish Holocaust iliyokua ikiendelea huko Ulaya Magharibi(Kama German nk) na Mashariki(Urusi). Walifanya hivyo kama solution to their problem.

Na walitumia Vizuri haki yao Pale United Nation. Wakapewa Ardhi kihalali na Uingereza iliyokua na Mandate ya kuamua. Kipindi Urusi iko bize na Bolshevic rEvolution Rejea mkataba wa Balfour.

Vurugu ilikuja kwasababu walijitangaza Taifa 1948.
Waarabu hawakutaka iwe Taifa.

Waarabu, kwasababu zilizojikita ndani ya imani yao, wanatamani kuangamiza Kizazi chao kisiwepo katika Uso wa Dunia. Chuki yao ina mizizi katika Imani. Sio swala la Occupation kama unavyotaka kuaminishwa.

Na wayahudi wana kila sababu ya Kujihami dhidi ya hatari inayowakabili kwasababu ya Uchache wa Watu katika Taifa lao.

Zingatia, imani ya Judaism haina itikadi zozote za Vurugu wala shari duniani kote. Haina tofauti na dini zingine kama Hinduism, Bahaism, Budhism, Rastafarian, Christianity, Zoarastarian(Iran), Taoisim. Hizi sio dini zenye misingi ya ku-bully imani za watu wengine.
Kwasababu Siri ya mafanikio yao ni kuwekeza utakaso wa Kiroho zaidi badala ya Kimwili tu.

Ku sum-up, Judaism sio miongoni mwa Dini hatari katika Ulimwengu huu. Licha ya Imani iliyojengeka kua ardhi wamepewa na Mungu. Na wanaoamini hii nadharia ni JudeoChristians.

Jewish wengi especially (Jewish Rabbi)hawaikubali. Na laiti wangekua wanaiamini, leo hii pasingekua na vurugu pale mashariki ya kati maana walikua na Muda wa kutosha wa kulikomboa eneo lao ila walichelewa kutokana na kutoafikiana katika hili na Imani yao enzi za Herltz.

Muda waliotumia kutofautiana ulibadilisha hali ya pale middle East, kiasi kwamba walipoamua kwenda, pale wakakutana na Ugumu. Ambao mwanzoni haukuwepo.
Kumbuka Palestine halikua eneo linalomilikiwa na mtu yeyote.
Lilikua eneo huru.
 
Asilia yao maana yake ni nini ? ata kitabu wanachokitumia kama ngao ya kupora lile eneo kinatambua kuwa pale sio asili yao,mbona unazungumza kana kwamba umetoka usingizini, nakubaliana na wewe kuwa uingereza alichangia sana Israel kurudi pale na kuanza kuchukua maeneo ya watu waliokuwa wakiisha pale , ila hawana asili ya pale ata kidogo ila ni watu kutoka mbali tu
 
Asilia yao maana yake ni nini ?
Wataalamu wa Masuala ya Kale wanatambua kua Moja ya Vyanzo vikuu vya kufahamu Taarifa za Kale ni Bibilia. Bibilia ni kitabu kikongwe sana kati ya vitabu vichache vikongwe ulimwenguni. Ndio kitabu cha kwanza kuchapishwa na Mashine ya Kwanza ya Kuchapa Vitabu ya Gutternburg. Kitabu hiki kimeeleza kuhusu asili ya Wana wa Israeli. Viko vyanzo vingine vinavyotambua Kua Wana Wa Israel asili yao ni pale Israel kama vile Qur'an na vingine vingi sana. Hakuna shaka duniani kua asili ya Wana wa Israel ni pale Mashariki ya Kati. Mpaka leo yapo maeneo yanatumia majina ya asili yaliokuwepo zamani hizo kama Hebron,nk.

ata kitabu wanachokitumia kama ngao ya kupora lile eneo kinatambua kuwa pale sio asili yao,mbona unazungumza kana kwamba umetoka usingizini,
Kitabu kipi wanachotumia. Kiwlonyeshe hapa na uweke nukuu. Usiwe unaropoka tu.

nakubaliana na wewe kuwa uingereza alichangia sana Israel kurudi pale na kuanza kuchukua maeneo ya watu waliokuwa wakiisha pale , ila hawana asili ya pale ata kidogo ila ni watu kutoka mbali tu
Inaonyesha unakuja na stori za kwenye kahawa. Ili twende vizuri, Eleza alichukua maeneo ya nani?
 
Back
Top Bottom