Rostam aibukia kanisani!

Rostam aliangukia Kanisa
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:01

"...Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,''

"Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,'' alisema.

Yeye Rostam ni muumini wa Dini gani?

Daily News, tafadhali!
 
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Rostam aliangukia Kanisa
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:01

Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Amkeni ya Usharika wa Kinondoni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambako alikuwa mgeni rasmi.

Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki na hivyo ni vizuri wakaitumia fursa hiyo kuliombea taifa. “Nawashukuru kwa kunialika kuwa mgeni rasmi leo hii…ni ishara kwamba mmeamua kupuuza vijimaneno na upuuzi wa vijiweni.

Nafurahi kuwa miongoni mwenu….hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,’’ alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo. Alisema inasikitisha kuwa katika zama hizi watu wanachukiana hadi kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo.

“Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,’’ alisema. Mbunge huyo ambaye katika siku za karibuni jina lake limekuwa likitajwa katika mijadala mbalimbali bungeni alisema licha ya matatizo ya kisiasa yanayolikabili taifa sasa, kuna matatizo ya jamii ambayo alisema ni vizuri yakashughulikiwa kama ya ndoa kuvunjika, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, madanguro, kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya na mengine yanayoongeza mmomonyoko wa maadili.

Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini.
Hao waliomshangalia RA ni watumwa wa AKILI na hao waliomwalika wachunguzwe na SAID Mwema kwenye kusaidia UCHUNGUZI!
Yani ameshangiliwa kanisani kwa milioni saba na sasa hata kashfa anaziita maneno ya vijiweni?!
Hapo ni kijembe kwa jf! Na wanaenda makanisani kujisafisha!
Waumini mnakubali kuuza UHURU wenu na kumshangilia mtuhumiwa wa mabilioni ya dola?
Kweli sasa kazi ipo!
Na makanisa pia yanaongozwa na MAFISADI?
 
Sheria zilizowekwa zikiwa ni za Watu...Then ni sheria za Mungu!
Kama ni HAKI...Then HAKI ni SHERIA!
Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.
Hatuwezi kusema kama kipindi hiki ni kile cha Musa jangwani!
Sheria zote za Duniani zimetokana na AMRI KUMI ZA MUNGU!
Sasa Sheria ndio haki kwa Mtanzania aliyopewa na MUNGU NA si MILIONI SABA NA VITISHO!

Sasa angalia kumbe kanisani ameanza kwenda siku nyingi hata kabla ya kuubiliwa ufisadi.

Kusema uongo Mungu anakataza
 
Hapo anapodai kuwa atawapeleka watoto wake huko...Haogopi atatengwa na waislam?

Ama ni kama haamini kuwa ujumbe huo huo wa kuliombea TAIFA angeweza kuutoa hata msikitini?

Kama kweli una ujumbe kuwa kuna vijimaneno vya wivu...Then kwanini usiende kutoa ujumbe wako huko unaposali kama si PR TU?

Cha muhimu ni kuwa RIPOTI IKISOMWA NA IKAGUNDULIKA KUWA HANA MAKOSA...Basi na MIMI NITATOA HIYO MILIONI SABA KAMA YEYE!

We ROSTAM ACHA HAYO MAMBO YA KUWAFANYA WATANZANIA NI WATUMWA WA AKILI!

Subiri RIPOTI zisomwe na baada ya HAPO...Na kushauri ufanye saba mara saba...Utowe milioni 49...Kwani nina imani hiyo ni pesa ambayo hailingani hata na gari lako ama hata la mtoto ama ndugu yako!

Milioni saba ni ela ya kula acha wananchi wakae kwani mlishawapa pilao na kandamili mkauza nchi na sasa mnafikiri tutakaa kimya?
 
Makanisa nayo kwa kukumbatia majambazi ndio wenyewe, hivi kuna haja gani ya kupokea michango ya watu kama Rostam?

Makanisa hayo hayo yanamweka viti vya mbele fisadi Mkapa. Pia walisema JK katumwa na mungu, makanisa siku hizi yamegeuka kuwa biashara. Ni aibu kweli kweli.

Mimi tangu waseme hii kauli, kwamba JK katumwa na Mungu, siwaamini kabisa hawa jamaa wa kanisa. Viongozi wa dini TZ ni sehemu ya tatizo. Nchi zingine zote zenye kusaka ukweli na demokrasia kama Kenya, Zambia, n.k viongozi wa dini wapo mbele lakini TZ ndio hivyo tena!
 
Rostamu asante kwa kusaidia kwaya!Kama ni ufisadi kwani unawaabia Wtz wenyewe wakiwa wapi?mjinga ndo aliwae!
 
Makanisa nayo kwa kukumbatia majambazi ndio wenyewe, hivi kuna haja gani ya kupokea michango ya watu kama Rostam?

Hawajapokea tu. Wamemuomba!

Wamemwalika aje kuwa mgeni wa heshima. Walijua hatakuja mikono mitupu.

Na RA alivyokuwa savvy politician, he made sure to highlight "...ahsanteni kwa kunialika."

Kwamba hakujileta mwenyewe.
 
Muacheni Rostam alete hela, kwani mnauhakika gani sadaka zote zinazotolewa na waumini huko makanisani kwamba ni safi....!?

Kwani hata Chenge nae si muumini na anatoa sadaka kanisani pia? Je zake ni safi au chafu? So Muacheni Rostam atoe sadaka hata kama ni chafu, cha muhimu ambacho mi NAPINGA ni yeye kujitafutia ujiko kwa kutoa sadaka na kuanza kujisifu kwamba amesaidia kanisa. Hilo ndio mimi silikubali.

Lakini sioni kama kuna makosa mtu kutoa sadaka/zaka.
 
Na tuhuma za Uraia wa Iran na Tanzania ni za Uwongo?
Na yeye kudai kuwa kumtuhumu yeye ni sawa na kutaka amani ipotee na hapo hapo anadai kuwa alishukuru kanisa hilo kwa kuto kumuhukumu!
Sasa kanisa ndio linalotoa hukumu? Kwanini tu hasisubiri mara baada ya bunge kujadili ripoti?
Hatutaki watu wajisafishe.
Na wakati wote alikuwa wapi hadi aende akajibu tuhuma kanisani?
Je alishawahi kusema maneno kama hayo huko anakosali kila siku ama ameamuwa kuyagawa makanisa kwa pesa zake?
 
Muacheni Rostam alete hela, kwani mnauhakika gani sadaka zote zinazotolewa na waumini huko makanisani kwamba ni safi....!?

Kwani hata Chenge nae si muumini na anatoa sadaka kanisani pia? Je zake ni safi au chafu? So Muacheni Rostam atoe sadaka hata kama ni chafu, cha muhimu ambacho mi NAPINGA ni yeye kujitafutia ujiko kwa kutoa sadaka na kuanza kujisifu kwamba amesaidia kanisa. Hilo ndio mimi silikubali.

Lakini sioni kama kuna makosa mtu kutoa sadaka/zaka.

ALah!
Kumbe kanisa la Kinondoni walimwita akatoe zaka na sadaka!?
Kwani huwa hatoi hizo zaka na sadaka huko anakosali kila ijumaa?
Mhafidhina umeniacha hoi na mambo ya zaka na sadaka!
Hapo wala hakutangaza kuhusu zaka na sadaka...Bali aliwapongeza kwa kumwalika ili aje kutoa zaka,sadaka na VIJEMBE!
 
Wanafunzi wa chuo cha tumaini SUSIENI MASOMO kishinikizeni chuo chenu kama hakitaki kujenga majengo mengine basi ninyi muache masomo.

Maana baadhi ya majengo yenu yamejengwa na fisadi,.

"Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini."
 
Wewe ni mmoja wa wale ambao mnawatetea mafisadi kwa kila hali na hatimaye kuzorotesha vita dhidi ya mafisadi. Mafisadi wanaiba mabilioni wakijenga vidarasa vichache vya milioni 20 mnataka kuwatukuza na kuwapa heshima wasiyostahili.

Yeye kishaiba bilioni 20 akitoa milioni 20 kujenga vidarasa ili mmuone wa maana na kuacha kumsakama kama fisadi, basi kishafanikiwa kutimiza lengo lake la 'kuuma huku anapuliza' ili Watanzania tusimshtukie. Acha udanganyika kaka fungua macho uone mafisadi wanavyoiangamiza nchi.
 
Tatizo tunashindwa kuelewana.
wewe kama waona namtetea RA na iwe hivyo ,mimi ninachotaka kubainisha ni kua kumulazimisha pasta arudishe zaka maana yake ni hukumu ya ROHO.

Ndio nikakweleza mchukueni RA mkamhukumu kwa sheria za Ki kaizar hapo hukunielewa tu.

Nyie ndio mnatukuza binadamu wezenu kwa kuwaita MHESHIMIWA.Tafuta sehemu yoyote nilipochangia posts karibu 1000 kama utakuta neno hilo. Mheshimiwa ni mmoja tu
 
Wewe ni mmoja wa wale ambao mnawatetea mafisadi kwa kila hali na hatimaye kuzorotesha vita dhidi ya mafisadi. Mafisadi wanaiba mabilioni wakijenga vidarasa vichache vya milioni 20 mnataka kuwatukuza na kuwapa heshima wasiyostahili.

Yeye kishaiba bilioni 20 akitoa milioni 20 kujenga vidarasa ili mmuone wa maana na kuacha kumsakama kama fisadi, basi kishafanikiwa kutimiza lengo lake la 'kuuma huku anapuliza' ili Watanzania tusimshtukie. Acha udanganyika kaka fungua macho uone mafisadi wanavyoiangamiza nchi.

Mkubwa kuhusu kuiangamiza nchi ,Taifa la Mungu linaangamia tz watoto wa Mungu tunatesekaka,tunakosa elimu,tunakosa huduma za afya,tunaangamia kwa majanga yasiyo ya lazima ni kwasabu ya mteule wa kulikomboa Taifa hili hajaja.

Vyama vingi vya uongo vitakuja na kusema mimi ndiye mkombozi wa Taifa hili .Lakini Tazameni tumepewa macho ya kuona ,masikio ya kusikia na AKILI pia ya kung'amua.Mkombozi wa Taifa hili Atatokea mtu mmoja kwa wakati muafaka na si GENGE la MBWA mwitu wakali.
 
Bila fedha ya mafisadi, tunafunga makanisa!!!!

Uto tu-milioni saba cha RA ni kajisenti tu kati ya mafedha mengi yanayochangiwa na mafisadi makanisani!!!!!
 
1. Rostam kwenda kanisa la Spika kutoa hela kwa kwaya ya kanisa hilo, hiyo ni politics tena chafu sana, ni lazima ikemewe kwa nguvu zote na jamii.

2. Rostam kutoa hela kwa kwaya ya kanisa, now this is God's call kwa sababu hata shetani ana-operate kwa kuruhusiwa na Mungu tu, na shetani hawezi gusa sehemu yoyote bila ya kuruhusiwa na Mungu, lets say Rostam ni agent wa shetani then kuna mawili hapa either ametumwa na shetani kuisadia kwaya ambayo inaweza kuwa inaonekana kuwa ni ya Mungu lakini ni ya shetani, au Mungu ameamua kumtumia shetani kuisadia kwaya yake, kama kweli ni yake,

Tukumbuke kuwa shetani hawezi kutuuibia wananchi bila ya kuruhusiwa na Mungu, na haya hutokea taifa linapokuwa limemuasi Mungu, hapo anaweza kuruhusu kina Rostam kuliibia taifa, na pia kumsukuma apeleke hela zile kanisani, yule bwana aliyemsaidia mwana wa Mungu wakati alipokuwa amekufa, aliyetoa hela za sanda na the rest of mazishi alikuwa ni fisadi aliyetumiwa na Mungu, sasa we should not get excited mpaka kushindwa kuuona ukweli ambao sisi JF tunahitaji ku-deal nao hasa to the next level nao ni kwa nini Rostam amekwenda kutoa hela kanisa la Spika?

Halafu huyu majuzi nilisema kuwa alikwenda kwa mmoja wa wabunge wa kundi la Mwakyembe in private na kujaribu kumlaghai kwa maneno mengi kuwa yuko innocent na Richimonduli, sasa sisi tulisema siku nyingi kuwa hawa mafisadi wameshikwa pabaya, tena sana na hizi ni dalili za wazi kabisa kuwa it is working na tunahitaji kuendelea kusukuma the envelope na mafisadi mpaka kieleweke!

A Luta Continua!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom