BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
JF ilikuwa mstari wa mbele katika mjadala huu, na hatimaye mawazo ya wengi kama yalivyotolewa hapa ukumbini kwa mara nyingine tena yameshinda!!. Hongereni JF.
Makanisa yaonywa kuepuka Mafisadi
2008-07-09 09:20:14
Na Anneth Kagenda
Viongozi wa dini, wameonya makanisa yasitumike kama uwanja wa kuwasafisha watu wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi nchini.
Hatua hiyo, imekuja siku chache baada ya Mbunge wa
Igunga (CCM), Bw. Rostam Aziz, anayetajwa katika kashfa hizo, kukaririwa mwishoni mwa wiki, akitoa kauli zenye mwelekeo wa kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi nchini.
Bw. Aziz, alisema kualikwa kwake kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua albam ya Amkeni ya kwaya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) ushirika wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, ni ishara ya kupuuza vijimaneno ya upuuzi wa kijiweni.
Mbunge huyo, alitajwa katika kashfa ya Richmond, iliyotolewa bungeni na Kamati Maalumu ya Bunge, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, wachungaji sita wa madhehebu tofauti, walisema hatua ya Mbunge huyo kutumia `madhabahu` ya KKKT, ni kutaka kulihusisha kanisa hilo na utetezi wa watuhumiwa wa ufisadi.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mchungaji Christopher Mtikila, alisema ingawa alifanikisha kulitumia kanisa hilo, lakini hatua hiyo haipaswi kutafsiriwa kama ni msimamo wa KKKT.
``Tunajua katika KKKT kuna waadilifu, wanaopiga magoti kwa ajili ya kuombea haki, amani na usawa, ukweli ambao hawa mafisadi wanaukiuka,`` alisema.
Alisema, kuna haja kwa makanisa kusimama imara na kuepuka kutumika kama `mapango\' kwa ajili ya kuwaficha watu wanaohusishwa na ufisadi.
Wachungaji wengine walioshiriki kutoa tamko hilo na makanisa yao kwenye mabano ni Gordon Kiyalo (Pentecostal Fellowship Church Int), Gwakisa Mwaibasa (True Light Shining Ministry), Isaac Kalenge (Pentecostal Vision), Ibrahim Sabuni (Jesus Ark Int Ministry) na Primus Ishobeza (Upendo Pentecostal).
Mchungaji Mtikila, alisema Bw. Aziz, anakabiliwa na shutuma za ufisadi zilizomfanya ashindwe kupata mwanya wa kujitetea ndani ya Bunge na katika majukwaa ya siasa.
``Huyu ndugu yetu amebanwa, amekosa pa kutokea, si ndani ya Bunge, katika chama chake cha CCM wala majukwaa ya siasa, kwa wapiga kura wake, ameona mahali pekee ni katika kanisa la KKKT,`` alisema.
Mchungaji Mtikila, ambaye mara kwa mara alirejea madai yake kuwa Mbunge huyo ni raia wa Iran alidai, kwa uzalendo wa wabunge na vyombo vya habari, Bw. Aziz ni mhusika katika kashfa ya Richmond, na baadaye Dowans zinazohusika katika kashfa ya kulipwa isivyo halalali, Sh. milioni 154 kila siku.
Pia alidai kuwa Bw. Aziz, anahusika katika vitendo vya uhujumu uchumi kutokana na kuitumia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, `kukomba` Sh bilioni 33 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha, Mchungaji Mtikila, alimshutumu Mkuu wa KKKT, Askofu Alex Malasusa, kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya kanisa hilo, kutumiwa na wanasiasa, katika kukidhi matakwa yao.
Askofu Malasusa hakupatikana kuzungumzia madai hayo, licha ya jitihada za Nipashe kumtafuta hadi kupitia simu yake ya kiganjani, lakini hakupatikana.
Mchungaji Mtikila, alidai kuwa miongoni mwa wanasiasa waliowahi kuichangia KKKT kwa ushirikiano na Askofu Malasusa, ni Rais Jakaya Kikwete, alipokuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.
Mchungaji Mtikila, alidai kuwa vitendo vya wanasiasa kuitumia KKKT kwa maslahi yao binafsi, ni kielelezo cha Askofu Malasusa kushiriki katika mtandao ulioshinda Uchaguzi Mkuu uliopita.
``Lakini huyu alikuwa mtu mmoja tu, na siyo KKKT?ieleweke kuwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe na kuhukumiwa kwa yale aliyoyanena mwenyewe,`` alisema.
Alisema KKKT kama kanisa, halipaswi kuhusishwa na kashfa ya kutumiwa na Bw. Aziz, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutaka kujisafisha.
Hata hivyo, alikifananisha kitendo kilichofanywa na Mbunge huyo, kama matendo yenye kulinajisi kanisa hilo nchini.
SOURCE: Nipashe