mkamanga original
JF-Expert Member
- Jan 21, 2015
- 614
- 597
Watoto wa madarasa ya awali na darasa la kwanza hawapokelewi mashuleni mpaka wazazi watoe michango.
Utafiti uliofanyika unaonyesha mzazi wa darasa la kwanza analazimika kuchangia kati ya tsh. 15,000 hadi tsh. 80,000. Wakati wale wa awali michango yao ni kati ya tsh. 20,000 hadi 100,000.
Mbaya zaidi michango yenyewe hawatoi hata risiti wanachofanya walimu kuandika jina tu kwenye daftari.
Serikali ilishatoa maelekezo na waraka wa uchangiaji lakini mwaka huu ni kama waziri mwenye mamlaka haoni kinachoendelea kwenye shule zake.
Mfano wa michango inayochangishwa ni ujenzi wa madarasa, chakula na madawati. Taasisi zake rais zifanye kazi, shule za serikali hazipaswi kuwakataa wanafunzi kisa umaskini wa mzazi.
Hii wizara ni bora angepewa Mh.Lukuvi kwa sababu anafuatilia mpaka kwenye grassroot lakini Jaffo na Ngalichako wamepoa mno ,hata hawajui kama wazazi wanakataliwa kupokelewa watoto wao kisa mchango.
Ningeweka baadhi ya risiti hapa za wazazi ambao nilibahatika kupata nakala ,lakini naona kila nikijaribu kuattach zinagoma, michango katika shule za msingi nimerudi kwa kasi