MAJIBU YA MTIKILA.
Ni kweli niliomba fedha kwa Rostam kama mkopo, na nikaandika kwa mkono wangu maelezo kwamba nitazirejesha. Nilimueleza kibanda changu pale Mikocheni kilikuwa kimechakaa na kilihitaji marekebisho. Sikwenda kwake kuomba fedha za ujenzi wa kanisa, alisema Mtikila ambaye alidai alikuwa akijiandaa kumchukulia hatua za kisheria mwanasiasa huyo. (Gazeti la Tanzania Daima).
**********************************************
Ni kweli, Rostam ni rafiki yangu sana, tena siku nyingi, lakini alinipa sh 3 milioni kama mkopo, si fedha za kuendeleza kanisa kama anavyosema. Muulizeni kanisa gani, mimi sijengi kanisa wala siendelezi, wapo wafadhili wa kanisa. Ni fedha za mradi wangu na ni mkopo, alisisitiza Mtikila.
Mtikila alipoulizwa tena katika mahojiano mafupi kwa njia ya simu, kwamba mkopo huo alipaswa kuurejesha kwa muda gani na ni mradi gani hasa aliufanya, alijibu tena: Ni mradi wangu fulani hivi, muda wa kurejesha mkopo ulipaswa kuwa within two months (ndani ya mienzi miwili),
Katika mahojiano hayo, Mtikila alipoulizwa zaidi, kwamba hadi jana miezi miwili ilipita vipi hakuweza kurejesha fedha hizo, alijibu:
Ahaa ni kana kwamba mkopo ni mkopo tu, hata serikali bado inadaiwa na wafadhili na haijalipa hadi sasa, ila mimi nitamlipa ndani ya wiki moja hadi mbili kuanzia sasa,
Mtikila alipoulizwa zaidi, kwamba hata kama ni mkopo, vipi alikopa fedha kwa mtu ambaye amekuwa akimuita fisadi na mwenye kumiliki fedha chafu kwa kuwa pia alipinga Rostam kutoa fedha kwa KKKT, alijibu:
Ni kana kwamba zile fedha si chafu ni za nchi yetu, ni za serikali yetu sema tu matumizi yake na amezipataje Gazeti la Mwananchi..