Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Mnyika katumia nguvu kubwa kuhalalisha mamlaka yake halafu jioni Halima Mdee anasambaza audio ya kumkejeli.

Mbowe, Mnyika na viongozi wa juu wa CDM umefika wakati wajiuzulu kwa kuambiwa na nafsi zao wenyewe na sio kusubiri fedheha za majukwaani na njiani.
Ikowapi hiyo audio mkuu? Tuwekee hapa.
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY

2. Tumia muda wako kula vizuri, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi

3. Hakikisha unatafuta future ya watoto wako na wewe mwenyewe kwa njia zingine zozote nje ya siasa

4. Sio kila unaemuona kanisani kavaa koti kafunga mikono kifuani anasali kwa unyenyekevu anakuwa ana maanisha


Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Hili nakuunga mkono
 
Ili mtu ateuliwe kuwa Mbunge Viti Maalum anatakiwa kujaza fomu za NEC namba 8D ambazo sehemu C Inatakiwa kujazwa na Katibu Mkuu wa Chama, na kiapo mbele ya Hakimu. Kama NEC imepokea hizo fomu, Mnyika alizijaza?

Kama Mnyika anatuambia akuzijaza, Nani alizijaza?

Je, NEC wanamjua Katibu Mkuu wa Chadema? Ndiye huyo aliyejaza?

Nusrat alikuwa Mahabusu, je, Nani alimjazia hizo fomu na alimjazia akiwa wapi na kuzirejesha Chadema? Je, mahakamani Nani alikwenda kuapa au Nusrati alitolewa akapelekwa mahakamani kimyakimya?

Je, sheria inaruhusu mtu kumjazia fomu za Ubunge mteule ambaye hayupo?Hakimu gani alimuapisha mtu asiyekuwepo?

Kama huu mchakato haukufuatwa Kuna umuhimu wa kuwa na taratibu na sheria?

Nasrati na wenzake walifutiwa mashtaka wakati gani na mbele ya hakimu Nani?

Kama lengo ni kuiua CHADEMA je tunaamini tunaiua au tunaua imani ya wananchi kwa vyombo vilivyopewa dhamana ya kusimamia haki?

Endapo mahakama ilimnyima Nusrat na wenzake dhamana, then over suddenly Jamhuri inajitokeza na kuwatoa ndani kisha bila kusita anatinga bungeni hatuoni Kama mahakama inatumika kuwaweka Mahabusu watu wasio na hatia kinyume kabisa na misingi ya uwepo wa chombo hiki?

Kama moja ya kazi ya Mahakama nikutenda haki, ni wakati gani Mahakama inapaswa kutenda haki? Ni baada ya kumnyima mtu Uhuru kwa miezi au miaka wakimtia Mahabusu? Au ni pale tu Mtuhumiwa anapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ndipo mahakama inapaswa kutenda haki?

Je, mahakama huru inaona ni haki kuendelea kupokea chaji zisizo na mashiko chini ya amri ya kiapo Cha DPP kuwatia watu ndani?

Kwanini tuendelee kuamini mahakama ni chombo Cha haki Kama binadamu wanaopaswa kusimia haki hawapo tayari kuisimamia?
 
Hata wakiwachukua hao wanawake 19 bado EU hawatoi 900B...wanajifanya wazungu hawajui kinachoendelea....Halima & Co watafukuzwa Chadema ijumaa wakawe wabunge wa Mahakama na EU hawatatoa $900m
 
Ili mtu ateuliwe kuwa Mbunge V.Maalum anatakiwa kujaza fomu za NEC namba 8D ambazo sehemu C Inatakiwa kujazwa na Katibu Mkuu wa Chama, na kiapo mbele ya Hakimu. Kama NEC imepokea hizo fomu, Mnyika alizijaza?...
Zetu dua. Ila nalifuatilia hili suala kwa ukaribu kabla ya kustaafu kufatilia siasa zetu hizi.
 
Hapo kwenye "natumai hakulala"

Alikuwa anapigwa miti, kupunguza kichupa cha mahabusu..

Hahaa...
 
Tunaendeshana kipumbavu sana. Hamna sheria wala taratibu ni mihemko tu, alafu utakutana na watu wanatetea ujinga.
 
Tunaendeshana kipumbavu sana. Hamna sheria wala taratibu ni mihemko tu, alafu utakutana na watu wanatetea ujinga.
Uzalendo kwa CCM ya sasa ni kuwabambikia kesi wapinzani na uonevu unyanyasaji mateso kwa wapinzani
 
Back
Top Bottom