TANZIA Rest in peace Valentina (JF Member)

Nina deni kubwa kwa Valentina na sijui nitalilipaje.. Labda kwa kichanga alichokiacha😭 Mungu nisaidie🙏🏿
Marehemu Valentina ndiye Mwana JF wa kwanza kufanya naye mawasiliano ya simu wayback 2013... Baadae nikawa mmoja wa wana JF aliowashirikisha kwenye fursa mbalimbali za kutafutq pesa na ajira.. Alipenda sana kuwa mbunifu wa fursa za pamoja japo nadhani wengi kama si wachache hawakumuelewa..
Tuliendelea kuwasiliana na akatamani tuonane ana kwa ana.. Lakini kila nilipokuwa na safari za Arusha mambo yangu yakawa mengi hivyo nikakosa kabisa muda wa kuonana naye😪

Mwaka 2021 nikiwa nafanya kazi Kigamboni Kibadq akanijulishq kwamba kwasasa yuko Dar.. Nikamuelekeza nilipo lakini akaniambia kwa situation yake hawezi kutumia usafiri wa jumuiya.. Nikaahidi kumchukulia usafiri wa binafsi ama mimi nimtembelee alipo lakini sikufanikiwa kufanya yote mawili mpaka naondoka Kigamboni🥱

Nadhani harakati na changamoto za maisha zinatunyima nafasi adhimu za upendo na kujali.
.. Tuliendelea kuwasiliana mara moja moja lakini mwishowe mawasiliano yakakatika kabisa mpaka nililokuja kusoma hii taarifa ya kutwaliwa kwake!

Kwa moyo wa dhati naamini nina deni kwake.. Lakini naamini kuna siku nitalilipa. Pumzika kwa amani rafiki mwema😪
 
Watu wanajuanaje humu kiasi wakiaga dunia taarifa zao huletwa? Ila wengine humu wakiaga dunia ndio basi, hakuna atakayejua
Haha wenzako tunasocialize nje ya JF kitambo na ni zaidi ya miaka 13 sasa tangia tufahamiane. Binafsi nakiri kwamba Valley alikuwa vyanzo vya mimi kujiunga na JF tukiacha kuingia na kujisomea tangia ikiitwa Jambo Forum.
 
Taarifa ya Msiba 🕊️

Kwa huzuni kubwa tunapenda kutangaza kifo cha mwenzetu @⁨Valentina Jf⁩ 💔, ambaye amefariki dunia baada ya kuingizwa kwenye operesheni katika Hospitali ya Babuu Mkoani - Arusha

Madaktari wamefanikiwa kumwokoa mtoto wa kiume, ambaye anaendelea vizuri.

Taarifa kamili kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tunaomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja familia pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 💔
 
Mimi. Sina maneno mengi ya kuandika ilaa nima huzuni kubwa juu ya taarifa ya msiba juu ya mpendwa wetu Valentina 😭😭

Wengi wetu tunamjua kwa kuunganisha watu na kujenga upendo katikati ya chuki na hasira, lakini leo Mungu amempenda zaidi.

Nitatoa updates kadri nitakavyojaliwa.
Ooh!! My dear good friend!!
May she rest in peace. Msiba utakuwa pale nyuma ya Arusha Tech?
 
Nipe maana ya RIP
Rest in Peace. Pumzika kwa Amani.

Hakuna Mungu hapo.

Ukifa unaondokana na matatizo yote ya maisha unapumzika kwa amani.

Ila wewe kwa sababu hujui kusoma kwa ufahamu, unasoma kitu ambacho hakipo.

Unalazimisha kuona Mungu sehemu ambayo hajaandikwa.

Mpaka sasa unanichafua sana kwa sababu Valentina ni mtu niliyeishi naye poa sana hapa JF halafu unaleta mabishano ya kijinga kwenye uzi huu wa msiba.
 
Taarifa ya Msiba 🕊️

Kwa huzuni kubwa tunapenda kutangaza kifo cha mwenzetu @⁨Valentina Jf⁩ 💔, ambaye amefariki dunia baada ya kuingizwa kwenye operesheni katika Hospitali ya Babuu Mkoani - Arusha

Madaktari wamefanikiwa kumwokoa mtoto wa kiume, ambaye anaendelea vizuri.

Taarifa kamili kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tunaomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja familia pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 💔
Kumbe amefariki kutokana na changamoto za uzazi 💔

Hizi complications zimekuwa sugu Kwa Nchi zetu za Daraja la Tatu 🙌

Ukiona mkeo ameingia "Leba" na kukuletea zawadi ya mtoto, ni jambo la kumshukuru sana Mola

Suala la kuendelea kuboresha mazingira ya kujifungulia ya Mama na Mtoto, tunapaswa kama Taifa kuliangalia kwa jicho la pekee sana

Otherwise, tutaendelea kuwapoteza Wake zetu/Mama/Dada zetu wakati wa Uzazi

Mungu amrehemu 🙏🙏🙏
 
Rest in Peace. Pumzika kwa Amani.

Hakuna Mungu hapo.

Ukifa unaondokana na matatizo yote ya maisha unapumzika kwa amani.

Ila wewe kwa sababu hujui kusoma kwa ufahamu, unasoma kitu ambacho hakipo.

Unalazimisha kuona Mungu sehemu ambayo hajaandikwa.

Mpaka sasa unanichafua sana kwa sababu Valentina ni mtu niliyeishi naye poa sana hapa JF halafu unaleta mabishano ya kijinga kwenye uzi huu wa msiba.
Which peace?

Ukisema RIP means rest in eternal peace

Anyway: ngoja tumtakie amani ya milele dada etu tuache mabishano
 
Taarifa ya Msiba 🕊️

Kwa huzuni kubwa tunapenda kutangaza kifo cha mwenzetu @⁨Valentina Jf⁩ 💔, ambaye amefariki dunia baada ya kuingizwa kwenye operesheni katika Hospitali ya Babuu Mkoani - Arusha

Madaktari wamefanikiwa kumwokoa mtoto wa kiume, ambaye anaendelea vizuri.

Taarifa kamili kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tunaomba Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape faraja familia pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 💔
Mungu apumzishe Vallentin namfahamu kwa sehemu ( moyo wake mzuri sana, na kwa mwenza wake alie kuwa rafiki yangu )

Dah! Kipindi cha kujifungu huwa ni kigumu sana kwa wanawake. Nakumbuka iliwahi mkuta mwanamke wangu, ila Dr. ilidi waruhusu mtoto afariki mama apone.
 
Sifahamu cha kusema baada ya kusikia habari hii ya kuhuzunisha.

Nikiri hapa JF kwamba Valentina ni dada pekee ambae ameweza kumuona Richard uso kwa uso nikiwa Arusha mwaka 2015. Na hiyo ilikuwa baada ya mazee wangu wa Arusha kufanya "vetting" kali sana maana ya siku hizi mtu huyafahamu.

Ni yeye ndiye alieanza kuja PM kwangu na mie nikamkaribisha kwasababu alikuja kipekee sana yaani alikuwa na nguvu ya kipekee ya kumfuata mtu (approach) na pia nguvu ya ushawishi (influence) khasa kwenye masuala ya ujasiriamali.

Wapo watu wengi waja PM lakini nawapotezea ila Valentina haikuwa hivyo nilijishusha ingawa si kimapenzi lakini tuliweza kuongea uzuri kama kaka na dada.

Ila hivi karibuni alipotea sana na nikahisi kuwa labda aumwa au yuko nje ya Arusha.

Pole sana Hornet.

RIP Valentina.
 
Nina deni kubwa kwa Valentina na sijui nitalilipaje.. Labda kwa kichanga alichokiacha😭 Mungu nisaidie🙏🏿
Marehemu Valentina ndiye Mwana JF wa kwanza kufanya naye mawasiliano ya simu wayback 2013... Baadae nikawa mmoja wa wana JF aliowashirikisha kwenye fursa mbalimbali za kutafutq pesa na ajira.. Alipenda sana kuwa mbunifu wa fursa za pamoja japo nadhani wengi kama si wachache hawakumuelewa..
Tuliendelea kuwasiliana na akatamani tuonane ana kwa ana.. Lakini kila nilipokuwa na safari za Arusha mambo yangu yakawa mengi hivyo nikakosa kabisa muda wa kuonana naye😪

Mwaka 2021 nikiwa nafanya kazi Kigamboni Kibadq akanijulishq kwamba kwasasa yuko Dar.. Nikamuelekeza nilipo lakini akaniambia kwa situation yake hawezi kutumia usafiri wa jumuiya.. Nikaahidi kumchukulia usafiri wa binafsi ama mimi nimtembelee alipo lakini sikufanikiwa kufanya yote mawili mpaka naondoka Kigamboni🥱

Nadhani harakati na changamoto za maisha zinatunyima nafasi adhimu za upendo na kujali.
.. Tuliendelea kuwasiliana mara moja moja lakini mwishowe mawasiliano yakakatika kabisa mpaka nililokuja kusoma hii taarifa ya kutwaliwa kwake!

Kwa moyo wa dhati naamini nina deni kwake.. Lakini naamini kuna siku nitalilipa. Pumzika kwa amani rafiki mwema😪
Alikuwa anatamani sana tukutane, ila ratiba zangu hazikuwahi kuwa easy. Kila akiwa Dar Mimi nakuwa mkoani mpaka nilipohama mazima Dar. Alinialika Arusha, ila sikuwahi pata route ya kule.

Anyways, pumzika kwa amani dada Valentina.
 
Back
Top Bottom