Miaka mitatu ya Rais Samia na ukwapuaji wa matrilioni ya pesa za walipa kodi

Shakari

Senior Member
Jul 6, 2022
157
440
MIAKA MITATU YA SAMIA NA UKWAPUAJI WA MATRILIONI YA PESA ZA WALIPA KODI.

Na Mwandishi wetu

5 November 2023. 23:05 Botswana

🔹Nimekuwa nikisema mara nyingi Uongozi makini ni ule uongozi unaowajali wananchi na kujali maslahi ya nchi na taifa lakini kwa uongozi huu ni bora uongozi na sio uongozi bora.

🔹Msomi au mtumishi wa umma anaanza kazi (ajira serikalini) akiwa na miaka 25 na anapofikisha miaka 55 anastaafu kwa hiari au anapotimu miaka 60 anastaafu kwa lazima. Bado anakatwa makato kibao bila ya huruma pesa ambazo kwa sasa kulipwa inakuwa kipengere.

🔹Watumishi wa Idara za Elimu na Afya wanafanya kazi masaa 24 lakini wanapostaafu wanalipwa kiinua mgongo kisichozidi milioni 150, na bado walipwe kwa masharti ya kutunziwa eti (kikokotoo).

🔹 Wanasiasa hasa Wabunge wanafanya kazi Bungeni kwa miaka mitano (5) tu wanalipwa kiinua mgongo zaidi ya milioni 400. Mshahara wa kila mwezi tsh milioni 16 kwa sasa ingawa zamani ilikuwa tsh milioni 12 wana bima za afya VIP na wanakopeshwa magari ya zaidi ya tsh milioni 500. Halafu tunasema tunatengeneza usawa huku watoto wao wanasoma shule za grade za juu na watoto wa mlalahoi wanasoma shule za changanyikeni?

🔹Ndio maana nasema tuweke utaratibu wa Mbunge kuongoza Jimbo iwe ni katika awamu 2 tu na ikitokea moja ameshindwa basi ni heri asirudie ili iwe fundisho na kumchagua mwingine ili tutengeneze mamilionea wengi. Kwa sababu Uongozi wa nchi hii imeonekana ni fursa na sio kazi ya kuwatumikia wananchi.

🔹Bunge limepitisha malipo na posho kwa wenza wa Viongozi huku hao Viongozi wakilipwa mishahara na posho lukuki za fedha ambazo ni mapato kutokana na fedha za walipa Kodi hii inasikitisha na kufedhehesha sana. Unapotembelea wilaya na majimbo unajionea umaskini uliokithiri kwa wananchi kukosa miundombinu ya barabara, maji na umeme huku madawa yakikosekana mahospitalini. Achilia mbali ya uhaba wa barabara na uhaba wa maji safi na salama. Lipo tatizo la uhaba wa waalimu na madawati mashuleni pamoja na watu kukosa uhakika wa mlo mmoja kwa siku.

🔹Wapo watu wanajisifia na kusema CCM itawale milele na Rais anaupiga mwingi? 🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️ Aisee kama ikitokea mbinguni kuna chanel za tv basi nchi ya Tanzania itakuwa ni Comedian chanel ya Dunia.

🔹 Raia anakamatwa na kipande cha nyama ya swala anafungwa miaka 30 lakini mwizi wa fedha zawalipa Kodi anatolewa Gerezani na kulipwa Mabilioni ya fedha na kuachwa mtaani akizurura.🤔🤔🤔🤔

HOJA KUU.
🩸Chama cha Mapinduzi katika umri wake wa kuanza kazi mpaka kustaafu mmefikia ukomo mnapaswa kujitafakari na kujiuzuru kwani mmetumiza umri wa kustaafu na kwenda kulea wajukuu na vitukuu.

🩸Haiwezekani katika kipindi cha vajeti ya mwaka mmoja tu muonekane mmeiba pesa kiasi cha trilioni 30 na bado tuendelee kuwaamini haiwezekani kamwe. Kama Mheshimiwa Rais hahusiki tunahitaji kuona umewachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwaondoa kazini na kuwafungulia mashitaka wahusika hao wote kwa ufisadi huu.

🩸 Niliwahi kusema ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka narudia CCM na utawala wake mnakwenda kupasuka. Yaani kwa kipindi cha muda mchache tu marafiki zako, wakwe zako, jamaa na marafiki wamejitajirisha na kuwa matrilionea na wewe ni trilionea wa kimataifa?

🩸 Fedha za umma zinawezaje kulipwa kwenye akaunt binafsi? Fedha za umma zinalipwaje kwa watu wasio watumishi wa Umma?
Miamala ya Fedha za umma zinaendaje moja kwa moja kwenye miradi bila kupitishwa na CAG?
Maidhinisho ya pesa za miradi ni lazima yaidhinishwe na Mhe Rais na CAG hii ripoti ya CAG ina maana mheshimiwa Rais hujui au uliidhinisha wewe bila CAG kufahamu na kujua?

🩸 Zaidi ya trilioni 30 zinakwenda kuingia mifukoni mwa watu?
Miamala ya tozo hesabu yake iko wapi?
Pesa za covid hesabu zake ziko wapi?
Pesa na mikopo ya nje zimekwenda wapi?

🩸Ripoti ya CAG ni kwa kipindi cha bajeti ya mwaka 2021/2022 bado Bajeti ya mwaka 2022/2023 hakika tumepigwa tunahitaji kufanya mabadiliko.

Paul Makonda amesema wastaafu wakistaafu nendeni mkalee wajukuu na sisi tunasema CCM mkastaaafu bila ya aibu na kulazimishia Dola.

🔑Utabiri huu ulitolewa mwaka 1995 pale Baba wa Taifa aliposema "CCM sio baba wala mama kama ccm itabadilika niko tayari kuhama" hakika leo angekuwepo angehama na kwa kuwa tunaishi naye mioyoni mwetu hakika Watanzania ondokeni CCM na vyama vya walamba asali ili tujiletee maendeleo kama Watanzania.

🔑Shekhe Yahaya mwaka 2007 alisema "Ipo siku atatokea Rais shupavu na mkali atakayeinyoosha nchi Rais huyu ataongoza kwa muda mchache na atafia madarakani halafu atatokea Rais mwanamke ataliongoza Taifa na baada ya hapo upinzani utashika Dola"

📌 Tanzania nchi yangu haya yanayoendelea ni ulevi wa madaraka na kugawana vyeo bila kuangalia mahitaji ya wanyonge na walalahoi maskini wanaotaabika.

Pitia hiyo ripoti uisome hakika utasononeka.

Mawaziri hawa kama sio kweli CCM mnakula wote kwanini waachwe makazini?

1. Mwigulu Nchemba
2. January Makamba
3. Nape Moses Mnawie
4. Mohamed Mchengerwa
5. Makame Mbalawa
6. Kitila Mkumbo
7. Ummy Mwalimu
8. Bashungwa.
9. Dotto Biteko
10. Stegomena Tax

Na wengine wengi?

Kwanza ni waongo na wanakudanganya na wanajidanganya.

Tunahitaji kuona mabadiliko kama ulivyoambiwa kuhusu VP uliyekuwa umeletewa na timu ileamvaye alikuwa awe Emanuel Nchimbi lakini tukakataa na kukuletea Isdory Philip Mpango.

Pigo la kwanza ni serikali zamitaa na Pigo la pili ni 2025.

Hata uwachukue watu uliowatukana kwa miaka 3 halafu Leo uwarejeshe katika madaraka ni kazi bure.

Mliitwa sukama Gang mkiongozwa na Luhaga Mpina Leo mikakati yao ni kumchukua Luhaga Mpina na kumpa cheo.

Luhaga
Luhaga
Luhaga

Nimekuita mara tatu ukiukubali kupewa cheo na Rais au kuitwa na Msoga Gang umekwenda kujiua kisiasa.

Ulitukanwa sana na ukavumilia vumilia imani na amani yaja wewe ndiwe.

Una mapenzi mema na nchi yako wewe ni chaguo la wapenda haki na kiongozi Bora.

Wapo nyuma yako watu wengi hata Majaliwa na kamati za Ulinzi zipo na wewe.

Kwa Leo naomba niishie hapo namalizia nakusema ushindi wa Yanga ni sawa sawa na ushindi wa wanyonge kwa CCM kushindwa katika chaguzi za serikali za mitaa 2024

Ni mimi Mghaibuni toka Ughaibuni.
 
ACT kazi myake ni kuhujumu vya,ma vingine ikiwa kama ccmc B!
ACT sio ile aliyoipenda Maalim Seif hata kdg, aliyeingia hapo kwa kukaribishwa ni ndumila kuwili hatari na mnafiki!
 
Mifuko ya kijamii wajanja wamekula pesa wananchi wanateseka, wengine wanakufa hospitalini na vitambulisho vyao vya NHIF Mkononi serikali haina pesa wakati wananchi wamekatwa pesa zao za matibabu direct na serikali kupitia mishahara yao. Viongozi, ndugu zao na watoto wao wakiumwa wanaenda kutibiwa nje ya nchi kwa pesa za wananchi wanao teseka na kufa mahospitalini kwa kunyimwa huduma wanayo ilipia kila mwezi kupitia makato ya mishahara yao na pesa zinaenda kwenye matumbo ya wapigaji.
 
Nani wa kumpigania Mkulima ? I wonder ?

Umeongelea Daktari anayepata 150m kwamba ni ndogo wakati mbunge anapata 400m.... Hii ni mbaya lakini suluhisho lako wabunge wabadilishane kila baada ya terms mbili ili wagawane kula pesa za mlipa Kodi...

Narudia tena ni nani wa kumpigania peasant ? Inaonyesha kabisa hapa kila mtu anavutia kwake yeye akipata basi anasahau wengine....

Na siku hawa masikini wakipata chizi wa kuwalaghai hakika kitanuka...., kinachosikitisha hawa wachuma janga watakula na sisi huku ambao hatujahusika na uchawi wao.....
 
MIAKA MITATU YA SAMIA NA UKWAPUAJI WA MATRILIONI YA PESA ZA WALIPA KODI.

Na Mwandishi wetu

5 November 2023. 23:05 Botswana

Nimekuwa nikisema mara nyingi Uongozi makini ni ule uongozi unaowajali wananchi na kujali maslahi ya nchi na taifa lakini kwa uongozi huu ni bora uongozi na sio uongozi bora.

Msomi au mtumishi wa umma anaanza kazi (ajira serikalini) akiwa na miaka 25 na anapofikisha miaka 55 anastaafu kwa hiari au anapotimu miaka 60 anastaafu kwa lazima. Bado anakatwa makato kibao bila ya huruma pesa ambazo kwa sasa kulipwa inakuwa kipengere.

Watumishi wa Idara za Elimu na Afya wanafanya kazi masaa 24 lakini wanapostaafu wanalipwa kiinua mgongo kisichozidi milioni 150, na bado walipwe kwa masharti ya kutunziwa eti (kikokotoo).

Wanasiasa hasa Wabunge wanafanya kazi Bungeni kwa miaka mitano (5) tu wanalipwa kiinua mgongo zaidi ya milioni 400. Mshahara wa kila mwezi tsh milioni 16 kwa sasa ingawa zamani ilikuwa tsh milioni 12 wana bima za afya VIP na wanakopeshwa magari ya zaidi ya tsh milioni 500. Halafu tunasema tunatengeneza usawa huku watoto wao wanasoma shule za grade za juu na watoto wa mlalahoi wanasoma shule za changanyikeni?

Ndio maana nasema tuweke utaratibu wa Mbunge kuongoza Jimbo iwe ni katika awamu 2 tu na ikitokea moja ameshindwa basi ni heri asirudie ili iwe fundisho na kumchagua mwingine ili tutengeneze mamilionea wengi. Kwa sababu Uongozi wa nchi hii imeonekana ni fursa na sio kazi ya kuwatumikia wananchi.

Bunge limepitisha malipo na posho kwa wenza wa Viongozi huku hao Viongozi wakilipwa mishahara na posho lukuki za fedha ambazo ni mapato kutokana na fedha za walipa Kodi hii inasikitisha na kufedhehesha sana. Unapotembelea wilaya na majimbo unajionea umaskini uliokithiri kwa wananchi kukosa miundombinu ya barabara, maji na umeme huku madawa yakikosekana mahospitalini. Achilia mbali ya uhaba wa barabara na uhaba wa maji safi na salama. Lipo tatizo la uhaba wa waalimu na madawati mashuleni pamoja na watu kukosa uhakika wa mlo mmoja kwa siku.

Wapo watu wanajisifia na kusema CCM itawale milele na Rais anaupiga mwingi? Aisee kama ikitokea mbinguni kuna chanel za tv basi nchi ya Tanzania itakuwa ni Comedian chanel ya Dunia.

Raia anakamatwa na kipande cha nyama ya swala anafungwa miaka 30 lakini mwizi wa fedha zawalipa Kodi anatolewa Gerezani na kulipwa Mabilioni ya fedha na kuachwa mtaani akizurura.

HOJA KUU.
🩸Chama cha Mapinduzi katika umri wake wa kuanza kazi mpaka kustaafu mmefikia ukomo mnapaswa kujitafakari na kujiuzuru kwani mmetumiza umri wa kustaafu na kwenda kulea wajukuu na vitukuu.

🩸Haiwezekani katika kipindi cha vajeti ya mwaka mmoja tu muonekane mmeiba pesa kiasi cha trilioni 30 na bado tuendelee kuwaamini haiwezekani kamwe. Kama Mheshimiwa Rais hahusiki tunahitaji kuona umewachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwaondoa kazini na kuwafungulia mashitaka wahusika hao wote kwa ufisadi huu.

🩸 Niliwahi kusema ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka narudia CCM na utawala wake mnakwenda kupasuka. Yaani kwa kipindi cha muda mchache tu marafiki zako, wakwe zako, jamaa na marafiki wamejitajirisha na kuwa matrilionea na wewe ni trilionea wa kimataifa?

🩸 Fedha za umma zinawezaje kulipwa kwenye akaunt binafsi? Fedha za umma zinalipwaje kwa watu wasio watumishi wa Umma?
Miamala ya Fedha za umma zinaendaje moja kwa moja kwenye miradi bila kupitishwa na CAG?
Maidhinisho ya pesa za miradi ni lazima yaidhinishwe na Mhe Rais na CAG hii ripoti ya CAG ina maana mheshimiwa Rais hujui au uliidhinisha wewe bila CAG kufahamu na kujua?

🩸 Zaidi ya trilioni 30 zinakwenda kuingia mifukoni mwa watu?
Miamala ya tozo hesabu yake iko wapi?
Pesa za covid hesabu zake ziko wapi?
Pesa na mikopo ya nje zimekwenda wapi?

🩸Ripoti ya CAG ni kwa kipindi cha bajeti ya mwaka 2021/2022 bado Bajeti ya mwaka 2022/2023 hakika tumepigwa tunahitaji kufanya mabadiliko.

Paul Makonda amesema wastaafu wakistaafu nendeni mkalee wajukuu na sisi tunasema CCM mkastaaafu bila ya aibu na kulazimishia Dola.

Utabiri huu ulitolewa mwaka 1995 pale Baba wa Taifa aliposema "CCM sio baba wala mama kama ccm itabadilika niko tayari kuhama" hakika leo angekuwepo angehama na kwa kuwa tunaishi naye mioyoni mwetu hakika Watanzania ondokeni CCM na vyama vya walamba asali ili tujiletee maendeleo kama Watanzania.

Shekhe Yahaya mwaka 2007 alisema "Ipo siku atatokea Rais shupavu na mkali atakayeinyoosha nchi Rais huyu ataongoza kwa muda mchache na atafia madarakani halafu atatokea Rais mwanamke ataliongoza Taifa na baada ya hapo upinzani utashika Dola"

Tanzania nchi yangu haya yanayoendelea ni ulevi wa madaraka na kugawana vyeo bila kuangalia mahitaji ya wanyonge na walalahoi maskini wanaotaabika.

Pitia hiyo ripoti uisome hakika utasononeka.

Mawaziri hawa kama sio kweli CCM mnakula wote kwanini waachwe makazini?

1. Mwigulu Nchemba
2. January Makamba
3. Nape Moses Mnawie
4. Mohamed Mchengerwa
5. Makame Mbalawa
6. Kitila Mkumbo
7. Ummy Mwalimu
8. Bashungwa.
9. Dotto Biteko
10. Stegomena Tax

Na wengine wengi?

Kwanza ni waongo na wanakudanganya na wanajidanganya.

Tunahitaji kuona mabadiliko kama ulivyoambiwa kuhusu VP uliyekuwa umeletewa na timu ileamvaye alikuwa awe Emanuel Nchimbi lakini tukakataa na kukuletea Isdory Philip Mpango.

Pigo la kwanza ni serikali zamitaa na Pigo la pili ni 2025.

Hata uwachukue watu uliowatukana kwa miaka 3 halafu Leo uwarejeshe katika madaraka ni kazi bure.

Mliitwa sukama Gang mkiongozwa na Luhaga Mpina Leo mikakati yao ni kumchukua Luhaga Mpina na kumpa cheo.

Luhaga
Luhaga
Luhaga

Nimekuita mara tatu ukiukubali kupewa cheo na Rais au kuitwa na Msoga Gang umekwenda kujiua kisiasa.

Ulitukanwa sana na ukavumilia vumilia imani na amani yaja wewe ndiwe.

Una mapenzi mema na nchi yako wewe ni chaguo la wapenda haki na kiongozi Bora.

Wapo nyuma yako watu wengi hata Majaliwa na kamati za Ulinzi zipo na wewe.

Kwa Leo naomba niishie hapo namalizia nakusema ushindi wa Yanga ni sawa sawa na ushindi wa wanyonge kwa CCM kushindwa katika chaguzi za serikali za mitaa 2024

Ni mimi Mghaibuni toka Ughaibuni.
Kwanza jiulize, hiyo miradi ya awamu ya 5 inakamilishwa na awamu ipi kama siyo ya 6, ikikumbukwa miradi mingi ndo ilikuwa hatua za mwanzo au asilimia ndogo za utekelezaji. Jitafakari acha ubwabwajaji.
 
Back
Top Bottom