Ramadhani ya mwaka huu imeanza na mimi. Kwani ni sheria kumnunia mwanaume ndani ya mwezi huu?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Baada ya kumaliza sala za asubuhi naingia zangu kwa mama Pima kupata chai. Nakuwa mteja wa kwanza kufika hapo. Mama Pima anabaki akinikodolea macho! Namuuliza chai vipi? Au hauuzi? Anaamua kunichemshia kikombe kimoja cha chai ya majani machungu na kiporo cha chapati mbili. Nampisha afanye usafi, naamua kulia nje. Watu wote wanapita huku wakinishangaa kama mchawi vile. Naamua kuacha chapati moja na kutokomea zangu

Njiani nakutana na kijana wa kahawa. Katika Hali ya kujuliana Hali, ananipakulia kikombe cha gahawa. Wakati nakitwanga nikiwa sina hili wala lile, anapita mzee moja ndani ya kanzu na kibandiko. Kwa sauti nzito ya koromeo ambalo halijasafishwa anatamka "Astakafuli". Loo! Naamua kuimwaga gahawa ile kisha kurudisha kikombe cha watu

Karibu na maeneo ya nyumbani, nakutana na Mama Grace, huyu huwa ananikubali sana, na anaamini kuwa ipo siku nitamuoa mwanae. " Afadhari nimekuona mwanangu, naomba unipitishie hii mikate nyumbani kwangu. Lahaula, njia nzima na mikate mkononi, zinasikika sauti za taratibu zikitamka "Lione hilo Kobe" Naamua kuvumilia

Njiani nakutana na Aisha chupi kubwa akiwa ndani ya vazi la heshima hadi naogopa kumpa salamu, napitiliza mbele kisha nacheka mwenyewe

Naondoka malangoni mwa mama Grace, nakutana na mabinti wawili ambao huwa wananikubali, nawapa salamu wanaishia kuninunia na kuchongoa midomo. Najaribu kumtangiza mmoja wao, anaishia kunambia, nimekustahi, usiniharibie swaumu.

Kwani salamu imekatazwa katika mfungo huu? Natikisa kichwa kisha nacheka mwenyewe kila nikikumbuka migugumio

Ndipo nafika maeneo ya gheto. Nasikia goma la amapiano linatoka kwenye moja ya chumba cha mule ndani. Kwa sauti ya jazba nauliza, "Ni shaitwani gani anataka kutuharibia swaumu humu ndani?" Afanaleki! Kumbe goma la Amapiano linachomozea chumbani kwangu, ooh! Kumbe sikuzima bufa nilipikuwa naondoka gheto. Kumbe qaswida kwenye flash yangu zilikwisha, ndipo Ngoma za Amapiano zikaunga mstari

Na hili nalo mkalitizame kwa kina
 
Jana,siku ya kwanza ya Ramadhani ,nimeamka nimekunywa chai,kama kawaida,nikaona watu wananitazama kwa mshangao. Baada ya hapo nikaamua na mimi nitafunga,sikula tena mpaka jioni. Kwa hiyo sasa nafunga siku ya pili ya Ramadhani.
Nakumbuka wakati ule nilifunga Ramadhani,mpaka mwisho,halafu ikaanza Mfungo wa Sita,nikaamua kufu ga sita(kufunga,I uad no choice,anyway,kwa sababu nilikuwa naumwa,nimelazwa hospitali,nilikuwa sina hamu ya kula).
Kwa hiyo,siku ya kwanza ya Mfungo wa sita,ndio Mama Samia kawaita watu Ikulu,ndio anawaapisha Ma RC. Mi nikaenda Ikulu,nilikuwa naenda kumuona Makongoro anaapishwa. (Actually nimeenda from the hospital bed)Baada ya ile event,ilikuwepo lunch,ambayo Mimi sikwenda.
 
Mkuu, uko bar gani sasa hivi. Nije kuumwagilia moyo?
 
Baada ya kumaliza sala za asubuhi naingia zangu kwa mama Pima kupata chai. Nakuwa mteja wa kwanza kufika hapo. Mama Pima anabaki akinikodolea macho! Namuuliza chai vipi? Au hauuzi? Anaamua kunichemshia kikombe kimoja cha chai ya majani machungu na kiporo cha chapati mbili. Nampisha afanye usafi, naamua kulia nje. Watu wote wanapita huku wakinishangaa kama mchawi vile. Naamua kuacha chapati moja na kutokomea zangu

Njiani nakutana na kijana wa kahawa. Katika Hali ya kujuliana Hali, ananipakulia kikombe cha gahawa. Wakati nakitwanga nikiwa sina hili wala lile, anapita mzee moja ndani ya kanzu na kibandiko. Kwa sauti nzito ya koromeo ambalo halijasafishwa anatamka "Astakafuli". Loo! Naamua kuimwaga gahawa ile kisha kurudisha kikombe cha watu

Karibu na maeneo ya nyumbani, nakutana na Mama Grace, huyu huwa ananikubali sana, na anaamini kuwa ipo siku nitamuoa mwanae. " Afadhari nimekuona mwanangu, naomba unipitishie hii mikate nyumbani kwangu. Lahaula, njia nzima na mikate mkononi, zinasikika sauti za taratibu zikitamka "Lione hilo Kobe" Naamua kuvumilia

Njiani nakutana na Aisha chupi kubwa akiwa ndani ya vazi la heshima hadi naogopa kumpa salamu, napitiliza mbele kisha nacheka mwenyewe

Naondoka malangoni mwa mama Grace, nakutana na mabinti wawili ambao huwa wananikubali, nawapa salamu wanaishia kuninunia na kuchongoa midomo. Najaribu kumtangiza mmoja wao, anaishia kunambia, nimekustahi, usiniharibie swaumu.

Kwani salamu imekatazwa katika mfungo huu? Natikisa kichwa kisha nacheka mwenyewe kila nikikumbuka migugumio

Ndipo nafika maeneo ya gheto. Nasikia goma la amapiano linatoka kwenye moja ya chumba cha mule ndani. Kwa sauti ya jazba nauliza, "Ni shaitwani gani anataka kutuharibia swaumu humu ndani?" Afanaleki! Kumbe goma la Amapiano linachomozea chumbani kwangu, ooh! Kumbe sikuzima bufa nilipikuwa naondoka gheto. Kumbe qaswida kwenye flash yangu zilikwisha, ndipo Ngoma za Amapiano zikaunga mstari

Na hili nalo mkalitizame kwa kina
.
IMG-20230402-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom