Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 45,869
- 101,839
Wanabodi
Hii ni Makala ya Jumapili ya Leo
Leo naendelea na ile mada ya kuhusu Haki za Kikatiba, zilizotolewa na Ibara moja ya Katiba, halafu zikaja kuporwa kwa kuchomekewa vifungu vinavyopora haki hiyo na ibara nyingine.
Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni batili. Mahakama Kuu ndio mamlaka pekee ndani ya JMT, inayoweza kutamka sheria fulani ni batili. Hili ninalozungumza hapa, Mahakama Kuu iliishalitamka ni Batili.
Bunge limetunga sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya mwaka 1977.
. Mahakama Kuu Ikatamka Sheria hiyo ni batili kwasababu inakwenda kinyume katiba!. Serikali yetu, kupitia Bunge, letu, ikafanya marekebisho ya katiba yetu na kuvichomekea hivyo vipengele batili, ndani ya katiba yetu!.
Mahakama Kuu chini ya Half Bench (Majaji 3) ikatamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Mahakama ya Rufani chini ya Full Bench (Majaji 7) wakaubariki ubatili huo not expressly but impliedly kwa kusema "the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.
Yaani Mahakama Kuu imesema jambo hili ni batili!,
Serikali ikaichukua batili hiyo ikaipitisha Bungeni kwa hati ya dharura, ikafanya marekebisho ya katiba, ikachomekea batili hiyo ndani ya katiba yetu.
Mahakama Kuu ikasema tena, hata uchomemekeaji huo uliofanywa na Bunge letu, kuichomekea hiyo batili ndani ya katiba yetu, nayo ni batili!.
Jambo la ajabu likafanywa na Mahakama ya Rufani, haizungumzi lolote kuhusu hiyo batili, wala ubatili uliofanyika wa kuichomeka batili ndani ya katiba yetu!, bali ikasema Mahakama sio custodian wa the will of the people, bali ni Bunge lenye wawakilishi wa wananchi, hivyo kulirudisha hilo jambo kwa bunge ndio iliondoe!, bila hata kutamka kuwa ni batili!. Huo ubatili mpaka ninavyoandika hapa sasa, bado ukingali upo ndani ya katiba yetu, Jee Turuhusu Ubatili Huu Uendelee Kuwepo Ndani ya Katiba Yetu Mpaka Lini?. Tunaomba Jicho la Haki la Mama, liuangazie ubatili huu, mimi kama mimi nasema "Tusiruhusu!", Jee vipi wewe mwenzangu?.
Haki ninayoizungumza hapa ni haki ya kila Mtanzania kuwa huru kuchagua kiongozi wake kwa kupiga kura kama ilivyotolewa na Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT ambayo ilipaswa kwenda sambamba na haki ya kila Mtanzania kuchaguliwa iliyotolewa na Ibara 21 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, jinsi ilivyokuja kuporwa na shurti la mgombea uongozi wa umma, kudhaminiwa na chama cha siasa hivyo kuipora kabisa ile haki iliyotolewa na ibara ya 21.
Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi
Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya kwanza ilikata rufaa kuipinga hukumu ya Jaji Lukakingira!. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!.
Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali katiba yetu ichezewe, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.
Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu
(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sheria No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.
(b) Kutamka wazi kuwa kila Mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.
Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!.
Lakini serikali yetu ya wakati huo, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench chini ya majaji 7, wakiongozwa na Jaji Mkuu mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu.
Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabingwa wabobezi watatu wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, (baadae akawa Mwanasheria Mkuu Zanzibar, sasa ni Makamo wa kwanza wa rais Zanziibar), Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa (Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)
Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua ifuatavyo, hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodians of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.
Hapa Mahakama ya Rufani Tanzania, ilijivua jukumu la kuilinda katiba. Kama ubatili unafanywa kwenye katiba yetu, halafu Mahakama yenye jukumu la kutafsiri katiba inajivua jukumu hili!, who is the custodian of the will of the people?.
Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki fulani, halafu Bunge likatunga sheria kuifuta haki hiyo, ilitegemewa mahakama kutumia mamlaka yake ya “checks and balance” kulia,nia Bunge haliwezi kutunga sheria inayokwenda kinyume cha katiba!. Mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?.
Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!. Yaani Bunge litunge sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kisha kipengele cha sheria hiyo batili kikachomekewa ndani ya katiba kwa mabadiliko yakatiba kwa hati ya dharura!. Mahakama Kuu inasema huu ni ubatili, Mahakama ya Rufaa inasema “hatuwezi kuliingilia Bunge!.
Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ukatufungua macho kuhusu political silent status za baadhi ya majaji wetu!. Kumbe baadhi ya majaji wetu nao ni makada wa vyama vya siasa!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama wakuu wa mhimili wa mahakama mara tuu baada ya kustaafu wanageuka makada!.
Wasalaam
Paskali
Uli kulielewa vema banndiko hili, lisomwe na Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Na Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!