kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.
2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.
3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.
Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.
Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.
2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala.
3. Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.
Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari.
Nadhani Nusrat anatuonesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu.
Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nusrat kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nusrat atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini.
Pole Nusrat na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona una kitu cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.
Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.