Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

Mkuu ES,
Naomba nikuulize kaswli kadogo tu. Assume wewe ni mwalimu na upo darasani unawafundisha wanafunzi namna ya kusolve swali moja la hesabu, then anatokea mmojawapo wa wanafunzi anasimama na kusema mwalimu unavyofanya sio sahihi? Je utampa nafasi huyo mwanafunzi aonyeshe njia yake ilivyosahihi au utamfukuza darasani?

Inategemea..Walimu wengine wanaweza kuchukulia tofauti wakaleta bifu.

Wengine sivyo..Inategemeana..Mimi nilikuwa darasani na kijana muhindi na alikuwa akienda ubaoni na kushuka equation ambayo imemtatiza mwalimu na wala hakuwa na bifu wala nini!

Lakini hatahivyo sisi tuliosoma na wahindi ilikuwa ni nadra sana kwa wao kulimwa bakora ukilinganisha na weusi.

Hii ni kwasababu wahindi walikuwa wakiwahonga pesa tosha kuliko hata mishahara yao.

Wahindi Walikuwa na vitabu vizuri kuliko hata hao waalimu wanavyovitumia kwenye syllabus!

Na ndio maana hata sisi tulikuwa tukienda majumbani kwa wahindi hao kwa ajili ya tuition ya kulipia!

Ni baadhi ya walimu wenyewe HOVYO TU!

Na ndio maana taaluma hiyo watu hawaitaki kwani walimu wenyewe wameidhalilisha mara baada ya wao kudhalilishwa na serikali kwa kutolipwa mishahara yao!

Na mafrustrations wanaenda kuwatolea wanafunzi wengine ambao hata ada yao ni familia inabidi ijifunge mkanda ki kweli kweli.

Sasa na wakati huu kila mtu anajuwa kuwa watoto wa Tanzania nzima wanaoendelea na masomo yao mara baada ya elimu ya msingi hawafikii hata nusu ya watoto wote Tanzania!

Sasa si kizazi cha watumwa tunatengeneza?

Tena na wachina na kila mtu wako mtaani hapo bongo?

Samahani Nyangumi kama nimetoka nje ya kusudio la swali lako lakini nilionelea nigusie hili.

Ahsante.
 
Mkuu Nyangumi,

Ya Mungu ni ya Mungu nayo ni kwamba Rostam ni kiumbe chake mwenye haki ya kufanya aonavyo bila kuvunja sheria za nchi, lakini ya dunia ni kwamba Rostam ni fisadi na hasa Lowassa aliyetayarisha huu mchezo mzima, sasa wanapokwenda kujaribu kuyanunua makanisa huenda wanatumiwa na Mungu kuyanunua makanisa ya shetani hayo ni ya wana-dini hayanihusu hapa,

Sisi wananchi hapa our interest ni Rostam fisadi kwenda kutoa sadaka katika kanisa ambalo Spika ni mmoja wa wazee wa kanisa lile, that has nothing to do na dini, now that is our problem yaani wananchi na taifa letu kwamba kwanini hawa wawili wana kiburi namna hii?

Lowassa in private anadai liwalo na liwe lakini atakuwa tu president wa nchi yetu, I mean na hizi ndio kampeni zenyewe alianzia jimboni kwake sasa inahamia kila kona and the man is coming bro, sasa swali ni tunafanya nini as a nation na hawa watu?
 
Hii ishu ingekuwa na maana sana kama hawa mafisadi wangechukuliwa hatua za kisheria, naona tunakesha tukijibishana kwa hoja nyingi tofauti, swali ni kwanini hawakamatwi? angekuwa mlalahoi kachomoa baiskeli au sufuria la mtu mda huu angekuwa ameishaivia keko.
 
Mkuu Nyangumi,

Ya Mungu ni ya Mungu nayo ni kwamba Rostam ni kiumbe chake mwenye ahki ya kufanya aonavyo bila kuvunja sheria za nchi, lakini ya dunia ni kwamba Rostam ni fisadi na hasa Lowassa aliyetayarisha huu mchezo mzima, sasa wanapokwenda kujaribu kuyanunua makanisa huenda wanatumiwa na Mungu kuyanunua makanisa ya shetani hayo ni ya wana-dini hayanihusu hapa,

Sisi wananchi hapa our interest ni Rostam fisadi kwenda kutoa sadaka katika kanisa ambalo Spika ni mmoja wa wazee wa kanisa lile, that has nothing to do na dini, now that is our problem yaani wananchi na taifa letu kwamba kwanini hawa wawili wana kiburi namna hii?

Lowassa in private anadai liwalo na liwe lakini atakuwa tu president wa nchi yetu, I mean na hizi ndio kampeni zenyewe alianzia jimboni kwake sasa inahamia kila kona and the man is coming bro, sasa swali ni tunafanya nini as a nation na hawa watu?

Mkuu nilidhani kausingizi kamekupitia tehe tee!. Sikuwa na maana ya kupinga comment yako mkuu kwani nakubaliana nayo na nilieleza hivyo.
 
Hii ishu ingekuwa na maana sana kama hawa mafisadi wangechukuliwa hatua za kisheria, naona tunakesha tukijibishana kwa hoja nyingi tofauti, swali ni kwanini hawakamatwi? angekuwa mlalahoi kachomoa baiskeli au sufuria la mtu mda huu angekuwa ameishaivia keko.

Hii ndio ilitakiwa tuishikie bango na sivinginevyo.Mambo ya kushinikizana kwa maaskofu wakati kunavyombo vya sheria vyetu inakua si utawala wa sheria bali utawala wa kushinikizana.
 
Nakumbuka Rev. Kishoka alituonya juu ya mahusiano ya karibu kati ya Askofu Mkuu Malasusa na Lowassa. Naomba huyu mkuu wa kidini atafutwe na kuwekwa kiti moto tujue msimamo wake juu ya hivi vya kaizari inavyoonekana kuviweka mbele sana.

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=240548#post240548

Wakati wengi wenu hapa mmetaharuki baada ya huu mkanganyiko uliotokea - unaweza kupata picha kwamba mpaka sasa KKKT haijatoa tamko lolote? Vyombo vya habari (kama ITV) jana walijaribu kupata neno kutoka kwao bila mafanikio.

Kwa upande mwingine ni vyema hili limetokea maana vinginevyo tusingejua wakuu wetu wa dini wamelalia upande gani. Nilitegemea tamko walau kutoka kwa mmoja wa maaskofu wa KKKT (hata lisilo rasmi) ndani ya masaa 24. Hiki kigugumizi cha wakuu hawa wa KKKT kinaashiria nini hapa wandugu?

.
 
Hela chafu itabakia kuwa chafu. Ukiipokea wakati mwingine yaweza kukutia nuksi tu. Lakini simhukumu mheshimiwa moja kwa moja ingawa sijui kama naye ni muumini wa KKKT au kakaribishwa kwakuwa 'anazo' ili awe mwezeshaji kwa shughuli ya kwaya naye akaamua 'kutuma salaam' kwa kumalizia ili waumini waifanye kazi ya kuiombea nchi...!

Angerahisisha angetutajia mchawi nani... Fuatilia Majira la kesho kwa habari zaidi

Viongfozi wa makanisa nao ni mafisadi tu kwani ndo kawaida yao kupokea pesa za mafisadi. Hawana lolote ni wanafiki tu!

Ole wao hawa viongozi wa dinii, hakika watageuka kuwa kuni za kuwaunguzia wenye dhambi siku ile ya kiama!
 
Hata aibukie makaburini ,still we need to know who is behind all Kunguni.
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Mashariki na Pwani, limetoa taarifa likimkana Rostam Aziz kwa kudai kwamba kanisa halikumualika rasmi kwani aliyemualika hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo na hakufuata taratibu zilizowekwa na kanisa hilo.

Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Balozi Richard Mariki, ndiye aliyesaini taarifa hizo zilizowaomba radhi waumini na watu wote waliokwazwa na taarifa za Rostam kutumia kanisa kujisafisha.

"KKKT na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao kwa namna moja au nyingine wamekwazwa na tukio hili. Jukumu la Kanisa ni kuokoa roho za watu na si kukumbatia mafisadi na wala rushwa." inaeleza sehemu ya mwisho ya taarifa hiyo ya KKKT.
 
Mhhh!! Hapo ni kama wememhukumu mtu wakati sio kazi ya kanisa kufanya hivyo. Unless kama hawakutamka hivyo, otherwise hilo tamko lina walaakini.
 
Ahsante kwa KKKT kung'amua hilo, lakini haitoshi kumkana tu we need more from them, watafanya nini na michango aliyoahidi na viongozi waliomualika?

Nashauri michango ya rostam isitumike kwa shughuli zilizokusudiwa yaani kwaya. Hizo 7m ziende kwa yatima au kununua vitanda vya hospitali vijijini, WASIMRUDISHIE, kwani ni pesa zetu!
 
Na waliomwalika pia wachukuliwe hatua kwani hawana nia nzuri na Wananchi na pia TAIFA.
Pia wanajali matumbo yao kuliko UTUMISHI WAO!
 
Ninajua kuwa hata mchungaji husika ameshachukuliwa hatua na Dayosisi yake .

Nilisema jana kuwa wasipokuwa waangalifu kwenye hili kuna uwezekano wa kanisa kupasuka na bado uwezekano huo upo .

Fuatilieni Askofu Laizer anaweza..........
 
Sasa hicho kitita kimeshaifaziwa na wajanja wa Kanisa na ujumbe wa Rostam umefika ila yaliobakia ni kubangaiza njiani ili jamaa wagawane kwa usalama ,si ajabu ukaambiwa na feza amerudishiwa mwenyewe.
Muhimu ni kwamba feza inaliwa na lengo lake linapigwa na chini kama walivyomtangazia ,ndio dawa ya mafisadi wakikupa unaitafuna tu halafu unarapu mbovu.
 
Hapo Tunaliona Tatizo La Wazi Kwetu Watanzania, Kkkt Wameingia Tena Mtegoni.

Hawakuwa Na Sababu Ya Kufanya Hicho Kilichofanywa Na Ndg.mariki, Huo Ni Upotofu Mkubwa Ktk Imani.

Kanisani Ni Mahala Pa Wadhambi Na Si Vinginevyo.

Kanisa Lipo Kutuunganisha Na Mungu Na Si Kututenganisha Naye.

Rostam Anaweza Kuwa Ni Mdhambi Kama Tulivyo Sote Hapa , Je Ni Nini Hatima Yetu Mbele Ya Mungu Endapo Watumishi Wa Mungu Wataanza Kututenga Na Upendo Wake??

Mariki Anapaswa Awajibike Mbele Ya Mungu Na Waumini Wote.
 
Mhhh!! Hapo ni kama wememhukumu mtu wakati sio kazi ya kanisa kufanya hivyo. Unless kama hawakutamka hivyo, otherwise hilo tamko lina walaakini.

Taarifa hii haijakaa sawa. Hawezekani Balozi Mariki akawa Katibu Mkuu wa KKKT,nadhani atakuwa katika kamati mojawapo. Pili, sidhani, mtu kama Mariki ataweza kutoa tamko la kutoa hukumu. He should know better! But anything is possible in Bongoland.
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Mashariki na Pwani, limetoa taarifa likimkana Rostam Aziz kwa kudai kwamba kanisa halikumualika rasmi kwani aliyemualika hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo na hakufuata taratibu zilizowekwa na kanisa hilo.

Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Balozi Richard Mariki, ndiye aliyesaini taarifa hizo zilizowaomba radhi waumini na watu wote waliokwazwa na taarifa za Rostam kutumia kanisa kujisafisha.

"KKKT na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao kwa namna moja au nyingine wamekwazwa na tukio hili. Jukumu la Kanisa ni kuokoa roho za watu na si kukumbatia mafisadi na wala rushwa." inaeleza sehemu ya mwisho ya taarifa hiyo ya KKKT.

Haya maneno mazito sana wamepigilia msumali. Rostamu akome kufata fuata watu na madhehebu yao.
 
Wacha pesa iliwe tu kwani wenye kutowa ni walionazo na walionazo Tanzania wengi wao ndio Hao kina Rostam.
 
Taarifa hii haijakaa sawa. Hawezekani Balozi Mariki akawa Katibu Mkuu wa KKKT,nadhani atakuwa katika kamati mojawapo. Pili, sidhani, mtu kama Mariki ataweza kutoa tamko la kutoa hukumu. He should know better! But anything is possible in Bongoland.

Mkuu watanzania mbona tunakimbia ukweli, huyu anaweza kutusaidia kufikisha kesi hii mahakamani kwani siri iko wapi? RA siyo FISADI?
 
Taarifa hii haijakaa sawa. Hawezekani Balozi Mariki akawa Katibu Mkuu wa KKKT,nadhani atakuwa katika kamati mojawapo. Pili, sidhani, mtu kama Mariki ataweza kutoa tamko la kutoa hukumu. He should know better! But anything is possible in Bongoland.

Imeandikwa: Balozi Richard Mariki, Katibu Mkuu, KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani... Si Katibu Mkuu wa KKKT Taifa.... Habari zinasema kwamba, Mchungaji na kwaya yake wamesimamishwa kwa muda, wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu nyendo zao. Nadhani Rostam anaweza kuanzisha kanisa na unaweza kusikia mgogoro kama ule wa Meru ama wa Pare
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom