Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Imeendelea na Ziara Yake ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Meatu Jimbo la Kisesa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

KAMATI YA SIASA MKOA WA SIMIYU IMEENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI WILAYA YA MEATU, JIMBO LA KISESA

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake Ndg Shemsa Seif Mohammed leo tarehe 23/11/2023 imeendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Meatu, Jimbo la Kisesa

Katika Jimbo la Kisesa jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya bilion 5.643 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.

Miradi hiyo ni pamoja na;
1. Mradi wa Uboreshaji wa Chanzo Cha Maji kinachohudumia Mwanhuzi mjini kilichogharimu Tsh 282,000,000/-

2. Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mbugayabanhya uliogharimu Tsh 584,000,000/

3. Ujenzi wa Daraja Barabara ya Mwandoya-Makomangwa-Mwandu Itinje uliogharimu Tsh 197,000,000/ ikiwa ni sehemu ya Mfuko wa Jimbo la Kisesa.

4. Mradi wa kuweka Umeme Shule ya Sekondari Mwabusalu iliyogharimu Tsh 40,000,000/-

5. Mradi wa Maji Kijiji cha Inonelwa kata ya Mwandoya uliogharimu Tsh 4,000,000,000/- na

6. Ujenzi wa Shule Mpya ya Mwandu Nkololo iliyogharimu Tsh 540,000,000/-

Kamati ya Siasa ya Mkoa Simiyu imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na Utekelezaji wa Miradi hiyo.

Lumen Mathias Ngunda
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu

WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.38.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.39.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.39.jpeg
    132.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.39(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.39(1).jpeg
    120.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.40.jpeg
    147.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.41.jpeg
    130.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.42.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 19.14.42.jpeg
    128.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom