Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi hi ni Makala ya Nipashe ya Jumapili ya Leo, 29 January 2023
Kwa Maslahi ya Taifa, bado inajikita kwenye Katiba yetu,
  • Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote yoyote inayokwenda kinyume na katiba, sheria hiyo ni batili!
  • Serikali yetu kupitia wanasheria wetu manguli, wabobezi na wabobevu, iliwahi kutunga muswada wa sheria wenye kipengele batili, kinachokwenda kinyume cha katiba!. Humo serikali kuna wanasheria wanaojua katiba!, waliwezaje kupeleka muswada wenye batili?

  • Bunge letu lenye wabunge makini, lililoshehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabebovu, wakaipitisha batili hiyo ikawa sheria! Wanasheria waliopitisha batili hiyo, hawa ni wanasheria wa aina gani?!.

  • Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahali pema peponi) akaipinga sheria hiyo Mahakama Kuu, akashinda, Mahakama Kuu ikatamka sheria hiyo ni batili!

  • Mahakama Kuu ya Tanzania, ndio mamlaka pekee yenye uwezo na mamlaka ya kutamka sheria fulani ni batili!. Sheria yoyote, inapotamkwa tuu na Mahakama Kuu kuwa ni batili, tangu baada ya tamko hilo, ubatili wa sheria hiyo unaanzia hapo hapo, sheria hiyo inakuwa imeisha batilishwa, ni kama haipo ab initio!

  • Sherikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi wa kuibatilisha sheria hiyo, na wakati huo huo, ikafanya jambo jingine kubwa la ajabu, ambalo mimi nimeliita "madudu", kwa kupeleka kwa hati ya dharura, muswada wa mabadiliko ya katiba, na kuuchukua ubatili huo uliobatilishwa na Mahakama Kuu, na kuuchomekea ndani ya Katiba yetu!. Waliofanya madudu hayo ni serikali yetu ya wakati huo, serikali hiyo iliyokuwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabebovu!, hawa ni wanasheria wa aina gani?!

  • Na Bunge letu la wakati huo, likayapitisha madudu hayo hivyo hivyo kama yalivyo, na kuyachomekea ndani ya katiba yetu!. Miongoni mwa wabunge hao, wapo wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu!, makalia hizi zinahoji, sisi Tanzania, tuna wanasheria wa type gani, na kujiuliza waliwezaje vipi kufanya madudu makubwa kama haya ya kuchomeka batili ndani ya Katiba yetu, huku tunajinasibu kuwa Tanzania tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabebuvu!, hawa wanasheria wetu unguli wao, ubobezi na ubebevu wao ni kwenye nini?!

Leo naendelea na sehemu ya tatu nay a mwisho ya mada ya wiki iliyopita kuhusu haki za kikatiba, zilizotolewa na ibara moja ya Katiba, halafu zikaja kuporwa kwa kuchomekewa ibara nyingine ambayo ni batili, iliyochomekewa kiubatili, ndani ya Katiba yetu!, mambo yote haya ya madudu ya ajabu, yamefanywa na wanasheria wetu ambao ni manguli, wabobezi na wabobevu huku wanasheria wengine wote Tanzania nzima, wamenyamaza kimya wakiangalia wakati katiba yetu inachezewa, inanajisiwa kwa kuchomekewa kinyume cha ... vifungu vyenye ubatili!.

Sasa leo naendelea pale nilipoachia wiki iliyopita, ambapo serikali imeishindwa mara mbili, na ndipo serikali yetu tukufu ya wakati huo ikaanza kufanya sarakasi kama ifuatavyo!

Screen Shot 2023-01-29 at 12.29.29 PM.png
Screen Shot 2023-01-29 at 12.29.50 PM.png

1. Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ambayo mimi nayaita ni sarakasi za kisheria!!, kwanza ilikata rufaa kuipinga hukumu ya Jaji Lukakingira!. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 11 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!.

2. Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali katiba yetu ichezewe, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 11 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

3. Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo 4, lakini kwa ajili ya makala hii, nitayataja mawili tuu, (a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 11 ya katiba kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba na (b) Kutamka wazi kuwa kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

4. Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, Jaji Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo 11ya katiba ya Tanzania ni batili!.

5. Lakini serikali yetu ya wakati huo, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama ya Rufani ikakaa Full Bench chini ya majaji 7, wakiongozwa na Jaji Mkuu mwenyewe wa wakati huo, Jaji Mkuu Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Eusebi Munuo, Jaji January Msoffe, Jaji Natalia Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Benard Luanda, na Jaji Nasor Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu.

6. Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabingwa wabobezi watatu wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, (baadae akawa Mwanasheria Mkuu Zanzibar, sasa ni Makamo wa kwanza wa rais Zanziibar), Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa (Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi), pia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Alikaribishwa.

7. Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua ifuatavyo, hapa naomba ninukuu
“So as to let the will of the people prevail, “We are definite that the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

8. Hapa Mahakama ya Rufani Tanzania, ilijivua jukumu lake kuu la kuilinda katiba ya JMT. Kama ubatili umefanywa kwenye katiba yetu, kwa serikali yetu kuandaa muswada wa sheria batili unaokwenda kinyume cha katiba, ukaupeleka kwenye Bunge letu, likatunga hiyo sheria batili. Mahakama Kuu yenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, likabatilisha ubatili huo, serikali ikaandaa mabadiliko ya katiba na kulitumia Bunge kuuingiza ubatili huo ndani ya katiba yetu, Mahakama Kuu ikashikilia msimamo kuwa huo ni ubatili, iweje Mahakama ya Rufaa ikalikalia kimya?.

9. Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the court is not the custodian of the will of the people!, hakuna will of the people ambayo ni kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, halafu Bunge likatunga sheria kuifuta haki hiyo, ilitegemewa mahakama kutumia mamlaka yake ya “checks and balance” kulizuia Bunge kuwa haliwezi kutunga sheria inayokwenda kinyume cha katiba!. Mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, ile kanuni ya “the doctrine of separation of powers, checks and balance?, iko wapi?.

10. Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 11 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!. Yaani Bunge litunge sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kisha kipengele cha sheria hiyo batili kikachomekewa ndani ya katiba kwa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura!. Mahakama Kuu inasema huu ni ubatili, Mahakama ya Rufaa inasema “hatuwezi kuliingilia Bunge!, sarakasi zote hizi zinafanyika vipi Tanzania hii huku tuna wanasheria, manguli, wabobezi na wabobevu?.

Hitimisho:
Kama serikali yetu, imetunga sheria batili, inayopora haki ya msingi ya kikatiba, Bunge letu likaipitisha sheria hiyo, Mahakama Kuu, ikatamka huo ni ubatili, lakini Mahakama ya Rufaa, ikaunyamazia ubatili huo, na kulitaka Bunge ndio liuondoe, Watanzania waende wapi ili kuidai haki yao hii!. Tumaini la pekee ni moja tuu!, Mama Samia!.

Tena kiukweli kabisa Mwenyezi Mungu, anaipenda sana Tanzania, kwanza kwa kutuletea Rais Magufuli kuja kuinyoosha nchi yetu hii, na baada ya kunyooka, Magufuli mwendo akaumaliza, sasa kwa upendo mkuu wa Mungu kwa Tanzania,ametuletea Mama Samia, mtu ambaye ni mpenda haki, msema haki, na mtenda haki, ameisha onyesha dalili ya kuwatendea haki Watanzania!,

Niliamini uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025, haki hii itarejelezwa

Tatizo kuu la chaguzi zetu kutokuwa huru na za haki, liko kwenye katiba ambapo haki zimetolewa kipengele kimoja cha katiba na kuporwa na kipengele kingine kilichochomekewa kwenye katiba kiubatili, hivyo ili uchaguzi wa serikali za mitaa na uchanguzi mkuu ujao uwe huru na wa haki, kwanza lazima tufanye minimum reforms za katiba yetu ya mwaka 1977 tuzirudishe haki zilizoporwa.

Naamini Mama ni msikivu, zile 4R zake is not paying lip services!.

Mungu Mbariki Rais Samia Ayaweze Mungu Ibariki Tanzania

Waslaam

Paskali
 
Kama iliyopo haikuheshimiwa mpya italeta mabadiriko?

Yule mwanasheria mkuu wa serikali aliyetolewa chuoni akiwa lecturer kama alihusika nadhani utakuwq umeelewq tatizo linapoonzia jiulize wanafunzi aliowafundisha watakuwa wqnasheria wa aina gani?
 
kama iliyopo haikuheshimiwa mpya italeta mabadiriko?

yule mwanasheria mkuu wa serikali aliyetolewa chuoni akiwa lecturer kama alihusika nadhani utakuwq umeelewq tatizo linapoonzia jiulize wanafunzi aliowafundisha watakuwa wqnasheria wa aina gani?
Iwapo katiba itaandikwa bila kutokea machafuko ni ngumu kuheshimiwa, lakini ikiandikwa baada ya machafuko, lazima itaheshimiwa.
 
Wazee waliamua kupaisha tuta, tena dakika ya 90+5. But Baadae tulikuja kuelewa, maana Chief justice alikuja akachukua fomu. Hiki Chama ni hatari sana. Talking of Lugakingira J and Mwalusanya J ni watu ambao walikuwa wajuvi Sana na walifanya makubwa sana hasa kwenye Constitutional Law, but they didn't make it to the Court of Appeal. Hiki Chama ni balaa tupu!

By the way, High Court siku zote wanajitahidi kuwa mbali na siasa!
 
kama iliyopo haikuheshimiwa mpya italeta mabadiriko?
Mkuu Mr Mwamba, kutoheshimiwa kwa katiba ni hulka binafsi ya kiongozi individually, ila katiba pia imeweka utaratibu wa kushughulikia uvunjifu wa katiba, lakini kwa jinsi tulivyo na wanasheria wa ...(naomba nisimalizie), we did nothing!.
yule mwanasheria mkuu wa serikali aliyetolewa chuoni akiwa lecturer kama alihusika nadhani utakuwq umeelewq tatizo linapoonzia jiulize wanafunzi aliowafundisha watakuwa wqnasheria wa aina gani?
Kuwa mwalimu wa sheria na utendaji wa kisheria ni vitu viwili tofauti!

Ukimsikoa mtu yoyote ambaye ni Profesa ujue alikuwa ni lecture wa chuo, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamisi Juma alikuwa lecture, UDSM, Prof. Palamagamba Kabudi alikuwa lecture UDSM, tena huyu GPA yake ya 4.9 ndio the highest UDSM tangu kuanzishwa na haijavinjwa mpaka leo! Prof. Sifuni Mchome alikuwa lecture UDSM, Dr. Tulia Ackson alikuwa lecture UDSM, Dr. Harrison Mwakyembe alikuwa lecture UDSM, etc, mambo waliotufundisha dasani ni theories tuu, tunapokuja kwenye practices mambo ni tofauti.
P
 
Mkuu Tindo , kuhamashisha machafuko ni uchochezi!. Tanzania tumeandika katiba ya 1977 bila machafuko. Samia atatupatia katiba mpya bora.
Be positive.
P.

Katiba gani itapatikana ambapo Makada wa CCM wanasema haileti ugali mezani? Hii ya 77 ndio hii haiheshimiwi. Machafuko pekee yake ndio yataleta katiba ya kweli. Huo ndio ukweli, ita uchochezi ama nini lakini habari ndio hiyo.
 
Mkuu Tindo , kuhamashisha machafuko ni uchochezi!. Tanzania tumeandika katiba ya 1977 bila machafuko. Samia atatupatia katiba mpya bora.
Be positive.
P.
Hamna mtu anahamasisha machafuko bali kinachosemwa ni ukweli kwamba nchi hii hatuwezi pata mabadiliko ya kweli bila damu kumwagika na watu flani kuumia.

Siku zote hamna maridhiano kwenye kutafuta haki toka kwa mwonevu ama mwenye mamlaka. Huwezi kuomba huruma ya mtesi wako ikiwa dhamira yake ni kukuumiza tu ili maslahi yake yapatikane.

Haina tofauti na kwenda dukani kuomba upewe kilo ya unga bure ikiwa huna hela eti kwa sababu wote ni binadamu. Mwenye duka ana mamlaka ya kukunyima na hakuna kitu utafanya mpaka njaa itakapokuua. Its either you fight upate pesa ya kulipia unga ndio uupate au uombe huruma hadi ufe njaa.
 
Katiba gani itapatikana ambapo Makada wa CCM wanasema haileti ugali mezani? Hii ya 77 ndio hii haiheshimiwi. Machafuko pekee yake ndio yataleta katiba ya kweli. Huo ndio ukweli, ita uchochezi ama nini lakini habari ndio hiyo.
Yani inatakiwa siku moja barabara zifungwe V8 zivunjwe vunjwe vioo hao watendaji wa gvnt wachezee kipigo kila kona ili ujumbe ufike kuwa tumeshawachoka.

Either watupe katiba mpya yenye mambo tunayotaka na wakate mazoea kabisa. Hatuwezi kuishi kama wakimbizi nchini mwetu huku wao rasilimali zikinufaisha watoto wao na jamaa na marafiki zao wakati watanzania huduma tu basic za afya na elimu zinasua sua.
 
Mkuu Tindo , kuhamashisha machafuko ni uchochezi!. Tanzania tumeandika katiba ya 1977 bila machafuko. Samia atatupatia katiba mpya bora.
Be positive.
P.
Mi Kama Msomi makini na Sina itikadi ya chama,Ila kwa uelewa na umri wangu CCM hawawezi kukubali katiba Mpya na ikitokea wanapiga vilaka ile ya 1977 jiulize hawataki ya jaji warioba licha ya kwamba tume ile ya warioba ni makada wa CCM wasitaafu. Kuna laana ndani ya CCM
 
Katiba gani itapatikana ambapo Makada wa CCM wanasema haileti ugali mezani? Hii ya 77 ndio hii haiheshimiwi. Machafuko pekee yake ndio yataleta katiba ya kweli. Huo ndio ukweli, ita uchochezi ama nini lakini habari ndio hiyo.
Ukweli huu MaCCM yanajifanya etii uchochezi,wakati hayataki kusikia katiba Mpya,kwani CCM wanaishi wapi si tuko nao huku mtaani washaanza kuja kwenye ofisi za serikali wanawambia watumishi etii mda umekaribia tubebeni tena sisi ni ndugu,,hivi hawa Mr Pascal watakubali katiba Mpya bila kulaluwana. Duh rotten nation tz
 
Yani inatakiwa siku moja barabara zifungwe V8 zivunjwe vunjwe vioo hao watendaji wa gvnt wachezee kipigo kila kona ili ujumbe ufike kuwa tumeshawachoka.

Either watupe katiba mpya yenye mambo tunayotaka na wakate mazoea kabisa. Hatuwezi kuishi kama wakimbizi nchini mwetu huku wao rasilimali zikinufaisha watoto wao na jamaa na marafiki zao wakati watanzania huduma tu basic za afya na elimu zinasua sua.
Nakwambia madiwani na wenyeviti wa CCM siku hizi wanashinda ofisi za vijiji na kata etii tunaomba mtubebe tena mda umekaribia hivi watu wa namna hii(CCM)watakubali hata rasmu ya katiba ya tume ya jaji warioba inayopendekeza wakuu wa mikoa na wilaya wasiwepo na wakiwepo wachaguliwe kweli haya MaCCM yatakubali yameshazoeza kula vya bure. Hata mama Samia anaijua CCM na anaitegemea mpaka kesho.
 
Nakwambia madiwani na wenyeviti wa CCM siku hizi wanashinda ofisi za vijiji na kata etii tunaomba mtubebe tena mda umekaribia hivi watu wa namna hii(CCM)watakubali hata rasmu ya katiba ya tume ya jaji warioba inayopendekeza wakuu wa mikoa na wilaya wasiwepo na wakiwepo wachaguliwe kweli haya MaCCM yatakubali yameshazoeza kula vya bure. Hata mama Samia anaijua CCM na anaitegemea mpaka kesho.
Ni ngumu
 
Mi Kama Msomi makini na Sina itikadi ya chama,Ila kwa uelewa na umri wangu CCM hawawezi kukubali katiba Mpya na ikitokea wanapiga vilaka ile ya 1977 jiulize hawataki ya jaji warioba licha ya kwamba tume ile ya warioba ni makada wa CCM wasitaafu. Kuna laana ndani ya CCM
Mkuu goleticia , kauli huumba!. Sometimes bila wewe kujitambua unapokuwa negative na kutoa kauli yenye negativity, then, hiyo kauli yako yenye negativity inauumbia hiyo negative!.

CCM kama CCM, japo ni chama kimoja lakini kuna CCM nyingi zinafanya mambo tofauti

kuna CCM ya Nyerere ile CCM ya Ujamaa na kujitegemea ilikuwa ya chama kimoja, ikaweka miiko ya uongozi. Ikaja CCM ya Mwinyi ikalizika Azimio la Arusha na kuleta Azimio la Zanzibar, lililofuta miiko ya uongozi, na kuruhusu vyama vingi.

Ikaja CCM ya Mkapa Mkapa na sera ya ubifsishaji na kubinafsisha mashirika. JK alipoingia tukaingia utandawazi na kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM hakukuwa na suala la katiba mpya lakini JK alianzisha mchakato hadi Bunge la Katiba na kuipitisha. CCM ya JPM ikaweka katiba kwenye ilani yake ya uchaguzi, JPM akasema katiba sio kipaumbele chake.

Sasa tuko CCM ya Samia, mambo ni kama ya enzi za Mwinyi, japo katiba haipo kwenye ilani ya CCM lakini huyu Mama atatupatia katiba mpya.

Just be positive na Mama, atatupatia katiba mpya.
P
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom