Rais, wananchi wanataka kujua Michango mashuleni imerudishwa? Tunaomba tamko la Serikali

Michango gani haikuwepo na michango gani ipo sasa hivi? Mimi mwanangu kaanza form one hapa Jijini Mwanza, sijatoa hata shilingi zaidi ya vifaa vya usafi.

Hakuna kiongozi wa ccm ambaye mtoto wake anasoma shule za kata. Tafadhali kaa kimya acha wanaokutana na dhahama waongee, sio kuleta upotoshaji ili kuficha ukweli.

Halafu mleta uzi unaposema hao mawaziri wasitegeane wajitokeze watoe ufafanuzi kwa wananchi, kwani wao wamechaguliwa na wananchi au wako hapo walipo kwa maagizo ya rais? Hawawezi kuwapa ufafanuzi watu ambao hawajawachagua kwa kura.
 
MOROGORO SHULE YA SEKONDARI KIHONDA MAGOROFANI WANAFUNZI WAMEAMBIWA WAJE NA DAWATI NA KITI CHA KUKALIA ..... USANII TUPU. CHATO OYEEE
Sasa kwani kupeleka kiti cha kukalia mwanao nalo la kulalamika? Kwa kweli watanzania tumeambukizwa ujinga na tumekuwa wajinga webkama hupeleki kiti na meza mwanao atakaa chini nani unamkomoa?
 
Sema wewe ndiyo unataka kujua wananchi gani waliokutuma uwasemee?

Michango hata ulaya watu wanatoa kwa maendeleo jinga wewe kama huna tulia siyo kuleta uchochezi humu.
Serikali ilikataza michango mashuleni kwa waraka rasmi na kusisitiza sere ya chama tawala ya elimu bure itekelezwe kikamilifu.
 
Mkuu inaonesha una sababu zako nyuma ya pazia. Ikiwa Huna ushahidi unafanya uchochezi. Hiyo michango ni Kwa ajili ya nini na Nani walikubaliana, ni wazi wenyewe au walimu ndo wameibua wenyewe? Ni vema ukawa na maelezo yaliyojitosheleza
Ameeleza alichokiona, unataka ushahidi gani
Acha mamlaka husika zifanyie kazi,
Kila taarifa mbaya kwenu ninyi ni kupinga tuuuu!!!
Mmelogwa?
 
Mkuu inaonesha una sababu zako nyuma ya pazia. Ikiwa Huna ushahidi unafanya uchochezi. Hiyo michango ni Kwa ajili ya nini na Nani walikubaliana, ni wazi wenyewe au walimu ndo wameibua wenyewe? Ni vema ukawa na maelezo yaliyojitosheleza
Vyombo vya habari ilivifungia ili uovu wenu usifichuke hadharani.
 
Michango Ni muhimu kwa baadhi ya shughuli za shule
Mfano chakula kwa shule za msingi...hili Ni uamuzi wa wazazi kupitia vikao halali vya shule
Huwezi kuniambia Kila siku nimpe mtoto hela ya kula shulen wkt kwa mchango wa 5000 mtoto anakula mwezi mzima.

Huko Kilimanjaro na Arusha lazima kuchangia chakula, huwezi kusema mtoto arudi home kula wkt wazazi tuko shamba mbali tunalima

Tena mzee baba akae apotezee vinginevyo WATOTO watatushinda, kumpa mtoto hela Kila siku hatuwezi sisi wa Kijijini.

Nyie wa dar msichange, sisi tumeona ugumu na tumeomba wenyewe kwa ridhaa yetu tuchangie baadhi ya huduma
 
MOROGORO KIHONDA MAGOROFANI WANADAI WAZAZI MADAWATI NA VITI...SANAAA ZIKOJE HIZI
 
Bila michango hakuna kitakachofanyika.
Be blessed

Mfano choo Cha shule matundu mawili

Tukae kumsubiri jafo au mzee baba atujengee...haiwezekan wazazi kwa vikao halali vya shule tunakubaliana mchango, tunapeleka makubaliano kwa mkurugenzi hela inachangwa tunajenga

Mambo ya Kila kitu kuisubiri serikali wkt WATOTO wanateseka U.T.I, wakati wanajisaidia vichakan kisa matundu ya choo machache Ni ujinga na kukosa uzalendo.

U.T.I haiishi kisa mtoto anaibeba shuleni
 
Sasa kwani kupeleka kiti cha kukalia mwanao nalo la kulalamika? Kwa kweli watanzania tumeambukizwa ujinga na tumekuwa wajinga webkama hupeleki kiti na meza mwanao atakaa chini nani unamkomoa?
Huyu mtu hajawah kutembelea hizo shule akajionea ndio maana analalamika
 
Sema wewe ndiyo unataka kujua wananchi gani waliokutuma uwasemee?

Michango hata ulaya watu wanatoa kwa maendeleo jinga wewe kama huna tulia siyo kuleta uchochezi humu.
Kuwa mwelewa wewe michango in utaratibu siyo kila Mwalimu aanzishe michango kwa sababu wazazi tuna hela.
 
Elimu bure ni kuwaonea waalmu ili kupata cheap popularity.

Kwa nini wasingesikiliza maoni ya wadau kwanza?
 
Back
Top Bottom