.......For a while nimepata mental block. Kwa upeo wetu wanadamu, sometimes ni vigumu sana kumuelewa Mungu! Inatia uchungu usio kifani kuona wale wale wanaojitoa kwa moyo wote pasipo hila kuwasemea wanyonge wa nchi hii ndio wanaoondoka mapema sana. Regia had a vision that we could all see. Aliwafikiria watanzania mno katika maisha yake. Alikuwa si wa watu wa Kilombelo tu, wala wa walemavu tu. Regia alikuwa ni Mbunge wa watanzania wote. Jimbo lake kiukweli lilikuwa ni Tanzania nzima. Kuthibitisha hili soma thread yake aliyokuwa ameanzisha hivi juzijuzi alipoomba yeyote mweye hoja ambayo anadhani inahitaji kusemewa ndani ya Bunge na CDM aiwakilishe kwake.
Nakumbuka siku moja Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa alisema unapokuwa Mbunge wa CDM unakuwa na kazi mbili. Moja ni kuliwakilisha jimbo lako lakini pili ni kuwawakilisha watanzania wote. Tumeyaona haya kwa Dr Slaa, Mh Mnyika, Mh Mbowe, Mh Tundu Lisu, Mh Zito na wengine wengi. This was also true for our beloved sister Regia Mtema. Japo tuna majonzi sana lakini tukumbuke tumeagizwa na mwenyezi Mungu kuwa tushukuru kwa yote. Yeye ndiye anayejua kwa nini anamchukua huyu na kwa nini anamuacha huyu. RIP our beloved sister Regia Mtema. Na jina la BWANA lihimidiwe.