Rostam aibukia kanisani!

Tuliombee Taifa – Rostam Aziz
Sunday, July 6, 2008
Asema watu wanachukiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008

MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kijamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.

Bw. Rostam ametoa mwito huo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi na kuweka wakfu albamu ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki, na kwamba licha ya kashfa za ufisadi anazozushiwa, wamepuuza hilo na wamejenga imani kwake.

"Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii," alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo.

Rostam alisema watu wanachukiana mpaka kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo. "Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi," alisema.

Rostam alisema licha ya matatizo ya kisiasa, kuna matatizo ya kijamii ambayo alisema ni ndoa kuvunjika kila kukicha, watoto wa mitaani kuongezeka, madanguro na dawa za kulevya kukithiri, mambo ambayo yanasababishwa na mmomonyoko wa maadili.

Katika hafla hiyo ya kuweka wakfu kanda za video, kaseti na dvd, Mbunge huyo alitoa mchango wa sh. milioni 5 kuchangia seti za vyombo vya muziki kwa kwaya ya Amkeni pamoja na jenereta yenye thamani ya sh. milioni 2.6. Hiyo ni albamu ya kwanza ya kwaya ya Amkeni iliyodumu kwa miaka 24 sasa.

Mwaka 2005, Rostam pia alishiriki katika harambee ya ujenzi wa jengo la Kanisa la KKKT Kinondoni ambalo kwa sasa linatumika kama Chuo Kikuu cha Tumaini.

Picha za tukio ni hizi hapa chini (attached), kwa hisani ya michuzijr

Ama unaweza click link hii kwenda moja kwa moja kwa michuzijr
http://michuzijr.blogspot.com/2008/07/tuliombee-taifa-rostam-aziz.html
 
Attachments

  • Rostam.jpg
    Rostam.jpg
    219.8 KB · Views: 52
  • Rostamh.jpg
    Rostamh.jpg
    212.5 KB · Views: 52
  • Amkeni.jpg
    Amkeni.jpg
    285.2 KB · Views: 42
By the way, according to the dataz ni kwamba hivi karibuni watoto wawili wa Balali, walikwenda Iringa huko nyumbani kijijini na ki-box kidogo kinachosadikiwa kuwa na mabaki ya mwili uliochomwa wa Balali na kufanyika maombolezo rasmi kwa wanafamilia huko Iringa, shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na waziri mmoja wa serikali ya sasa,

Wanafamilia wamekasirika sana kuona mjane hakutokea na watoto na mabaki ya mwili, samahani wakuu nilitaka kuhabarisha tu the up-to-dates.

Ahsante Wakuu!
 
Tuliombee Taifa – Rostam Aziz
Sunday, July 6, 2008
Asema watu wanachukiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008

MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kijamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.

Kalakabaho man.....umekula chini SIR GOD hahongeki!!!!!!!!!
 
Tuliombee Taifa – Rostam Aziz
Sunday, July 6, 2008
Asema watu wanachukiana na kuombeana vifo
Adai wanazushiana uchawi, anapakaziwa fisadi
Aomba kanisa litumike kurejesha taifa katika mstari
Dar es Salaam, Julai 6, 2008

MBUNGE wa Igunga, Bw. Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu kisiasa na kijamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.

Bw. Rostam ametoa mwito huo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi na kuweka wakfu albamu ya kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki, na kwamba licha ya kashfa za ufisadi anazozushiwa, wamepuuza hilo na wamejenga imani kwake.

"Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii," alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo.

Mwaka 2005, Rostam pia alishiriki katika harambee ya ujenzi wa jengo la Kanisa la KKKT Kinondoni ambalo kwa sasa linatumika kama Chuo Kikuu cha Tumaini.

Wale wote mnaopigia debe Upinzani, kaeni chonjo Kinondoni inarudi CCM!

Cha kupima hizi kelele zetu za harakati ni kujua kuwa hawa waumini wa pale Kinondoni kuanzia Hananasif, Kinondoni Shamba, Ada Estate, Mkwajuni, Morocco, Mwananyamala, Vijana Hostel na kwingineko walituma mwaliko kwa Rostam aje kuzindua na kusimika CD ya kwaya.

Sasa najiuliza, kwa nini hawakumuita Zitto, Mwakyembe, Anna Killango, Dr. Slaa, Ole Sendeka na wale wengine ambao tunadai kuwa ni wanamapinduzi?

Ikiwa Kanisa la Kinondoni na waumini wake walikubali kumualika Rostam Aziz mtuhumiwa wa Ufisadi na walimshangilia kwa nderemo na vifijo, na wote tunajua kuwa Kinondoni iko Dar ambako ni mjini na kuna wasomi wengi na inawezekana kuna Wana JF walioko mitaa ya jirani, jiulizeni kama Kinondoni ilimshangilia Rostam pamoja na kusoma kote magazeti na JF kuhusu Ufisadi, je itakuwaje huko vijijini ambako Uanaharakati wetu wala haufahamiki?

Ina maana Nyani Ngabu yupo sahihi, Ndivyo Tulivyo?
 
Balali huko aliko akiskia story kua inadhaniwa alichomwa moto basi lazma mwili umsisimke kwa hisia za kiberiti..

Hiyo ni katika mikakati ya kutuzuga Watanzania. Wangemzika si tungetafuta kaburi? Sasa hapo juu Mkjj anahoji kama kweli mwili wake ulichomwa moto

1. Familia inasema alifia nyumbani Washington, SIRIKALI inasema alifia hospitali Boston.

2.Wengine wanadai mwili ulichomwa moto, wengine wanadai alizikwa.

3. Padri aliyeuombea mwili wa marehemu anadai pamoja na kuwa ni kawaida ya padri kufungua angalau uso wa aliyekufa ili amuombee marehemu yeye hakufanya hivyo hivyo hawezi kuthibitisha kama kweli kulikuwa na mwili wa binadamu au gogo

4. Mpaka leo familia imeshindwa kutoa post mortem report kuonyesha marehemu ni kipi kilichomsibu mpaka akakutana na umauti wake na pia death certificate ya kutuhakikishia Watanzania kama kweli Ballali amekufa hadi hii leo hatujaiona.

Wangeweza kuwazuga Watanzania wa mwaka 47, lakini wa mwaka 2008 tuna maswali mengi kuhusu 'kifo' cha Ballali ambacho bado kimezungukwa na utata mkubwa.
 
FMES... utazua kasheshe... nani kawaambia mwili wa Ballali ulichomwa..?

Hii ni mfano wa kitabuni wa sababu zinazofanya wengine tuswalishe, au tukatae kata kata, credibility ya hizi dataz na ya mleta dataz.

Sio kwamba tuna letu.
 
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!

Naona sasa polepole utabiri wa Nyerere unatimia. Kabla hajafa alituambia watu watajaribu kumhonga Mungu. Na kweli tunaona sasa mmoja ameenda kuhonga, na ajabu watu wa mungu wamekubali kupokea hongo.
Sijui ana maana gani kwenda kwenye kanisa la Sitta, nadhani anataka kuwaambia watu kuwa Sitta mchawi. Inawezekana kuwa yeye ndio aliyeagiza huo unga!
 
Mimi nafikiri Sitta ana mbeep JK huko Japan!
Kwani kuna UVUMI kuwa JK ndiye main character! Na EL na RA ndio wanadai hivyo na six naona na yeye anafanya mambo ya ajabu ajabu!

Wewe kama spika utaamua vipi kumwalika kanisani kabla hamjatuambia ukweli?
Kabla hata ya ripoti kusomwa? Ripoti ambazo hata nyingine ziko kwa mkaburu na huku SPIKA akiwapeleka mafisadi kanisani?

Je wananchi hawana haki ya kujuwa anachofikiria spika?

Nani asiyejuwa kuwa sasa hata Mwakyembe mwenyewe anasemekana kuwa alificha mambo!

SITTA sasa kila kitu kiko mikononi mwako na tunaomba utoe NAFASI YA UKWELI kuwekwa wazi mbele za wananchi kwani umeamua kumsafisha mtuhumiwa kabla ya bunge kuwahoji!

Sasa kama six anajuwa ukweli kwanini hakuliongoza Bunge inavyotakiwa?

Nani ana uhakika kwamba six na yeye atahakikisha haki inapatikana kama alivyotowa ahadi?
 
By the way, according to the dataz ni kwamba hivi karibuni watoto wawili wa Balali, walikwenda Iringa huko nyumbani kijijini na ki-box kidogo kinachosadikiwa kuwa na mabaki ya mwili uliochomwa wa Balali na kufanyika maombolezo rasmi kwa wanafamilia huko Iringa, shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na waziri mmoja wa serikali ya sasa,

Wanafamilia wamekasirika sana kuona mjane hakutokea na watoto na mabaki ya mwili, samahani wakuu nilitaka kuhabarisha tu the up-to-dates.

Ahsante Wakuu!

Hayo tutayafahamu tu muda si mrefu! Wao wanafikiri hii ni dunia ya enzi za ujamaa!
Na mi nakwambia watu wakae tu mkao wa kula!

NB:Kwenye issue hii ya kanisa...Hatutawalaumu waumini peke yake!
Bali spika Sitta mwenyewe!

Yeye ndiye aliyemwalika na kusema kuwa hawawezi kutoa hukumu!

Sasa kwasababu kila mtu anajuwa wazi kuwa SITTA anaujuwa ukweli wote na kwa mantiki hiyo...Haamini kuwa RA ana makosa!

Sasa spika asipotowa nafasi za mjadala huu kujadiliwa inavyotakikana basi ajuwe na yeye atabebeshwa lawama kwenye uvunjaji wa haki za binadamu!

KWANINI SPIKA AJIHUSISHE KWENYE PROPAGANDA ZA KISIASA ZA WATUHUMIWA?
SPIKA SITTA WEWE UNAMTUMIKIA NANI?
 
JMushi.
Salama mkuu. Mie siamini RA kwenda kanisani anakosali Sitta ni makosa ya Sitta. Siamini kama kweli Sitta anajaribu kumsafisha RA. Tusijeanza kupandikiza chuki dhidi ya Sitta kisa RA kaenda pale na kuchangia Kwaya. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi linapokuja suala la dini. Mtu anaweza kwenda kuabudu mahala popote bila kuvunja sheria.
Mtu yeyote naamini alikuwa ana uwezo wa kuchangia pale awe mkatoliki au muislamu. Mie nilipokuwa huko niliwahi kwenda msikitini mara kadha nikiwa ni aliyekuwa boss wangu (Marehemu) ambaye pia alikuwa msaidizi wa Rais. Lakini mie nimezaliwa, nikakulia na nitazikwa kama mkristo.

Naamini tatizo tulilonalo hapa si RA kwenda kanisani bali hizo fedha alizochangia tunaamini ni fedha chafu. Na fedha chafu haziwezi kupelekwa kanisani au msikitini. Watu wengine wanaweza kuamini pesa hizo ni safi kutokana na shida zetu watanzania lakini ukweli hizo pesa ni chafu. Hakuna anayemdanganya Mungu bali tunajidanganya sisi wenyewe,

Hivyo ningependa uondoe hiyo dhana kuwa Sitta anajaribu kumsafisha Rostam. Hili ni ombi na wala si lazima. Ombi laweza kukubaliwa au kukataliwa, naogopa kuwa watu wanaweza kujenga dhana kulingana na maneno hayo kuwa Sitta anamsafisha RA halafu wakajenga chuki dhidi yake kwa kitu ambacho hatuna ushahidi. Siko hapa kumtetea RA. Hata Makamba (akiwa Mkuu wa Mkoa Dar )alipokuwa anachangisha harambee kwa ajili ya shughuli za KKKT kule Arusha siamini kama alikuwa anajisafisha lakini twende KULIA, KUSHOTO, NYUMA na MBELE ukweli ni kwamba Pesa za RA ZINANUKA but but..... Siamini kama Sitta anajaribu kumsafisha tena kanisani.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi flani lakini si ni SIX mwenyewe anayedai hana siasa za MAJI TAKA?
Sasa hii ni MAJI SAFI?
Honestly..Ni RA mwenyewe kasema kuwa amealikwa...Na mimi ninavyoelewa ni lazima walimwuliza six kabla hawajaamua kumwalika!
Ingekuwa RA ndio kaomba mwaliko...Basi hiyo ni different case...LAKINI KUNA WATU WAMEJITOLEA KUMSAFISHA!
Sasa ni Mchungaji,wanakwaya ama Six mwenyewe ndiye aliyemwalika?
Kwa mtizamo wangu ni WOTE WALIOMWALIKA!
Na wala hakujialika mwenyewe!
 
Na kama hautaki sitta ahusishwe...Then ni kwanini wao walimwalika?
Je ni kwasbabu ya pesa za kwaya?
Ni kwaya ngapi za makanisa mangapi zenye kuhitaji pesa?
Why the church chose RA na kufanya siasa na kumshangilia kama si kanisa la wajumbe?
 
...Sasa ni Mchungaji,wanakwaya ama Six mwenyewe ndiye aliyemwalika?
Kwa mtizamo wangu ni WOTE WALIOMWALIKA! Na wala hakujialika mwenyewe!

Nakubali.

Tunachojua 100% ni kwamba aliitwa na kanisa. Hakuja mwenyewe.

Je, Sitta anahusika na huu mwaliko?

Inawezekana yumo.

Na nimesikia pundits wengine pia wanasema hii itakuwa ni Sitta's connection. Kwaya sidhani inaweza kumkaribisha prominent MP Rostam bila prominent congregant Sitta kujua.

Unless, Sitta hakuwepo kanisani siku hiyo. Hapo ndio angeweza kuji-distance na hii bad public relation. Tungekuwa tuna magazeti Tanzania, wangesema kama Sitta alikuwepo. Press inapenda umbea na udaku lakini umbea unapohitajika ndio hawawezi kuuleta. Lakini nakubali kabisa uwezekano wa Sitta kuwemo humu.
 
some reasoning is not just flawed but extremely unreasonable..!

Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi… ni ishara kwamba mmeamua kupuuza maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…. hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,” alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo.
 
Mie bado sijaamini RA kutoa mchango atakuwa kajiosha. Kila mtanzania mwenye kufuatilia habari za uchumi wetu anajua nini kinaendelea Bongo. Huyu RA hata kama angetoa bilioni kwa kanisa au msikiti bado hajaiosha. Kujiosha kwake ni kwujipeleka yeye mwenyewe mahakamani kabla kesi haijafunguliwa dhidi yake na kueleza uozo wote kuanzia Igunga mpaka uvunguni Ikulu. Ataje uchafu wake pamoja na washirika wake wote. Kisha atumie ujasiri wake anyamaze bila kujitetea kuomba ufupisho wa adhabu. Ale njiti kwanza kabla hajaenda Segerea miaka 20 na ushee.
Matatizo mengi yaliyojitokeza kuhusu uchumi na ugumu wa maisha kwa njia moja au nyingine uumesababishwa na huyu NDULI.

Watatoa misaada sana lakini ukweli unabaki pale pale. THIS GUY is SENIOR FISADI, period.
 
Rostam alisema watu wanachukiana mpaka kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo. "Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi," alisema

Hivi kweli Rostam anakwenda kumtetea CHENGE kanisani mbele za Sitta?
Sitta mwenyewe keshatoa ripoti za "Unga Unga?"

Na kuna waliyozushiwa uchawi na waliyo ombewa vifo...Hivi hakuna walio kufa na majibu hatuna? ooh..ok Ballali alipotea..!?

Sitta utakubali vipi mtu aje kanisani kabla ya bunge mnaloliita tukufu halijasoma ripoti na kuwahoji watuhumiwa?

Ama ni bungeni kumesharogwa na utukufu wake umeisha na sasa kesi ni kanisani?

Kwanini msiwaachie wananchi wajiamulie mara baada ya ripoti kusomwa na wao kuhojiwa na ama kusafishwa na mahakama?

Mnatudharau watanzania kiasi hicho?
 
Nyerere hawezi kuepuka lawama juu ya hili, alidumaza mwamko wa watanzania kiasa, ndiyo maana tunachezewa na mafisadi kiasi hiki bila hata kung'amua kiwango cha dhihaka hii. Rostam na mafisadi wengine wataendelea kutuchezea bila wasiwasi wowote mpaka tutakapo amka!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom